Like Us On Facebook
Showing posts with label Bongo fleva. Show all posts
Showing posts with label Bongo fleva. Show all posts

“NILIWAHI KULIPWA MIL 10 KWA KUFANYA SHOW MOJA YA MUZIKI MSIFIKIRI DIAMOND NDIO WA KWANZA”….MB DOG

mbdogKama ulifikiri bongo fleva ilianza kulipa mamilioni miaka ya akina Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na wengine, nikimaanisha kuanzia mwaka ya 2010, kwa leo inabidi ubadili mawazo yako.
“Lakini uzuri wakati mimi naanza kufanya, kazi zilifanyika na misingi za ile kazi zilikuwa zimekaa tofauti na watu wanavyosikia. Kwa hiyo uoga hata wa mapromota ulikuwepo wakati wanatusogelea. Kwa hiyo hatukuwa tunalipwa laki tatu viiile.” Mbwana Mohammed aka MB Dog ameiambia tovuti ya Times Fm.

Huenda inawezekana ulikuwa hujui kwa sababu wakongwe waliokuwa wanahit enzi hizo hawakuwa na tabia ya kuweka wazi kiasi wanacholipwa kama wanavyofanya wakali wa bongo flava wa kizazi hiki cha dijiti.

Mkali huyo wa ‘Latifa’ ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa alikuwa anakutana na milioni kadhaa kwenye show zake, na kwamba kiasi kikubwa zaidi alichowahi kulipwa kilikuwa shilingi milioni kumi nchini Burundi.

“Yaani mimi show ya kwanza nimeanza kuifanya nimelipwa milioni tatu, show ya mwisho mimi kuifanya nimelipwa milioni kumi…ambayo ndiyo ilikuwa show ya maajabu yaani…kwa ubongo wangu  nawaza naweza kufanya show tena ya watu wengi kama wale!! Nadhani ilikuwa mwaka 2006.” Amesema MB Dog na kusisitiza, “milioni kumi za kitanzania”Kumbe Bongo Flava ilianza kulipa zamani japo kwa wachache! Na huenda ni kwa sababu tu watu walikuwa hawaweki wazi wanachoingiza.

Hapa tumpigie picha Mr. Nice wa enzi hizo kwa kutumia mfano wa MB Dog.

Kama kweli mambo yalikuwa hivi, inaweza kuwa moja kati ya sababu zilizozaa wazo kati ya wakongwe Juma Nature na Lady Jay Dee kutaka Leo iwe ‘Kama Jana’.

MAJANGA:NIMEVURUGWA YA SNURA MUSHI YAPIGWA MARUFUKU KUONESHWA KWENYE TV.

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limeifungia video ya wimbo ‘Nimevurugwa’ ya mkali wa muziki wa mduara, Snura Mushi ‘Snura’ kwa madai ya kukosa vigezo vya kimaadili kwa jamii.clip_image002Akizungumza hivi karibuni, Snura alisema hajui ni sababu gani iliyofanya kazi yake kufungiwa kupigwa katika vituo vya televisheni.

“Nilipigiwa simu na rafiki zangu na kuambiwa hivyo, lakini mpaka sasa sijui ni kwa sababu gani maana sioni kama nimefanya kitu cha ajabu katika video hiyo na cha kushangaza hata sijaulizwa na yeyote, ila ndiyo hivyo,” alisema.

Snura alisema wakati amesambaza video ya wimbo wake ‘Majanga’, kuna baadhi ya mashabiki walimshangaa ni kwanini hajacheza katika kazi hiyo kitu kilichosababisha video ya wimbo huo kupooza na kutokuwa na mvuto kwa mashabiki wake.

clip_image001“Nilivyopata malalamiko hayo, nikaona nisiwaboe kwa kuendelea kutoa video ambazo sichezi. Katika wimbo uliofuata nikacheza, kumbe nilikuwa naandaa mazingira ya kufungiwa,” alisema.

Snura ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni kutokana na ubora wa kazi zake ambazo zinaliteka soko la muziki nchini.
Na hii ndio kazi ya Msanii huyo ambayo Imefungiwa kuchezwa katika Stasheni za Televisheni hapa nchini


TAZAMA HOTEL YA KIFAHARI ALIYOFIKIA DIAMOND HUKO NCHINI KENYA JIJINI NAIROBI


 Baada ya kuwasili toka airport
 Hotel naitwa EKA,ipo mjini Nairobi

MAMBO HADHARANI,DIAMOND NA WEMA WAKIWA KITANDANI

Mwanamuziki nguli wa miondo ya bongo fleva Diamond na mpenzi wake Wena Sepetu wameamua kupiga picha inayonyesha wakiwa kitandani wamelala pamoja na kuvuta fununuzi zilizokuwa zikizagaakuwa wapo hao sio wapenzi.

ALICHOKISEMA TUNDA MAN KUHUSU YEYE NA ROSE NDAUKA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man, amesema mpenzi wake wa kwanza katika maisha yake ni mwanadada muigizaji wa filamu nchini Rose Ndauka,ambaye waliachana tangu 2006.
Akizungumza na XXL ya Clouds Fm leo Tunda amesema walikuwa wakikutana na mwanadada huyo katika studio moja huko kariakoo hali iliyowapelekea kuanza mahusiano yao yamapenzi.
“Kuna studio moja kariakoo,wanadada walikuwa wanakuja kuchana na yeye anakuja studio anaangalia situation zinavyoenda, kwahiyo kuanzia hapo ndiyo akaanza kunijua nini, nikaenda kwao kila kitu kikawa fresh kila kitu kikawa kinaenda poa ni 2006 kitu kama hicho, yani tumeachana kabla, hamna hata mmoja aliyekuwa star, sasa tumejikuta kila mmoja anafanya issue zake na mimi nafanya issue zangu, mpaka sasa hivi nikikutana nae, nasikia ameolewa peace tu ,kama na shida na yeye kwasababu na yeye sasa hivi anapiga mapigo ya movie na mimi na movie zangu kama vipi namdondosha halafu namlipa”, alisema Tunda

PICHA 8 TATA ZILIZOSABABISHA VIDEO HII YA KIBONGO IFUNGIWE NA BASATA,ZITAZAME HAPA

Ni mara chache kusikia video flani ya bongofleva haichezwi kwenye vituo vya TV kwa sababu ya wamiliki wa vituo hivyo kuona haina maadili hivyo haiwezi kuruhusiwa kuonyeshwa kwa mamilioni ya Watanzania.

Video ya Jux toka mwaka 2013 mwishonimwishoni stori zilikua zinazunguka kwamba hii video imefungiwa kwenye vituo vya TV za bongo sababu picha zinazoonekana ndani yake zimezidisha kuvuka mipaka ya kimaadili. 

Kwa sababu taarifa hizi ‘inadaiwa’ hazikutokea BASATA, wengi walisubiria Jux mwenyewe akirudi Tanzania atasema nini kuhusu hii ishu manake labda ni vituo vya TV vyenyewe ndio vimeamua kuisimamisha bila agilo la BASATA hivyo kama ni TV zenyewe basi vingekua vimemwambia.
 

Anachosema ni hiki >>> ‘Mimi nilikua China ndio B12 akaniambia video yako imefungiwa, nilivyorudi Tanzania BASATA tulipoulizia wakasema hawana hizo taarifa na ni lazima wapitiwe kwanza wao kwenye ishu kama hii… na lazima wakichukua hatua wanatoa taarifa kwa muhusika, wakasema kuna vitu viwili inawezekana kuna michezo imechezwa’
 

Swali : Toka umerudi bongo umeshawahi kuiona hii video ikichezwa kwenye TV?

Jux : ‘hapana ila kuna watu waliniambia wameshawahi kuiona EATV, pia mimi sio mtazamaji wa TV sana’

DOGO YOUNG KILLER AFUNGUKA NA KUSEMA KUWA KWA SASA HAITAJI MPENZI,SOMA ZAIDI UJUE SABABU!

Youngkiller1
Young Killer anasema pamoja na umri wake kumruhusu kuwa mrembo katika maisha yake, bado hafikirii kuanzisha uhusiano na msichana kwa sasa.
“Umri wa kuwa na mpenzi nimeshafikia lakini sasa hivi nafanya mambo yangu halafu baadaye naamini ntakuja kufanya hayo masuala, so sasa hivi najipanga kwanza,” Killer aliiambia Bongo5. “Kusumbuliwa nasumbuliwa sana tu sema kuna msemo mmoja ambao nakuambia wa Fid Q ‘Usiache ulichotaka maishani ghafla tu na kufuata kile ambacho umetamani’. Nimekuja kwaajili ya muziki, nilitegemea utanipa vitu vingi ila sio mademu tu.”
Wakati huo Handsome Boy huyo asiye na matunzo, amesema video ya wimbo wake ‘Mrs Supastaa’ iliyoongozwa na Adam Juma ni moto wa kuotea mbali.
“Ni video kali, naamini katika video zangu zote ile ndio inaweza kuwa video yangu ya kwanza kufanya video kali. Naamini zingine zitakuja ila ile kiukweli kali yaani,” alisema. “Nategemea mashabiki wangu wataipokea vizuri kwasababu ni video nzuri, binafsi nimeridhika nayo, sijawahi kufanya video kama ile.”

MSANII WA BONGO FLEVA FEROUZ ANASWA NA BANGI HUKO SINZA,SOMA ZAIDI UJUE MKASA HUO

Vijana ni nguvu kazi ya taifa, lakini vijana hao hao wanaweza kuwa chanzo cha taifa kutoendelea nakubomoka. Ubomoaji wa taifa huwa kwa namna nyingi ikiwemo uvivu, ufisadi, na kadha wa kadha. Lakini hapa, tuangalie hili la madawa ya kulevya na bangi.

Kila kukicha kuna wasanii wa maigizo na filamu ambao tunasikia wamekamatwa na madawa ya kulevya, "unga" katika jitihada za 'kusaka maisha', wenyewe wanasema kuna ajali kazini. Wasanii hao ambao wengi ni vijana, na pale wanapoonekana kwenye runinga huwa hamasa kwa wadogo zao na jamii kwa ujumla, wakipenda kuwa kama wao.

Na mchana huu, maeneo ya Sinza, kuna taarifa ya mwanamuziki aliyetamba kwenye muziki wa bongo fleva, Ferouz, sanasana kwa wimbo wake wa Starehe, ambao ulikuwa ukionyesha madhara ya UKIMWI na virusi vya UKIMWI. Ferouz anadaiwa kukutwa na bangi, na picha ambazo Gospel Kitaa imezipata eneo la tukio, zinamuonyesha akisindikizwa na maafande kunako mbele ya vyombo husika. Vijana wa Tanzania tuna shida gani? Kama ni ardhi tunayo, kama ni nguvu tunazo, sasa nini shida zaidi? Ipo haja ya Operesheni ambazo Askofu Sylvester Gamanywa ameitisha za Takasika iliyomalizika hivi karibuni, na kisha kupokelewa na Operesheni Milikisha, kuwahusisha pia wasanii wa aina zote, maana wanaonekana kukumbwa na janga hili kwa sana, vinginevyo, vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa watakuwa wakijaa jela za ndani na nje, wakiacha wageni kuja kutawala.

Video: Diamond Platnumz Feat. Davido – Number One ‘Remix’



Tazama hapa video mpya kutoka kwa Diamond Platnumz ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu akiwa amemshirikisha Davido kutoka Nigeria kwenye remix ya ngoma yake ‘My Number One’.

BABY MADAHA AMSHIKA UCHAWI DIAMOND KWA KWENDA KWA MGANGA TANGA.

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘amemshika uchawi’ msanii mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kufuatia madai kuwa, kuna msanii maarufu Bongo alikwenda kwa mganga wa kienyeji Tanga akitaka kumfanyizia ‘madongoloji’ mrembo huyo ili mambo yake yaende ndivyo sivyo.
Baby Joseph Madaha.
ILIKUWAJE KWANI?
Desemba 22, mwaka jana, mtu mmoja aliyedai ni sangoma aishiye Tanga mjini alituma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kupitia simu ya chumba cha habari Global akiomba namba ya Baby Madaha.
Mtu huyo alisema anaomba namba hiyo kwa sababu kuna mtu alikwenda kwake (Tanga) akitaka amfanyizie Baby Madaha mambo yaende kombo.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
NAMBA YA BABY MADAHA YARUSHWA
Baada ya meseji hiyo kusomwa, mtu huyo alirushiwa namba ya Baby Madaha kisha ujumbe wake ukafowadiwa kwa mrembo huyo.
BABY MADAHA AENDA HEWANI
Dakika tano baada ya Madaha kufowadiwa ujumbe huo, alikwenda hewani kwa simu iliyomtumia ujumbe ambapo bila salamu alisema:
“Huyo atakuwa Diamond tu, hakuna mwingine. Mimi nimeaga  kwetu, hata siku moja Diamond asifikirie kuwa mambo yangu yanaweza kuniendea kombo.
“Kwa chochote alichonifanyia akae akijua lazima kimrudie hii namba nyingine kabisa, hajui uzito wangu. Ni heri asinifuatilie, kitakachomtokea asubiri tu kukiona, atajuta milele,”alisema msanii huyo.
Alisema: “Tatizo kubwa la Bongo, wasanii hatupendani. Unapokwazana na mtu kidogo tu, basi atakufanyia ubaya mambo yako yayumbe.
“Sababu kubwa ya Diamond kuniendea kwa ‘mtaalam’ ni lile bifu lilozuka baina yangu na yake,” alisema Madaha.
DIAMOND ASAKWA
Baada ya madai ya Baby Madaha, paparazi wetu alimsaka Diamond kwa njia ya simu ili ajibu tuhuma zinazomkabili lakini hakupokea simu.
Ilibidi Amani limtumie ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na kumweleza kila kitu, lakini pia supastaa huyo hakujibu kitu.
Hata hivyo, kufuatia bifu la Diamond na Baby Madaha  kumekuwa na pongezi kwenye mitandao ya kijamii ikimpe 5 Diamond kwamba ukimya wake wa kutojibizana na Madaha ni ukomavu.
Wengi wamesema anachokifanya Diamond ndiyo ustaa na si Baby Madaha ambaye kila kukicha anaweweseka kwa jina la Diamond.
TUJIKUMBUSHE
Awali, wasanii hao waliingia kwenye bifu zito baada ya Baby Madaha kumtupia kashfa nzito Diamond akidai kuwa ni fuska, umaarufu alionao hauendani na ubora wa kazi zake.
Katika madai hayo, Diamond alisema  hawezi kijibizana na mwanadada huyo kutokana na ‘levo’ yake kuwa juu.


ANGALIA PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA RICH MAVOKO PALE MAISHA CLUB






Msanii Rich Mavoko usiku wa kumkia leo alizindua rasmi video yake ya wimbo wa 'Roho Yangu', katika ukumbi wa Maisha Club iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam,katika uzinduzi huo Rich Mavoko alisindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Jux Vuitton,Barnaba,Dully Sykes,Shetta,Mr Blue na wengineo.












































MENINA "SIWEZI KUTOA RUSHWA YA NGONO ILI NITOKE KIMUZIKI"

MWANAMUZIKI aliyeibukia kwenye Shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Menina Atick amesema licha ya kusikia kuwepo kwa baadhi ya wanaume wenye nafasi kwenye ‘game’ la muziki ambao huomba rushwa ya ngono kwa wasanii wa kike ili wawatoe, yeye atakomaa na anaamini atasimama.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Menina ambaye sasa anasumbua na wimbo wake



wa Shaghala Baghala alisema anachoamini ni kwamba msanii wa kike mwenye kipaji hata asipotoa rushwa ya ngono, nafasi ya kung’ara anayo, hivyo yeye atakuwa mfano kwa wengine.
“Mimi…nitoe rushwa ya ngono ili nitoke, mh…kwa kweli hiyo haiwezekani, najiamini na sitakubali kuutumia mwili wangu kwa kugawa penzi ili nisimame kwenye muziki, kwanza nitatembea na wangapi,” alihoji msanii huyo.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari