Like Us On Facebook
Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

MWANDISHI WA HABARI WA MWANANCHI AMEJERUHIWA NA KUNDI LA WANANCHI LINALODAIWA KUWA NI WANACHAMA WA CHAMA FULANI CHA SIASA.!

Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd mkoani Mara, Christopher Maregesi amejeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Bunda, baada ya kundi la watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa moja ya vyama vya siasa wakiwa na viongozi wao kumteka ambapo walimmpiga, kumtesa na kumjeruhi huku wakimpora vitendea kazi vyake ikiwamo kamera.
 

 Habari zinasema Maregesi alikutwa na mkasa huo wilayani Bunda juzi saa 12:30 jioni, wakati akipiga picha tukio la vijana wa chama hicho kumteka na kumpiga kijana anayedaiwa kuwa kada wa Chadema.

 Akisimulia mkasa huo akiwa katika wodi ya wanaume Hospitali ya Bunda, Maregesi anadai kuwa alikabwa na viongozi wa chama hicho wakati akipiga picha za tukio la kada huyo wa Chadema aliyeshushwa kutoka ndani ya gari na kuanza kushambuliwa na vijana waliokuwa pamoja na viongozi hao.

 Anafafanua wakati akiendelea kupiga picha tukio hilo, ghafla Mwenyekiti wa chama hicho wa mkoa alimkaba kwa madai kuwa atawaumbua na kusaidiana na kiongozi mwenzake ambaye alichukua kamera na ghafla kundi la vijana wa chama hicho wakamvamia,kuanza kumpiga na kumpora mkoba aliokuwa nao, kisha wakamfungia ndani ya chumba
cha ofisi yao.

 "Ndani ya chumba nikaingizwa mimi na huyo kijana anayedaiwa kada wa Chadema na kuanza kutupiga, ndipo mtu mmoja akasema mtawaua hawa iteni polisi baadaye askari wa JKT walioletwa maalumu wilayani Bunda kulinda Kata ya Nyansura ndiyo waliotufikisha Kituo cha Polisi Bunda," alibainisha Maregesi.

 Anataja vitu alivyoporwa kuwa ni kamera aina ya Sony digital, risti zake, daftari la kuandikia habari (Note Book), Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, simu ya mkononi aina ya Adio pamoja na vitu vingine mbalimbali.

 Akizungumzia hali ya Maregesi mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Bunda, Dk Nimrod Mzuma alisema mwandishi huyo anakabiliwa na maumivu makali katika uti wa mgongo, kichwani na mkono wa kulia na kwamba alifikiswa hospitali hapo akiwa na watu wengine wawili waliojeruhiwa katika tukio hilo pia.

 Akizungumzia tukio hilo, Emanueli Imanani Katibu wa Chadema wilaya anavitaka vyama vya
siasa kuheshimu taaluma ya uandishi wa habari.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Fernandi Mtui,alikanusha kuumizwa kwa Maregesi na kueleza kuwa ameonana na mwandishi huyo kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi akiwa hana majeraha yoyote.

 Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mara (MRPC) Emanuel Bwimbo,alilaani tukio hilo akisema linavunja haki ya upatikanaji habari na kwamba limefanywa na viongozi waliopaswa kuwa mfano wa kuigwa.

 "Tunaomba wamuombe radhi Maregesi na waandishi wote, pia wamrudishie vifaa vyake haraka ili aendelee na majukumu yake. Wasipotekeleza hayo chama kitachukua hatua ikiwa pamoja na kumsaidia kuendesha kesi mahakamani ili kupata haki yake,"alisema Bwimbo.
source: mwananchi.

MWANASIASA MMOJA ASHITAKIWA KWA KUMFANANISHA RAIS NA KIAZI

frank 
Mwanasiasa wa Zambia bwana Frank Bwalya ameshtakiwa kwa kosa la kumfananisha rais wa nchi hiyo na kiazi.
Kutokana na mashtaka aliyofunguliwa akikutwa na hatia anaweza kufungwa jela kwa muda wa miaka mitano.
Siku ya Jumatatu akiwa kwenye radio mwanasiasa huyo wa upinzani alimtaja rais wa Zambia kama “chumbu mushololwa” ambapo alikuwa akimfananisha na kiazi.
Mwanasiasa huyo ambaye anatoka National Restoration Party (NRP) ameshafunguliwa mashataka na kesi itaanza kusikilizwa.
Mwaka 2005 kwenye nchi hiyohiyo ya Zambia mwanaume mmoja alifungwa jela miezi 9 kwa kumuabisha kwenye bar rais wa kipindi hicho Levy Mwanawasa.
Mwaka 2002 mhariri wa gazeti moja alikamatwa kwa kumuita Mr Mwanawasa “cabbage” na baadae mashtaka yalifutwa.

HAYA NI MANENO YA TUNDU LISSU BAADA YA ZITTO KABWE KUSHINDA KESI ZIDI YA CHADEMA

 Tundulisu aklizungumza na waandishi nje ya mahakama

Jana Januari 7 2014 ni siku ambayo Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam ilitoa uamuzi juu ya Kesi iliyokuwa ikiwahusu Mbunge wa Kigoma Kaskazini  Zitto Kabwe na Chadema ambapo baada ya uamuzi kutangazwa, paparazi wetu aliongea na wakili wa Chadema Tundu Lissu juu ya uamuzi huo wa Mahakama.

Tundu Lissu ameanza kwa kuongea >> 

‘Walau leo Mahakama imethibitisha kwamba ni mbunge wao kwa hiyo bunge la Tanzania lina wabunge watatu sasa hivi ambao ni wabunge wa Mahakama,  Hamad Rashidi Mohamed, David Kafulila na Mheshimiwa Zitto Kabwe’


‘Mahakama kuu ilichosema ni kwamba Zitto Kabwe asijadiliwe uanachama wake mpaka kesi itakapoisha, tunasubiri aje athibitishe mashtaka yake Mahakamani amri ya kuzuizi ni ya kumlindia Ubunge tu na uenyekiti wake wa P.A.C kama alivyosema Jaji’


‘Ni hivi Zitto Kabwe ni mbunge wa Mahakama na ubunge wa Mahakama una mwisho wake, kama mbunge wa Mahakama  atapokea posho, atapokea mishahara ataenda safari za PAC kwa hiyo ana haki zote kama mbunge, Kwenye vikao kama ni  mwanachama kwenye tawi lake atashiriki lakini kwenye vikao vingine vya chama kama sio mjumbe hatoweza kushiriki’


‘Kambi rasmi ya Upinzani ina taratibu zake vile vile na moja ya taratibu ni kwamba kama mjumbe wa kambi haendani na matakwa ya kambi, moja ya adhabu ni kuzuiliwa kuingia kwenye vikao vya  kambi na tutavuka huo mto tukiufikia’


‘Zitto Kabwe anaweza kuzungumzia masuala ya chama mahali popote amri ya Mahakama inasema kuwa kamati kuu au chombo kingine cha chama kisizungumzie wala kuamua uanachama wake tu, haijamziba mdomo kuzungumza masuala ya chama kama ambavyo mimi naweza kuzungumzia mambo ya chama’


‘Suala ambalo tumelisema ni muhimu ni kwa wanachama wetu tu wahakikishe kwamba hawampi nafasi lakini kama atataka kuandaa mikutano kwa jina lake ye mwenyewe kama ambavyo amekua anafanya si umeona kwenye mikutano yake hana bendera ya chama, ile anaweza kuendelea kwa sababu kwa mujibu wa Mahakama Zitto Zuberi Kabwe bado mwanachama wa Chadema’


‘Hati ya kiapo sisi tulishindwa kuwasilisha, tumewasilisha hati ya kiapo iliyosainiwa na wakili Kibatala na kama tulivyosema Mahakamani, Mahakama ya rufaa ilishasema kwamba wakili ana uwezo wa kula kiapo kwa niaba ya mteja wake kulingana na mazingira ya kesi’


‘Tulimwambia Jaji kwamba kesi siku ya kwanza iliisha saa12 na nusu jioni tukaambiwa tuwasilishe hati ya kiapo kesho yake saa 2 na nusu asubuhi sasa kwa mazingira hayo wakili kama ambavyo Mahakama ya rufani ilivyosema wakili anaweza kula kiapo lakini sisi tunavyoamini kiapo kile kilikua sahihi kabisa katika mazingira ya kesi hii, kwa kusema tulikurupuka wakati tuliambiwa tupeleke kiapo saa 2 na nusu kesho yake asubuhi kwa kweli sio sawa sawa’


‘Tulishindwa kuwasilisha hati ya kiapo ya Dokta Slaa kwa sababu hakuwepo kwa sababu usiku tumetoka hapa tumeambiwa tupeleke kiapo saa 2 asubuhi, huo muda wa kumtafuta dokta Slaa ulikuwa wapi’

HATARI:ANGALIA PICHA ZAIDI YA 10 ZA MWENYEKITI WA CHADEMA TEMEKE ALIYEPIGWA NA KUTUPWA USIKU WA LEO.

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam.

Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.
‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja.. tulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’


















Mamluki na Wafuasi wa Zitto kabwe wachapana Makonde Nje ya Mahakama

Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wanaounga mkono uongozi wa juu, jana walitwangana tena muda mfupi baada ya kuondoka eneo la Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Tukio hilo limetokea huku Mahakama hiyo ikiahirisha hadi leo, kutoa uamuzi wa maombi ya Zitto kuzuia kujadiliwa na Kamati Kuu ya Chadema.
Katika maombi hayo namba 1 ya mwaka 2014, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, anaiomba Mahakama iizuie Kamati Kuu ya Chadema kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake hadi kesi yake ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Uamuzi wa maombi hayo ulipangwa kutolewa jana na Jaji John Utamwa ambaye hata hivyo, alisema alikuwa hajamaliza kuandika uamuzi huo na kuahirisha shauri hilo hadi leo mchana.
Maombi hayo ya Zitto ya zuio la muda la kujadiliwa na kuchukuliwa uamuzi wowote kuhusu uanachama wake yametokana na kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Katika kesi hiyo, Zitto pia anaiomba Mahakama Kuu imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie mwenendo na taarifa za kikao cha Kamati Kuu za kumvua nyadhifa zake zote alizokuwa nazo ndani ya chama na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake ya ubunge wa Kigoma Kaskazini.
Mapigano
Baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, wanachama wa makundi yote waliondoka eneo la Mahakama wakiendelea kuimba na kushangilia lakini walipofika eneo la Mahakama ya Rufani ghafla walianza kupigana ngumi na mawe. Baadhi yao walikamatwa na askari kutokana na vurugu hizo.
Awali, wafuasi hao walifika mapema asubuhi katika viwanja vya Mahakama tayari kusikiliza uamuzi huo.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa na askari polisi wakiwamo wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliokuwa na silaha pamoja na mabomu ya machozi walikuwa wametanda.
Pia kulikuwa na askari wa Kikosi cha Mbwa pamoja na gari la maji ya kuwasha.
Licha ya kuwahi, ni wafuasi wachache walioruhusiwa kuingia ndani ya u`kumbi wa Mahakama tena baada ya kuandikisha majina yao huku wakitambuliwa na viongozi wao waliokuwapo

KATUNI YA LEO:MTOTO WA MKULIMA KITI CHA MOTO,VUMILIA SI ULIYATAKA MWENYEWE


hAHahahaha, this is very funny....mie "SIWAJUI " hao waliopo kwenye picha labda wewe msomaji unisaidie..

Baada ya Sugu, Afande Sele, na Profesa J kuchukua kadi ya Uanachama CHADEMA...Roma mkatoliki naye atangaza kuchukua kadi ya Uanachama CHADEMA wiki Ijayo..!

Roma Mkatoliki akiongea na mabest zake Wa Mtaani huko Tanga amesema ana mpango Kuingia Kwenye Uringo wa Kisiasa ili apate nafasi Nzuri ya Kuikosoa Serikali baada ya Muziki wake Kupuuzwa na Viongozi wa Taifa hili.

Naplan Kuzamia Kwenye Mambo ya Politics hivi sasa, By the Way Wiki Ijayo naweza Kuchukua Kadi ya Chadema Rasmi”… Pia amesema Atahakikisha Wasanii Wenzake wanaoimba Muziki wa HipHop akina Kala Jeremiah nao Wanaunda timu ya Maangamizi Kuing’oa CCM Madarakani, ila aliwasihi sana Viongozi wa Chadema Kuwa Karibu nao pale Wanapozushiwa Shutuma za ajabu ajabu Kisa Wamejiunga na Chadema.

Mpaka sasa baadhi ya wanamuziki wa Bongo Fleva waliojiunga na ambao wanampango wa kujiunga na Chama Cha kuwakomboa wanyonge CHADEMA ni Afande Sele wa Morogoro, Joseph Haule ambaye anajulikana kama Prof J, Soggy Doggy na Wengineo wengi.

Mazingaombwe ya CHADEMA jijini Mwanza....Vurugu kubwa zaibuka kati ya Meya na Madiwani wa CHADEMA



ILIKUWA ni kama uwanja wa vita na mipasho, ndivyo unavyoweza kusema, baada ya kuibuka vurugu kubwa kati ya Meya wa Halmashauri ya Ilemela, Henry Matata na madiwani wake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). 

Vurugu hizo ziliibuka jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela baada ya Matata kuwataka madiwani watatu wa Chadema kutoka nje ya ukumbi kwa kuwa tayari alikwishawafukuza hivyo si madiwani tena.
 

Madiwani waliotakiwa kutoka nje ya ukumbi na Kata na zao katika mabano ni Marieta Chenyenge (Ilemela), Abubakar Kapera (Nyamanoro) na Daniel Kahungu (Kirumba).

Hali hiyo ilizua tafrani kwa pande zote mbili kwani walikuwa wakishambuliana kwa maneno makali na ya kashfa huku Meya Matata akitumia nafasi yake kuwaamrisha polisi waliokuwapo ndani ya ukumbi huo kuwatoa nje madiwani hao nguvu.

“Nasema leo hamtakaa ndani ya ukumbi huu na lazima mnijue mimi ndio Meya wenu na posho hamtapata, naomba polisi watoeni nje na mkishindwa nitawaita mabaunsa wangu waingie ndani.

“Wengine hapa mmekuwa mkiombana posho na ndizo zinazowaleta hapa, watu sio madiwani lakini mnang’ang’ania kuja kwenye vikao,”alisema Matata kwa ukali.

Wakati Matata akitoa kauli hizo, madiwani hao nao walikuwa wakimjibu wakidai kuwa hata yeye si diwani wa Chadema, hana kadi na kwamba chama hakimjui na wanashangaa kuona akiendelea kuwa Meya wa Ilemela.

Hata hivyo wakati vijembe hivyo vikiendelea, polisi walishindwa kuwatoa nje madiwani hao na baada ya kutetea haki yao ya kuwamo ndani ya kikao hicho kwa kutumia vifungu kadhaa vya sheria.

Sekeseke lilizidi kupamba moto, pale kitabu cha kujiorodhesha majina kilipofika kwa madiwani hao kwa ajili ya kujiandikisha, jambo ambalo lilimfanya Matata amuagize muhudumu wa Manispaa hiyo kuwanyang’anya.

Hata hivyo muhudumu huyo aliposhindwa kuwanyang’anya kitabu hicho, Matata aliomba msaada kwa polisi ambao nao walikataa hali iliyomfanya ainuke katika kiti chake na kwenda kukichukua kwa nguvu.

Hali ndani ya ukumbi iliendelea kuwa mbaya pia baada ya madiwani hao kunyimwa majoho na taarifa za vikao huku wenzao wa CCM wakipewa huduma zote kitendo ambacho kilionekana kuwakera.

Visa vya Matata havikuishia hapo kwani pia aliamuru meza na viti vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili ya madiwani kuhamishwa na kuvisogeza mbele karibu na meza kuu isipokuwa vile vilivyokaliwa na madiwani wa Chadema ambavyo viliachwa nyuma.

Katika hali isiyo ya kawaida madiwani hao nao waliamua kuhama walipoachwa na kwenda pale walipokaa madiwani wenzao.

Kitendo hicho kilionekana kumkera Matata na kuamua kutoka nje huku akisema anawafuata makomandoo wake jambo ambalo lilizua hofu kwa baadhi ya wajumbe wengine ambao walikimbilia nje.

Wakati wote wa vurugu hizo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Zuberi Mbyana na Naibu Meya, Sule Debe walikuwa kimya mbele ya meza kuu.

Hata hivyo muda mchache baada ya Matata kutoka nje, Mkurugenzi na Naibu meya nao walitoka nje na kutelekezwa kikao kwa zaidi ya saa moja kabla ya kurejea tena ukumbini.

Baada ya kurudi ukumbini bila makomandoo, kikao kiliendeshwa bila kuwapa nafasi madiwani wa Chadema kuhoji wala kupewa taarifa zozote za vikao licha ya kunyoosha mikono kuhoji hali hiyo.

Kitendo hicho kiliwafanya Madiwani wa Chadema kuwa kama wasikilizaji kwa zaidi ya nusu saa na baadaye kuamua kutoka nje na kwenda Ofisi ya Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia kufanya kikao cha dharura na kutoa tamko.

Wakati kikao cha Chadema kikiendelea, Meya, Mkurugenzi na Naibu Meya waliendelea na kikao hicho kilichokuwa na ajenda ya kupitisha mapendekezo ya kuzigawa tarafa na kata za Wilaya ya Ilemela.

Baada ya kumalizika kikao hicho, Matata alisema alishindwa kuingiza makomandoo wake kutokana na kushauriwa na viongozi wanzake huku akisisitiza kuwa kamwe hawezi kuwaruhusu madiwani hao kuingia kwenye vikao wakati alikwishawafukuza.

Pia aliwalaumu polisi kuzembea kuchukua hatua pale wanapoagizwa huku akimtaka Mkurugenzi kujipanga vema na kuweka ulinzi wa kutosha wakati wa vikao vya aina hiyo.

Tamko la Chadema

Katika taarifa yao waliyoitoa baadaye jana baada ya kikao chao, Madiwani hao wa Chadema walidai kuwa kilichokuwa kikitokea kati yao na Meya ya Halmashauri hiyo ni mkakati wa serikali kutaka kuihujumu Halmashauri ya Ilemela ili isifikie malengo yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kiongozi wa Operesheni Kanda ya Ziwa Magharibu, Tungaraza Njugu alisema vurugu zinazotokea Mwanza ni matokeo ya udhaifu wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Tamisemi na Rais Jakaya Kikwete.

“Kinachoendelea hapa ni hujuma ambayo inaanzia kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Waziri Mkuu, Tamisemi na Rais, mkakati huu wameupanga na kumweka Meya Matata kihuni wakati si diwani.

“Leo hii ni mwaka mzima wananchi wa Ilemela hawana huduma yoyote na barabara zao mbovu, shida hii ni kwa sababu wamekosa wawakilishi badala yake kumeundwa genge ndio linaloendesha Halmashauri.

“Chadema Mkoa  wa Mwanza tunaungana kuhakikisha Pinda anaondolewa madarakani kwa sababu ya kushindwa kuziongoza hizi Halmashauri na badala yake analea uchafu” alisema.

Kwa upande wao, madiwani hao walisema wao ni madiwani halali na hata Pinda alitangaza kupitia Bunge lililopita kwamba anawatambua huku wakidai kuwa barua za wao kutambulika zipo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

source:Rai jumatano.

CHADEMA WAASWA KUMALIZA MIGOGORO ILI KULETA MAENDELEO NCHINI NA SIO MUDA WOTE KULUMBANA

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumaliza mgogoro wake ili kuweka nguvu kwenye Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwakani.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema hayo jana wakati akitoa maoni ya Baraza Kuu la CUF na kuongeza kuwa suala la kupata Katiba mpya yenye misingi imara ya demokrasia na utawala bora linapaswa kupewa kipaumbele na kuunganisha viongozi wa Chadema kulisimamia.

Mgororo ndani ya chama hicho ulitokana na Kamati Kuu (CC) kuwavua nyadhifa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto aliyekuwa mjumbe wa CC, Dk Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Arusha, Samson Mwigamba, huku wakidaiwa kukabiliwa na mashitaka 11.

“Kwa hali ilivyo sasa na kama itaendelea hivyo, ni dhahiri nguvu kubwa ya Chadema ikaelekezwa kwenye mgogoro wao, jambo ambalo litaathiri ushiriki wao katika mjadala wa Katiba kwenye Bunge la Katiba,” alisema Profesa Lipumba.


Alisema katika mchakato wa kupata Katiba Mpya, Chadema ni miongoni mwa vyama vilivyotoa mchango mkubwa, umoja wao unahitajika kuhakikisha chama hicho kinatumia fursa hiyo muhimu na adimu kwa maslahi ya Taifa.


Aliongeza kuwa wakati mwingine wamekuwa wakifanya kazi na Chadema ili kuhakikisha Katiba mpya inapatikana ikiwa shirikishi na kwamba wakati huu si wa kuendelea kushikana koo wao kwa wao.


Kuhusu kama walishakiandikia chama hicho kutaka kisitishe mgogoro wake, alisema hawajafanya hivyo ingawa yamekuwapo mazungumzo yasiyo rasmi na viongozi hao.

Bunge la Katiba

Kuhusu Bunge la Katiba, Profesa Lipumba alisema Baraza Kuu la CUF linatoa mwito kwa vyama vyenye wabunge kuacha kupigania maslahi yao wakati wa mjadala wa Bunge la Katiba.

“Ni dhahiri, kwamba Katiba inayoandikwa ni ya nchi si chama, hivyo ni muhimu kwa wabunge wa Bunge hilo kuwa wazalendo kwa kutoa michango itakayowezesha kupatikana Katiba bora badala ya michango itayowezesha kupatikana kwa Katiba yenye maslahi na vyama vyao,” alisema Profesa Lipumba.


Katika hatua nyingine, Baraza Kuu la CUF, lilitoa mwito wa kuwapo mkutano wa wadau hususan vyama vya siasa na asasi za kiraia, kujadili Rasimu ya mwisho ya Katiba kwa lengo la kufikia maridhiano kwa mambo muhimu yaliyomo.


Alisema baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwasilisha Rasimu ya pili, ni vema wadau wakafanya mkutano utakaorahisishia kazi Bunge la Katiba kufikia mwafaka kuhusu vipengele muhimu vya Katiba mpya.


Hata hivyo, alisema chama hicho kinaamini kuwa Rasimu ya pili ya Katiba Mpya haitakuwa na mabadiliko makubwa kuhusu muundo wa Muungano wa serikali tatu uliopendekezwa katika Rasimu ya kwanza.


Alisema Baraza Kuu linaamini, kwamba uwepo wa serikali tatu katika muundo wa Muungano ni jambo muhimu na ni njia ya kumaliza kero za Muungano na kuitaka serikali kusimamia kikamilifu mchakato wa Katiba ili ipatikane kabla ya uchaguzi wa 2015.

“Ni wazi, kuwa wananchi hawatakubali kuingia kwenye uchaguzi mwaka 2015 kwa kutumia Katiba ya sasa ambayo imekataliwa na wengi waliotoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,” alisema.

Wavurugaji waonywa


Wakati huo huo, vyama vya wafugaji wa asili vimemwomba Rais Jakaya Kikwete aangalie kwa makini baadhi ya watu wanaotaka kuharibu mchakato wa mapendekezo ya wawakilishi kwenye Bunge la Katiba.

Ombi hilo lilitolewa na Mwakilishi wa Mtandao wa Katiba Initiative, Saikon Justin wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchakato wa kupata wawakilishi tisa ambao wameufanya kwa kushirikiana na mashirika zaidi ya 32 ya vyama vya wafugaji wa asili Tanzania.


Alisema baadhi ya watu wanatumia mchakato wa uundwaji wa Bunge hilo ili wajinufaishe badala ya kuangalia maslahi ya Taifa na wadau wanaopaswa kuchangia kupatikana kwa Katiba mpya.

Aliongeza kuwa tabia hiyo inaweza kudhoofisha makundi halisi ya kijamii ambayo yameshiriki kikamilifu kwenye mchakato wa uandikaji wa Katiba kuanzia hatua za awali hadi sasa.

Alisema vyama hivyo vilifanya mkutano juzi na kuchagua wawakilishi tisa huku jinsia kizingatiwa kwa wanawake wanne na wanaume watano wenye sifa kuchaguliwa ili kutoa mawazo yao na kuwakilisha wenzao wanaohitaji mawazo yao yawe ndani ya Katiba.

*Imeandikwa na Lucy Lyatuu, Dar na Veronica Mheta, Arusha.- habarileo

DR SLAA AMPIGA MARUFUKU ZITO KUFANYA MIKUTANO,NI BAADA YA ZITO KUFUNIKA KATIKA MIKUTANO HIYO


 
Zitto Kabwe jana  amefanya mkutano wa 3 ndani  ya Mkoa wa Kigoma,mikutano hii  ilianza siku ya Jumamosi kwa  sehemu ya Mwandiga mahali alipozaliwa na kukulia,Kasulu ilikua juzi  na jana kafanya Kigoma mjini eneo la Mwanga kwenye uwanja wa Community Centre....
 
Mkutano ulianza sa 10 kiitifaki ulitanguliwa na viongozi wa Chadema wa mkoa,kisha Zitto Kabwe kupanda Jukwaani na moja kati ya vitu alivyovizungumzia ni kuhusu tamko la Dr.Wilbroad Slaa alipokuwa kwenye mkutano wake  wa Kuimarisha chama uliofanyika Igunga Mkoani Tabora....
 
Dr.Slaa alizungumzia kuhusu mikutano anayoifanya Zitto Kabwe kuwa si halali yeye anatakiwa kufanya kwenye jimbo lake tu ambalo ni Kigoma Kaskazini .
 
Hiki ndicho alichokizungumza kufuatia tamko hilo la Dr.Slaa  "Sasa jana (juzi ) Katibu Mkuu kasema Kwanini nafanya ziara zaidi ya Kigoma Kaskazini siruhusiwi kwenda sehemu nyingine yoyote baada ya kusikia yale mapokezi ya Kasulu.
 
"Mimi nawaambia katiba ya Nchi hii inaniruhusu kwenda mahali kokote,sehemu yoyote nchi hii kwa mujibu wa katiba maana mimi bado ni Mbunge.Kama wamenifukuza waseme kuwa wamenifukuza lakini kama hawajanifukuza mimi bado mbunge"
 
"Kwa hiyo nitaenda Kigoma Kaskazini,nitaenda Kigoma Kusini,nitaenda Kasulu,nitaenda Kigoma Mjini kuhutubia Wananchi na siyo hivyo tu nitaenda Mpanda,nitaenda Tabora,nitaenda Shinyanga,nitaenda Mwanza nitaenda hadi Arusha na hakuna mtu wa kunizuia."
Add caption
 
 
 

"WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NAE ANAPASWA KUJIUZULU"...DK. SLAA

Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Dr.Wilbroad Slaa amesema serikali nzima na Baraza la Mawaziri linapaswa kujiuzulu na kwamba kitendo cha kujiuzuru kwa mawaziri wanne tu hakitoshi na badala yake amesema Pinda kama "kiranja" mkuu anapaswa kuwajibika.

 
Dr.Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara huko mkoani Tabora.

CHANZO:ITV

JK kumng’oa Pinda? ....Yasemekana kaandika barua ya kujiuzulu , Mbinu ya Kikwete kumnusuru yabainika


HATUA ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia kutengua uteuzi wa mawaziri wanne, sasa ina kila dalili za kumpa nafasi ya kuchukua uamuzi wenye mwelekeo mpya ndani ya muda mfupi ujao kuanzia sasa...

Ni katika mwelekeo huo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye naye alitakiwa na wabunge kujiuzulu, licha ya juzi kutokuwa tayari kulizungumzia jambo hilo wakati akitangaza uamuzi wa Rais kutengua uteuzi wa mawaziri hao wanne, anaaminika kutangaza uamuzi huo huku hatma yake ya kuondoka madarakani ikiwa imezungukwa na wingu la shaka.

Ingawa hadi sasa Pinda mwenyewe amekwishasema yuko tayari kung’oka na kwamba atafurahi kama uamuzi huo utachukuliwa dhidi yake, lakini hatua iliyochukuliwa na Rais Jakaya Kikwete sasa inadhihirisha kuwepo kwa dalili za kutaka kumnusuru kiongozi huyo dhidi ya shinikizo la wabunge, ambao mara kwa mara wamekuwa wakimtaka ang’oke, wakimtuhumu kwa uzembe.

Baadhi ya wadadisi na wafuatiliaji wa mambo waliochambua uamuzi huu wa sasa wa Rais Kikwete, wanaeleza kuwa huenda kiongozi huyo akawa anatumia staili ile ile aliyoitumia mwaka mmoja uliopita kumnusuru Pinda.

Wanaeleza kuwa, mwaka 2012, Kikwete alilazimika kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri kwa kuwaweka kando mawaziri nane ambao wabunge walikuwa wakishinikiza wang’olewe pamoja na Pinda, baada ya kukasirishwa na ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), iliyowatuhumu mawaziri hao kwa ubadhirifu.

Hata hivyo, baada ya kufanya mabadiliko hayo, yaliyoshuhudia mawaziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Afya Hadji Mponda, Viwanda na Biashara Cyril Chami, Uchukuzi, Omari Nundu na wengine, Rais Kikwete hakumuondoa Pinda na tishio la wabunge kutaka kumuondoa kwa kura ya kutokuwa na imani naye nalo lilififishwa na hatua hiyo.

Wakati wadadisi na wachambuzi wa mambo wakiwa na mtizamo huo, zipo taarifa zinazoeleza kuwa ugumu wa Rais Kikwete kuchukua hatua ya kumuondoa Pinda unatokana na hatua yake ya kutaka kuinusuru serikali na mzigo wa gharama za kuwalea mawaziri wakuu pindi wanapoondoka kwenye nyadhifa zao.

Hatari hiyo ya serikali kubaki na mzigo mkubwa wa viongozi wakuu wastaafu, ndiyo inayotajwa wakati fulani mwaka 1994 kumlazimisha Rais Ali Hassan Mwinyi kumrudisha kwenye nafasi ya uwaziri mkuu, Cleopa Msuya, aliyepata kuhudumu kwenye nafasi kama hiyo wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere.

Hadi sasa Tanzania ina mawaziri wakuu wastaafu watano, ambao ni John Malecela, Cleopa Msuya, Jaji Joseph Warioba, Frederick Sumaye na Edward Lowassa.

Hata hivyo, taarifa ambazo RAI Jumapili limezipata zinaeleza kuwa, Pinda binafsi yuko tayari kukabidhi madaraka, ingawa uamuzi huo haijulikani utachukuliwa namna gani na Rais Kikwete pindi atakaporejea Alhamisi wiki hii, akitokea Marekani, alikokuwa kwenye matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizolifikia gazeti hili, tayari Pinda amemueleza Rais Kikwete juu ya azma yake hiyo, huku nyingine zikieleza kuwa amekwishamuandikia barua ya kujiuzulu.

Ingawa si Pinda wala Ikulu waliopatikana kuthibitisha taarifa hizo hadi tunakwenda mitamboni usiku wa kuamkia leo, ni wazi kwamba, hatua ya sasa ya Rais Kikwete inakuja kama mbinu ya serikali yake kutaka kujisafisha kupitia mabadiliko hayo ya Baraza la Mawaziri, ili kukwepa lawama ambazo zimekuwa zikielekezwa mara kwa mara na jamii dhidi ya serikali yake kuhusu vitendo mbalimbali vya ubadhirifu na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tayari mawaziri wawili majina yao yameanza kutajwa kurithi nafasi ya Pinda, ikiwa ataondoka katika nafasi hiyo.

Mawaziri hao ni Waziri wa Miundombinu, Dk. John Magufuli na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira.

Aidha kitendo hicho cha Rais kuamua kutengua uteuzi wa mawaziri wa aina ya Emanuel Nchimbi wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki wa Maliasili na Utalii, na David Mathayo wa Kilimo kwa tuhuma zilizotokana na Operesheni Tokomeza, inatajwa kuliweka njia panda Baraza zima la Mawaziri, hususan wale wanaotajwa kuwa ni mawaziri mizigo.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa uamuzi huo wa Rais Kikwete umewashtua mawaziri karibu wote, huku baadhi yao wakipata shaka kama wataendelea kubaki katika nyadhifa zao.

Ni hatua hiyo pia inatajwa kumpatia nafasi ya kuwaondoa au kuwahamisha wizara mawaziri wengine, wakiwamo wale waliopachikwa jina la mawaziri mizigo pindi atakapofanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Mawaziri wanaotajwa kuwa ni mizigo na ambao tayari wamekwishahojiwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia.

Wengine ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Waziri wa Fedha, William Mgimwa, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, na Waziri wa Nchi Menejimenti na Utumishi wa Umma, Celine Kombani.

Katika mabadiliko hayo ya Baraza la Mawaziri yanayotarajiwa kufanywa ndani ya muda mfupi, pia huenda yakatoa nafasi kwa baadhi ya mawaziri ama kuondoka au kubaki, lakini pia kuwajumuisha wapya.

Miongoni mwa wanaotajwa kujumuishwa katika baraza jipya la Mawaziri ni pamoja na Dk. Asha Rose Migiro, ambaye hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alimteua kwenye nafasi ya ubunge.

-RAI JUMAPILI 

TAZAMA JINSI ZITTO KABWE ALIVYOPOKELEWA MKOANI KIGOMA,MAMIA WAJITOKEZA KUMPOKEA

 Zitto Kabwe  akisalimiana  na  wafuasi  wake...
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Mkutano wa CHADEMA mkoani kigoma wasambaratishwa kwa mawe....Polisi watumia mabomu ya machozi kumuokoa Dr. Slaa


 
Taarifa za kusikitisha ni kwamba mkutano wa Dr.slaa wilayani Kasulu-Kigoma umevunjika baada ya vurugu kubwa kuibuka....
 
Kwa mujibu wa mtandao wa jamii forums ,Slaa anadaiwa kupigwa mawe na vijana wasiojulikana  wakati akiwa Jukwaani....
Baada ya vurumai hilo, polisi walilazimika kupiga mabomu ya Machozi ili kutawanya watu ....

Bado haijulikani, Slaa ameumizwa kiasi gani lakini polisi waliwahi kumuokoa na kumtorosha kusikojulikana....


Picha tano za mikutano ya Dr. Slaa mkoani Kigoma..Mwenyekiti wa mtaa ajitoa CCM na kuhamia CHADEMA

 Baadhi ya waandamanaji wakiwa na mabango ya kumpinga Dr. Slaa...
Polisi  wakimsulubu  kijana aliyeleta  vurugu  eneo  la  mkutano....
Polisi wakidumisha  ulinzi  kwa  kukabiliana  na  waandamanaji....
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Community Center mjini Kibondo baada ya waleta vurugu kukabiliwa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akipokea kadi ya uanachama, kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti Kitongoji cha Mtaa wa Shule katika Kijiji cha Mabamba kupitia CCM, Sevelino Damian, ambaye amehemia Chadema, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo

MADIWANI CCM,CHADEMA WAPIGANA NGUMI KAVUKAVU KISA KUHOJI MATUMIZI YA MILIONI 95/-

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya,Diwani Athuman
Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, wamejeruhiwa vibaya hadi kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa kile kinachodaiwa kupigwa na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo la ukumbi wa halmashauri wa Mkapa wakati kikao.
Diwani wa Kata ya Mwakibete ambaye pia ni Katibu wa Mwenezi Chadema wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki, jana aliwaeleza wandishi wa habari kuwa tukio hilo lilutokea Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Mkapa ambao unamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Mwampiki aliwataja madiwani waliojeruhiwa na kulazwa kuwa ni wa Kata ya Sinde, Fanuel Kyanula na wa Kata ya Ilemi, Furaha Mwandalima.

Mwampiki alisema kabla ya kutokea kwa vurugu hizo, madiwani wa vyama vya upinzani walikuwa wakihoji uhalali wa ziara ya baadhi ya maofisa wa Halmashauri ya Jiji wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, kwenda China kwa kutumia fedha za halmashauri bila kufuata utaratibu.

Alisema katika ziara hiyo, Meya Kapunga aiongozana na maofisa watano ambao ni Mkurugenzi wa Jiji, Mchumi, Afisa Mipango na diwani mmoja wa CCM ambayo iliigharimu halmashauri hiyo zaidi ya Sh. milioni 95 ambazo hazikuwa kwenye bajeti wala kuidhinishwa na kikao chochote.

Alisema madiwani wa Chadema na NCCR-Mageuzi walifuata taratibu zote za kuhoji suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuorodhesha majina yao na kusaini ili mkutano wa madiwani uitishwe na hoja hiyo ijadiliwe.

Kwa mujibu wa Mwampiki, kikao cha Madiwani kilichoketi Ijumaa waliamini kuwa ajenda hiyo itaingizwa, lakini wakashangaa kuona haimo kwenye orodha ya ajenda zilizopaswa kujadiliwa.

Alisema madiwani wa upinzani walipohoji juu ya kuondolewa kwa ajenda hiyo, Meya Kapungu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, alikuja juu na kuamuru mlango ufungwe ili madiwani wapigane.

“Tulishangaa kusikia Meya akisema kuwa kila siku madiwani wa Chadema tunawafanya wasiishi kwa raha mjini na kutamka kuwa inabidi milango ifungwe ili zipigwe,” alisema Mwampiki.

Alisema madiwani wa Chadema kuona hivyo waliamua kutoka haraka nje ya ukumbi wa mkutano, huku wakirushiwa chupa za maji na baadhi ya madiwani wa CCM.

Mwampiki alidai kuwa hata baada ya madiwani wa Chadema kuwa wametoka nje ya ukumbi wa mkutano, madiwani wa CCM waliwafuata na kuanza kuwashambulia kwa kipigo mpaka walipoachanishwa na polisi waliokuwepo eneo hilo.

Alisema katika vurugu hizo, madiwani wawili wa Chadema walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa kwa matibabu na walilazwa.

Asema Diwani wa Ilemi, Mwandaliwa alijeruhiwa sehemu za shingo kiasi cha shingo yake kutogeuka kila upande huku Diwani wa Sinde, Fanuel akiwa amejeruhiwa kwenye shavu kutokana na ngumi walizokuwa wakipigwa.

Akizungumza baada ya kutoka hospitali, Mwandalima alisema alikuwa miongoni mwa madiwani wa mwisho kutoka ukumbini na kuwa alipofika nje ya ukumbi alijikuta akivamiwa na kundi la madiwani wa CCM ambao walianza kumshushia kipigo huku wengine wakimkaba na kumuumiza vibaya maeneo ya shingoni.

Meya wa Kapunga alikanusha kuhusika na ugomvi huo huku akisema kuwa hakuna diwani aliyepigana ndani ya ukumbi wa mkutano.

Alisema anachokumbuka ni kwamba madiwani wa upinzani walikuwa na hoja ya kutaka kujua juu ya ziara ya watumishi wa Halmashauri nchini China, lakini hawakufuata utaratibu na kanuni  walizojiwekea katika kuhoji masuala mbalimbali ya halmashauri.

Alisema baada ya kupitia orodha ya majina ya madiwani waliokuwa wakihoji suala hilo, walibaini kuwa kuna baadhi ya saini za madiwani zimeghushiwa, jambo ambalo alisema ni kinyume cha taratibu za halmashauri na sheria za nchi.

Alisema miongoni mwa saini zilizobainika kughushiwa ni za baaadhi ya madiwani ambao hawapo jijini Mbeya kwa muda mrefu.

Alisema baada ya hoja ya madiwani hao kukataliwa, ndipo walipoinuka kutoka ndani ya ukumbi wa mikutano huku wakiwatolea matusi ya nguoni madiwani wenzao wa CCM.

“Ninachokumbuka ni kwamba wakati madiwani wa Chadema wakitoka nje walikuwa wakitukana matusi ya nguoni inawezekana matusi hayo yaliwauma wenzao wa CCM ambao waliwafuata huko nje, hivyo kama walipigwa nje ya mkutano mimi sina taarifa,” alisema Kapunga.

Akizungumzia ziara ya watumishi wa halmashauri ya akiwamo yeye nchini China, Kapunga alisema ziara hiyo ilitokana na agizo la serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (Tamisemi).

Alisema kabla ya kufanya ziara hiyo alifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kulijulisha Baraza la Mdiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Ofisi ya Katibu Tawala ya Mkoa wa Mbeya, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Mussa Zungiza, alipinga kiwango cha fedha cha Sh. milioni 95 kinachodaiwa na madiwani wa Chadema kuwa kilitumika kwenye ziara hiyo, badala yake alisema zilitumika Sh. milioni 54.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema yuko nje ya Mkoa wa Mbeya kikazi, hiyo hakuwa na taarifa zozote.

Pamoja na Kamanda Diwani kusema hana taarifa, lakini Mwandalima alisema walipewa fomu za polisi PF 3 kabla ya kupatiwa matibabu hospitali.

CHANZO: NIPASHE

Lema Atungiwa Nyimbo kama Shujaa wa Tanzania na vijana wa Arusha...Isikilize hapa




LEMA ATUNGIWA NYIMBO ARUSHA ISILKILIZE HAPA BONGE LA HIT ...NA HII NINYIMBO MOJA WAPO KUTOKA KWENYE MIXTAPE YA KABURI LA FISADI ITAKAYO ACHIWA JANUARY 2014




Isikilize Nyimbo hapo chini.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari