Like Us On Facebook
Showing posts with label Vituko. Show all posts
Showing posts with label Vituko. Show all posts

HURUMA:CHEKI KILICHOWATOKEA WALE WAUMINI WALIOLISHWA NYASI NA MCHUNGAJI WAO,NI BALAA TUPU

Waumini wa Mchungaji Daniel walijikuta wakianza kuumwa mara baada ya Mchungaji huyo kuwafanya wale wale majani.
Picha zinazofuata zinaonyesha watu tofauti wakiwa wagonjwa kwenye vyoo -  picha za vyooni zinawaonyesha wanawake wakishikilia matumbo yao, huku wanaume wakiwa wanatapika kwenye masinki.
Japokuwa Mchungaji huyo bado hajasema lolote juu ya tukio hilo ila kupitia ukurasa wake wa Facebook hapo jana aliandika: 'Mungu yupo kazini na watu wake wanatoa ushuhuda sasa' 
Mchungaji Lesego Daniel
TAARIFA ZA KUIBUKA KWA KANISA HILO
Taarifa za kuibuka kwa kainsa hilo zilianza kusamba katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo kwa nyakati tofauti iliripoti kuwepo kwa kanisa linaloimiza waumini wake kula nyasi kama ishara ya kutangaza miujiza ya Mungu.
Uchunguzi uliofanywa na Wadadisi wa Habari, ulibaini uwepo wa kanisa wa aina hiyo maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam na huduma yao inafanywa kwa kutumia jina la Rabboni Centre Ministries yenye makao yake makuu jijini Pretoria, Afrika Kusini.
Waandishi wa Habari hizi, walifika Upanga, kwenye nyumba inayodaiwa kuwa ndilo kanisa hilo lakini hakuna mtu aliyekutwa hapo.

Hata hivyo, baadhi ya majirani walisema huwa wanawaona watu wakiingia katika nyumba hiyo lakini ajabu kunakuwa hakuna kelele zozote.

Chanzo chetu cha habari kimesema kuwa waumini wa kanisa hilo hula nyasi na baadaye kutapika, hali inayowafanya waamini kuwa kwa kufanya hivyo, wametakasika kiroho kwa kujazwa Roho Mtakatifu.
“Mchungaji wao huwakusanya waumini wake wanaopandisha mashetani wakiwa kanisani, hiyo hufanya shetani kumtoka mtu haraka,” kilisema chanzo.

Habari zinasema huduma hiyo ilianzishwa Afrika Kusini na Mtu anayejiita kuwa ni Mchungaji na Nabii Daniel Lesego mwaka 2002.
Imedaiwa kuwa kwa sasa waumini hao wapo kwenye mfungo ambao watu hufika kanisani na baadaye kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo wakisema kwamba Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote huku ikidaiwa kuwa manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.

"WASANII WA VICHEKESHO TUNADHARAULIKA SANA KWASABABU WENGI NI MASKINI"..KINGWENDU



Mchekeshaji mkongwe wa Tanzania Rashidi Mwishehe aka Kingwendu amedai kuwa sanaa ya vichekesho Tanzania haiwalipi vizuri wasanii hao.
 
Akiongea kupitia Hatua Tatu ya 100.5 Times Fm, Kingwendu amesema kutokana na kipato kidogo wanachokipata wasanii hao, hujikuta wakitengwa na wasanii wenzao wa Bongo Movies ambao huingiza kiasi kikubwa cha pesa kwa kucheza movies hizo.
 
“Kwa kweli tasnia yetu ya filamu upande wa comedy haitulipi vizuri na ndio maana wasanii wengi wa comedy hatuna magari, hatuna nyumba nzuri, tunachokipata tunakaa na watoto wetu hivyo hivyo tunakula. Lakini kiukweli kabisa filamu ya comedy haitulipi vizuri, wanatulalia sana.”
 
 Kingwendu ameongeza kuwa wasanii wa comedy wanatengwa na waigizaji wenzao kwa    kuwa wao ni masikini.
 
“Kwa sababu sisi wanatutenga kwa sababu kama nilivyokwambia, ni masikini. Hatuna usafiri, na usafiri wetu sanasana mtu akijitahidi kwa comedy utakuta Kingwendu ana pikipiki. Lakini wenzetu utakuta wana ma-Hammer, wanaendesha magari mazuri mazuri.
 
“Japo mashabiki wanasema kuwa wanauzia sura yale magari sio ya kwao, lakini sisi tunaamini ni ya kwao kwa sababu filamu wanauza kwa bei nzuri sana. Hasa kwenye soko la Steps pale wanauza kwa bei nzuri sana kama una filamu nzuri.”
 
Mchekeshaji huyo amewashauri wasanii wa Bongo Movie kuwa wamoja na kutowatenga wachekeshaji kwa kuwa ubaguzi huo utaipoteza tasnia ya filamu Tanzania. 

HOUSEGIRL ANASWA AKIKOJELEA CHUNGU CHA KUPUKIA CHAKULA..!! TAZAMA VIDEO YA TUKIO ZIMA

  
A man suspecting the behavior of his housemaid decided to install secret cameras in the kitchen. 

When he later checked the film, he got the shock of his life when he saw the maid urinating in the cooking dish.


MSANII WA KUNDI LA VITUKO SHOW BAADA KUCHEZEA KICHAPO CHA MBWA MWIZI SIKU ZA KARIBUNI SASA ASWEKWA RUMANDE MKOANI TANGA KWA KUMTUKANA MPENZI WAKE WA ZAMANI NA KUDAI KAMUAMBUKIZA UKIMWI


"Kazi kijeba" picha hii ni ya siku chache zilizopita baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa huyo mpezi wake wa zamani walioachana.


MSANII huyu amekuwa mgumu wa kuelewa kila akielezwa na uongozi wa kampuni ya Al-riyamy Production na wasanii wenzake kwa ujumla kuwa apunguze unywaji wa pombe kupita kiasi hadi kubebwa na wananchi wenye huruma kuletwa kambini yeye huitikia na
kukiri kwamba hatorudia lakini hazipiti siku mbili lazima usikie kalewa kaenda kumtukana mpenzi wake walioachana..!

 Hivi majuzi aliripotiwa kambini na muendesha baiskeli (bodaboda) kwamba alimkodi akamwambia ampeleke Usagara maeneo akanywe bia mara bodaboda anashangaa anaelekezwa mitaa isio na dalili yeyote ya kuuzwa bia..! 

Ghafla wakafika kwenye nyumba flani wakamkuta dada na mpenzi wake wametulia nje kwao wanapunga upepo, Ndipo Msanii aliposhuka kwenye baiskeli nakuanza kumporomoshea matusi ya nguoni yule dada na mpenzi wake huku akijitapa kwamba yeye ana ukimwi na kashamuambukiza huyo mwanamke kwahiyo huyo mpenzi wake mpya ajiandae kufa kwa gonjwa hatari la ukimwi...!,

Dada huyo ambaye alikuwa mpenzi wake kweli enzi hizo lakini kwasasa walishatengana aliamua kupiga simu kwa mmoja kati ya wasanii waVITUKO SHOW na kutoa malalamiko yake usiku huohuo Akakiri kutokurudia sualahilo Wasanii wenzake baada ya kufikishiwa taarifa hiyo na muendesha baikeli pamoja na simu iliyopigwa na dada huyo wamkalisha chini tena Kazi chini kama kawaida na kumuonya, Akakiri kutokurudia suala hilo. Amakweli siko la kufa halisikii dawa..! 

Cha ajabu jana kalewa tena na kuenda kumtukana dada huyo tena, Dada akaenda kuripoti polisi leo wamemtia mbaroni Kazi A.k.a Kijeba yupo kituoni


MAAJABU YA DUNIA...MWANAMKE AJIOA MWENYEWE BAADA YA KUKOSA MWANAUME WA KUMUOA

Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ametoa kali ya mwaka kwa kuamua kuandaa harusi na kujioa yeye mwenyewe kanisani. Nadine Schweigert mwenye umri wa miaka 36 amekuwa gumzo kwenye vyombo vya
 habari nchini Marekani baada ya kuandaa harusi  na kujioa yeye mwenyewe ambapo yeye ndiye alikuwa bi harusi na yeye pia ndiye aliyekuwa bwana harusi.Nadine ambaye ni mkazi wa Fargo, North Dakota nchini Marekani alijioa mwenyewe kwenye sherehe iliyohudhuriwa na jumla ya watu 40.

Alikula viapo vya ndoa mbele ya umati huo wa watu ambapo mwisho wa viapo alipuliza busu angani badala ya hali iliyozoeleka ya bibi na bwana harusi kubusiana.

Harusi hiyo ilifuatiliwa na fungate la nguvu (honeymoon) kwenye hoteli moja mjini New Orleans.

Akiielezea ndoa yake hiyo kwenye kipindi cha televisheni moja nchini humo, Nadine alisema kuwa hivi sasa anajihisi ni mwenye furaha sana na ndoa yake imeweza kuyabadilisha maisha yake toka kwenye huzuni na kuwa mwenye furaha sana.

Nadine alisema kuwa aliamua kujioa mwenyewe baada ya ndoa yake na mumewe aliyezaa naye watoto wawili ilipovunjika na watoto wake kuamua kwenda kuishi na baba yao.

Nadine alisema kuwa alipita kipindi kigumu sana cha machungu ya kuvunjika kwa ndoa yake lakini baadae aliamua kukaa chini na kutafakari maisha yake badala ya kujiingiza kwenye ulevi ili kupoteza mawazo.

Nadine aliongeza kuwa ndipo alipogundua kuwa furaha ya kweli na mtu anayempenda sana ni yeye mwenyewe hivyo akaamua kujioa yeye mwenyewe na hivi sasa haitaji tena mwanaume kwenye maisha yake.

Nadine aliongeza kuwa katika maisha yake haya mapya amekuwa akijitoa out mara kwa mara na amekuwa akijinunulia zawadi yeye mwenyewe.

MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA

              Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘The Great’.

Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda.
VIFO MILIONI 605
Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini.
Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao.

Steven Kanumba.

WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU
Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kundi la Five Stars wapatao 14, Kanumba, Sharo Milionea na mwanamuziki James Dandu ‘Mtoto wa Dandu’.
Pia alidai kuwa alihusika katika vita kati ya aliyekuwa Rais wa Iraq, Sadam Hussein na Marekani kwa kutumia pepo la uchonganishi alilolitaja kwa jina la ‘Magweju’.
Pia mchungaji huyo alidai kuhusika na  shambulio la hivi karibuni la Al-Shabaab katika maduka ya Westgate la Nairobi nchini Kenya na matukio mengine mengi hadi kufikia idadi hiyo ya vifo vya watu milioni 605.

Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’.


AWAONEA HURUMA WASANII, AWAONYA
Mchungaji huyo aliendelea kusimulia kuwa alipokuwa katika ulimwengu wa giza aliwahi kuwaonea huruma wasanii kama Kanumba, Sharo Milionea na Mtoto wa Dandu na kuwatokea kimiujiza akiwaonya waokoke kabla ya kuchukua roho zao huku mashabiki wao wakibaki na simanzi wakiamini kuwa vifo vyao ni vya kawaida.
Alidai kuwa baada ya kuwafuata mastaa hao na kuwaonya walikataa na badala yake akawaua.
Akiendelea kulishuhudia kanisa, Mchungaji Mayanga alisema kuwa kwa sasa ameokoka na kuachana na mambo ya giza, hivyo haogopi kuzungumza ukweli kwa kuwa roho wa Bwana anamuongoza kushuhudia kila kitu alichokifanya ili waumini watambue uwezo wa Mungu.

Gari la Sharo baada ya ajali.

ANA SIRI NZITO ZA VIGOGO
Huku akiomba hifadhi ya majina ya wahusika, mchungaji huyo alihitimisha ushuhuda wake kwa kudai kuwa ana siri nzito za vigogo au watu wakubwa ambao aliwahi kwa namna moja au nyingine kuwapa utajiri wa nguvu za giza.

UTABIRI
Hata hivyo, baadaye jamaa huyo alijitabiria kuwa atakamatwa na kufungwa siku moja kutokana na siri alizonazo.
“Yaani nina siri za watu wengi sana, nikiwaambia mtaogopa na nchi itatikisika. Najua siku moja watu watanikamata na kunifunga pingu kwa siri nilizonazo, lakini kamwe siogopi kwa kuwa Bwana ananiongoza,” alisema Mchungaji Mayanga.

Jeneza la Kanumba.

KANUMBA, SHARO MILIONEA
Kanumba alifariki dunia mwaka jana akiwa nyumbani kwake Sinza-Vatican, Dar huku Sharo Milionea akipoteza uhai kwenye ajali ya gari iliyotokea wilayani Muheza, Tanga wakati msanii huyo akienda kwao mkoani humo akitokea Dar.

VUNJA MBAVU NA METHALI ZA MPOKI A.K.A MWARABU WA DUBAI HAPA.

          Kutana na tweets za mkali wa comedy kutoka Orijino Komedi Mpoki a.k.a Mwarabuwadubai ambapo hizi ni baadhi tu ya tweets amewahi kuziandika kwenye page yake ya twitter na unaweza kumfata pia kupitia @mwarabuwadubai
2
3
4
5
6
7 
9
10
11
12
13
14
15
16

VIDEO: HAWA NDIO WATU WALIOISHANGAZA DUNIA KATIKA MATUKIO MBALIMABALI NA KUWEKWA KWENYE RECORD YA DUNIA..

           Katika tafiti zetu za hapa na pale tumegundua kuwa kuna watu wa ajabu sana katika Dunia tunayoishi.... Hivyo tunakuletea video kwa ufupi iliyokusanya matukio tofautitofauti kutoka kwa watu tofauti duniani walioishangaza Dunia kutokana na Vipaji vyao ama uwezo Binafsi walipewa na Mungu. Hivyo katika hili Basi watu hawa wamengizwa katika Kumbukumbu za dunia hii kama ukumbusho.

JAMAA AMFUNGA KUFULI MPENZI WAKE NA KUONDOKA NA FUNGUO ILI ASIMSALITI..!

                Mwanamme mwenye wivu amfungia na kufuli mpenzi wake ili asi cheat na kuondoka na  funguo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 25 aliamua kumshtaki mpenzi wake kwa polisi  baada ya kuchoka kuvumilia maumivu ya kukaa masaa bila kwenda haja na kuogopa kukata Jeans kwa mkasi kwa kumuogopa mpenzi wake huyo mwenye Umri wa miaka 40 angeweza kumuacha.HII KALI SANA WIVU NOMA DAHH

GIRLFRIEND AMLAZIMISHA BOYFRIEND WAKE APIGE MAGOTI HUKU AKIMCHAPA MAKOFI HADHARANI KWA KUMSALITI

                     Unajua kama kitu hicho kingetokea hapa Africa,watu wengi wangesema kala 'majani' ni msemo unaotumika kwa mwanaume anayetawaliwa na mwanamke wake.

Seriously,mwanaume gani anayeweza kumruhusu girlfriend wake,mchumba au mke wake amdhalilishe hadharani namna hiyo?

Mwanamke mmoja wa kichina amekamatwa na polisi baada ya kumlazimisha boyfriend wake apige magoti huku akimpiga makofi usoni.

Udhalilishaji huu ulitokea ijumaa iliyopita kwenye mji wa Kowloon,Hong Kong baada ya Chui(boyfriend) kumchukua msichana mwingine na kumpeleka nyumbani kwake wakati  anamahusiano na Cheng(mpiga makofi).


Cheng alijua na akampigisha magoti boyfriend wake huyo mbele za watu wakipita.
Aliposisitiza kuwa hakumuita yule msichana kwake akisema 'sikiliza kwanza kabla hujanipiga',Cheng akaanza kumchapa makofi usoni huku anapiga kelele
 'You're slandering me!'




Watu wakajaa na kuanza kufilm tukio hilo la aina yake ambapo lilitumwa siku hiyohiyo YouTube.Watu wengine walipoanza kuingilia ugomvi huo wa kimapenzi Cheng akapayuka 'Haiwahusu!'
Watu wengi walioshuhudia walikuwa upande wa Chui,mwanamke mmoja akamwambia 'simama achana na mwanamke huyu mwenye sura mbaya,unastahili mzuri zaidi'
Mpita njia mmoja akawapigia simu polisi ambapo Cheng alikamatwa.
Mwanamke huyo mwenye miaka 20(Cheng)alikamatwa kwa kesi ya udhalilishaji wakati boyfriend wake mwenye miaka 23,Chui akipelekwa hospitali

BINTI AJIKOJOLEA BAADA YA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI




                Huyu ni mwanamke  aliyekutwa  akiwa  hoi  baada  ya  kunywa  pombe  kupita  kiasi.....

Sakata hili ambalo  lilitokea katika  party  ya rafiki yake lilizua  gumzo  kubwa baada  ya  mrembo  huyu  kujikojolea....

Mwanzo  alionekana  akiwa  ni  mtu mwenye furaha na  mchangafu.Baada  ya  pombe kumwelemea,  binti huyu alijisogeza pembeni na  kujilaza  na  ndipo  aibu  ya kujikojolea  ilipomkumba

PANYA ACHEZEA KIPIGO KIKALI BAADA YA KUTAFUNA PESA ZA MSHAHARA WA MPALESTINA



               Mwanaume mmoja nchini Palestina amempa mateso makali panya baada ya kudai amemtia hasara kwa kuteketeza mshahara wake wa wiki (Kiasi cha Sh. 85,000/=)

- Baada ya kumpa adhabu hii, alimpiga picha na kuisambaza Facebook

Unakichukuliaje kitendo hiki?

-JF

WATU NA VIPAJI VYAO BWANA,TAZAMA MTU MWENYE KIPAJI CHA KUCHORA KWA KUTUMIA UUME WAKE

                 Ni kweli kwamba ubunifu katika biashara ni njia ya kuongeza wateja lakini kwa ubunifu wa Tim Patch msanii wa kuchora kutoka Australia nadhani ubunifu wake umepitiliza.
Msanii huyo ameamua kutotumia brush maalum kwaajili ya kazi ya kuchora na badala yake ameamua kutumia ‘uume’ wake kuchora michoro mbalimbali huku akiwa mtupu mbele ya wateja wake wa jinsia zote.
Tim ambaye anafahamika zaidi kwa jina la kisanii Pricasso katika maonesho ya sanaa yaliyofanyika hivi karibuni aliwasilisha michoro yake mbalimbali aliyoichora kwa kutumia uume wake na kujitangaza kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa P*n*s-Art.

SOURCE:BONGO5

KALI YA LEO:MTU NA MPENZI WAKE WAKUTWA WAMELALA MCHANA KWEUPEE KWA RAHA ZAO


             Mhh Unazani nini kilikuwa kinaendelea hapa .....mchana mchana kama huu ?

MWANAMKE ANASWA AKIMNYONYESHA MBUZI BAADA YA KUMALIZA ALICHUKUA MBELEKO NA KUMUWEKA MGONGONI

 
Na Rashid Mkwida — Katika hali isiyozoeleka, mwanadada huyu alikutwa na kamera ya Mkwidna blog katika mitaa ya Jijini Dar es salaam akihaha na mwanambuzi mgongoni huku mwanambuzi huyo akilia mee meee!!

 Mwanadada huyo alilazimika kumbembeleza kwa  kujaribu  kumnyonyesha mwanambuzi huyo aliyekuwa akilia kwa sauti kiasi cha kuwashangaza wapita njia..

 Kuna wakati mwanambuzi huyo alitaka kuchoropoka katika mbeleko ya mwanadada huyo lakini mwanadada huyo alijitahidi kuifunga vyema mbeleko yake ili mwanambuzi huyo akae vyema, haikufahamika mara moja mwanadada huyo alikuwa akimpeleka wapi mwanambuzi huyo.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari