Like Us On Facebook
Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

MWANAFUNZI WA CHUO AJINYONGA BAADA YA KUFELI MITIHANI

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Ualimu  cha Winneba, nchini Ghana, amejiua kwa kujinyonga mara baada ya jina lake kubandikwa kwenye ubao wa matangazo (notice board) kuwa amefeli masomo matatu.



Jina la mwanafunzi huyo limehifadhiwa kwa sasa, ila inasemwa kuwa sababu ya kujinyoga kwake ni kutokana na kufeli masomo hayo matatu ambapo kungepelekea kufutwa kwake shule hapo.

Sababu hasa ya kifo chake haijajulikana moja kwa moja ila inaaminika ilitokana na hofu ya kutimuliwa chuoni hapo kutokana na kufeli mitihani mitatu.

Wilson Dabuo, ambaye ni muwakilishi wa wanafunzi kwenye baraza la chuo hicho, alieleza kupitia Joy News kwamba chuo hicho kina sheria ya kutimua wanafunzi wanaofeli masomo matatu kwenye mitihani yao.

MHADHIRI WA CBE AFUKUZWA KAZI KWA KUJIHUSISHA NA NGONO NA WANAFUNZI

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), tawi la Dar esSalaam, kimemfukuza kazi mhadhiri wa chuo hicho anayedaiwa kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa maadili ikiwamo kufanya ngono. Mhadhiri huyo ambaye jina halikutajwa alinaswa nakamera za kisasa za kurekodi matukio za CCTV zilizofungwa kwenye vyumba vya madarasa ili kudhibiti nidhamu, miongoni mwa wanafunzi na wahadhiri.Kamera hizo zimefungwa kwenye vyumba vya madarasa 20 ili kudhibiti vitendo vya ngono baina ya walimu na wanafunzi, wizi wa mitihani na matendo mengine yanayovunja sheria.

Hayo yalibainishwa jana jijini na mkuu wa chuo hicho, Profesa Emanuel Mjema (pichani), alipokuwa akizungumza na wanahabari wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene.

Profesa Mjema, alisema, walifikia maamuzi ya kuweka kamera hizo za kisasa ndani ya madarasa Aprili mwaka jana baada ya kujiridhisha na taarifa za kuwapo matukio ya ukosefu wa maadili miongoni mwa wahadhiri ikiwa ni pamoja na kutoa alama za juu kwa baadhi ya wanafunzi wa kike baada ya vitendo vya ngono. 
“Nilipoingia chuoni hapa Januari mwaka jana, nilisikia kuwa kuna baadhi ya wahadhiri wamekosa maadili, wanatoa alama za juu kwa wanafunzi wa kike kwa masharti hata kama hawajafaulu kwa kiwango hicho. Nikaona vyema tuweke vifaa hivyo ili kudhibiti vitendo hivyo,” alifafanua Profesa Mjema.
Alieleza kuwa baada ya kuweka kamera hizo 20 kwa kila darasa kuwa na kamera moja, walifanikiwa kumnasa mwalimu mmoja kwa kitendo cha kukiuka maadili yake ya kazi na kumfukuza kazi.
Alisema kuwa, kamera hizo pia, zinasaidia kuwadhibiti wanafunzi wenye tabia ya kuiba mitihani, kwani mikakati iliyopo hata wakufunzi na wanafunzi hawajui anayetunga mitihani ili mradi ipo ndani ya silabasi ya chuo. 
Kamera hizo zinadaiwa kuwa na uwezo wa kumvuta karibu mwanafunzi aliyeko darasani na kujua anachokiandika, pia mhadhiri iwapo anachokifundisha ni cha ukweli au anadanganya kwa hiyo zinatumiwa wakati wote kwenye vipindi na mitihani.
Alisema, chuo kimeajiri walinzi kwa ajili ya kuwadhibiti wanafunzi ambao wanavaa nguo ambazo hazina maadili mazuri na pia hukagua vitambulisho wanapofika getini, lengo likiwa ni kukifanya chuo hicho kubakia katika heshima yake.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Mbene, alipongeza jitihada hizo zilizofanywa na chuo hicho, huku akikemea vikali tabia inayofanywa na baadhi ya wahadhiri hao, akiongeza kuwa, ni lazima mwanafunzi apewe madaraja ya matokeo ya mitihani kutokana na ufaulu na uwezo wake. 
Pia, aliahidi kushughulikia suala la uvamizi wa eneo la chuo hicho pamoja na maombi ya kuongezewa madarasa ikiwa ni pamoja na kupewa majengo ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula cha Taifa (NFRA).

SOURCE: NIPASHE

KUTANA NA MREMBO MWANACHUO MWENYE KALIO LA AJA AMBAYE, WATU WANAHISI ANALITUMIA KUFAHURU MITIHANI


Anaitwa faith anasoma chuo kikuu cha mt kenya ambaye unaambiwa kila akikatisha korido za chuo hicho lazima watu waache wanachokifanya kwa jinsi alivyojaliwa huko nyuma.... na unaambiwa midume kibao wakiwemo mawaziri wanajigonga kila kukicha kwa binti huyo... hata hvyo inasemekana faith ni moto wa kuotea mbali linapokuja swala la peper jambo ambalo linawaacha watu na maswali kama kweli na akili zake au kalio linafanya kazi yake.








Aibu! Shule ya Msingi Jijini Dar, Wanafunzi wakaa chini huku waalimu wakitumia Khanga kama Majamvi.

Shule ya Msingi Mtambani  iliyoko Kinondoni jijini  Dar es Saalam, haina  samani  hali inayosababisha wanafunzi kukaa chini, wakati walimu wanalazimika kutandaza khanga wanazokalia chini ya miti.
 
“Shule hii ina upungufu wa madawati,  nusu ya wanafunzi wanakaa chini, hatuna ofisi za kutosha za  walimu 
shule 
wale wasio na nafasi  wanakaa chini ya miti”, alisema Mwalimu Mkuu Emmanuel Munisi.
 
Aliongeza kuwa tatizo hilo linawalazimisha wengine kutandika khanga chini ya miti  ili kufanya kazi kwa sababu ya  ukosefu wa meza za kufanyia kazi na kwamba mvua inaponyesha wanalazimika kujikusanya pamoja na wanafunzi madarasani, alisema Munisi.
 
Shule ya Mtambani iko taabani wakati serikali ilipata chenji ya rada ya shilingi bilioni 43 ambayo ilielezwa kuwa pamoja na kununua vitabu mashuleni pia itawezesha upatikanaji wa madawati.
 
Serikali ya Uingereza ilirudisha fedha hizo kuanzia mwaka jana na kwamba jukumu la kununua vifaa hivyo liliachwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambayo inasimamia shule za serikali za msingi na sekondari. 
Shule hiyo ina walimu 41 na wanafunzi 1,830 inakabiliwa na  uhaba wa madawati,  viti na meza  za walimu kwa mujibu wa   Munisi. Aliiambia  NIPASHE Jumamosi kuwa  mazingira mabovu ya shule hiyo ni pamoja na upungufu wa vyoo, ukosefu wa sakafu madarasani badala yake madarasa yana  mahandaki na vumbi kila wakati. Akifafanua, alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa na wanafunzi 77 na ofisi moja ndongo kwa ajili ya walimu. Hata hivyo, kwa  sasa ina wanafunzi 1,830  wa kike 917, wavulana 913 na walimu 41.
 
Alisema hakuna maji safi ya kunywa na wanafunzi wengi wanakabiliwa na matatizo ya njaa yanayosababisha kudondoka mara kwa mara.
 
Alieleza kuwa wastani wa kuanguka  ni kati ya watoto watano na zaidi ambao hutibiwa kwa kuwekewa drip za kuongeza maji na sukari  mwilini. Madaktari wanasema tatizo ni ukosefu wa chakula na nguvu mwilini kwa hiyo wanapotundikiwa drip wanapona.
 
Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Mtambani,  Steven Ngonye, akizungumzia tatizo hilo alisema litashughulikiwa pamoja na upatikanaji wa maji na ukarabati wa shule hiyo.
 
Naye Diwani wa Kata ya Mtambani  Maji Safi Sharifu, alisema serikali inalitambua tatizo hilo na imetenga bajeti ya Sh. milioni 108 kwa ajili ya madawati na ukarabati wa vyumba vya madarasa na kwamba hadi sasa madawati 50 yameshapelekwa shuleni hapo.
 
Akifafanua zaidi alisema kuna mpango wa kuongeza vyumba vya madarasa mawili pamoja na kufikisha maji safi kazi itakayogharimu Sh. milioni 20.
CHANZO: NIPASHE
 

KWA MAMBO HAYA YA HOSTEL ZA VYUO VIKUU TUTAPONA KWELI?

Sisi ni wanafunzi tunaishi kwenye hostel moja mchanganyiko wasichana na wavulana sasa kuna binti mmoja ambaye mara kadhaa huwa nakutananae kwenye korido nikiwa naenda kujisaidia, nilishawahi kukutana nae akiwa anatoka chooni na mimi naingia nakumbuka siku hiyo alikuwa amevaa kipensi kifupi sana na sidiria tu.
Kama wiki tena iliyopita mimi nilipofungua tu mlango wa chumbani kwangu kuelekea chooni alitoka na yeye akiwa amevaa kanga moja tu sidhani kama alikuwa amevaa hata chupi, sasa ya juzi ndio ilikuwa kali, nilipofungua tu mlango wangu majira ya kama saa sita hivi usiku nilikutana nae uso kwa uso akiwa amevaa nguo laini yenye kumuonyesha hadi upande wa pili. kwa kweli nili shuhudia kila kona ya umbo lake,Nilipo muona nilishtuka hadi yeye mwenyewe pia akanishangaa, akaniuliza vipi Dav? nilimjibu aisee wewe ni mrembo daah. nikamuambia hebu nisubiri kidogo hapo hapo, niliiingia ndani nikatoka na simu nilimuomba kumpiga picha , huwezi amini yule binti alikubali, nikamtwanga picha, yani wala hakuona kama ni big deal, akaniuliza umemaliza. nikamuambia basi inatosha.huku yeye akiwa anatabasamu. Aliingia ndani , kwakweli aliniacha nimepigwa na butwaa. sikuweza tena kwenda chooni hata mkojo wenyewe pia ulikata nilirudi tu ndani nikalala. daaahh Hostel hizi jamani yani kama hujapitia maisha ya chuo kwakweli umepitwa sana..!! 

MWANAFUNZI IFM AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI, SOMA KILICHOTOKEA HAPA

Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha kupumzikia kilichopo chuoni hapo bila mwili wake kuwa najeraha lolote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea saa 11:30 juzi jioni katika chumba namba 118 jengo namba D kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi akiwamwaka wa pili.
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala nawanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili yamasomo.
“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla hajajiunga na chuohiki, kwa hapa chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea mara kwa mara,” alisema Mushi.
Aliongeza kuwa mara baada ya kupewa funguo alikwenda kupumzika katika chumba hicho na baadaye alikutwa amefariki huku mwili wake ukiwa umelala kitandani.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa katika kituo cha polisi napolisi walifika katika chumba hicho na kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Mushi alisema wamewasiliana na wazazi wake waliopo wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha mwili huo zitafanyika leo.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu, Peter Alphonce, aliliambia NIPASHE kuwa alikuwa na marehemu siku moja kabla ya kifo chake wakicheza mpira na walimaliza kucheza vizuri na kuagana kuelekea hosteli.
“Nilikuwa naye jana (juzi) tukicheza mpira, hadi saa kumi tulipomaliza aliniaga na kuelekea katika MachavaHostel ndiko anakolala,” alisema Alphonce.
@NIPASHE.

Diamond awapeleka shule ya kimataifa watoto walioshinda kucheza "Ngololo Style"



Hatimaye uwezo na utundu wa kucheza wimbo wa Diamond Platinumz ‘My Number One’ hususani mtindo wa Ngololo umewapa nafasi ya kusoma shule ya kimataifa watoto walioshinda katika shindano lililoendeshwa na mkali huyo katika tamasha lake la Christamas.
 
Kupitia Instagram, Diamond ameshare picha zinazoonesha akiwakabidhi watoto hao katika shule ya kimataifa ‘East Africa International School’ iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam.
 
“Kama unakumbukumbu nzuri wakati nafanya tamasha langu la Christmass na Ngololo niliuliza mtoto atakae cheza vizuri Ngololo na kushinda nimpe zawadi gani?...na wengi walisema Nimuendeleze kielimu.... Hawa ndio washindi wetu walioshinda siku ile, ambao siku ya leo niliwapeleka Rasmi katika Shule ya East Africa International School iliyopo Mikocheni Dar es salaam ili waanze Masomo yao...Niliona ni vyema kama mtoto yupo shule ya kawaida nimuhamishe international school ili niweze kumsaidia elimu bora zaidi...Niushkuru pia uongozi Mzima na wanafunzi wa Shule ya East Africa International School kwa kuwapokea vizuri.” Aliandika Diamond. 
 
Kwa upande mwingine, baraka zinazidi kumiminika kwa video ya  wimbo wa Diamond ‘My Number One Remix’ aliyofanya na Davido wa Naija ambayo inazidi kupata mafanikio na tayari imeanza kuchezwa katika vituo vikubwa vya runinga duniani vikiwemo TRACE, na Sound City ya Naija.

MITANDAO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WANAOJIUZA MTANDAONI YAGUNDULIKA HAPA BONGO..!! SOMA SOMA ZAIDI

PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa matumizi mabaya ya teknolojia hasa mitandao ya kijamii yamechochea ongezeko la uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya na zaidi biashara ya ukahaba vyuoni. 
Mitandao ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa namna inavyoweza kuwaunganisha watu kutokana na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi Jumapili limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga mitandao ya kibishara, kidini, michezo, burudani, vichekesho na mengine ambayo mara nyingi huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na kuona kinachoendelea ndani.
Mbali na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi yanayoendesha biashara ya ukahaba, yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Uchunguzi umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kutumia mitandao wameweka picha na namba kwa ajili ya mawasiliano kwa mteja atakayekubaliana na bei waliyoweka.
Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia katika mitandao ya Facebook, Twitter, BBM, Instagram, utabaini kuwapo kwa makundi yaliyoundwa kutengeneza mitandao ya ngono, ambayo huweka pia namba za simu za wahusika, zikiambatana na picha, ambao ikiwa utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza ukapiga simu husika kuzungumza naye kwa kufanya mapatano kabla ya kukubaliana.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao hiyo.
Baadhi ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na kujitangaza kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha

-Mwananchi


SHULE HII INA MWALIMU MMOJA VIDUDU MPAKA LA SABA...LAKINI YAFAULISHA WANAFUNZI WOTE!!!



Katika hali isiyo ya kawaida, shule moja wilayani Bagamoyo imekutwa ikiwa na mwalimu mmoja tu anayefundisha wanafunzi kuanzia chekechea hadi darasa la saba, wote wakifundishwa katika chumba kimoja kwa kutumia ubao mmoja. 

Hata hivyo, katika matokeo ya Darasa la Saba Mwaka huu, wanafunzi wote 12 walifaulu kuingia kidato cha kwanza.

Shule hiyo ya msingi Machala, iliyokuwa na idadi ya wanafunzi 198 na imejengwa kwa majani kuanzia chini hadi kwenye paa.

Mwandishi wa habari hizi aliyetembelea shule hiyo, alimkuta mwalimu huyo akiwafundisha wanafunzi hao wa madarasa tofauti wakiwa kwenye chumba kimoja, huku ubao wa kufundishia ukiwa umechorwa mistari mitatu kutenganisha masomo ya chekechea hadi darasa la pili, mstari mwingine darasa la tatu hadi la tano na mwingine darasa la sita hadi la saba.


Mwalimu huyo, Christopher Rukutu, aliliambia NIPASHE Jumamosi kuwa shule hiyo hutumia kivuli cha mti kama ofisi.

Shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Mihunga Kata ya Miono, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, ilianzishwa na serikali tangu mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 12 ambao wamemaliza darasa la saba, mwaka huu na kubahatika kufaulu wote.

Kwa mujibu wa mwalimu Rukutu, wanafunzi wote waliofaulu walipata alama za A na B isipokuwa mmoja aliyepata alama C. 

Pamoja na kuwa katika mazingira magumu, shule hiyo kiwilaya ilishika nafasi ya sita na kimkoa nafasi ya 20.

Alisema shule hiyo haina vitabu vya kiada wala vya kufundishia na amekuwa akiazima kutoka shule za jirani.

“Ninafundisha kwa akili za kuzaliwa sina kitabu cha mtaala wa elimu, nguvu zangu zote nilimalizia kwa darasa la saba ili wajue kusoma, kuandika na kuhesabu.

Kwa mwaka mzima sijafundisha darasa la nne nina wasiwasi matokeo yao hayatakuwa mazuri kwa sababu niko peke yangu," alisema kwa masikitiko.

Alifafanua kuwa tangu shule hiyo ianzishwe, serikali ilikuwa imewapanga walimu wawili tu, ambao kutokana na mazingira kuwa magumu waliripoti bila kuingia darasani na kuaga baada ya kuonyesha vyeti vya hospitali vinavyonyesha kuwa afya zao haziwezi kustahimili mazingira magumu.

Aliilalamikia serikali kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya kwa kuisahau shule hiyo bila kuipa msaada wowote.

Mbali na kukosa msaada, shule hiyo pia inatumia tundu moja tu la choo kwa wanafunzi wa kike na kiume na kusababisha wengi wao kujisaidia vichakani.Alisema kutokana na hali hiyo, wanafunzi wengi hushambuliwa na ugonjwa wa kichocho.

Aliiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuwapangia wanafunzi wake 12 waliofaulu katika shule yake ya Machari kwenye shule za sekondari zenye mahitaji muhimu ili kuwapunguzia mateso wanafunzi hao.

Alisema wanafunzi wake hawajawahi kuona vitabu vya kujisomea na huduma muhimu za kiafya.
-NIPASHE

Serikali yatangaza majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza


 
Jumla ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule za Serikali.
 

Hata hivyo, kwa mujibu wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, wanafunzi 16,484 watashindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa wakati muafaka kutokana na uchache wa madarasa.
 

Akitangaza idadi ya wanafunzi walichoguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini amesema kutokana na tatizo la upungufu wa madarasa ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa hadi ifikapo machi mwaka mwakani.
 

Aidha, Sagini anaeleza takwimu za wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.
 

Amesema idadi ya ufaulu kwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana na hivyo kusababisha kuwepo cha changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 412.
 

Jumla ya wanafunzi 867,983 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 455,896 sawa na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48

JE WEWE NI KILAZA DARASANI?KAMA JIBU NI NDIYO BOFYA HAPA KUPATA UFAFANUZI WA TATIZO LAKO




KCSE candidates at Lions High School in Kisumu begin their English test. Photo credit: Standard Digital News. Mwanafunzi ambaye anataka kupata alama za juu katika mtihani wake lazima awe mtu wa kujiandaa kila siku kwa kutumia dondoo zifuatazo ili kujihakikishia uwezo wa kufaulu na kuepukana na dhana ya kuishi kwa kutegemea bahati.
 KWANZA: Kama nilivyosema hapo juu jambo la kwanza ni kuzingatia muda, si vema kukurupuka na kukimbizana nao na kujinyima usingizi wakati ratiba ya mtihani ilikuwa inafahamika na muhusika alikuwa na uwezo wa kujiandaa taratibu kuelekea kwenye siku ya kutahiniwa kwake.
 PILI: Jindae mwenyewe kwa kutafuta na kufanya mitihani iliyopita, huku ukinakili maswali ambayo watunzi wamekuwa wakiyarudia rudia kila mwaka.
 Njia hii itakuwezesha kujiandaa kwa kuzingatia shabaha na mahitaji halisi ya maswali yatokayo mara nyingi kwenye mitihani.  Hakikisha unapata mitihani ya nyuma ya ngazi uliyopo isiyopungua kumi au zaidi na uifanye huku ukihakikisha hakuna swali hata moja ambalo linakushinda.
 Pamoja na ukweli kwamba ubahatishaji wa vitu si njia sahihi sana, lakini umeonekana kuwasaidia wale ambao ubahatishaji wao huambatana na umakini, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuwa na tabia ya kubahatisha maswali ambayo anadhani mwalimu wake anaweza kuyatoa kutoka kwenye daftari lake na hivyo kujiandaa.
 Ubaharishaji huu, lazima uambane na kile nilichosema awali, yaani  kuwa na kumbukumbu ya mitihani iliyopita. Wanasema watalaamu kuwa ulimwengu una tabia ya kurudia matukio, hivyo hata kwenye maswali kuna tabia hii ya kujirudia rudia.

 TATU: Orodhesha maeneo yote ambayo huyaelewi kwenye mtihani hiyo ya nyuma na uyafanyie mazoezi kwa kupata ushauri kwa waalimu wako. Kama kuna mada ambazo hujazielewa kwenye daftari lako hakikisha muda uliojiwekea utatosha kuzielewa.
 NNE: Hakikisha unajizoeza kufanya mitihani ya majaribio  mara kwa mara, ambayo utaifanya kwa kuzingatia muda na masharti yote ambayo hutolewa siku ya kufanya mtihani halisi. Haifai mwanafunzi kukimbia majaribio yanayotolewa darasani na mwalimu wake, kwani hayo ndiyo yatamuwezesha kufahamu kama amekamilika kwa kutahiniwa au bado kuna eneo linamtatiza.
  TANO: Hakikisha kuwa kumbukumbu zako kichwani zinaongezeka kadiri unavyojifunza, usiwe mtu wa kusahau sahau uliyojifunza na ikiwezekana eneo ambalo unaonekana kulisahau ndilo ulipe kipaumbele cha kujikumbusha, ikibidi hata kila siku.
 SITA: Angalia kwa makini alama zako za mitihani ya majaribio, ikiwa unapata alama za chini ujue kuna mahali panahitaji nguvu za ziada, shauriana na mwalimu wako maeneo yote unayokosa au yanayokusumbua kabla ya siku ya mtihani.
 SABA: Ili mwanafunzi awe na uhakika wa kufanya vema mtihani wake anatakiwa kuzingatia dondoo zote zilizotolewa kwenye kipengele cha kuimarisha kumbukumbu kichwani, ambazo zimo ndani ya kitabu hiki.
   NANE: Wakati mwingine ni vema ukausikiliza mwili, si vema kuulazimisha kusoma hata kama unaona kuna udhaifu, baadhi ya wanafunzi hukesha wiki mbili mfululizo wakisoma, matokeo yake mwili na akili huchoka na kushindwa kupokea masomo vizuri. Muda wa kupumzika unahitajika.
 TISA: Kabla mwanafunzi hajaingia katika chumba cha mtihani anatakiwa kujiamini kwa kushinda hofu. Eneo hili ni muhimu sana kwani kuna wanafunzi hufeli si kwa sababu hawakujiandaa, bali hukumbwa na hofu muda mfupi kabla ya kuanza mtihani. Hivyo ni muhimu mwanafunzi akaandaliwa kisaikolojia na waalimu pamoja na wazazi wake jinsi atakavyoweza kufanya mtihani bila hofu.
 KUMI: Imani ni hitimisho la mafanikio ya mwanafunzi, haifai kuingia katika chumba cha mtihani ukiwa na mawazo hasi. Kinachotakiwa ni ari ya ushindi au kwa lugha nyingine ni mawazo chanya. “LAZIMA NIFAULU MTIHANI HUU” Imani hii inaweza kujengwa na mtu kupitia kujiamini mwenyewe au kuamini kwa msaada wa nguvu za imani yake ya dini.

Mwalimu wa Shule ya Msingi atuhumiwa kwa kosa la kuwatia mimba Madenti wake wawili kwa Nyakati tofauti...!

MWALIMU mmoja wa Shule ya Msingi Sintali (jina tunalo) anatuhumiwa kwa kuwatia mimba wanafunzi wawili mmoja akiwa wa shule anayofundisha yeye na mwingine wa Shule ya Sekondari Sintali hali iliowafanya wanafunzi hao kukatisha masomo. Tukio hilo limetokea Katika Kijiji cha Sintali, Wilaya ya Nkasi na baada ya taarifa kuenea kijijini hapo mwalimu huyo alitoroka kituo chake cha kazi na kukimbilia pasipo julikana. Akizungumzia tukio hilo Ofisa Elimu Msingi, Wilaya ya Nkasi, Bw. Misana Kwangura alisema mwalimu huyo anadaiwa kufanya kosa hilo tangu mwezi Agosti, 2013 na baada ya kuanza kufuatiliwa alikimbia kituo chake cha kazi. Alisema baada ya kutoroka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ulilazimika kusitisha mshahara wake jambo ambalo lilimlazimu ajilete mwenyewe ndipo alipokamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kosa linalomkabili. Hata hivyo Kwangura alisema wanafunzi hao mmoja wa darasa la saba na mwingine wa kidato cha pili wamekana mwalimu huyo kuwatia mimba na kudai wametiwa mimba na watu wasiojulikana ambao walikuja kijijini hapo kununua mazao. Mwalimu huyo amekana kuhusika na kitendo hicho. Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limemuachia mwalimu huyo baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani. “…Uongozi wa Kijiji pamoja na wa shule wanaamini kuwa yeye (mwalimu huyo) ndiye aliyewatia mimba lakini wao wanakataa, sisi tunaamini wanamtetea ili asichukuliwe hatua za kisheria lakini sisi hatujakubali tunasubiri wanafunzi hao wajifungue kasha tutatumia DNA kupima tujue ukweli…tayari mmoja amejifungua tunamsubiri mwingine,” alisema Ofisa Elimu, Kwangura. Alisema vipimo vitapelekwa kwa Mkemia wa Serikali ili hatuhakikishie bila utata. Alisema tayari wamemkamata mwalimu mwingine wa Shule ya Msingi Itindi ambaye naye amemtia mimba mwanafunzi wa darasa la saba wa shule anayofundisha tangu mwezi wa nane mwaka huu. Huyu naye baada ya kumtia mimba alipotea lakini baada ya kusitisha mshahara amejileta mwenyewe na tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi Nkasi kwa kosa alilolifanya. tuajabu huyo alikutoroka. Akizungumzia kwa ujumla matukio ya wanafunzi wa Shule ya Msingi kutiwa ujauzito, Ofisa Elimu huyo alisema matukio ya mimba kwa wanafunzi shule za msingi yanapungua kwa sasa kwani tangu Januari hadi Novemba 2013 jumla ya wanafunzi 9 wametiwa ujauzito na kukatizwa masomo yao, idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo wanafunzi 11 walitiwa mimba.
Ofisa Elimu Msingi, Wilaya ya Nkasi, Bw. Misana Kwangura akizungumza na Thehabari.
Aidha aliongeza kuwa kwa mwaka 2011 jumla ya wanafunzi 16 wa shule za msingi walitiwa mimba na kukatizwa masomo yao. “…Kimsingi naweza kusema matukio haya kwa sasa yanapungua ukilinganisha na hapo nyuma, na hii inatokana na elimu ambayo tunaitoa kwa kuzunguka kwenye shule mbalimbali kwa kutumia ofisi ya Ofisa Elimu Sayansi Kimu,” alisema Kwangura

KUMBE MADENTI WENGINE ‘WANAJILENGESHA’ KWA MATICHA


KWA takribani wiki tatu sasa tumekuwa tukijadili kuhusu tabia ya baadhi ya walimu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi, hasa wa kiume. Nashukuru kwamba nimepata mrejesho mzuri kutoka kwenu.
Lakini kuna mwalimu mmoja msomaji mzuri wa safu hii, yeye ni msichana anayefanya kazi mikoani. Alinitumia ujumbe mmoja ambao ulinivutia sana, nikabadilishana naye maneno mawili matatu na kujikuta nimepata kitu ambacho ni lazima tushirikiane pia kujadili.
Kwanza alinipongeza kwa makala ile, lakini baadaye akaniambia kuwa mara nyingi wanafunzi wa kike ndiyo wanaoanza kujitongozesha kwa walimu ambao wanachokifanya wao ni kama kumalizia tu.
Aliniambia kwamba wanafunzi wa kike wakiwa mbele ya walimu wa kiume hujishaua, wakati mwingine hata kupandisha juu sketi zao, kurembua macho na viuchokozi vingine ili mradi tu walimu wausome mchezo.
“Sasa anko kwa hawa walimu wenyewe vijana unategemea nini? Lakini ngoja tuwaite sisi walimu wa kike, wanakuja wamebetua midomo, wanaonyesha ishara ya dharau na vitu kama hivyo, mimi kwa kweli siwalaumu walimu, mara nyingi wanalazimishwa,” alisema mwalimu huyo.
Katika kukolezea na kuniaminisha anachokisema, alinipa mchapo mmoja unaomhusu yeye mwenyewe kiasi cha kuniacha hoi kabisa.

Aliniambia kuwa hapo awali, aliishi kinyumba na mwalimu mwenzake na walijaaliwa kupata mtoto mmoja. Kumbe jamaa kimya kimya akawa anajipigia kabinti kamoja ka darasa la sita hapo shule waliyokuwa wakifundisha. Dada akashtukia, ikawa bonge la msala. Huku na huku soo likafika kwa wazazi wa mtoto ambao nao hawakukubali, ikibidi sheria ichukue mkondo wake!
Polisi wakaipeleka mahakamani, kesi ikaanza kunguruma. Katikati ya shughuli, mtoto wa kike akatoa mpya. Akasimama mbele ya hakimu na wazazi wake, akawaambia kuwa yeye anampenda mwalimu, akawataka waachane na ile kesi na kama wataendelea nayo, atajiua!

Mchezo ukaishia hapo na dada yangu akaamua kumwachia mwanafunzi wake aendelee na mzigo, yeye akashusha manyanga!
Huo ni mfano ulio hai, lakini wanafunzi huko mashuleni wanaelewa zaidi. Ninakumbuka katika moja ya matoleo yaliyopita nilizungumzia kuhusu hili.

Wasichana wa aina hii mashuleni wako wa aina nyingi, lakini sana utakuta ni wale ambao hawana kitu kichwani au ambako kiasili ni wahuni. Mungu bwana wa ajabu sana, hawezi kuwanyima vyote wanadamu. Wasichana wasio na akili darasani hujaaliwa uzuri wa sura na umbo.
Nao hutumia uzuri wao kujiegemeza kwa walimu kwa mategemeo ya kusaidiwa mambo wanayoamini hawayawezi. Si rahisi kukuta mwanafunzi mwenye akili zake darasani na anayejua kitu alichokifuata shule, akambania pua mwalimu wake kwa lengo la kumteka kimapenzi.
Na kuna hawa wanafunzi vicheche wa asili, mtaani ana mabwana, shuleni anao, kwa ndugu zake anao ili mradi tu kila anapokwenda lazima apate mtu. Hawa ndiyo wanaoingia katika lile kundi la kujitongozesha, ingawa hata hivyo, wakati mwingine, mwanafunzi anaweza kumpenda mwalimu kama binadamu ye yote anavyoweza kufanya.
Labda niwaase maanko zangu kwamba pamoja na kuwa uhusiano wa kimapenzi haupendezi wakati ukiwa bado shule, hasa hizi za msingi na sekondari, ni vibaya zaidi kushiriki tendo hilo ovu na mwalimu wako.

Ni lazima tukubali kwamba kwa kufanya hivyo, moja kwa moja ni kwamba hakutakuwa na heshima baina yenu na hapa ndipo mkazo wa masomo kwa mwanafunzi unapowekwa kando. Mwalimu badala ya kumsisitiza mwanafunzi wake kujisomea, atataka muda ambao alistahili kuwa akijisomea, autumie kwa mambo yao ya mapenzi.
Nirudie tena wito wangu ambao nimekuwa nikiutoa kila mara. Tutumie vizuri muda wetu wa shule, tukiuchezea, tutakuja kushtuka muda umeenda. Haya mambo yote mnayotaka kuyafanya sasa, yapo, mtayakuta na kuyaacha.

-GPL

HUU NI UKATILI:DENTI ABAKWA, APIGWA MIMBA NA KUTOROKA KWAO...MSHITAKIWA AMFUKUZA KAMA MBWA AKIWA NA MTOTO MCHANGA

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya Bujingwa, iliyopo Nyakato Mwanza (jina linahifadhiwa), mkazi wa Mabatini jijini Mwanza, alibakwa, kutoroshwa nyumbani kwao na hatimaye kupewa mimba na mtu aliyefahamika kwa jina la Roja (27).

Denti huyo akiwa na mwanaye.
 
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Mwanza akiwa hoi kimaisha baada ya kufukuzwa kwa mwanaume huyo, denti huyo ambaye sasa ana mtoto mwenye umri wa miezi saba, alisema baada ya kutoroshwa kwao, mwanaume huyo alimpa mateso mengi, ikiwa ni pamoja na vipigo vya mara kwa mara.
Mtuhumiwa aitwaye Roja.

Akisimulia kwa masikitiko, alidai kuwa Roja alimpa mimba akiwa bado mwanafunzi wa  kidato cha tatu mwaka 2012 na kumshawishi atoroke nyumbani kwao ili akaishi naye.
Alidai kuwa, usiku wa Desemba 9 mwaka huu, Roja akiwa na baba, alifika nyumbani na kumtaka aondoke mara moja huku akimtupia virago vyake nje ya nyumba bila kujali kuwa na kitoto kichanga.
Hati ya makubalianao.

“Siku hiyo alifika nyumbani na kunitaka niondoke , nilipokataa akaanza kunipiga na chuma kichwani na kunikaba shingoni bila kujali nilikuwa na mtoto mgongoni. Nilipoona hali inazidi kuwa mbaya nikaamua kuondoka zangu na kuja hapa ili nisaidiwe,” alisema mwanafunzi huyo ambaye wakati huo alikuwa katika ofisi za taasisi inayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu iitwayo Farijika.
Katika kuchimba ukweli wa madai hayo, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ilizungumza na wazazi wa denti huyo ambao  kwa muda tofauti walikiri taarifa za mtoto wao kutoroshwa na kubakwa hadi kuzalishwa na mwanaume huyo.
PF3.
Kuhusu manyanyaso anayopata mtoto wao, walisema anastahili  matibabu (PF3) ambapo vipimo vilionesha kuwa kweli alifanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa alikuwa na majeraha ya ndani kwa ndani.
Baada ya kuthibitisha hilo, Roja aliitwa mbele ya watetea haki hao na kukiri kumnyanyasa mkewe lakini akiahidi kutomnyanyasa tena kabla ya kusaini hati ya makubaliano iliyoshuhudiwa na mashahidi watatu, hati ambayo kama akiivunja atafikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo kubaka na shambulio la mwili.
Mama na mtoto wanaonyanyaswa na kijana Roja.

CREDIT: GPL

MAJANGA:Upepo mkali waezua paa la shule ya msingi Luganga

1 892ea
Wanafunzi wa shule ya msingi Luganga kata ya Ilolompya Tarafa ya Pawaga Mkoa wa Iringa, wakiangalia sehemu ya paa la chumba cha darasa lililo ezuliwa na upepo mkali...
2 e40f4
Nyumba ya Mwalimu
4 10483
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Luganga wakicheza nje ya Darasa lililo ezuliwa
5 ff967
Wanafunzi Shule ya msingi Luganga wakiendelea na Masomo ndani ya Darasa lililo ezuliwa na Upepo mkali ,(Picha na Said Ng'amilo.)

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AKUTWA SHULENI AKIWA MTUPU AKIWA KATIKA USINGIZI MZITO.....UCHAWI WAHUSISHWA KWA YEYE KUJIKUTA MTUPU

clip_image002
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina. Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye, Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam. Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi) huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito. Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha  ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana  na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao. Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi alisema  walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama nyumba zao  kwa muda na badala yake kwenda kukesha  kwenye ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee. Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo. Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wa kumhamisha  mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao. Hili ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule  akiwa uchi wa mnyama.

WALIMU WAZICHAPA KAVUKAVU OFISINI WAKIGOMBEA PESA

 
Afisa Elimu msingi wilaya ya  Sengerema Bw,Juma Mwajombe alipokuwa akimvua madaraka Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Luhama kwa kosa la kutotimiza majukumu yake.
 ****************

AFISA Elimu wa Shule za Msingi Sengerema Mkoani Mwanza, Bw Juma Mwajombe amemvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Luhama iliyoko kata ya Katwe kwa kushidwa kutekeleza majukumu yake.
 
Amesema kuwa amefikia maamuzi hayo kutokana na mwalimu huyo kushindwa kusimamia vema majukumu yake na kutokusimamia maadili ya walimu wake wanapokuwa kazini.
 
Bw, Mwajombe amemtaja aliye mvua madaraka hayo kuwa ni Mwalimu  Maila Majula baada ya kuchochea ugomvi kati ya mwalimu Emanuel  Joely  na Mwalimu Alfonsia Ndalahwa uliosababisha walimu hao kutwangana makonde ofisini  kwa kile kinachodaiwa kuwa walituhumiana kula fedha za ujenzi wa kisima cha shule hiyo.
 
Aidha amesema kuwa Mwalimu Mkuu anapaswa kusimamia vema majukumu yake na kushauri walimu kuacha migogoro isiyo ya lazima na kuzingatia maadili ya kazi na siyo kukuza migogoro isiyo ya lazima na kusababisha walimu kutokuheshimiana sehemu za kazi.

UKATILI:Mtoto avunjwa kidole na mwalimu wake baada ya kuingia darasani na nywele ndefu huko Mbeya.



Wiki ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto ikiwa imeanza kuadhimishwa duniani Novemba 25 mwaka huu bado vitendo hivyo vimezidi kushamiri Mkoani Mbeya ambapo mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Aiport Kata ya Iyela jijini Jacline Staniely [9] ameumizwa mkono wake wa kushoto.

Jacline akiongea kwa ridhaa ya mama yake amesema alipigwa kwa kutumia ubao na mwalimu wa shule hiyo Novemba 19 mwaka huu na mwalimu Kanyika kwa kosa la kuwa na nywele ndefu.
 
Mwanafunzi huyo amedai kuwa siku ya tukio alipigwa vibaya na kumsababishia maumivu makali ambapo siku hiyo mama yake alikuwa safarini Nairobi Kenya hivyo hakupata matibabu ambapo alilazimika kumwambia mwalimu jirani[Bibi]ambaye alimpeleka hospitali kutibiwa.
 
Picha  ya  X ray ikionesha  kidole kilichovunjika :
 
Hata hivyo Jackline amesema kuwa kutokana na maumivu makali alilazimika kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne bila kupata matibabu ya kutosha.

Baada ya kurejea kutoka safari mama yake mzazi aitwae Rehema Adamson Ndeje[28] mkazi wa Block T jijini Mbeya amesema baada ya maumivu ya mwanae usiku ilimlazimu kwenda shuleni ili kujua kulikoni,ndipo alipoonana na mwalimu Kanyika baada ya kukutanishwa na Mwalimu mkuu.

Mama Jackine amesema hicho ni kipigo cha tatu kukubwa kwa mwanae kupigwa na mwalimu huyo ambapo alionesha makovu yaliyodaiwa yalitokana na vipigo vya mwalimu huyo miguuni akidai majeraha hayo yalidumu kwa miezi mitatu.

Hata hivyo Rehema aliamua kwenda Polisi Mwanjelwa kutoa taarifa za tukio na kila alipoitwa mwalimu huyo hakutokea ndipo jalada likapelekwa kituo kikuu cha kati ambapo mwalimu alikamatwa na mhanga kupewa PF 3 kwa ajili ya matibabu ambapo alipigwa picha na kuonekana moja ya kidole cha kati cha kushoto kimeathirika kutokana na kupigwa kwa kutumia ubao.
PF3

Mzazi huyo amesema hana nia mbaya na mwalimu Kanyika lakini kitendo cha kumwadhibu mwanae mara kwa mara ndicho kimemtia shaka hata kuamua kutoa taarifa Polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
 
Mwandishi wa habari hii alipofika shuleni ili kujua mustakabali wa suala hili, mwalimu alimtoa nje  akidai yeye ana majukumu mengine .

Mwandishi alimtafuta mmoja wa wanaharakati wa kijinsia ambaye alikiri kupokea lalamiko hilo ingawa alijibu kwa mkato kuwa mtoto huyo kaumia kidogo tu na ni usanii mtoto huyo kufungwa POP na kwamba bado PF3 haijajazwa kitu hivyo hawezi kuzungumzia lolote.

Kumekuwa na malamiko mengi katika Dawati hilo kutokana na matukio kutochunguzwa kwa wakati , hali inayotoa mwanya kwa vitendo hivyo kuibuka mara kwa mara na wahalifu kutoroka mkono wa sheria .
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya ameahidi kulifuatilia suala hilo na ikibainika mtuhumiwea atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Na Ezekiel Kamanga 
Mbeya yetu

MWANAFUNZI AUAWA NA MPENZI WAKE WAKATI AKISUBIRI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE JIJINI DAR....CHANZO CHA MAUAJI NI WIVU WA MAPENZI..


Mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne mwaka huu, Sharifa Abdallah (18) ameuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na mbavuni chumbani kwa mvulana aliyedai  kuwa mpenzi wake maeneo ya Kimara Golani, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 8:30 mchana na baadaye mvulana huyo aliyetambuliwa na Polisi kwa jina la Abdul Alpha (22) kujisalimisha katika kituo cha Polisi cha Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo, akidai alikuwa akitaka kutoroka lakini aliona amefanya dhambi kubwa.

Akizungumza na mwandishi jana, mama mkubwa wa marehemu, Mwajuma Khamis alisema Sharifa alimaliza kidato cha nne katika sekondari ya Luguruni na alikuwa akisubiri matokeo.

Alisema juzi waliporejea kutoka kazini hawakumkuta nyumbani, waliulizia kwa ndugu kutokana na kwamba hakuwa na tabia ya kutoka nyumbani, lakini hawakufanikiwa kumpata hadi jioni ndipo polisi walipowataarifu kupatikana kwa mwili wake.

Alisema mwili wa marehemu ulikutwa chumbani kwa kijana huyo karibu na nyumbani kwao ukiwa na majeraha mwilini, lakini hawakujua kama mtoto wao ana mwanaume, wanatarajia kumzika kesho saa saba mchana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema polisi walipata taarifa za tukio hilo katika kituo cha Ubungo na kwenda katika chumba cha kijana huyo kilichokuwa kimefungwa kwa ndani na kukuta mwili wa msichana huyo ukiwa umejeruhiwa.

Alisema baada ya kumhoji mtuhumiwa, alisema alifanya hivyo kutokana na wivu wa kimapenzi, kwani alikuwa na uhusiano na msichana huyo lakini wazazi wa msichana hawakutaka amwoe, hivyo kumtaarifu kuwa amepata mchumba mwingine.

Alipoulizwa kwa nini hakutoa taarifa katika kituo cha Polisi Kimara alikofanyia mauaji, alisema aliogopa watu wa maeneo yale wangempiga na kumwua, kwa kitendo hicho.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Tumbi, Kibaha, huku kijana huyo akishikiliwa na Polisi.

-Zero99

JE, UNATAMANI KUACHA KUANGALIA PICHA ZA NGONO NA UNASHINDWA..?? SOMA HAPA ILI UPATE NJIA ZA KUKUSAIDIA KUACHA KABISA..

 
Kuacha kutazama picha za ngono kunahitaji nidhamu, 
ujasiri na imani ndani yake.
Kwani bado madhara yake huwa hayaonekani mbele ya macho ya mtumiaji.
Je, kuangalia picha za ngono kuna madhara gani?

1.MAHUSIANO:

Si tu katika mahusiano yako na mchumba wako bali hata kwa marafiki,
 familia, wanafunzi wenzako, na hata wafanyakazi wenzako.


Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha wazi kuwa watu wanaoangalia picha za ngono,
 wana msongo mkubwa wa mawazo na kujihisi wapweke kuliko wasioangalia.

2.UBONGO:

Sehemu ya ubongo inaathirika na mihemko bandia inayotengenezwa  na anayeangalia,
 na hivyo kusababisha unalemaa na kushindwa kabisa kujibu mihemko halisi.
Picha hizi zitakufanya ujitenge na jamii yako, kwani kila muda utataka uwe peke, 
yako eneo unalokaa ili upate wasaa wa kuangalia vizuri kwa kujinafasi.
Maisha yanakosa shauku ikiwa ubongo utazoeshwa kujibu mihemko ya bandia
 kwa kiwango cha juu.

3.KUFURAHIA MATUKIO:

Unaweza ukajikuta kila kitu kwako kinachukiza kuangalia au kujihusisha nacho,
hata ukiangalia kitu kingine utaona bora kiishe ili uangalie picha zako.
Na hii ni hatari kubwa sana kwani utaufanya ubongo ukose taarifa za ziada na zile za ngono ndio zitatawala.

Fuata hatua zifuatazo kujiachisha na tabia hii:

1.AMUA KUACHA LEO USISEME KESHO:

Mara kwa mara watu ambao wamebobea katika uangaliaji wa picha hizi,
 wanapomaliza kuangalia hujipa ahadi kwamba kesho tu nitaacha kuangalia.
Baadaye wanajikuta kesho haifiki,
 kwani kila siku ina kesho yake.
Ukitaka kweli kuacha amua muda uliopo sasa usipange kesho ambayo hujaifikia.

2.USIKAE KARIBU NA MAZINGIRA YA PICHA HIZO:

Ukitaka kujisaidia kuondokana na tatizo hili, hakikisha una kaa mazingira
 ambayo hayajatawaliwa 
na picha za ngono.
Kama unatumia kompyuta, simu au 
hata iPad ambayo 
ndani yake umehifadhi picha hizo zifute sasa,
na ikiwa unatumuia 
DVD au CD ziharibu usikae nazo ndani,
 na hata katika 
historia ya anwani ya 
mitandao uliyotembelea,
 kama zipo zifute kabisa kwani ukiziona utarudi kule kule.

3.USIHESABU SIKU AMBAZO HUJAANGALIA:

Mara nyingi kama umebobea kuangalia huwa haipiti siku bila 
kutupia jicho picha hizo.
Na kuna muda mwingine unabanwa na shughuli nyingi kukupelekea 
kufikisha siku kadhaa hujaangalia,
sasa usikae chini kuanza 
kuhesabu siku ambazo hujaangalia utajikuta unajipa kibali cha 
kutaka kuziangalia haraka iwezekanavyo.

4.USIKAE MAZINGIRA YA PEKE YAKO:

Mara nyingi kama uliwahi kuangalia picha za ngono na ukajikuta uko 
mazingira ya peke yako,
 ya ama unaangalia tamthilia au 
kusoma kitabu chochote kitakachokuwa na habari ya masuala ya watu 
kujamiana itakukumbusha kamchezo kako.
Usichague pia kuangalia
 peke yako picha ziliwekwa
 alama ya miaka 18 zitakuchochea urudi ulipotoka.

5.EPUKA MAZUNGUMZO MACHAFU NA MARAFIKI:

Mara nyingi tunapokaa na marafiki zako ambao wanapenda kuhadithia 
masuala ya ngono tu watakuchochea.
Maana kuna wengine ni mafundi wa kuhadithia hizo vitu,
 kana kwamba wao ndiyo watengenezaji,
sasa unapoona wanaanzisha hizo habari kama huwezi kuwasimamisha basi ni heri ujitenge nao.

6.EPUKA HISIA CHOCHEZI ZA NDANI:

Siri kubwa katika hizi picha zinampa hisia nzuri mtazamaji,
 na kuona hakuna chenye thamani yoyote muda huo.
Kwa hiyo epuka hisia za hasira, 
upweke, na huzuni kwani 
zitakufanya uone eneo pekee la kwenda kujipumzisha ni kuangalia picha hizo.

7.FUTA FIKRA POTOFU:

Achana na fikra potofu za mtaani kuwa kuangalia picha za
 ngono ni kujifurahisha nafsi na hazina madhara.
Lakini kiuhalisia madhara yanayoambatana na tukio lake utayaona baadaye.
Kuna wengine watakwambia kuwa usipoangalia hizo picha utakuwa mshamba na hauendi na wakati.

8.USIJISEMESHE KUWA HUWEZI KUACHA:

Unapokuwa unaangalia hizi picha mara nyingi akili yako inajizoesha,
 na kuona ni utaratibu 
wake wa kila siku.
Kwa hiyo moyoni utakuwa unajisemesha kuwa kuacha kitendo hiki 
hautaweza kamwe,
kitu ambacho kitakufanya uwe dhaifu wa kujitawala.

9.ACHA KUJIKUMBUSHA PICHA ULIZOANGALIA:

Mara nyingi unapokuwa mazingira fulani ya kuwaza mambo mbali mbali, 
mawazo ya picha ulizoangalia ukiyatanguliza kwanza utajifanya 
uwe na shauku ya kwenda kuangalia upya.
ukiona kuna kazi unafanya kazi
 katika kompyuta au umeshika kifaa chochote chenye uwezo wa kukuonesha 
picha hizo ni heri ukizime 
kwa muda huo halafu fikiria kitu kingine kwa haraka.

LINAPOKUJA SUALA LA KUACHA TABIA,
 HII NI VYEMA UKAFIKIRIA ZAIDI KAMA KUNA FAIDA YOYOTE UNAYOPATA.
 NA JE KUNA SIKU UTAKAYOKAA CHINI KUJIVUNIA ULICHOPATA KWA KUANGALIA HIZI PICHA? 

CHUKUA LEO HATUA YA KUACHA ILI KUEPUKA MADHARA YATAKAYOKUJA KUTOKEA SIKU ZIJAZO.



WEKA NIA, UNAWEZA.

 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari