Mchezaji huyo ghali duniani alifanya
mazoezi peke yake gym jana, wakati wachezaji wenzake wengine wakijiandaa
na mechi hiyo ya Kundi B na hakutajwa katika kikosi cha kocha Carlo
Ancelotti.
Ilitarajiwa kocha huyo Mtaliano
angemrejesha kikosini baada ya kipigo cha mwishoni mwa wiki kichoifanya
sasa Real Madrid izidiwe pointi tano na Barcelona katika ligi ya kwao.
Nje: Gareth Bale ataukosa mchezo wa leo wa Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa
Uangalizi: Winga amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja siku za karibuni
Lakini Bale hayuko tayari kuitikia wito wa kocha wake, kutokana na maumivu ya misuli ya paja la kushoto aliyoyapata siku 11 zilizopita wakati akipasha misuli moto kwa ajili ya mechi dhidi ya Getafe na kumfanya aondolewe kikosi cha kwanza.
Anafiiri mara mbili: Kocha Carlo Ancelotti atalazimika kufikiri kwa kina, angalau anaye Cristiano Ronaldo (chini)
Bale na Cristiano Ronaldo katika moja ya mechi za timu hiyo
Naye beki Rio Ferdinand ataukosa mchezo wa timu yake, Manchester United dhidi ya Shakhtar Donetsk kutokana na maumivu ya nyonga.
Lakini kocha wa United, David Moyes amemtukuza mshambuliaji Robin van Persie kama mchezaji bora zaidi kuwahia kufanya naye kazi.
"Tumewaacha wachezaji au mmoja,"alisema Moyes. "Rio Ferdinand, Anderson, Fabio na Wil Zaha hawapo nasi. Sijawahi kumtumia Rio popote, lakini amepata matatizo ya nyonga. Si makubwa,".
Nje: Moyes amethibitisha Rio Ferdinand hatasafiri kwenda Ukraine
Wa mbele tishio: Wayne Rooney na Robin van Persie wakitaniana wakati wa mazoezi ya Manchester United jana