Like Us On Facebook
Showing posts with label Maajabu. Show all posts
Showing posts with label Maajabu. Show all posts

MAAJABU:HUYU NDIO SAMAKI WA AJABU ALIYEWAHI KUVULIWA TANZANIA

 
AJABU NA INASTAJABISHA:Mchangamle kizimkazi,walikusanyika na kumshanga 
samakihuyu wa ajabu ambae wavuvi na wakazi wa maeneo hayo hawakuwahi 
kumwona,maana samaki huyu aelewiki ni CHUI, DUMA au ni nini.Nikaona 
nisistajabike mwenyewe nikuweke hapa wewe mpitiajiwa This is diamond 
upate kujua yanayoendelea Dunia. kwangu mimi ni ajabu sijawahi kuona 
kiumbe kama hicho.

HATARI SANA:ANGALIA PICHA JINSI KIJANA "MAD DOG" ANAVYO KULA NYAMA ZA WATU WA DINI YA KIISILAMU BAADA YA KUWACHOMA MOTO HUKO JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

KIJANA ALIYEFAHAMIKA KAMA MAD DOG AKIKATA SEHEMU YA MWILI WA MAITI YA KIISLAM WALIYOICHOMA MOTO KISHA KUILA'Mad Dog' licks blood off a knife, as a crowd prepares to burn the body of a lynched Muslim man in BanguiAKIWA ANAKULA SEHEMU YA MWILI WA MAITI YA KIISLAMMen carry the body of a lynched Muslim man through a street in Bangui, Central African Republic, on SundayWAISLAM WAWILI WALIKAMATWA NA KIKUNDI CHA WATU WENYE SIRAHA ZA JADI KISHA KUUAWA NA KUBURUZWA MTAANIA French soldier looks on as the body of one of the lynched Muslim men burnsASKARI WA KIFARANSA WAKISHUHUDIA MWILI WA MAITI YA KIISLAM ILIYOCHOMWA MOTO NA KIKUNDI CHA WA KIKRISTU WENYE HASIRA KALI HUKO BANGUI.HATA HIVYO UMOJA WA ULAYA UMEKUBALIANA LEO HII KUONGEZA JESHI LA ASKARI 1,000 ILI KULIPA NGUVU JESHI LA UFARANSA AMBALO WAPO 1600 PAMOJA NA JESHI LA MISCA FORCE LA UMOJA WA AFRIKA AMBAO WAPO 4400Horrific: Ouandja Magloire - who also calls himself 'Mad Dog' -  is seen eating the leg of a Muslim slaughtered by a rampaging Christian mob in the Central African RepublicAKIWA NA KIPANDE CHA NYAMA YA MAITI MDOMONI MWAKE Magloire said that his action was revenge for the murders of his pregnant wife, his sister-in-law and her babyHUYU NDIO KIJANA OUANDJA MAGLOIRE(MAD DOG) ALIETAFUNA SEHEMU YA MWILI WA MAITI HIYO YA KIISLAM ILIYOCHOMWA MOTO.KWA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA DAILYMAILKUPITIA RIPOTA WA BBC INADAIWA KWAMBA KIJANA HUYO ALIAFANYA HIVYO IKIWA NI KULIPA KISASI CHA KIFO CHA MKE WAKE ALIEKUWA MJAZITO,DADA YAKE PAMOJA NA MWANAEBloody: The charred and dismembered body is dragged through the streets with Magloire at the head of the mobKilled: The body is dragged through the dusty streets by the cheering crowdMAITI ZA KIISLAM ZIKIWA ZINABURUZWA MTAANI KWA SHANGWE

MWISHO WA DUNIA WATABIRIWA KUKARIBIA HIVI KARIBUNI,SOMA ZAIDI

WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, 
utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet, sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
Askofu Zakaria Kakobe.
ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu mbalimbali.
Mwadhama Polycap Kadinali Pengo.
Mbali na dunia kutikisika na matetemeko, milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani.
DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia itafunikwa na giza nene  na matope kwa wakati wote wa usiku na mchana huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah 1:14-17.
NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa).
WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya nyota.
MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu.
Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.
BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru).
Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12, wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12. Nibiru.
IMANI NYINGINE YASEMA MWISHO WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New York, Marekani umesema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu.
Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia.
Wamesema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.
WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho wa dunia na ni siri ya Muumba.
Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe.
 
FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja.
Mitandao ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba, upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao upotevuni  wakiwa wengi.
MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA
Kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au ikapita kidogo).
Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni miaka 2000 ambapo katika karne hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo halijawahi kutokea.

MAAJABU...!! KIJANA AZINDUKA KUTOKA KATIKA CHUMBA CHA MAITI(MONCHWARI)


 Wananchi wa Kenya wameshangazwa na taarifa ya mwanamume mmoja aliyezinduka akiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja mjini Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji mkuu Nairobi.

 Mwanamume huyo Paul Mburu mwenye umri wa miaka 24, alipelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai,kutokana na ugomvi wa kinyumbani na babake ingawa alisemekana kufariki Jumatano usiku wakati akipokea matibabu.

 Wafanyakazi wa hospitali hiyo walipigwa na butwaa na hata kutoroka walipoona mwili wa mtu waliyedhani ni maiti ukisonga na kuonyesha dalili za kuwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti.

 Afisa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo ya wilaya, Dokta Joseph Mburu, alisema kuwa dawa iliyotumiwa kumtibu Mburu hufanya moyo kupiga polepole hali ambayo huenda ilimfanya muuguzi kudhani kuwa mgonjwa alikua amefariki.

 Mwanamume huyo alisikika akimtaka mmoja wa wafanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti kumsaidia kwani alikuwa anahisi baridi kali na hapo ndipo mmoja wa wafanyakazi alipotimua mbio kwa hofu.

 Nusura Mburu awekwe kwenye jokovu la kuhifadhia maiti.
Jamaa za mwanamume huyo akiwemo babake walikuwa wametembelea chumba cha maiti siku ya Alhamisi ili kujiandaa kwa mazishi , lakini baadaye mchana walifahamishwa kuwa Mburu alikuwa hai.
-BBC

HUYU NDIYE MTOTO WA AJABU JIJINI DAR...HIVI NDIVYO VITU VYA KUSHANGAZA ANAVYOWEZA KUVIFANYA

AMA kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao, Andrea Marcus (13), mkazi wa Mbezi-Kibanda cha Mkaa, Dar anadaiwa kuwa wa ajabu kutokana na vitendo vyake.
Mtoto huyu amedaiwa kuwa ni wa kichawi kutokana na maajabu yafuatayo:

 

Mkazi wa Mbezi-Kibanda,  Andrea Marcus.

Ana uwezo wa kula ubwabwa sufuria moja la familia, anamudu kunywa maji ndoo moja, ana uwezo wa kuingiza tumboni mikate mikubwa saba kwa mlo mmoja,  amewahi kula mchele (si ubwabwa) ndoo nzima.

Mbaya zaidi baada ya kula milo hiyo huwa haoneshi ameshiba.
Maajabu mengine ambayo yanawashangaza watu wanaoishi naye ni jinsi anavyokula chakula kwa kumwaga chini kisha kukomba mpaka udongo.

“Sina amani ya moyo, naomba Watanzania wanisaidie, mwanangu ananiuma sana, hata kujisaidia ni hapohapo, chakula anakula kupita kiasi, kama nilivyosema hashibi na bado hali kama mwanadamu wa kawaida,” alisema mama wa mtoto huyo.

Akizungumzia madai ya uchawi, mama huyo, Angelina Marcus alisema mwaka 2001 alimzaa Andrea katika mimba ya miezi nane kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar.
“Nilipofika nyumbani tu, alikuja mwanamke mmoja, akasema amekuja kunipa hongera. Wakati anaingia alianguka, kichwa ndani miguu nje, alipoamka akaaga akisema anakwenda kuniletea kisamvu.

“Mama yangu akamwambia mzazi hali kisamvu, kama anataka akanichinjie bata. Yule mwanamke aliondoka, hakurudi tena,” alisema mama Andrea.
Aliendelea kudai kuwa, baada ya wiki tatu mtoto wake alianza tabia ya kulia usiku wa manane.
“Hiyo tabia ya kulia amekuwa nayo miaka yote, tulikwenda kwa waganga lakini wapi! Tukahamia makanisani kwa wachungaji kidogo mtoto alipata nafuu mwaka jana.

“Mwezi Novemba tarehe kumi na moja, mwaka jana (2013) yule mwanamke alikuja hapa nyumbani na kuniambia kuwa, mguu ule ni wangu.

“Alikaa chini mimi nikiwa nafua, akaanza kuniambia ‘mjukuu wangu samahani, nimeona unateseka sana na mwanao, nataka nikurudishie kwani mimi uchawi sasa basi.’
“Nilishtuka, nikamuuliza bibi unasema nini? Akajibu, ‘n imekuja kukwambia huyu si mtoto ni picha tu, mtoto wako ninaye mimi nyumbani kwangu na nina watoto wengi ila wa kwako ananisumbua, bora uje umchukue kesho asubuhi,” alisema mama Andrea.

“Siku iliyofuata nilikwenda kwake, sikumwona mtoto ila cha kushangaza aliniambia kuwa yeye anajua kuroga lakini hajui kutegua, ana mganga wake yupo Songea (Ruvuma), atampigia simu aje amtegue mtoto wangu arudi katika hali ya kawaida,” aliongeza mama Andrea.
Mama huyo alisema kuwa aliporudi nyumbani, aliwaambia wazazi wake kilichotokea na maneno yote waliyoongea na mwanamke huyo.

Wazazi wa mama Andrea walimuita mwanamke huyo akiwa na mumewe na mtoto wao mmoja, wakamuuliza kuhusu madai hayo, akaomba msamaha kwa kilichotokea.
Sakata hilo likaenda Serikali ya Mtaa Misigani ambapo mwanamke huyo alikiri mara ya kwanza na kusema kuwa amempigia simu mganga wa Songea atafika wakati wowote.

“Cha kushangaza alikaa kwa nusu saa na kusema amewapigia simu ndugu zake wamesema huyo mganga amefariki dunia. Kila mtu alimuuliza amepigaje simu mbona wamekaa naye na hajatoka nje? Akanyamza,” alisema mama Andrea.

Mama Andrea alisema serikali ya mtaa waliliona sakata hilo ni kubwa na kuamuru babu wa Andrea (jina lipo) kuchukua barua kuipeleka kwenye Kata ili kesi ihamie huko.
Mama huyo alimalizia kwa kusema kuwa anashindwa cha kuamua kwani kwa maelezo ya mwanamke huyo hajui akubali mtoto Andrea si wake au la!

DHEHEBU LA AJABU:MCHUNGAJI ASEMA KULA MAJANI NI KUMKARIBISHA MUNGU MAISHANI,HII NI ZAIDI YA HATARI

Miaka ya hivi karibuni kumekua wimbi kubwa la madhebu mabimbali ya dini ya kikristo kuibuka...Sio Mbaya sana kwani hata viwanda vya pombe, na kumbi za disco nyingi hufunguliwa...

But kwa hili ni fungua mwaka. Baada ya mchungaji  Lesego Daniel wa Rabboni Centre Ministries katika mji wa  Pretoria nchini Africa ya kusini kuwambia waumini watoke nje wale majani ili wawe karibu na Mungu. Daah hii hatari sana.
Jionee mwenye picha 10 za tukio zima.....Kuna moja anawakanyaga waumini wake.....Mchungaji anambwewe sana.





MAAJABU: SAMAKI AINA YA SATO AONYESHA MAAJABU WILAYA YA BUNDA, AINGIA TUMBONI MWA MSICHANA WA MIAKA 12 KUPITIA SEHEMU ZA SIRI, DARUBINI ZA ASILI ZATHIBITISHA KUOONEKANA TUMBONI.

 

MAISHA ya mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 12, (jina tunalihifadhi), anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Bwanza, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, yako hatarini baada ya kurukiwa na samaki aina ya sato, kuingia sehemu ya siri na kukimbilia tumbani.

Tukio hilo limetokea Januari mosi mwaka huu, saa 11 alfajiri,wakati mtoto huyo akichota maji katika Ziwa Victoria ili aweze kumwagilia bustani ya nyanya, vitunguu iliyopo kandokando
ya ziwa hilo.

Akizungumza na Majira, kaka wa mtoto huyo (jina tunalihifadi), mwenye miaka 31, alisema tukio hilo limewashangaza wakazi wa Kijiji cha Bwanza na vitongoji vyake.

Alisema mdogo wake alikuwa akichota maji katika ziwa hilo akiwa amechuchumaa ndipo samaki huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa wa nchi nne, aliruka kutoka majini, kuingia sehemu yake ya siri na kukimbilia tumboni.

"Mdogo wangu alifanya jitihada za kumvuta ili aweze kumtoa lakini alikimbilia tumboni na kuanza kupata maumivu makali,kutokwa na damu nyingi baada ya kuparazwa na miba ya
mgongo wa samaki huyo.

"Baada ya tukio hilo, alirudi nyumbani kwa shida akijivuta na kuugulia maumivu...alimweleza mama na ndugu zake juu ya mkasa huu, walimchunguza na kujaribu kuingiza mkono sehemu za siri wakidhani watampata lakini hawakufanikiwa," alisema.

Aliongeza kuwa, baada ya kumpeleka zahanati iliyopo kijijini hapo, hali yake ilizidi kuwa mbaya akilalamika maumivu makali tumboni ambapo familia inaamini tukio hili limetokana na imani za kishirikina hivyo waliamua kumtoa katika zahanati hiyo.

"Tulimpeleka kwa mganga wa kienyeji kijiji cha Amuyebe,wilayani Ukerewe...katika hali ya kawaida samaki hawezi kumrukia mtu sehemu yake ya siri na kuzama tumboni.

"Pamoja na kuchukua uamuzi wa kumpeleka kwa mtaalamu,hali yake bado inazidi kuwa mbaya, hata baba yetu alifariki katika mazingira yenye utata mwaka 2003," alisema.

Aliongeza kuwa, hata kaka zake watatu na mtoto huyo nao walifariki kwa mfululizo mwaka 2004, 2005, 2006 ambao vifo vyao viligubikwa na utata mkubwa.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Alwego anakoishi mtoto huyo, Bi. Reticia Bituro, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limewashangaza watu na kuahidi uongozi wa kitongoji hicho utaendelea kufanya uchunguzi zaidi.

Diwani wa Kata ya Napindi, Bw. Elias Magoti ambaye yuko safari kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Bunda Mjini,alikiri kupokea taarifa za tukio hilo kwa mshangao mkubwa.

"Nitalifuatilia kwa karibu baada ya kurudi kijijini kwa kufanya uchunguzi ili kubaini kilichotokea kwani sijawahi kusikia tukio kama hili katika umri nilionao," alisema.

Taarifa zilizopatikana kutoka Ukerewe anakotibiwa mtoto huyo, zilisema kwa sasa hawezi kuzungumza akizidi kulalamika maumivu makali ya tumbo na samaki huyo bado hajatolewa.

- MAJIRA.

KWELI DUNIA INAZUNGUKA...!! TAZAMA KALENDA YA MWAKA 2014 ILIVYOKUWA SAWA KABISA NA YA MWAKA 1947..

Dunia inazunguka na sasa tumerudi miaka ya 1900 

Hii hapa chini ni kalenda ya ya mwaka 2014 unaoanza masaa machache yajayo
 

Na hii kalenda hapa chini ni ya mwaka 1947 
 Hakuna utofauti baina ya hizi kalenda hapo juu...

PICHA:JIONEE MWANAMKE MWENYE SHAPE YA KIPEKEE ZAIDI DUNIANI,NOMA SANA

CHEKI MAMBO HAYO!!! …HUYU NI MWANAMKE MWINGINE ANAYEJUMUIKA KWENYE LIST YA WATU WACHACHE WENYE MAUMBILE ADIMU DUNIANI

ANAITWA Sarah Massey mama wa watoto wawili mkazi wa Chicago nchini Marekani, amejitokeza kama mwanamke mwenye umbo kubwa zaidi sehemu ya makalio.
Record-breaking rear: Sarah Massey shows off her seven foot wide posterior while cooking at home
Sarah ambaye amewahi kuvunja choo mara tu baada ya kukikalia, ana mzunguko wa futi 7 ambapo mara kadhaa amekuwa akipata shida kupita mlangoni.

Hata hivyo mwanamama huyu mwenye umri wa miaka 33 anasema  anajivunia kuwa mmoja wa wanawake wenye ‘figa’ la kufa mtu hapa ulimwenguni.
Problems: But the mother-of-two admits she suffers from limited mobility caused by her vast posterior 
Older: Sarah says her bottom attracts men years older than her, including Albert (left), the father of her sons
Tight fit: Along with doors, Sarah confesses to having problems doing up her seat belt because of her rear

RECORD...HUYU NDIYE DADA ANAYETOKA MACHOZI NA JASHO LA DAMU.ANGALIA PICHA NA STORY YAKE




Miaka minne iliyopita msichana huyu mwenye umri wa miaka 19, Delfina Cedeno, alianza kupata tatizo hili la ajabu, lililokuwa likimfanya alie na kutoka jasho la damu. Kwa kuongeza zaidi, wakati mwengine damu zimekuwa zikitoka hata kwenye kucha na kitovu.







Hali hii ilipomuanza, alianza kwa kulia machozi mekundu, kutokwa na damu puani na kunyunyukwa nywele kichwani.

Hali ilipokuwa mbaya, alikuwa akienda hedhi kwa siku 15 mpaka ikafika kipindi alihitaji kuongezwa damu kutokana na hali hiyo iliyokuwa ngumu. Licha ya vipmo vingi alivyofanya, madaktari wa mji wake wa Veron, kwenye Jamhuri ya Dominica, walishindwa  kumsaidia.

Cedeno alisema: 'Hali hii ilipoanza kwangu sikuwa najua nini cha kufikiri - nilishtushwa na kuogopa.

Anasema alijisikia vibaya kutokana na hali aliyokuwa nayo mpaka ikambidi aondoke nyumbani kwao alipokuwa akiishi na mama yake aitwaye Mariana, 36.

Aliacha shule huku marafiki zake wengi wakimtenga kutokana na hali hiyo wakihofu kupata maambukizo au usumbufu kutokana na hali yake.

'Nilitengwa, ila Mungu mkubwa. Kwa sasa najisikia poa maana baada ya muda mrefu nimeanza kujisikia vizuri.'

Miezi michache baadae alifanikiwa kupata boyfriend, Recaris Avila, ambaye alimtembelea hospitali mara baada ya kusikia stori yake.





Sasa, miaka minne baada yote kuanza, madaktari wa wamefanikiwa kutatua tatizo lake.


VIDEO:MAITI NYINGINE YAGOMA KUZIKWA NCHINI KENYA,NDUGU WAFANYA MATAMBIKO KUMSIHI MAREHEMU AKUBALI KUZIKWA


 
Hii  ni  maiti  nyingine  iliyozua  kizaa zaa  nchini  Kenya  baada  ya  kugoma  kuzikwa.....

Zaidi  ya  magari  10  yalishindwa  kuisafirisha  maiti  hii  na  ndipo  ndugu  wa  marehemu  akiwemo  dada  yake   Kitinda  walipompigia  magoti  marehemu  wakimuomba  afungue  njia  ili  akapumzike  kwa  amani.....

Tazama  video  hapo  chini...

MAAJABU:MBUZI AZAA MTOTO ANAYEFANANA NA BINADAMU HUKO KENYA,ANGALIA VIDEO

Wakazi wa eneo la Likoni, Mombasa nchini Kenya walipatwa na mshangao mkubwa mara baada ya mbuzi mmoja kujifungua mtoto mwenye sura inayofanana na binadamu.

Tukio hilo lilifanya shughuli mbalimbali kwenye kijiji hicho kusimama huku wakazi wa eneo hilo wakiwa wanastaajabu juu ya tukio hilo la ajabu.
 
Tazama video ya tukio hilo hapo chini....

MAAJABU:MTANZANIA AFAIKI DUNIA NA KUZIKWA ,BAADA YA KUZIKWA AKUTWA WODINI...SOMA MKASA HUU ULIOTOKEA MUHIMBILI

 
Mtanzania Yahya Msemakweli, 34, (pichani) alifariki dunia, akawekwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari), ndani ya jokofu kwa siku tano na ndugu zake akiwemo mkewe, waliushuhudia mwili wake na kujiridhisha kuwa ni yeye.
Hata hivyo, siku ya sita ambayo ndiyo ilikuwa tarehe ya mazishi, walipoufuata mwili wa Yahya hawakuukuta mochwari, droo aliyowekwa, ilikutwa maiti ya kike, majokofu yote yakafunguliwa lakini hawakuuona.

Siku iliyofuata, yaani siku ya saba, Yahya akakutwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Alitokaje mochwari Temeke hadi Muhimbili wodini? Hakuna anayejua!

Nyongeza ni kwamba kaburi lilishachimbwa, sanda ilishanunuliwa tayari kwa mazishi ya Yahya lakini mambo yalipogeuka, ilibidi wazike mgomba kwa kile kilichoelezwa: “Kimila kaburi huwa halifukiwi tupu.”
MKE WA YAHYA ANASIMULIA
Mke wa Yahya, Mwanjaa Juma, alisema: “Mimi na mume wangu tunaishi Mtoni Madafu, Temeke. Mume wangu ni dereva wa bodaboda.”

Mwanjaa aliendelea kusimulia kuwa Novemba 22, mwaka huu, saa 5:15 usiku, alipigiwa simu na Yahya akamwambia yupo njiani anarudi nyumbani.
“Wakati huo aliniambia yupo Kilwa Mivinjeni. Mpaka saa 6:00 usiku alikuwa hajarudi, nikampigia simu ikawa haipatikani.
“Niliingiwa na wasiwasi sana, kulipopambazuka tu nilikwenda Mtoni Kwa Azizi Ally ambako ndiyo kituo chake cha kupaki bodaboda. Niliwauliza wenzake, wakanijibu kuwa tangu apeleke abiria jana yake saa 4 usiku, hakurudi tena,” alisema na kuongeza:

“Nilirudi nyumbani na kuanza kuwapigia simu baadhi ya ndugu na jamaa lakini sikupata jibu la mahali mume wangu alipo. Baada ya siku mbili nilikwenda Kituo cha Polisi Mtongani, nikakuta pikipiki yake ikiwa imeharibika vibaya kutokana na ajali.
“Nilipowauliza polisi walisema mwenye pikipiki hawamjui na alipelekwa pale usiku wa siku mbili zilizopita na msamaria mwema akiwa hajitambui, ikabidi wamkimbize Hospitali ya Temeke kwa matibabu.

“Tulipofika Hospitali ya Temeke mapokezi jina lake halikuwepo katika kitabu cha orodha ya wagonjwa waliopokelewa, tulikwenda ICU nako hatukumuona.
“Kesho yake asubuhi, tulilazimika kwenda mochwari ya Hospitali ya Temeke, tukakuta mwili wake kwenye jokofu na kujiridhisha ni wenyewe. Wahudumu wakakiri kwamba ule mwili una siku tatu pale.

“Hatukuwa na cha kufanya zaidi ya kupanga taratibu za mazishi. Tuliwataarifu ndugu, tukapanga tarehe ya mazishi iwe Novemba 27, kaburi likachimbwa.
“Siku ya mazishi, watu walikwenda na gari kufuata mwili hospitali lakini hawakuukuta kwenye jokofu alilokuwa amehifadhiwa.
“Walipokwenda kuulizia kwa uongozi wa hospitali, wakasema kwanza waende kituo cha polisi wapate askari wa usalama barabarani, wakapime ajali ndipo watapewa mwili.

“Ikabidi waende Kituo cha Polisi Mtongani, wakaambiwa waende Kituo Kikuu cha Mkoa wa Polisi, Temeke, Chang’ombe, pale alipatikana askari wa usalama barabarani, wakaongozana hadi eneo la ajali na kupima na kuchora ajali ilivyokuwa.
“Baada ya mchoro, polisi walitoa kibali cha mazishi. Ndugu walikwenda na kibali kwa uongozi wa hospitali wakaomba wapewe mwili lakini danadana zikaendelea, maana haukuonekana mochwari.

“Wakiwa na sanda mkononi, waliuliza maiti ilipokwenda lakini hawakujibiwa, hakuna aliyekuwa na maelezo ya kueleweka.
“Ulifanyika msako pale mochwari lakini hakuna kilichopatikana.

“Ikabidi ndugu warudi Kituo cha Polisi Mtongani, wakapewa askari hadi Hospitali ya Temeke. Yule askari alipouliza ndiyo wahudumu pale hospitali wakasema kuna mgonjwa mahututi alihamishiwa Muhimbili pale Moi (Kitengo cha Mifupa na Mishipa ya Fahamu).
“Kweli walikwenda Moi, walimkuta mume wangu akiwa ICU anaendelea na matibabu.”

NINI KILIFANYIKA
Mwanjaa alisema, baada ya kumkuta Yahya yupo ICU, hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kurudi nyumbani na kuwataarifu kila kitu ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya mazishi.
“Hakuna aliyeamini haraka, wengine walikwenda mpaka Moi kuhakikisha, waliobaki waliamua kuzika mgomba kwa sababu kimila kaburi halifukiwi bila kitu.

“Japo tulitumia fedha nyingi kwa ajili ya maandalizi ya mazishi, tuliandaa chakula kingi lakini kimedoda, ila yote kwa yote namshukuru Mungu mume wangu bado mzima.
“Namuomba Mungu amponye mume wangu haraka, arudi nyumbani tuendelee na maisha yetu. Hivi sasa kila mara nipo Moi kwa ajili kuhakikisha anapata huduma kwa ukaribu na anapona haraka,” alisema Mwanjaa.


DADA MTU AZIMIA MARA SABA
Zafarani Msemakweli ambaye ni dada wa Yahya, alizimia mara sita mara ya kwanza alipopewa taarifa ya msiba.
Habari ambazo zimethibitishwa na Zafarani mwenyewe, zinasema kuwa baada ya kupewa taarifa kaka yake yupo hai ICU Moi, alizimia tena, hivyo kufikisha mara saba.

Zafarani alisema: “Nilipopokea taarifa kwamba kaka yangu amekufa niliishiwa nguvu, unajua yule ni tegemeo la familia yetu. Ndugu zangu wanasema nilizimia mara sita.
“Nilipoambiwa ni mzima kwa mshtuko nilizimia tena. Ni maajabu, mtu amehifadhiwa mochwari na madaktari wamethibitisha amekufa baadaye tunaambiwa yupo hai, inashangaza sana.”

UWAZI LAMSHUHUDIA YAHYA ICU
Mwandishi wetu alikwenda Moi kumwangalia Yahya na kujiridhisha kweli yupo hai anaendelea na matibabu.
Jitihada zinaendelea za kumtafuta mganga mkuu wa Hospitali ya Temeke, aseme nini kilitokea kwenye hospitali yake mpaka Yahya akawekwa mochwari na kuwekwa ndani ya jokofu kwa siku tano kisha kupelekwa Moi akiwa mgonjwa mahututi.

Awali mwandishi wetu alikwenda hospitalini hapo na kuomba kuzungumza na mganga mkuu lakini alikosa fursa na kila akipiga simu yake haipatikani.

-Gpl

NOUMA SANA!!! MBABA AOTA MANYONYO BAADA YA KUIBA MIFUGO...CHEKI HAPA

A 40-year-old man from Nherera in Mhondoro, Zimbabwe suddenly grew breasts after he allegedly stole and sold some cattle.
The Villagers believe the man identified as Acry Chinhivi Shayamano has been punished by the cattle owner.
50-year-old Hamilton Magaisa said, “We all know that Acry grew boóbs because of his thieving. People who steal are punished in so many ways. I have no sympathy for him.”
Shayamano did admit that he was a thief but denied ever stealing cattle. “Who told you that I have grown boóbs. Mine are not that bad. I never stole anyone’s cattle. Acry said his boóbs were not painful but were still growing.
“I steal but not cattle. I stole some DVDs and I was arrested and ordered to pay a fine,” he said.
He said his grandmother lost two cows in February and that was the time he noticed his boóbs growing. He said people just made a connection, which was not the case.
Acry said his boóbs were not painful but were still growing. He said the boóbs could be a side effect of the ARVs he was taking. He has been taking them for the past three years.

MAAJABU:HIKI NDO KIATU CHENYE AC NDANI!!!

7 Hydro-Tech ambayo ni kampuni ya Japan ndio imetengeneza hiki kiatu ambacho bei yake ni dola za Kimarekani 75 ambazo ni kama laki moja na 20 za kibongo. As MobileMag explains, the way these shoes work is a bit different from our conventional understanding of “air conditioning”: The shoes don’t have a mini air conditioner integrated inside, but rather rely on a new filter technology that releases heat and humidity and allows air to flow, for your feet to feel refreshed and clean 4 1

MTOTO ANAYEDAIWA KUFUFUKA ANENA KWA MARA YA KWANZA

  Ni hivi karibuni, Mji wa Geita na maeneo jirani ulikubwa na taharuki ya aina yake,pale mtoto Shabani Maulid (15) anaedaiwa kwamba alifariki dunia miaka miaka mitatu iliyopita, alipoonekana akiwa hai katika Kijiji cha 14 Kambarage, Mtaa wa Mbugani.
 
Tukio hilo lilizua hofu kwa wakazi wa Mji wa Geita huku waliowengi wakitaka kujua mtoto huyo aliyekutwa amefariki dunia baada ya kupotea kwa siku nne mwaka 2011 na mwili wake kuzikwa, inakuwaje leo hii anaonekana akiwa hai?
 
Tukio hilo lililotokea Septemba mwaka huu linashuhudiwa na wazazi wa Shaban, ndugu zake, jamaa na hata majirani wa eneo hilo ambao pia wanahoji, je aliyezikwa wakati mwili wa mtoto huyo ulipookotwa ni nani na je mwili wake uko kaburini au la?
 
Maswali haya na mengine, yalikosa majibu kwani baada ya kuonekana kwake, Shaban hakuweza kuongea vizuri na alionekana kutofahamu kabisa Kiswahili, lugha ambayo kabla ya kutoweka kwake aliifahamu vyema. Wakati huu mtoto huyu anaongea Kiha, japo nayo kwa tabu.
 
Hali hiyo iliwalazimisha wazazi wake kushirikiana na Jeshi la Polisi kumpeleka Haospitali ya Wilaya ya Geita ili apatiwe matibabu, lakini ni kama hawakuona mtoto wao akipata nafuu hivyo waliondoka naye na kuamua kumpeleka Kigoma Kambako anapatiwa tiba za jadi.
 
“Niliamua nimpeleke kwa waganga wa jadi huku nyumbani Kigoma na sasa hali inaendelea vizuri kwani anaweza kuongea japo ni kwa muda mfupi kisha hunyamaza”, alisema baba mzazi wa mtoto huyo, Maulidi.
 
Shaban alikuwa wapi?
Shaban hivi sasa anaendelea vizuri na ‘tiba’ anayopata huko Kigoma na aliweza kuzungumza na gazeti hili kwa simu, huku akieleza kutoweka kwake, pia huko alikokuwa kwa miaka mitatu, huku akiweka bayana kwamba hivi sasa anawatambua vizuri
 
wazazi na ndugu zake.
Alisema anakumbuka Januari 1, 2011 aliondoka nyumbani kwao na kuelekea malishoni kuchunga mbuzi, na wakati akiwa machungani ghafla lilitokea kundi la watu ambalo lilimzunguka.
 
Shabani anasema katika kundi hilo alikuwamo mwanamke ambaye hakumtaja kwa maelezo kwamba anashindwa kutamka jina lake, ambaye alimshika mkono na kumtaka waondoke eneo hilo.
 
“Walikuja watu wengi wanaume kwa wanawake, ghaflla walinizunguka na nikasikia kama kizunguzungu na akili yangu ikawa kama imezubaa,”alisema Shaban na kuongeza kuwa baada ya watu hao kumzingira walimwamuru aswage mbuzi zake na kuwarudisha nyumbani.

“Niliongozana na watu hao tukiswaga mbuzi hadi nyumbani, lakini wakati nafika hapo nyumbani hawakuweza kuniona japo mimi nilikuwa naona kila jambo lilikuwa likiendelea,”anasimulia Shaban na kuongeza:
 
“Hao watu walionizingira walijibadili sura na kuonekana kama majirani zetu na mimi pia nilikuwa katikati ya kundi holo ila wazazi hawakuweza kunitambua.
 
Alisema kuwa baada ya kukabidhi mbuzi hao, watu hao waliondoka na yeye alibaki pale nyumbani akiwa na mwanamke aliyemshika mkono, lakini wakati huo hakuwa akionekana wazi wala kutambuliwa.
 
“Tulikaa pale nyumbani kwa nusu saa tangu tulipofikisha mbuzi na baadaye tuliondoka na huyo mwananke ambaye alikuwa amenishika mkono, na tukarudi nilikokuwa nachungia na hapo tuliwakuta wale watu wengine wakiwa wamesimama karibu na dimbwi la maji,”alisema Shaban.
 
Alisema baada ya kufika katika dimbwi hilo walisimama katikati ya maji na baadaye alishtukia akiwa chini ya bahari, ambako kulikuwa na senta (kituo) kubwa na watu wengi wakiwa wanafanya shughuli mbalimbali.
 
“Tulisimama katikati ya dimbwi la maji, gafla nilistukia niko katikati ya senta kubwa ambayo iko ndani ya maji kama ziwa,”alisimulia mtoto huyo na kuogeza kuwa eneo hilo kubwa kama mji ama kijiji ambako watu wanaishi. Hata hivyo kila alipotaka kutaja watu hao alishindwa kutamka.
 
“Kunawatu wengi kwenye eneo hilo na mimi nilistukia tu nikiwa huko na watu wenyewe sikuwajua kwani walikuwa wageni kwangu,”alisema Shaban.
 
Hata hivyo alipohojiwa wakati akiwa huko alikuwa akifanya nini, akila nini na watu wanaoishi huko wanafanya shughuli gani, alishindwa kuongea na kumkabidhi baba yake simu.
 
Kwa upande wa baba yake huyo anasema tangu alipompeleka mwanaye Shaban kwa mganga wa jadi aliyemtaja kwa jina la Seleman Bundala, aliyeko Kijiji cha Nyankintonto, Kigoma amekuwa akipata nafuu.
 
Alisema toka waanze matibabu ya jadi kumekuwa na mabadiliko makubwa kwani,mtoto huyo alikuwa haongei, lakini kwa sasa anaongea japo kwa shida na kwamba anaeleza alikokuwa na jinsi alivyopelekwa.
 
“Hatoi maelezo mazuri kwani kunawakati anaongea vizuri na wakati anaonekana kama ulimi unakuwa mzito hasa tunapomuuliza maswali kwamba ilikuwaje akatoka huko na alikuwa akifanya nini na watu waliomchukuwa ni akina nani,”alisema Maulidi.

Alitowekaje?
Maulidi alitoweka ghafla Januari 1, 2011. Wazazi wake wanasema siku hiyo aliondoka nyumbani asubuhi na kupeleka mbuzi malishoni, na kwamba siku hiyo hakurudi, jambo lililowatia mashaka wazazi wake hivyo kuamua kutoa taarifa polisi na kwa uongozi wa kijiji.
 
Taarifa za kupotea mtoto huyo zilienea kijijini hapo na ndipo walianza juhudi za kumtafuta na baada ya siku nne, alikutwa amekufa ndani ya kisima cha maji.
 
“Mtoto wetu aliondoka kwenda kulisha mbuzi siku ya sikukuu ya mwaka mpya muda wa saa nne asubuhi, hadi inafika saa 12 jioni hakuonekana na badala yake tuliona mbuzi wakiletwa na watoto wa majirani,”alisema Aziza Ramadhani mama mzazi wa Maulidi.
 
Aziza ndiye alikuwa wa kwanza kumtambua mtoto wake katika Mtaa wa Mbugani eneo la Majarubani na wakati huo alikuwa akitoka kwenye shughuli zake za kibiashara. Anasema alimwona Shaban akikatiza barabara.
 
“Nilimuona mwanangu akiwa anakatiza njiani ndipo nilimuita, Shabani mwanangu ni wewe? Niliposema hivyo alishtuka, nikaamua kumsogelea huku nikimwita jina lake ndipo alipoitika lakini hakunitizama usoni,” alisema mama huyo na kuongeza:
 
“Baada ya kuthibitisha kwamba ndiye, watu walijaa na ndipo kwa kushirikiana na majirani tulitoa taarifa polisi, na polisi wakaja kumchukua na kumpeleka hospitali huku akiwa haongei na tulitumia ishara kuwasiliana naye”.

-Mwananchi
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari