Like Us On Facebook
Showing posts with label Wasanii wengine. Show all posts
Showing posts with label Wasanii wengine. Show all posts

MSANII RECHO AKIWA KATIKA POZI LA NUSU UCHI



MSANII wa filamu za kibongo, Rachel Haule ‘Recho’ hivi karibuni aligeuka kituko baada ya kutupia picha ya nusu utupu katika mtandao wa kijamii.

Picha hiyo ambayo Recho amevaa shati tupu (inayoonesha ndani) bila kuvaa kitu kingine chochote, aliitupia kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo mashabiki na marafiki zake walichangia huku wakimlaumu kuwa hakufanya vizuri kuiweka picha hiyo ya aibu mtandaoni.

Mwandishi  wetu alimuuliza Recho kulikoni? Akajibu hivi:
“Nawapenda sana marafiki zangu lakini mimi sijaona tatizo la hii picha kwa sababu ni ya kawaida sana sioni ubaya wake.”

FEZA KESSY AVAMIWA NA MAJAMBAZI WENYE SILAHA NZITO.....MWENYEWE AFUNGUKA NA KUONGEA KWA MASIKITIKO..!!


            Feza Kessy mshiriki wa Big brother the Chase amepatwa na matatizo ya kuvamiwa na majambazi wenye silaha siku mbili zilizopita. Feza Kessy amesema kwamba tangu avamiwe na majambazi hao hajisikii kuwa na amani kabisa. Feza Kessy anaendelea kuwashangaa hao majambazi kwamba silaha walizobeba zilikuwa za nini?, au walidhani kwamba anapesa wakati hakushinda Big brother na alikuwa hana kazi kwa muda miezi mitatu iliyopita. Pole sana Feza Kessy na hizi ni tweet zake akielezea tukio hilo

JOHARI AAMUA KUJIFUNGIA NDANI BAADA YA FUMANIZI ILI KUKWEPA AIBU



               Muigizaji maarufu Blandina Chagula(Johari) anadaiwa kuishi kwa kujificha ficha baada ya hivi karibuni kumshushia makonde muigizaji mwenzake Chuchu Hans ambapo kisa kilidaiwa ni kugombea penzi la Vicent Kigosi(Ray). 

Inadaiwa Johari hataki hata kukutana na watu wake wa karibu wakiwemo wasanii wenzake. 

Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kilisema  kuwa  kwa sasa Johari hataki kabisa kuonana na watu wake wa karibu, hata mtaani amekuwa haonekani mara kwa mara, anawakwepa hata wasanii wenzake, hii ni kutokana na lile sakata lake na Chuchu...

Nae Johari alipoulizwa na mtandao huo juu ya sababu ya kujifungia ndani alisema: "Niko nyumbani, sitaki kutembea sana kwani niko na likizo fupi, halafu hata hili sakata langu na Chuchu bado halijapoa"

AISHA MADINDA ASIMULIA JINSI "UNGA" ULIVYOMFILISI NA KUUZA NYUMBA ZAKE NA GARI, ASEMA LIWE NI FUNDISHO KWA WENGINE!

 
         WIMBI la uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya limeshika kasi hivi sasa kwa wasanii na watu mbalimbali huku Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe akilivalia njuga kulikomesha
Wakati hayo yakiendelea, mnenguaji aliyetikisa anga la muziki wa dansi nchini, Aisha Mohammed Mbegu ‘Aisha Madinda’ amejuta kutokana na kufilisika baada ya kutumia madawa ya kulevya, Ijumaa linakupasha kwa kina.
Akizungumza katika mahojiano maalum hivi karibuni, Aisha alisema alipokuwa juu kwa unenguaji alifanikiwa kumiliki mali mbalimbali zikiwemo nyumba tatu pamoja na gari lakini madawa yamemlostisha.
Akisimulia jinsi nyumba zake tatu zilivyopotea, Aisha alisema alianza kuweka rehani ‘bondi’ nyumba yake ya Kigamboni akiwa anachukua fedha kidogokidogo hadi alipoambiwa fedha zake zimekwisha.
“Baada ya kuiweka bondi nyumba ya Kigamboni na kuambiwa sina changu nikaenda kuuza nyumba ya Kimara mwisho,” alisema.
Baada ya kumaliza nyumba zake, mnenguaji huyo akadai kuwa aligeukia gari lake aina ya Toyota Mark II ambalo nalo aliliuza.
“Niliona ujinga nilikuwa nikipata tabu ya kutafuta fedha za kununulia unga wakati gari nilikuwa nalo, nikaisukumia mbali,” aliongeza huku akisikitika kwa uamuzi huo ambao sasa anaujutia.
Aidha, Aisha alisema hivi sasa anawachukia wanaouza madawa ya kulevya kwa kuwa wanatajirika wakati wao kama watumiaji wanafilisika kifedha na kuumia kiafya.
“Sisi wanunuzi tunakuwa na maisha magumu wakati wenzetu wanatajirika, binafsi sikuwahi kutegemea kama ningeishi maisha kama haya, nawashauri mastaa wengine wanaondelea kutumia madawa hayo waache mara moja kwani madhara yake ni makubwa kiuchumi na kiafya,” alimalizia mnenguaji huyo ambaye hivi sasa yuko fiti na anaweza kupanda jukwaani wakati wowote.

IZZO BIZNESS APATA AJALI MBAYA AKIELEKEA AIRPORT MWANZA...

 
Haya ni Maneno ya Izzo
Tumepata Ajali Mbaya Eneo la MSITUNI wakati tunatokea GEITA kwenye Show kuelekea Airport MWANZA...Tunamshukuru Mungu Tupo salama...Pole kwa brother Philbert KABAGO kwa kuumia maeneo ya Pembeni ya Jicho lake...Get well soon bro...Mungu ni Mwema

 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari