Like Us On Facebook
Showing posts with label Bongo movie. Show all posts
Showing posts with label Bongo movie. Show all posts

KESI YA KIFO CHA KANUMBA... LULU AANIKA UKWELI,MAMA KANUMBA AMWAGA MACHOZI!!

MWANGA umeanza kuonekana juu ya kesi inayomkabili staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kumuua bila kukusudia staa mwenzake wa muvi, Steven Charles Meshack Kusekwa Kanumba ambapo safari hii aliamua kukiri vipengele kibao, Risasi Mchanganyiko lina habari yote.
Elizabeth Michael 'Lulu' aliyeambatana na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ wakiwa eneo la mahakama.
Akikiri mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania juzi (Jumatatu) wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, nyota huyo aliweka wazi mambo ambayo hapo awali hakuwahi kuyakubali kortini jambo lililovuta hisia za wasikilizaji waliokuwa wamefurika ndani ya chombo hicho cha kutoa haki kujua kinachoendelea.
Mwendesha mashitaka wa upande wa serikali, Monica Mbogo alivitaja vipengele kadhaa ambavyo Lulu alitakiwa kuvikana au kuvikubali.
Lulu, mama yake mzazi Lucresia Karugila wakiongea na mwanasheria wao, Peter Kibatala mahakamani.
Katika kesi hiyo iliyoendeshwa kwa ustadi mkubwa wa wanasheria kuoneshana ujuzi wa kusoma na ‘kubugia’ vipengele vigumu vya sheria, Lulu alipata wakati mgumu wa mambo kiasi cha kumwita wakili wake, Peter Kibatala mara kwa mara.
MADAI YA KUMUUA KANUMBA BILA KUKUSUDIA
Lulu alikiri kwamba, mashitaka yake mahakamani hapo yalikuwa ya kumuua bila kukusudia, marehemu Steven Kanumba Aprili 7, mwaka 2012.

Lulu akiongea na mama yake kabla kesi yake kuanza kusikilizwa.
KUWEPO ENEO LA TUKIO NA KUTOKEA KWA UGOMVI
Katika maelezo yake, Lulu aliweka bayana kuwa siku ya tukio alifika nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza ya Vatican jijini Dar saa 6 usiku na kuingia moja kwa moja chumbani.
Alizidi ‘kuchezesha taya’ kuwa, kulitokea ugomvi kati yake na marehemu licha ya kutotaja chanzo cha ugomvi huo.

Aliongeza kwamba, Kanumba alimvuta mkono na kumrudisha ndani wakati alipokuwa akijaribu kukimbia na kuufunga mlango, mwishowe alifanikiwa kutoka na kukimbia kusikojulikana.
KUKAMATWA KWAKE BAMAGA
Lulu aliweka wazi kuwa, siku ya tukio, saa 11alfajiri alikamatwa maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam alipokuwa akijaribu kutorokea kusikojulikana.

KUHUSU UHUSIANO
Bila kupepesa macho wala kuchezesha kope, Lulu alikubali kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Kanumba kwa muda ambao hakuutaja hali ambayo baadhi ya watu walionesha kuwa ‘sapraizidi’.

AMWAGA MACHOZI KORTINI
Awali, Lulu alipofika mahakamani hapo akiwa ameongozana na mama yake mzazi, Lucresia Karugila na staa wa muvi za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ alionekana kuwa na amani.

Msanii huyo alimudu kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda ambalo liliingia mtaani siku hiyo. Lakini baada ya kuanza kwa kesi, ilifika mahali alidondosha machozi hali iliyomlazimu kujifuta uso kwa kitambaa.
Baadhi ya watu walinong’ona kuwa, mrembo huyo alikuwa analizwa na kumbukumbu za tukio la kifo cha Kanumba na kwa sababu ya kuogopa kesi.

MAMA KANUMBA ASUSA
Habari nyingine zilidai kuwa, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa hakutokea mahakamani hapo licha ya umoja na udugu alionao kwa sasa na familia ya  Lulu.

Ilidaiwa kuwa sababu kubwa ya kushindwa kufika kortini ni kukosa uamuzi wa upande gani angekaa kati ya mshtakiwa (Lulu) na mshitaki (Jamhuri) kwa vile kote kuna muhusu kwa sasa.
“Unajua mama Kanumba alipogundua kwamba anayetakiwa kujibu madai ni Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu alimtangaza ni mwanaye na anayelalamika ni serikali, alishindwa kujua akija leo (juzi) angekaa upande gani? Akaamua kutokufika kabisa,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Mchanganyiko lilimsaka kwa simu mama huyo lakini bila mafanikio kufuatia simu yake ya mkononi kuita muda mrefu bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Lulu alikamatwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa galacha wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba mnamo Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza Vatican jijini Dar.

Baada ya kukamatwa na kuswekwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar, Lulu alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo hakutakiwa kujibu ndiyo au hapana.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ya madai hayo.
Aliachiwa kwa dhamana Januari 29, 2013 na kuambiwa kwamba kesi yake itakaporudi, itakuwa chini ya mahakama kuu. Juzi ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza.

-GPL

MUIGIZAJI WA KIKE BONGO MOVIES AWASHANGAZA WATU KWA ALICHOKIFANYA JUKWAANI,TAZAMA ALICHOKIFANYA!!


'Yuster Nyakachara 
'MUIGIZAJI wa kike Bongo Movie's mwenye vipaji vingi kuliko muonekano wake, Mashabiki hupagawa sana na upana wa sanaa yake anapopanda jukwaani na kuvaa uhusika wa kudance katika Show zake huacha gumzo kwani kazi hio ya kucheza ngoma za utamaduni hajaianza leo wala jana, Kaianza siku njingi sana lakini habweteki ametumbuiza nje ya bara la Africa mara nyingi sana.

Uuuwiiiiii...! Hii kweli Valentaines Day..!


PICHA
hizi unazoziona hapa ndugu msomaji ni picha za jana katika Tamasha la (Sanaa Sana) na
Malaika Bend Jijini Dar Es Salaam, Dada huyo pamoja na kumiliki kampuni ya filamu iitwayo  EAGLE ENTERTIMENT lakini akipanda jukwaani ni balaa.. M/mungu abariki kipaji chake. 




MSANII WA BONGO MOVIES "SABBY ANGEL" AAMUA KUJIUZA MTANDAONI...TAZAMA PICHA ZAKE ALIZOPIGA..

Tanzanian actress Salma Tamim(Sabby Angel) has posed topless for a photoshoot in Kenya. The actress who has already started to make waves in the industry with movies opposite big names including Vicent Kigosi(Ray) and Muhsin Awadhi(Dr.Cheni) looks extremely hot in the shoot. Sabby was in Kenya for almost two weeks and news is that there are some Kenyan film companies which have already shown interest to work with this Tanzanian bombshell actress. No doubt Sabby is one of the most sexiest actresses in Tanzania. She is also a singer and model and you can like her page Here

Check out the exclusive  images below..................
 
          Oooh babyy..................

oohh.......... this is definetly Sabby "Angel"
and we loved the styling....
Does she look hot or not...?
COVER

Part 2 of her photoshoot coming soon right here.........

18+:KAMA HUKUBAHATIKA KUONA PICHA ZA BEHIND THE SCENE ZA MOVIE YA NGONO YA KWANZA YA KENYA, HIZI HAPA




The controversial and

highly hyped House of Lungula is about to hit the silver screens. If 

you have not heard about the film, it’s about the weird s3x#@l 

habits of Kenyans packaged with some humor.

Some of the actors and actresses acting in the controversial film 

which will rock the industry include TPF judge Ian Mbugua, 

former BBA contestant Sheila Kwamboka, KTN’s Nice Githinji, 

Citizen TV’s Sarah Hassan, Liz Njagah among others.

Below are behind the scene photos of the making of the film:








USHOGA WA DK.CHENI HUU HAPA...!! SOMA HAPA KUJUA KIUNDANI...

SIKU chache baada ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuzuia filamu ya mkongwe katika sinema za Kibongo, Mahsein Awadh Said ‘Dk. Cheni’ ijulikanayo kwa jina la Nimekubali isiingie sokoni kwa madai kuwa imekiuka maadili ya Kitanzania, msanii huyo ameibuka na kueleza kinagaubaga, Risasi Jumamosi limenasa sauti yake.
Akizungumza na mwandishi wetu Jumatano ya wiki hii maeneo ya Mlimani City jijini Dar, msanii huyo alisema amesikitishwa na maamuzi ya bodi hiyo huku akidai kuwa lengo la filamu hiyo ni kukemea tabia za kishoga zinazoendelea kuibuka kwa vijana ikiwa ni pamoja na kupinga uhalali wa ndoa za jinsia moja.
Mkongwe wa sinema za Kibongo, Mahsein Awadh Said ‘Dk. Cheni’.
Katika maelezo hayo, DK. Cheni ambaye huzitendea haki filamu zake kwa kuvaa uhusika halisi, alisema moja ya kigezo ambacho bodi hiyo imekitumia kuzuia filamu hiyo ni pamoja na muonekano wa bango la filamu hiyo ambalo linamuonesha msanii huyo akiwa amevaa vazi la shera huku akiwa amejiremba kwa madai kuwa ni kuchochea ushoga jambo ambalo msanii huyo amelipinga vibaya.
“Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, hakika wamenionea sana, lengo letu ni kuonya na kukemea vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo ndani ya filamu hiyo.
Mkurugenzi wa bodi ya filamu,  Joyce Fissoo.
“Lakini, ndani ya filamu hiyo, kuna kipande ambacho kinaonesha kiongozi wa serikali akikemea kitendo hicho, sasa hapo ushoga wangu uko wapi? Kuvalia shera kwenye kava? Siyo sahihi,” alisema Dk. Cheni.
Mbali na kava hilo, msanii huyo alidai haoni kosa lolote katika filamu hiyo hivyo ataendelea kupigania haki yake na kwamba hayuko tayari kuonewa.
Jitihada za kumpa mkurugenzi wa bodi ya filamu,  Joyce Fissoo ili kuelezea juu ya sekeseke hilo, ziligonga mwamba hadi gazeti hili linaingia mtamboni lakini imedaiwa kuwa bodi hiyo itasimamia msimamo wake. 
-Risasi

BAADA YA KUPOKONYWA MALI ZOTE NA ALIYEKUWA MWANAUME WAKE...MASTAA WA BONGO MOVIE WAMPA MAKAVU WEMA...!

MASTAA wa kike Bongo wamecharuka na kutoa yao ya moyoni baada ya nyota mwenzao, Wema Sepetu kubwagwa na aliyekuwa mpenzi wake, anayetambulika kwa jina moja la Clement na kumnyang’anya vitu alivyompa kama zawadi wakati wa mapenzi yao.
Wema Sepetu.
Kuhusu Wema kuporwa ofisi yake ya Endless Fame Film Production, kupewa notisi ya nyumba aliyokuwa amepangiwa na kigogo huyo anayeelezwa yupo serikalini na kunyang’anywa magari siyo stori kabisa mjini.
Risasi Mchanganyiko lilifanya mahojiano na mastaa hao wikiendi iliyopita, kwa njia ya simu na kuwahoji kuhusu kitendo alichofanyiwa mwenzao ambapo walifunguka bila wasiwasi wowote.
USENGENYAJI
Wakali hao, waliopata kuzungumza na waandishi wetu kwa nyakati tofauti, baadhi wamemponda Wema kwa kutokuwa makini wakati akiwa kwenye uhusiano na kigogo huyo kwa kutaka kukabidhiwa hati za vitu alivyopewa.
Wa kwanza kuzungumza ni Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye alisema: “Mimi namshukuru Mungu kwa sababu sijapangiwa nyumba na mwanaume.  Naishi maisha yangu simpo ya furaha na amani, sipendi kuigiza maisha. Hao wasanii wanaopenda mambo makubwa wakati hawana uwezo,  nawashauri wafanye kazi, filamu zinalipa sana. Wasipende vitu vya haraka, maana siku zote vizuri huja taratibu.”
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
“Mastaa tusijiachie sana kwa wanaume, kama ukipewa gari, upewe na kadi... tusidanganyike na tusipende kuhongwa, tutafute vya kwetu. Kama mtu anakupenda na anakusaidia kwa mapenzi mema, sawa mheshimu.”
WASTARA JUMA
“Inabidi tujitambue jamani, maana kuna watu wanatembea na mastaa makusudi ili wajulikane au kwa manufaa yao wenyewe. Tuache kuishi kwa kutegemea migongo ya wengine. Wengi hawana mapenzi ya kweli. Hata kama mmeachana, sasa kuna sababu gani ya kumnyang’anya mtu vitu ulivyompa?”
 

NURU NASSOR ‘NORA’
 
“Mimi najisikia vibaya sana... kama mtu unajiamini una kipaji, kwa nini usifanye kazi?  Mastaa tuache kujitangaza, kwa sababu tunatumika kama vyombo vya starehe tu.  Tutafute ndoa, tusitumie ustaa kufanya ufuska kwa sababu mali zinapita na mwisho wa siku tunaharibu maisha yetu.”
 
TAMRINA POSH ‘AMANDA’
 
“Utapeli ni mwingi, haya mambo ya kupewa vitu siyo vizuri kabisa, tuache.  Wanawake tuna akili fupi sana na tunajisahau tunapokuwa na wanaume wakati wenyewe wana kitu moyoni mwao, akishapata anachotaka anaanza matatizo.

“Bora nitembelee taksi au Bajaj kuliko kudhalilishwa... wanawake ni wajinga na huwa tunajidanganya kwa vitu visivyo vyetu, mwisho wa siku tunaumbuka. Tuache sifa za kijinga.”

credit :gpl 

PICHA CHAFU ZA KIMAPENZI!!!! UKITAKA KUA NA DEMU BONGO MUVI KUBALI KUCHAPIWA


Tasnia ya uigizaji Tanzania maarufu kama bongo muvie imekua ikipanda kila kukicha na kuwanufaisha wengi wanaoamua kujiingiza huko na kubahatika kupata mafanikio makubwa. Wengi wamenufaishwa kama kina Ray, Shilole, JB, Ndauka na wengine wengi. Lakini bongo muvie hiyohiyo imejaa uchafu mwingi ambao behind the scene hauelezeki......


Mademu wa bongo muvie
wamekua ni watu wa kujiachia sana na kujisahau linapokuja suala la kwenye scene za mapenzi, Je kama wewe ni mwanaume rijali uliekamilika unaangalia mchumba wako anashikwashikwa kimahaba na jidume lingine utajisikiaje? Angalia Uwoya kwenye Oprah au Rose Ndauka kwenye Clinic Love....dah ni aibu tupu. 


Wakati mwingine unaweza ukashangaa sana wanawezaje kuishi na mabwana zao huku wakirudi nyumbani jioni wakiwa wametoka kushikwashikwa na wanaume wengine... 


Pia kuingia bongo muvie siku hizi hakutegemei kipaj sana, uzuri ndo silaha yako lakini ndio ujiandae kutoa mzigo kwa ma-legendary wa kiumeni.
Moja ya picha za nusu uchi za rayuu
Hivyo sishauri mdada mzuri kwa sasa kua na ndoto za kuingia huko kwani ni ufuska ndio umetawala tu na wewe mwanaume unaemruhusu demu wako aende akaigize mapenz na mwanaume mwingine ujiandae kuchapiwa japo ni siri ya ndani. Huwa najiuliza BASATA hawaoni au ??? 

Hayo ni maoni yangu tu kama na wewe unayako tunaweza share na mm kwa comment

Baada ya LULU kupata Mchumba, SINTAH ampa darasa la Mapenzi..!!

Ninakutakia kila la kheri ila kuwa muangalifu na wanaume maana kuna wa aina mbili masikini na matajiri, wale masikini watakupenda kwa dhati wakiwa hawana ila siku wakipata utawajua wao nani, ama uongo wadau?
na wale matajiri watajua umependea pesa zao na hata kama umempenda kwa dhati mambo ya manyanyaso na nk yatahusika, esp matajiri watakuhonga kila kitu make
sintah 
sure hata akikununulia kijiko kiwe katika jina lako Elizabeth Michael.              All the best maana sasa umekuwa yaliyopita si ndwele tugange yajayo, one more thing, mfiche mtarajiwa wako we anza kumtangaza anaitwa J haaa kuna makubimbiri yanan’gaa macho kazi yao kusubiri kutongozwa halafu yalivyokuwa mahayawani yenyewe yanakuja kwa nia moja tu ya kuharibu na kusepa so TAKE CARE…….
 

KASHFA YA KUSAGANA KATI YA IRENE UWOYA NA MARIAM ,SOMA ZAIDI

Mariam Ismail
Mastaa wa filamu nchini Mariam Ismail na Irene Uwoya wanadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi(usagaji) na kudaiwa kuishi pamoja kabisa. wiki kadhaa nyuma muigizaji mmoja chipukizi anayekuja juu kwa kasi aliutonya mtandao huu kwa kusema " Mariam Ismail na Uwoya wanasagana tena wanaishi pamoja kabisa, fuatilieni mtajua".

Baada ya habari hizo ilibidi Swahiliworldplanet kuwatafuta mastaa hao, wa kwanza kutafutwa akiwa Irene Uwoya lakini namba yake ya simu kwa takribani wiki 2 ilikuwa haipatikani na hata jana alipotumiwa ujumbe kupitia namba yake nyingine hakujibu.

Baada ya hapo ilibidi kumtafuta Mariam Ismail ambaye wamecheza filamu nyingi na Irene Uwoya kama vile Sobbing Sound, Omega Confusion, The Return Of Omega na Apple, Hata hivyo Mariam anafanya vizuri katika filamu alionekana kuwa busy na kuchelewa kujibu ujumbe wa madai ya kusagana na Uwoya lakini jana star huyo aliyejipatia umaarufu kwa kuuvaa vizuri uhusika katika filamu zake alitoa ushirikiano mzuri kwa kujibu madai hayo akidai sio kweli ila yeye na Uwoya ni marafiki wa karibu sana na wanasaidiana katika shida na raha ndiyo maana baadhi ya watu wameshaanza kusema vibaya...

"Nadhani mimi ndio mtu wa kwanza kupiga vita upumbavu kama huo... mimi ni mwanamke ambae nimeumbwa kikamilifu.. sina kasoro yoyote ya kunifanya niwe na mwanamke mwenzangu....hao wanaofanya upumbavu huo nadhani wana vijikasoro kwenye mili yao.... Irene Uwoya ni rafiki yangu sana tena urafiki wetu sio wa leo wala kesho... ni marafiki wa kushibana kabisa... nikoseapo huwa ananikosoa na yeye akoseapo huwa namkosoa....sometimes huwa tunagombana na kupatana vitu ambavyo ni vya kawaida katika maisha." alisema Mariam ambaye hajawahi kukumbwa na skendo yoyote ile kabla.
 

Irene Uwoya
Mariam ambaye kipaji chake cha filamu hujionyesha waziwazi alimalizia kwa kusema "Irene ananiheshimu sana na mimi humuheshimu sana Irene, imefikia hatua ya mimi na yeye tukakaa chini na kupanga tuishi wote kitu ambacho sioni tatizo na hilo. Ingekua ni chumba kimoja hapo sawa... lakini ni nyumba kubwa yenye kujitosheleza...kila mtu na room yake...tunaishi kwa amani na kwa kushirikiana penye tatizo hulitatua wenyewe bila kumshirikisha mtu.Ukimya wetu na kupatana kwetu kusiwafanye watu kuanza kuhisi upumbavu juu yetu... natumai ujumbe wangu utawafikia mashabiki wangu wote. Asante. In god I trust."

NIMEMISS KUMBATIO LA KIMAHABA JAMANI..WASTARA

Leo majira ya asubuhi msanii wa Bongo movie aliweka picha huku akiwa amekumbatiwa na mwanaume na kusema kuwa “nimemisi kumbatio la huba” kutokana na kauli hiyo wadau wameweka maswali mengi na kuuliza je huyu ndiye mume mtarajiwa wa Wastara au la. tunatafuta ukweli wa swala hili kisha tutalifikisha kwenu wadau wa Tovuti yetu
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari