Like Us On Facebook
Showing posts with label wasanii wa Bongo. Show all posts
Showing posts with label wasanii wa Bongo. Show all posts

MASHABIKI WAMUAMURU SHILOLE ACHEZE UCHI STEJINI

NCHI yetu imejaaliwa kuwa na vijana wengi wenye vipaji karibu katika kila nyanja. Wapo waliojaaliwa kupewa na hawajui kuvitumia pasipo mwongozo, lakini wengine wanajua kuvitumia na kujiongoza.
Shilole akijiachia stejini na shabiki.
Katika Bongo Fleva na Filamu, fani zinazokimbiliwa zaidi na vijana, lipo kundi kubwa la watu wanaotoka kimaisha kupitia huko. Na mmoja wa vijana wenye vipaji, ni Zuwena Mohamed, ambaye mashabiki wa muziki wanamtambua kama Shilole.
Niwe mkweli, simfahamu msichana huyu kwa maana ya kuwahi kufanya naye kazi, ila nimewahi kusikia kazi zake hasa wimbo wake huu unaotamba sasa, Nakomaa na Jiji.

Pamoja na kwamba bado ni msanii mchanga, lakini ameonyesha kuwa anaweza ubunifu. Wengi wanapenda kuimba, lakini waimbe vipi ndiyo huwa tatizo. Ni kama Snura alivyojishauri na kuamua kuipa kisogo fani ya uigizaji na kujikita kwenye mduara.
Lakini ndani ya fani, Shilole ni aina ya binti anayewakilisha mastaa uchwara wa kike Bongo, wasiojitambua na bahati mbaya, hatambui hata mahitaji ya wateja wake.
Nimewahi kuona mara kadhaa akiandikwa magazetini kuhusu mambo yake mengi yanayokera, hasa aina ya uvaaji. Moja ya jambo lililonitatiza, ni jinsi wakati mwingine anavyovaa blauzi zake tata, zinazoruhusu matiti yake karibu yote kuwa nje!
Lakini nimejikuta nikisita kukaa kimya baada ya kukutana na kauli yake katika moja ya magazeti ya kila siku nchini, akidai kwamba anavaa vile ambavyo watu wamekuwa wakimlalamikia, kwa sababu mashabiki wake ndiyo wanapenda!

Yaani anavyovaa nguo za ajabu ajabu, yaani zenye kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake hadharani, ndivyo ambavyo watu wanaofurika katika majukwaa anayoimba wanavyopenda.
Ni kweli kwamba katika biashara, ni jambo la msingi sana kutazama nini mahitaji ya wateja. Muziki ni biashara na mashabiki ndiyo wateja wenyewe. Sitaki kuamini kama wale watu wanaojitokeza katika matamasha ambayo Shilole hualikwa kutumbuiza wanafurahishwa nayo.

Kwanza ni jambo la msingi kumfahamisha Shilole kwamba hana mashabiki. Nasema hivi kwa sababu kama leo hii mtu atajitokeza na kuandaa shoo ya mtu mmoja tu, ambaye ni yeye, sidhani kama atafanikiwa. Na katika hili, kuna watu wachache sana wanaweza kujaza watu katika nchi hii, wakiongozwa na Nasib Abdul ‘Diamond’.
Shilole anaalikwa katika matamasha kwa ajili ya kuchanganya ladha tu na wala asije akaona watu wanavyopiga kelele anapokuwa jukwaani basi wanashangilia mavazi yake. Huwezi jua, huenda huwa wanamzomea!
Kuvaa ovyo hakuwezi kuwafanya watu waupende muziki wako. Sijawahi kumuona msanii wa kike mvaa ovyo aliyefanikiwa kuuza sana nakala zake katika Tanzania tokea nianze kufuatilia Bongo Fleva. Sana naona wanashindwa tu, wakiongozwa na Ray C!

Lakini kuna wasanii wengi tu wa kike waliofanya vizuri na kujilundikia mashabiki, lakini bado wanavaa mavazi ya heshima jukwaani, kwenye video zao na hata wanapokuwa kwenye matukio ya kijamii. Hapa upo mfano wa Lady Jay Dee kwani ndiye msanii wa kike mwenye mafanikio zaidi lakini anayejiheshimu.
Kwangu, kuvaa mavazi yenye kuonyesha sehemu kubwa ya mwili ni kutojiamini. Anataka watu wavutike kwa kuangalia mwili badala ya kazi. Ndiyo hawa hawa waliojazana katika Muvi zetu, wanavaa nusu uchi kuwachota watu akili ili concentration yao iwe kwenye miili yao badala ya kazi zao!
Tubadilike. Nimesema mara kwa mara, ukishakuwa staa, unapaswa kuwa mfano ulio bora!

WEMA AWAJIBU WAIGIZAJI WA BONGO MOVIES WALIO SUSIA MSIBA WA BABA AKE

Kupitia kipindi chake cha ‘In My Shoes’ cha jana, Wema Sepetu alieleza jinsi alivyojisikia baada ya baadhi ya waigizaji wenzie wa Bongo Movie kugoma kuhudhuria msiba wa baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, mwishoni mwa mwezi uliopita kwa madai kuwa yeye hakuwa akifanya hivyo kwenye misiba mingine.


“Imeshatokea, wameacha kuja kwenye msiba, ni wao,” alisema Wema. Sio Bongo movie nzima, ni baadhi tu ya watu ambao wanauelewa na upeo mdogo ambao waliamua kutokuja. Lakini niliona Bongo movie wengi, walikuwepo marafiki zangu wengi, akina Batulli, akina Esha, Wolper alikuja, Lulu, JB alikuja, Jokate alikuja, Adam Kuambiana alikuja. Ambaye napenda nimpe my special thanks and appreciation, ambaye alijitolea from the beginning wa msiba mpaka to the end ni Dokta Cheni kwakweli. Dr Cheni, I thank na ntazidi kumshukuru,” alisema.

“Marafiki zangu kama akina Kajala, akina Zamaradi, wale sio marafiki, wale tayari ni ndugu, kwahiyo siwezi kuwaweka kwenye appreciation wala kwenye thanks.”

Katika kipindi hicho pia, Wema alisema yeye na ndugu zake walijua kuwa baba yako ni muumini wa dhehebu la Roman Catholic siku chache kabla ya kufariki dunia.

Balozi Issac Abraham Sepetu (71), alizikwa kikristo katika kijiji cha Mbuzini,mkoa wa Kusini Unguja October 30 ambapo mazishi yake yalihudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohammed Shein pamoja na viongozi wengine.

Bongo5.com

WEMA,ROSE NDAUKA NDANI YA VITA KALI


MASTAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka na Wema Sepetu wanadaiwa kuingia vitani, mpambe mmoja wa Wema akitumia mtandao wa kijamii wa Instagram alimtuhumu Rose kwamba aliwahi kushiriki kikao kimoja kilichokuwa kikimjadili ‘madam’ huyo sanjari na kumtukana.

Mpambe huyo aliyetumia picha ya Wema (huenda akawa Wema mwenyewe), alisema kuwa siku moja isiyokuwa na jina hivi karibuni, Rose alishiriki kikao hicho kilichofanyika kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam ambapo sehemu kubwa ya mazungumzo ilikuwa ikimchambua Wema.

Akizungumza na Amani kwa njia ya simu juzi kuhusiana na tuhuma hizo, Rose alisema anashangaa matusi anayotukanwa na mtu huyo kwani ana mwaka mmoja hajawahi kukanyaga katikia viwanja hivyo vilivyopo Kinondoni, Dar.

“Kiukweli huyo mtu amenitukana bure, hajakaa na kufanyia uchunguzi hizo taarifa alizopewa, mimi sikumbuki kama kuna siku niliwahi kukaa Leaders na kuanza kumsema vibaya Wema kwani nina mwaka sijawahi kufika Leaders.

“Binafsi sina muda huo wa kumzungumzia mtu au kukaa na mtu ambaye hana faida kwangu. Mimi rafiki yangu ni mchumba wangu (Malick Bandawe), mama yangu na ndugu zangu zaidi ya hapo tunakutana shutingi tukimaliza narudi kwangu, namsihi huyo mpambe wa Wema afanye tena uchunguzi,” alisema Rose.

Juzi, Amani lilimsaka Wema kwa njia ya simu ya mkononi ili azungumzie madai hao lakini hakupatikana. Hata hivyo, habari zinasema kuwa mtu aliyemtukana Rose kwenye mtandao alitumwa na Wema au Wema mwenyewe.

Tangu Diamond kurudiana na Wema na kusambaza picha zao katika mitandao ya kijamii, hivi karibuni Wema kufiwa na baba yake mzazi (Isaac Sepetu) na baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi kususia msiba huo, kumeibuka makundi ya watu kazi yao kubwa ni kutukana watu ambao wako tofauti na Wema.

DIAMOND AZUA BALAA INSTAGRAM. FANS WA WEMA SEPETU WAMJIA JUU BAADA YA KUTANGAZA HATOMUOA.

Mwanamuziki Diamond Platnumz aka Rais wa Wasafi anaetamba kwa wimbo wake No. 1 haishi drama na warembo wa mujini.

Baada ya hivi  karibui kuonekana na Wema na kuwapa fans wake na wa Wema matumaini kwamba wamerudiana ghafla ameibuka kupitia Global Publishers na kusema “Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond na kuendelea kusema “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.”
 Maneno hayo yamewakera fans wa Wema aka #teamwema kupita kiasi wakiwemo [dougiemasta12, matikibokoyao na wengine wengi] ambao wametiririkia kupitia Instagram na kuonyesha hasira zao kwa kile wanacho dai kwamba Diamond hana adabu na anadhalilisha wanawake especially Wema wao. 

Yaani hi #teamweam wako tayari na standby kumtetea Wema wao katika hali yeyote ile. Na ni kwamba wamejitolea muhanga kumsupport Wema 100%. 

Haya ndo mambo yanayoendelea huko Instagram jamani eee Diamond atajutajee kumkataa Madam Wema... hebu jisomeeee


 Yaani comment ni nyingi sana unaweza ingia instagram ukajisomea. Wadau wana hasira sana na Rais ama kweli Wema yuko juu na hawa ni 100% ride or die loyal fans wa Wema. 

Majangaaaaaaaaaaaa

PICHA YA DIAMOND PLATNUM AKIWA AMEVAA BOKSAAA TU HUKO NIGERIA!!!! TAZAMA HAPA



Leo katika Ukurasa wake wa Facebok msaniii Diamond Platnum ametupia PICHA inayomuonesha akiwa amevalia Boksa huku akiwa kifua wazi akiendelea na harakati za kuaanda chakula akiwa Nchini Nigeria.

MCHINA AJITOSA BONGO MOVIE NA KUKABIDHIWA KIPANDE CHA MAPENZI NA DR CHENI,BOFYA HAPA UJIONEE


 
Dr Cheni baada ya kumtambulisha Steven shabiki wa damu wa club ya Yanga kwenye bongomovie , hivi sasa amemtambulisha mchina kwenye tasnia hiyo. 
Moja ya sentensi anayosema Dr Cheni kwenye scene ambayo mchina amehusika ni hii, “Nyinyi mmekuja kuwekeza kwenye nchi yetu mnawekeza hadi kwa wake zetu”.
Angalia hii scene ambayo mchina kahusika akimchukua mke wa Dr Cheni

Video na Picha mbalimbali toka msibani kwa msanii Nyawana Fundikira aliyefariki juzi kwa ugonjwa wa Malaria..

Marehemu Nyawana Fundikira enzi za uhai wake.




Vilio vimetawala ulipo msiba wa Nyawana Fundikira, maeneo yaGongoni, Tabora mjini wakati waombolezaji walipokuwa  wakiusubiri   mwili wa aliyekuwa mwimbaji na mtangazaji wa kipindi cha taarab ‘Ambaa na Mwambao’ kinachorushwa na Passion Fm, Nyawana Fundikira  ulioanza  kusafirishwa  jana  toka  jijini  Dar es  Salaam  kuja  Tabora  kwa  maziko..

Nyawana alifariki juzi baada ya kusumbuliwa kwa muda mfupi na malaria na upungufu wa damu  ambapo ameacha mjane na watoto wawili.


Video ya  baadhi  waomboleza  waliofika  msibani.

PICHA:DIAMOND NDANI YA STUDIO YA DAVIDO WAKIMALIZIA AUDIO YA NUMBER 1 REMIX


 Siku zote sitoacha kumshukuru Mungu kwa kila hatua
ninayopiga katika safari yangu ya Music,na sitokutendea 
haki nisiporudisha shukrani za dhati 

kwa wewe shabiki yangu wa kweli unae 
endele kunipa sapoti inayonifanya nizdi kukaza 
kukutengenezea mambo mazuri zaidi..hii ikiwa ni ziara
 yangu mhimu kabisa nchini Naija,kwa ajili ya kupika kile
 unachkisubilia kwa hamu,my number one remix na
 mwanangu Davido,hii ilikuwa ni jana usiku
 tukiwa studio,hii ni studio ya Davido iliyopo nyumbani
kwake na kkubwa tulichokuwa tunakifanya ni kumalizia kabisa 
audio kabla ya kuingia mzigoni kushoot kideo.......
Davido nyuma ya screen akifanya mambo yake kwa umakini kabisa.....!!!


 Team yote hii ni kuhakikisha kila kitu 
kinaenda sawa kabisa..Babu tale kwa mbali mwenyewe kamechishaa.....!!!

When Skelewu meet Ngololo..stay tuned..we coming baby..WCB for life huny

DUUH,P-FUNK APATA AJALI YA AJABU AKIWA CHOONI,NI NOMA SANA

Paul Matthysse ‘P-Funk’ akionesha jeraha alilolipata kichwani baada ya kuanguka chooni.
P alidamka alfajiri kwenda msalani kujisevu mambo ya short-call, akiwa huko alishikwa na kizunguzungu cha ghafla kisha akaanguka kama mzigo.
Ajali hiyo, ilimkuta P alfajiri ya Ijumaa iliyopita na kuhusu hilo, mwenyewe alifunguka: “Nilishangaa sana, unajua siku hiyo sikuwa nimekunywa pombe kusema labda nilikuwa nimelewa, nilishangaa tu napatwa na kizunguzungu kisha nikaanguka.”
Chooni alipodondoka P-Funky.
HAIKUWA AJALI NDOGO
Stori kwamba mtu kaanguka chooni, inaweza kuchukuliwa ni ndogo lakini inabainishwa ukubwa wake kutokana na athari ya baadaye.

KWANZA; Kichwa kimepasuka sehemu ya usoni, juu ya macho na alipofikishwa Hospitali ya Aga Khan, alishonwa nyuzi 12.
PILI; Pale chooni, sehemu aliyoangukia, imepasuka. Hii ni kuonesha kuwa kishindo kilikuwa kikubwa. Inafahamika kuwa sinki la choo ni gumu sana kwa sababu hutengenezwa na malighafi imara.

‘P-Funk’ akiwa na jeraha kichwani baada ya kuanguka chooni.
BAADA YA KUANGUKA ALIZIMIA
Japokuwa P a.k.a Majani alikuwa hataki kulizungumzia hili lakini alipobanwa sana na Showbiz alisema: “Baada ya kuanguka pale chooni, nilizimika kabisa. Nikawa sijitambui kwa dakika kadhaa, zinaweza kuwa 10 mpaka 20. Nilipozinduka nilikuwa na maumivu makali.

“Nilipata kampani ya nyumbani, tukaenda Aga Khan ambako nilipewa matibabu. Nilishangaa baada ya kushtukia nimeshonwa nyuzi 12.”
HII INAMAANISHA NINI KWA P?
Hana tatizo lolote la kiafya linaloweza kumlazimisha kuanguka ghafla, zaidi kwa siku hiyo hakuwa amelewa, hii inamaanisha nini?


P anajibu: “Sijui nimepatwa na nini, inabidi nifanye uchunguzi zaidi kubaini tatizo hasa linalonikabili. Ni vizuri kulishughulikia mapema.”
Hata hivyo, wakati P akisema anataka kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na afya yake, Showbiz linazo data kuwa katika siku za karibuni Majani amekuwa mwenye pilika nyingi, akifanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.

Uchunguzi umebaini kuwa prodyuza huyo yupo resi na kazi zake za uprodyuza, akifanya kazi mpaka usiku wa manane, vilevile akidili mstari wa mbele na uanzishwaji wa Chama cha Maprodyuza wa Mapigo ya Muziki Tanzania (TSPA), yeye akiwa ndiye mwenyekiti.
Majani anakiri hilo: “Ni kweli, daha! Mzee katika siku za karibuni nimekuwa bize sana, inawezekana hilo nalo likawa tatizo.”
AAMUA KWENDA MAREKANI
Kuhusu uchunguzi wa afya yake, Majani ambaye ni Mkurugenzi wa Studio ya Bongo Records, alisema: “Japo kwa sasa naendelea vizuri ila nina safari ya Marekani very soon, huko nitafanya checkup ya uhakika, ili kama kuna matatizo ya kichwa au mishipa ya fahamu nipate tiba haraka.”

PETTY MAN AFUNGUKA JUU YA KUVUNJIKA KWA PENZI LAKE YEYE NA KAJALA KISA NI KUBAMBWA NA MDOGO WAKE NA VANESA MDEE

Msikilize hapa chini petty man na kajala wakifunguka juu ya KUVUNJIKA kwa mapenzi yao chanzo kikiwa ni petty man kufumaniwa na mdoo wa Vannesa mdee..
MSIKILIZE HAPO CHINI...

JOHARI APATA BUZI LA KISUNGU KUTOKA KANADA,UWOYA AMPA MANENO MAZITO,SOMA MWENYEWE

 
Mwanadada Irene Uwoya amefunguka na kuandika ya moyoni kuhusu Johari ambaye amemwita "rafiki yake kipenzi'. Kupitia Instgram yake Irene aka #ireneuwoyaonepieceintownameandika maneno yafuatayo " Yan wewe ni rafiki yangu kipenzi...bahati haiji mara mbili...sasa ukifika Canada usinisahau...maisha ndo hayo...wazungu hawataki uswahili tuliaaa." na kuambatanisha na picha ya rafiki yake kipenzi Johari kama inavyo onekana hapo chini. 
Hi ndo habari ya mujini na tunamtakia Johari aka#mukeyamzungutobe kila la kheri. 

Hayo ndo maneno ya Johari

Zifuatazo ni baadhi ya comments za wadau baada ya kupokea habari hii





 




SINTAH AWACHANA WANAWAKE WOTE VING'ANG'ANIZI WA MAPENZI KWA KUWAPA UJUMBE HUU


"This goes out to my ladies ambao ni glues heee kama superglue yaani wanajifanya wenyewe tutabanana hapa hapa, jamani kama mwanamme hakupendi muache maana kuna other potentials out there  unakazana na asie wako ili iweje??

jamani penny hausiki ktk hili maana anaishi na diamond so naombeni kwa heshima mumuache apumzike tuendelee na yetu" Sintah

COLETHA WA BONGO MUVI NAE AACHIA PICHA ZAKE ZA UTUPU MTANDAONI...!!

Picha  za  uchi  zimeendelea  kuwa  fasheni  kwa  wasanii wa  kike  Tanzania  ambao  wengi  wao  wanaamini  kuwa  bila  kujianika  uchi  hawawezi  kuuza  filamu  zao...

Huyu  ni  Coletha Raymond  'Koleta' , mrembo  niliyedhani  anajiheshimu  kumbe  naye  chenga  tupu....
Hii  ni  picha  ya  kiuno  chake  kilichopambwa  shanga  za  kila  rangi  ambayo  imevujishwa  na  yeye  mwenyewe.....Nadhani  hiki  kiuno  kipo  sokoni  kinauzwa.....

HATIMAE JACKLINE WOLPER AFUNGUKA BAADA YA KUBADILI DINI KWA MARA YA PILI


Hatimaye mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.

“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabk zangu stak maswal nawapenda wote…”

Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.

Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa?

DIAMOND AMCHANA WEMA SEPETU AMWAMBIA ASAHAU KUOLEWA NA YEYE ASIJIDANGANYE



RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alifunguka kuwa kwenye maisha yake ya ndoa atakayoingia siku chache zijazo, aliyekuwa mchumba wake wakamwagana na kurejeana hivi karibuni, Wema Sepetu asitegemee kuolewa naye. 
 
Diamond ambaye ni staa wa Bongo Fleva aliyasema hayo mbele ya mwandishi wetu   Novemba 7, mwaka huu jijini Dar kufuatia kuulizwa anamchagua nani wa kumuoa kati ya Wema Sepetu na mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
 
Swali kwa Diamond liliibuka baada ya kuzagaa kwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba yu mbioni kumvisha pete ya uchumba mmoja wa mademu zake.
 
Swali hilo lilimfanya Diamond afunguke kwa kusema kwamba anachokijua yeye na ambacho kipo kwenye mikakati yake, mke wake mtarajiwa ni Penny.
 
“Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond.
 
Akaendelea: “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.”

 
Diamond alikwenda mbele zaidi kwa kumwanika Penny kwamba ana sifa ya kuwa mke kwani ni mvumilivu sana na anaonesha upendo wa dhati kwake.
 
“Kwa maana hii basi hakuna mwanamke mwenye jina  kubwa wala sura nzuri zaidi ya Penny ninayeweza kumwita mke wangu. Najua kila mtu ana namna yake ya kuchagua ampendaye, ndiyo maana utaona watu wanasema hili mara lile, lakini hawajui nafsi yangu inataka mwanamke wa aina gani,” alisema Diamond na kuongeza:
 
Kama kuna demu anayejipa matumaini hayo basi asitegemee hata siku moja kwa sababu kuoa kwangu kutazingatia mke mwema na si bora mke, Penny pekee ndiye mwenye sifa za kuwa mke wangu,” alisema Diamond.

-GPL

WATAZAMAJI WA KIPINDI CHA WEMA SEPETU "In My Shoes" WAMESEMA HAWAKIELEWI KABISA SABABU, ANAONGEA SANA KINGEREZA..

Ilani: Ukitaka kuangalia kipindi cha reality TV cha Wema Sepetu, ‘In My Shoes’ na shule hukwenda, nakushauri ukae na kamusi ya Kiingereza – Kiswahili ili uweze kwenda naye sawa. Hii ni kwasababu, asilimia 50 ya lugha anayoitumia mrembo huyu ni Kiingereza ambayo kwa Watanzania wengi imewapita kushoto. 

 Nimesikia watu wengi mno wakilalamika kuwa matumizi ya Kiingereza kingi kwenye show yake yamewafanya wasikipende kipindi hicho na kunifanya nihoji, nani walengwa hasa wa kipindi chake? Kwa niaba yao ningependa kulifikisha ombi lao kwa Wema kuwa atumie zaidi Kiswahili katika kuongea ili wengi wamwelewe. 

Pamoja na kwamba Wema ndivyo alivyo na hata wakati akihojiwa kwenye TV/RADIO ndivyo huongea, ajizuie katika kipindi chake ili kila mtu amfuatilie.

 

Katika elimu yangu ya uandishi wa habari na utangazaji wa radio/TV nilifundishwa kuwa, wakati wa kuandaa kipindi chochote kile, ni lazima ubainishe, walengwa wa kipindi chako (target audience).
 Kwa kuangalia umaarufu wa Wema Sepetu, hakuna shaka kuwa walengwa wake wakubwa, ni watu wa kawaida kabisa ambao ndio wanunuaji wakubwa wa magazeti ya udaku yaliyolikuza jina lake nchini na wamekuwa wakimpenda sana. 

Kwa namna anavyokiendesha kipindi chake kwa kusimulia matukio yanayooneshwa kwenye kipindi, walengwa ni wale wanaokielewa Kiingereza. Swali ni je, wasomi, raia wa kigeni au watoto wa Masaki, Osterbay na maeneo mengine ya watu wa hali ya juu wanaosoma ama waliosoma kwenye shule za kishua wanakiangalia kipindi hicho? 
Sio kweli na kama wapo basi ni wachache. 

Watu kama hao kwanza hawatumii ving’amuzi vinavyotumika na watu wa hali ya kawaida ambako TV za kibongo zipo. Watu wa maeneo hayo, huangalia DSTV zaidi ambako huko hupenda kuangalia vipindi vya kinyamwezi kama, Keeping Up With the Kardashians, Ice Loves Coco, The Hustle Family ya T.I na Tiny ama The Real Husbands of Hollywood na zingine kibao. 

TV za kibongo huangaliwa kwa nadra na tena labda wakati wa taarifa ya habari saa 2 usiku, na baada hapo huendelea kuangalia TV za nje.
Kipindi cha Wema Sepetu ambacho huoneshwa na runinga ya EATV, kinaangaliwa zaidi na watu wa kawaida ambao kwa bahati mbaya amekuwa akiwatenga kwa kupenda mno kuongea Kiingereza.

 Tanzania bado hatujafika huko na hilo Wema anapaswa aliweke kichwani mwake. Asiletee maisha ya Hollywood kwenye kipindi kinachoangaliwa na Mtanzania wa kawaida.
Kama angekuwa hajui kabisa Kiswahili, basi hilo lingeeleweka. Abadilike..


HUYU NDIYE MSANII WA BONGO FLEVA AMBAYE BABA YAKE ANA UMRI MKUBWA KULIKO WASANII WOTE,ANAMIAKA 107

 
Ukimuona Timbulo akiwa na baba yake, ni rahisi kuwa na imani kuwa huyo ni babu yake kutokana na Uzee wake. Ukweli ni kwamba, baba mzazi wa msanii huyo, ana umri wa miaka 107. Akiongea kwenye kipindi cha Sunrise cha Times FM, leo, Timbulo alisema wazazi wake wamekuwa wakiugua mara kwa mara kutokana na umri wao. Katika hatua nyingine, leo ni siku ya kuzaliwa ya mama yake mzazi, ambaye hata hivyo mama yake huyo hakumbuki mwaka aliozaliwa. Kupitia Instagram, Timbulo ameandika: “Kiukweli upendo wako kwangu ni unreplaceable, cjapata na am sure cwez kupata mwanamke mwenye upendo wa dhati kama ule unaonipa, furaha na nuru hii hugeuka huzuni na giza kila nikifikiri cku utakayoniacha ntakuwa katika hali gani, daaaaah mola nipe la hili swali maana,,,, happy birthday mama yangu mie japo umri na muonekano wako ni kama bibi yangu na hata umri wako hujui ni miaka mingapi ila cwez kuubadili ukweli huu ur my mother, am proud of n I love u so much.” 
Source: Times Fm

DUDU BAYA AELEZEA HASARA YA WADAIWA KUTOPOKEA SIMU ZA WADENI WAO

Ni mapema sana ila inabidi niiweke kama alivyonisimuliwa mwenyewe Dudu Baya a.k.a Mamba.

Ni hivi, Dudu Baya alikuwa na mdeni wake wa siku nyingi ambaye aligeuka kuwa mdeni sugu hivyo alikuwa anamkwepa kwa kuwa alikuwa anamsumbua mara kwa mara.

Siku moja mwimbaji huyo wa ‘Matope’ alikuwa katika safari zake na gari lake, mara ghafla akafika eneo ambalo kulikuwa kumetokea ajali mbaya ya gari na watu wakawa wanafanya kila njia ili waweze kuwaokoa abiria waliokuwa pale, kwa moyo wa huruma Dudu alijiunga nao katika zoezi hilo.

“Nilipofika pale nikaona mke wa yule jamaa yangu ninaemdai akiwa na mtoto wake wanavuja sana damu masikini, ilinisikitisha sana nikaamua kuwasaidia lakini hali yao ilikuwa mbaya sana.

Sasa nikampigia simu yule jamaa mdeni wangu nimwambie kilichotokea huku, jamaa akanichunia hataki kabisa kupokea simu yangu anadhani nataka kumdai lile deni. Nikapiga simu mara nyingi sana lakini hakupokea.” Ameeleza Dudu Baya.

Dudu amesimulia kuwa baada ya kufanya taratibu zote na kuwafikisha hospitalini, bahati mbaya mke na mtoto wakapoteza maisha. Baadae sana, ndio jamaa akapokea simu aliyopigiwa na Dudu kiasi cha kumaliza chaji ya kimeo cha mtoto wa Mwanza, na alipopokea tu alianza na maneno yanayoashiria kuchoshwa na usumbufu wa Dudu.

Eti baada ya familia yake kupoteza maisha ndo anapokea simu halafu ananimaindi kuwa namsumbua wakati ameshaniahidi tarehe ya kunipa..aah, si ndo nikamwambia tukio lenyewe mara akaanza kulia, na kumbe alikuwa kwenye starehe tu anakula bata.” Ameeleza Dudu.

Tutaimalizia story yote wimbo ukishatoka na video kabisa. Duh, hivi nilikuwa sijasema kama ni wimbo wake unaotarajiwa kutoka mwaka huu mwishoni au mwanzo wa mwaka ujao!

Wimbo unaitwa ‘Pokea Simu’ na umepikwa ndani ya Golf Records ilikofanyika 'Matope'.

Dudu ameiambia tovuti hii exclusively kuwa aliamua kufanya wimbo huu kwa mtindo wa story ya majonzi  ili kutoa fundisho kwa watu wenye tabia za kupotezea simu wanazopigiwa kwa hisia zao binafsi.

-Times Fm

BONGO MOVIES WAUKIMBIA MWALIKO WA BUNGE ILI KUSIKILIZA MSWADA WAO

Waigizaji wa filamu nchini wanadaiwa kukwepa mwaliko bungeni walikotakiwa kwenda kutoa muswada wa marekebisho kwenye sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza (1976).
 
Kupitia Twitter muigizaji mrembo, Yobnesh Yussuph maarufu kama Batuli, amesema amefuatilia mjadala huo kupitia TV lakini amesikitishwa kubaini kuwa wapo wasanii walioalikwa lakini hawakwenda bungeni.
 
Yes nimefuatilia bunge ila cha kusikitisha ni wasanii waliopewa mwaliko halafu hawajaudhuria,” aliandika Batulli.
 
Nalaani sana kitendo cha walioalikwa kutokufika bungeni kwenye hoja nyeti kama hii nikiwajua sitawanyamazia,” aliongeza.
 
Naye Lulu alijibu: Hatujichukulii serious ndo mana hatuchukuliwi serious pia..unaachaje kuhudhuria mwaliko unaokuhusu halafu umealikwa? Ndo tatizo la kutokuwa na umoja, haya tutaendelea kulia tu.”

VIDEO MPYA YA BABY MADAHA "SQUEEZE ME TIGHT" YAZUA UTATA

Video ya muziki ya mwanadada Muigizazji na mwanamuziki Baby Madaha “Squeeze me tight” imeanza kuzua utata kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutazamwa na watu wengi sana kwa muda mfupi tangu ilipowekwa hewani kwenye mtandao wa youtube.
Video hiyo ambayo imerekodiwa huko nchini Kenya chini ya Studio za Candy n’ Candy Records ina mahadhi ya kijamaika flani hivi  na pia ukiichunguza kwa umakini zaidi ina vionjo flani vya “kizombie” na pia ipo “too sexy” kitu kilichotafsiriwa kama mambo yale  ile “dini ya wavaa suti” na sababu ya video hii kutazamwa sana. Tuliamua kumtafuta baby Madaha mwenyewe ili ajibu tuhuma hizi lakini kwa bahati mbaya simu yake ya mkononi likuwa inatumika muda wote tuliompigia. Tutaendelea kumtafuta na kuwajulisha atakayosema.
<<BOFYA HAPA KUITAZAMA>>
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari