Like Us On Facebook
Showing posts with label Wema Sepetu. Show all posts
Showing posts with label Wema Sepetu. Show all posts

MKOROGO WAMFANYA WEMA SEPETU AJUTE KUJICHUBUA

MISS Tanzania 2006 aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amevunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa, mkorogo umemtia adabu na anajuta kuutumia  mwilini mwake.
Wema Sepetu.
Akizungumza juzi na paparazi wetu ofisini kwake jijini Dar, Wema alisema  kuwa baada ya kwenda kliniki nchini China na kupata matatibu ya ngozi yake ambayo sasa imerudi kama mwanzo amejifunza kitu.
NI KITU GANI HICHO?
Wema alisema amejifunza kuwa, binadamu anatakiwa kuishi alivyoumbwa na Mungu, mambo ya rangi ya mwili hayana nafasi katika uwezo wa binadamu.

ALIAMINI USTAA NI LAZIMA UWE MWEUPE PEE!
Wema akatoa mpya zaidi aliposema kuwa, uamuzi wake wa kutumia mkorogo ili awe mweupe kama mzungu (yeye ni mweupe) ulitokana na kuamini kwamba, weupe na ustaa ni mambo yanayokwenda pamoja, kumbe sivyo.
“Niliamini weupe sana na ustaa ni Kulwa na Doto, lakini sivyo. Ngozi yangu ya awali ni nzuri, imerudi kama ilivyokuwa, namshukuru sana Mungu,” alisema Wema.

AWAONYA MASTAA WENZAKE
Akiendelea kuzungumza na paparazi, Wema alitoa ujumbe kwa mastaa wenzake wanaotumia mkorogo kuwa, hakuna faida yoyote, kwa sababu mkorogo unaondoa vitamini yote mwilini.
“Daktari kule China aliniambia kuwa licha ya kupoteza vitamini nyingi mwilini, pia mkorogo unakufanya mtu uzeeke kabla ya  wakati. Mimi nawaomba kabisa mastaa wenzangu wajiepushe na hii kitu inaitwa mkorogo,” alisema Wema.

ALICHOJIFUNZA KUHUSU KUJIKOBOA
Kujikoboa ni kuwa mweupe sana, lakini Wema anasema alichojifunza kuhusu hali hiyo ni kwamba, ni rahisi sana kuiondoa ngozi ya awali kwa mkorogo lakini inapofika ngozi ya awali inatakiwa kurudi inagharimu sana.
“Ukitaka kuona maajabu sasa, ngozi yako mwenyewe kuibadilisha si kazi na wala si gharama lakini ukitaka irudi kama mwanzo ni lazima ugharimike sana, mimi sitaki tena jamani,” alisema Wema.

PENZI LA DIAMOND NA PENY LADAIWA KUVUNJIKA,WEMA SEPETU ATAJWA KUWA CHANZO



NDIYO habari ya ‘mujini’ kwa sasa, kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, mtangazaji wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wamemwagana.....

KAMA UTANI, WEMA ATAJWA
Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, ‘mtonyaji’ wetu ambaye ni mtu wa karibu wa wawili hao aliliambia gazeti la Risasi  kuwa chanzo cha Diamond na Penny kuingia kwenye listi ya ‘zilipendwa’ kilianza kama utani.
 
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona mwenye thamani mbele ya mwenzake huku Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo.

“Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.
 
“Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
 
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?” alihoji ‘kikulacho’ huyo ambaye ni rafiki wa Diamond.

RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa za awali kutoka kwa rafiki huyo, timu ya Risasi kwa kuwatumia ‘wahangaikaji’ wake maalum, iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi hizo.
 
Watu kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo rais wake ni Diamond walihojiwa ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa sasa Diamond na Penny imebaki stori!

 SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake makini juu ya uvumi huo, hivi karibuni Diamond alionekana ‘singo’ kwenye pati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya ‘dada wa mjini’, Halima Haroun ‘ Halima Kimwana’ ambayo aliiandaa Diamond.
 
Minong’ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa vitendo vya ufuska.
 
“Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.

“Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana kwa sababu kwenye pati zote huwa wanakuwa pamoja tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi,” alisikika mmoja wa waalikwa katika sherehe hiyo.
 
Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na mwandishi  wetu na kujibu kwa kifupi: “Naumwa. Halafu si lazima nije kwani kila mtu ana ratiba zake.”
 
PENNY KIZIMBANI TENA
Baada ya kukamilisha udadisi huo kupitia kwa watu wao wa karibu, Risasi  lilianza na Penny kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini alionekana kuwa ‘mzito’ kwa kutoingia ndani kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
 
“Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo, lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
 
Mwandishi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini.”

DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya kiganjani, hakupokea licha ya kupigiwa mara kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji yenye maelezo yote, hakujibu.

MAMA DIAMOND
Ili kujiridhisha na madai hayo, waandishi wetu walimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye alisema hajui na hana taarifa hizo.

NDUGU WA KARIBU SANA
Baada ya mama Diamond, paparazi wetu alimpigia simu ndugu wa karibu sana na Diamond, sikiliza:
 
Mwandishi: “Kumbe Diamond na Penny wamemwagana we huniambii. Sasa wifi yako mpya ni nani?”
Ndugu: “Aka! Sikwambii. Kwanza mi nipo mbali, sipo Dar.

WADAU WANAJUA
Haikuishia hapo, timu yetu ilizungumza na wadau mbalimbali ambao walionesha kusikitika huku baadhi yao wakisema walitabiri tangu awali.
 
“Duh! Penny ameachia ngazi mwenyewe. Sisi tulijua hawawezi kufika mbali, maana penzi lenyewe lilikuwa na mbwembwe nyingi,” alisema mwanamke mmoja anayejua kila kitu.

TUJIKUMBUSHE
Siku za hivi karibuni Diamond alifanya mahojiano kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii ambapo moja kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na mpango wa kuoa ambapo alisema kuwa hana mpango huo kwa sasa na hatarajii kumuoa yeyote kati ya wanawake wanaotajwa kwa sana midomoni mwa watu (akiwemo Penny).
 
Source: Gazeti la Risasi / Gpl

WEMA SEPETU SASA HALI YAKE NI MBAYA KIUCHUMI,YULE BOSI ALIYEKUWA AKIMMWAGIAA MIFEDHA AFIRISIKA

Wema Isaac Sepetu.

NI kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha? Kama ni kweli, basi ile jeuri ya fedha ya Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia hufanya vyema kwenye gemu la sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu inadaiwa imefikia nchani,
Baadhi ya magari anayomiliki Wema.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hali ya kifedha ya staa huyo si nzuri kiasi kwamba kwa sasa amekuwa mtu wa kushinda ndani kwa kuwa hana mpunga unaomuwezesha kwenda kujirusha kama zamani.
SABABU NI NINI HASA?
Chanzo kilidai kwamba, binadamu aliyekuwa akimmwagia manoti staa huyo aliyetajwa kwa jina moja la Clement ambaye ni mwajiriwa wa Ikulu jijini Dar, yu hoi kwa kipato baada ya kunyofolewa kwenye kitengo kilichokuwa na uwezeshaji mwingi wa fedha.
Wema akiwa ofisini kwake.
Inadaiwa kuwa, baada ya Clement ambaye ni mume wa mtu, kuondolewa kwenye kitengo hicho amepelekwa sehemu nyingine ambayo mchana kutwa ni kupiga miayo mpaka muda wa kutoka kazini.
MKONO WA MKEWE WATAJWA
Katika madai hayo, inasemekana mke wa Clement (jina tunalo) ana mkono wa kile kilichompata mumewe, kuondolewa kwenye kitengo chenye ulaji na pia amekuwa akiwawinda wawili hao ili awafanyie fumanizi kwa sababu Clement ni mumewe wa ndoa.
Wema akiwa ndani ya nyumba aliyodai yake.
KILICHOTOKEA SASA
Chanzo kikaendelea: “Baada ya kuondolewa kwenye sehemu yenye fedha na kutupwa kwenye ukame, jamaa akaanza kupata tabu kwani fedha alizokuwa akimpa Wema zamani zikawa hazipo.
“Hilo likamwathiri na Wema mwenyewe kwani ile jeuri mliyokuwa mnamuona nayo akiifanya kwa rungu la fedha, mara sherehe, mara kumlipia Kajala (Masanja) makahamani (Kisutu), mara kwenda baa na wapambe imekatika ghafla.
“Siku hizi Wema ndani na yeye, yeye na ndani. Naamini hata mkienda kwake muda huu (juzi Jumatatu saa 5 asubuhi) mtamkuta.”

INADAIWA AMEUZA MAGARI MAWILI
Habari zaidi kutoka chanzo hicho, hali ilipozidi kubana sana, Wema aliamua kuuza magari mawili kati ya matatu anayomiliki ili apate fedha za kuendelea kujikimu katika maisha ya kila siku.
Magari hayo mawili yanasemekana ni Toyota Mark II GX 110 na Toyota Harrier na kubakiwa na Audi Q7.

YALIYOMPATA CLEMENT
Habari zinazidi kudai kwamba hali ikazidi kuwa mbaya kwa Clement kiasi kwamba alijikuta akikabwa koo na benki moja ya jijini Dar es Salaam ambayo aliiomba mkopo wa Shilingi mil. 120 akitumia hati ya nyumba ambayo pia si yake.
Benki hiyo ilipozidi kumbana, mkewe (sasa wametengana) ambaye naye anadaiwa kuwa ‘mzuri’ kwenye fedha alikwenda kulipa fedha hizo benki ili nyumba ya watu isinadiwe na benki hiyo iliyokuwa haitaki mambo ya utani kwenye marejesho.
Madai mengine ambayo hayajathibitishwa yanasema kuwa, mtikisiko huo wa kifedha kwa Clement umesababisha awe ‘choka mbaya’ kiasi cha sasa kuanza kupiga mizinga kwa rafiki zake.

WEMA ASAKWA ASEME UKWELI WAKE
Baada ya kupokea ishu hiyo, Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka Wema ili aseme lolote kuhusiana na tuhuma hizo.
Saa 4:32 Wema alipigiwa simu yake ya mkononi ambayo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa hata pale iliporudiwa tena na tena.
Baada ya jitihada hizo kugonga mwamba, gazeti hili liliamua kumwendea hewani meneja wake Martin Kadinda ambaye naye hakupokea simu licha ya kupigiwa zaidi ya mara tatu.
Risasi Mchanganyiko halikukata tamaa, kwani ni haki ya msingi kwa Wema kuongelea suala hilo. Likampigia msaidizi wake wa karibu anayeitwa Pat Man, yeye alipokea, akaulizwa kuhusu bosi wake huyo, akasema:
“Wema anaumwa (hakutaja ugonjwa), ametoka hospitali sasa hivi  (hakusema hospitali gani) yuko nyumbani.”
Mapaparazi wetu wakafunga safari kutoka Bamaga – Mwenge, Dar yalipo Makao Makuu ya Nyumba ya Magazeti Pendwa Bongo, Global Publishers hadi nyumbani kwa Wema - Makumbusho (lakini ni Kijitonyama).
Getini alikutwa mlinzi mahiri kwa mwonekano ambapo alipoombwa kumwita Wema au kumwambia kuna waandishi wa Global wapo nje, alisema:
“Mh! Kwa kweli si rahisi kutoka, amelala anaumwa... alikwenda hospitali amerudi muda si mrefu.”
Alipochombezwa kwa maneno ya ‘kisiasa’ kwamba awaambie wasaidizi wake wa ndani wakamwamshe, alikataa akisema litazuka timbwili ambalo yeye hakuwa tayari kuliona.
“Bosi akilala huwa hapendi kuamshwa, hasa kama hayuko sawa. Watu wanaomwamsha ni wale wenye ahadi naye,” alisema mlinzi huyo.

WEMA ATUMIWA MESEJI
Baada ya kuondoka nyumbani kwa Wema, Risasi Mchanganyiko lilimtumia ujumbe mfupi (SMS) ‘mreeefu’ wenye madai yote na ikaonesha ‘delivered’ kwenye simu ya Wema, lakini pia haikujibiwa.

TUNARUDI KWA CLEMENT  
Simu yake haikuwa ikipatikana hewani alipopigiwa ili na yeye apewe nafasi ya kusema lolote kuhusu sakata hilo.

MKE WA CLEMENT AVUNJA UKIMYA
Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka kwa simu ya mkononi mke wa Clement ambapo alipopokea na kusomewa mashitaka ya mumewe na nafasi yake kama shahidi muhimu alikiri hali ya jamaa kuwa tete kimfuko.
“Kuhusu hilo la nyumba ni kweli ilikuwa inadaiwa na benki (aliitaja jina) na walitaka kuinadi ili wapate fedha zao, lakini nikaingilia kati ili kulinda heshima ya familia.
“Unajua ile nyumba kuna mtu alituuzia, kwa hiyo Clement alitoa kiasi cha fedha lakini hakumalizia na akatumia hati ya nyumba kwenda kuombea huo mkopo. Kwa sababu benki walikuja juu nilitafuta mtu akainunua, kiasi cha fedha nikammalizia aliyetuuzia na kulipa benki,” alisema mwanamke huyo.

KUHUSU KUMFANYIA FITINA MUME AKAHAMISHWA KITENGO
Huyu hapa mke wa Clement: “Hilo si kweli bwana. Kwanza mimi ndiyo nilimfikisha pale alipofika. Sasa mtu nimuinue mwenyewe nitamfanyiaje fitina?
“Kwanza mimi siko naye siku hizi. Nilipoona anachukua magari ya nyumbani na kuyapeleka huko kwa nani sijui (Wema) nikaamua kukaa pembeni na kunyamaza kimya.
“Kama ni mabalaa anayapata hukohuko aliko, nisisingiziwe mimi kwa lolote lile.”
KUHUSU KUMWANDALIA FUMANIZI WEMA
“Aaa wapi! Nimwandalie fumanizi la nini? Yeye ana maisha yake mengine mimi niko na mambo yangu, muda huo sina kabisa, yaani niko bize sana,” alisema mwanamke huyo huku akidai muda huo alikuwa akidraivu.

PRODYUZA WA WEMA ALIJUA HILI?
Wiki mbili zilizopita, gazeti damu moja na hili, Ijumaa Wikienda liliandika katika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; MAGARI YA WEMA YAGEUZWA GESTI.
Katika habari hiyo, Wema alidaiwa kumtimua kazi prodyuza wake katika Kampuni ya Endless Fame, Rashid Mohammed ‘Chid Classic’ kwa sababu ya kumtuhumu kufanya ufuska kwenye magari yake maeneo ya Ufukwe wa Coco, Dar.
Siku chache mbele, prodyuza huyo alifunguka katika gazeti lingine pendwa ndani ya mjengo, Amani kuwa, Wema ‘amechoka’ siku hizi, halipi mishahara wafanyakazi wake na alitaka yeye awe kuwadi ndiyo wangeendana jambo ambalo yeye hakuwa tayari. Baadhi ya habari zilizowahi kuandikwa  kuhusu jeuri ya fedha ya Wema.
HABARI NYINGINE YA MJINI
Yapo madai kuwa, kutokana na maswahibu hayo ya kuwa kwenye wakati mgumu kifedha, kampuni yake imeanza kudoda na mbaya zaidi, marafiki zake anaokuwa nao kwenye raha, wamemkacha na kumwacha akihangaika mwenyewe.
“Msiniandike gazetini lakini ukweli ni kuwa, huu ndiyo wakati wake wa kujifunza kuchagua marafiki. Ona sasa, wale wote aliokuwa akila nao raha, wamekaa pembeni. Ni tatizo sawa, lakini pia ni funzo kwa upande mwingine,” alisema mpambe mmoja anayefanya naye kazi kwa karibu sana.
 

WEMA AFUNGA MWAKA KWAKUWEKA PICHA MTANDAONI IKIONYESHA UZURI WA MGONGO WAKE

Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu hivi karibuni ameachia picha tata kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram zikimuonesha akiwa ameacha mgongo wazi, jambo lililotafsiriwa na wengi kuwa ameamua kufunga mwaka huu kwa staili hiyo ya kuacha mgongo nje, Showbiz inakudondoshea.
Wema Sepetu akiwa ameacha mgongo wake wazi.
Katika picha hizo, Wema anaonekana kujichora tatoo kibao kuanzia shingoni na kumfanya aonekane tofauti na alivyozoeleka jambo lililofanya wengine wamsifie huku wengine wakimponda mbaya.
“Sasa Wema kujichora hivyo mgongoni ndiyo nini? Bora ungeuacha mgongo wako kama ulivyokuwa zamani,” alichangia mmoja wa wadau na kuungwa mkono na wenzake.
Showbiz ilipomvutia ‘waya’ Wema ili kumuuliza kulikoni ameamua kupiga picha za kuuanika mgongo wake, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
-GPL

NOMA:Picha tatu za Wema Sepetu akiwa ndani ya pozi la nusu uchi.



Wema Sepetu amejikuta  akijishushia  heshma  yake  baada ya kutupia  picha mtandaoni zikimuonesha akiwa amevaa mavazi yaliyoacha wazi baadhi ya sehemu nyeti za mwili wake  hasa  matiti, kitovu  na  kifua  kwa  ujumla.. 
 
Katika  picha  hizo  ambazo zinapatikana  instagram, Wema Sepetu anaonekana  akiwa amevaa kiblauzi chenye matundu kiasi cha kuifanya sidiria aliyovaa ionekane huku sehemu nyingine  kama  kitovu, tumbo  na  kifua  kwa   ujumla   zikiwa  wazi  pia.

Wema Sepetu ahukumiwa miezi mitatu jela au faini ya sh. laki moja baada ya kukutwa na Kesi ya kumtukana meneja wa hoteli



Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar, Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Isaac Sepetu imetolewa hukumu yake kama ilivyokuwa ile ya shosti’ake, Kajala Masanja.

Habari kutoka kwa chanzo makini  kilieleza kuwa Wema alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja kwa maana ya elfu hamsini kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo mawili ya kupiga na kutukana.
 
WEMA AOMBA IHARAKISHWE
Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu wa Wema au Madam zilieleza kuwa hukumu ya kesi hiyo ilikuwa iahirishwe lakini staa huyo akaomba itolewe kwa kuwa alitaka kusafiri.
 
Ilisemekana kuwa mbali na kuwa na safari pia aliomba itolewe kwa sababu yupo ‘bize’ na maandalizi ya arobaini ya baba yake, Isaac Sepetu aliyeaga dunia hivi karibuni.
 
Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe, Dar ambako ndiko kesi hiyo ilipokuwa ikirindima tangu mwezi Agosti, mwaka huu.

ASUBIRIWA KUPELEKWA GEREZANI, ACHOMOA ‘MADOLARI’
Ilielezwa kuwa katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa takriban saa mbili, Wema alikuwa akisubiriwa nje tayari kupelekwa gerezani lakini kama kawaida yake fedha iliongea ambapo alizamisha mkono laini kwenye ule mkoba wake na kuchomoa ‘madolari’.
 
Chanzo kilidai kuwa zilihitajika fedha za Kibongo hivyo Wema alichambua mkoba wake na kutoa ‘wekundu’ kumi huku akirejesha zile dola za Kimarekani.
 
“Wema alifanya kama alivyomfanyia Kajala siku ile pale Kisutu. Kwa Wema ishu ya fedha siyo tatizo sana. Kuliko kumpotezea muda, Wema yupo tayari kutoa kiasi chochote cha fedha.
 
“Kwa Wema muda ni kitu cha muhimu zaidi kuliko hata hiyo fedha ndiyo maana alitoa tu hiyo faini mara moja,” kilisema chanzo hicho.
 
Baada ya kupokea maelezo hayo, GPL  ilimsaka Wema ili kupata mzani wa habari hiyo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

Hata hivyo, alipotafutwa meneja wake, Martin Kadinda na kuulizwa juu ya suala hilo alifunguka:
 
“Ile kesi iliisha tangu Ijumaa iliyopita, watu hawakujua tu. Wema alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu au faini ya shilingi laki moja.
 
“Alichokifanya Wema alilipa faini hiyo na sasa yupo freshi na mishe zinaendelea. Unajua haruhusiwi kufanya mahojiano hadi amalize arobaini ya baba yake.”
 
Chanzo kilisema kuwa kabla ya hukumu hiyo, Wema alikuwa katika hali kama ile iliyomkuta Kajala wakati wa hukumu yake miezi kadhaa iliyopita kwani alikuwa akilia, kujuta na kumuomba Mola amuepushe na balaa hilo lililosababishwa na kuwa ‘tilalila’.
 
Hata hivyo, hukumu hiyo iliwashangaza watu kwani iliendeshwa kwa muda mrefu na kwa mbwembwe nyingi lakini hukumu yake ikawa ya kawaida tofauti na matarajio ya wengi.

KAJALA NAYE KICHEKO TENA
Wakati Wema akikenua, wiki hii Kajala naye ilikuwa chereko chereko baada ya  Mahakama ya Rufaa Kanda ya Dar kuridhika na hukumu yake iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema mwaka huu kufuatia rufaa iliyokatwa na mume wa staa huyo Faraji Chambo.
 
Katika kesi ya awali, Kajala alihukumiwa kifungo cha miaka mitano au faini ya Sh. milioni 13 baada ya kupatikana na hatia ya kushirikiana na mumewe kwenye msala wa kutakatisha fedha haramu wakati mwanaume huyo akifanya kazi Benki ya NBC, Dar.
 
Hata hivyo, Wema alimlipia faini hiyo kama alivyofanya kwenye kesi yake.
 
Katika hukumu ya rufaa hiyo, majaji walijiridhisha kwamba kesi hiyo iliendeshwa ipasavyo na Kajala alitimiza taratibu za kuwa huru kwa kulipa faini lakini mumewe aliyehukumiwa miaka saba alishindwa kulipa faini ya Sh. milioni 213.
 
MAOMBI YAO YASIKIKA
Wema na Kajala wamekuwa kwenye maombi ya kufunga wakisali na kufanya dua ili kuwaepusha na kifungo hivyo kwa sasa wote ni vicheko.

-GPL

KAMPUNI YA MWANADADA WEMA SEPETU KUTOKA BONGOMOVIE YAINGIA MADOA.!!! GARI LAKE LAGEUKA NYUMBA YA UZINZI

Taarifa za sababu kubwa zilizopelekea Wema Sepetu kumtimulia mbali aliyekuwa director wake aliyefahamika kwa jina moja la Chid kuwa ni ufuska uliokubuhu kwa director wake huyo huku akitumia magari yake kama gest ya kumalizia haja zake.

Website hii inakupa mchongo mzima Habari za uhakika zilizotua mezani kwenye meza yetu ya habari zilisema kuwa Wema aliamua kuchukua maamuzi hayo magumu ili kunusuru kashfa kubwa ambayo ingeweza kuikumba kampuni yake"

 Kwa kweli Wema Sepetu alikuwa
anampenda sana Chid kutokana na ubunifu wake kazini na alimpa uhuru wa kufanya kila kitu ikiwemo kumuachia magari ambayo yeye alikuwa kama kiongozi hivyo alikuwa na uhuru nayo sana na alikwenda kila mahali "

 Kilisema chanzo hicho ambacho ni ndugu na Wema aidha habari zaidi ziliendelea kusema baada ya kupata taarifa hizo aliamua kumtimua Chid kwenye kampuni yake ili kulinda heshima ya kampuni hiyo ambapo Chid na vijana walikuwa wakitumia gari hiyo kung'olea watoto wakali"

 Unajuwa Wema ana mashabiki sana hata ile gari wakati mwingine alikuwa anavunja hata sheria za barabarani bila kufanywa chochote hii ilitokana na upendo wa mashabiki kwa Wema na wasichana wengi walikuwa wakiiona ile gari basi wanaingia wenyewe kwenye gari wakidhani ndani yuko Wema hivyo ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Chid na wenzake kuwamaliza wasichana hao"

 Alisema dada huyo Aidha baada ya taarifa hizo tulivuta waya kwa kumcheki hewani Chid na Wema ili kuthibitisha madai hayo ama kuna jingine lililopelekea kutimuana kwa bahati mbaya watu hao hawakupatikana kuzungumzia hilo hadi habari hii inaruka hewani:
Source:XDEEJAYZ

WEMA AWAJIBU WAIGIZAJI WA BONGO MOVIES WALIO SUSIA MSIBA WA BABA AKE

Kupitia kipindi chake cha ‘In My Shoes’ cha jana, Wema Sepetu alieleza jinsi alivyojisikia baada ya baadhi ya waigizaji wenzie wa Bongo Movie kugoma kuhudhuria msiba wa baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, mwishoni mwa mwezi uliopita kwa madai kuwa yeye hakuwa akifanya hivyo kwenye misiba mingine.


“Imeshatokea, wameacha kuja kwenye msiba, ni wao,” alisema Wema. Sio Bongo movie nzima, ni baadhi tu ya watu ambao wanauelewa na upeo mdogo ambao waliamua kutokuja. Lakini niliona Bongo movie wengi, walikuwepo marafiki zangu wengi, akina Batulli, akina Esha, Wolper alikuja, Lulu, JB alikuja, Jokate alikuja, Adam Kuambiana alikuja. Ambaye napenda nimpe my special thanks and appreciation, ambaye alijitolea from the beginning wa msiba mpaka to the end ni Dokta Cheni kwakweli. Dr Cheni, I thank na ntazidi kumshukuru,” alisema.

“Marafiki zangu kama akina Kajala, akina Zamaradi, wale sio marafiki, wale tayari ni ndugu, kwahiyo siwezi kuwaweka kwenye appreciation wala kwenye thanks.”

Katika kipindi hicho pia, Wema alisema yeye na ndugu zake walijua kuwa baba yako ni muumini wa dhehebu la Roman Catholic siku chache kabla ya kufariki dunia.

Balozi Issac Abraham Sepetu (71), alizikwa kikristo katika kijiji cha Mbuzini,mkoa wa Kusini Unguja October 30 ambapo mazishi yake yalihudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohammed Shein pamoja na viongozi wengine.

Bongo5.com

WEMA,ROSE NDAUKA NDANI YA VITA KALI


MASTAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka na Wema Sepetu wanadaiwa kuingia vitani, mpambe mmoja wa Wema akitumia mtandao wa kijamii wa Instagram alimtuhumu Rose kwamba aliwahi kushiriki kikao kimoja kilichokuwa kikimjadili ‘madam’ huyo sanjari na kumtukana.

Mpambe huyo aliyetumia picha ya Wema (huenda akawa Wema mwenyewe), alisema kuwa siku moja isiyokuwa na jina hivi karibuni, Rose alishiriki kikao hicho kilichofanyika kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam ambapo sehemu kubwa ya mazungumzo ilikuwa ikimchambua Wema.

Akizungumza na Amani kwa njia ya simu juzi kuhusiana na tuhuma hizo, Rose alisema anashangaa matusi anayotukanwa na mtu huyo kwani ana mwaka mmoja hajawahi kukanyaga katikia viwanja hivyo vilivyopo Kinondoni, Dar.

“Kiukweli huyo mtu amenitukana bure, hajakaa na kufanyia uchunguzi hizo taarifa alizopewa, mimi sikumbuki kama kuna siku niliwahi kukaa Leaders na kuanza kumsema vibaya Wema kwani nina mwaka sijawahi kufika Leaders.

“Binafsi sina muda huo wa kumzungumzia mtu au kukaa na mtu ambaye hana faida kwangu. Mimi rafiki yangu ni mchumba wangu (Malick Bandawe), mama yangu na ndugu zangu zaidi ya hapo tunakutana shutingi tukimaliza narudi kwangu, namsihi huyo mpambe wa Wema afanye tena uchunguzi,” alisema Rose.

Juzi, Amani lilimsaka Wema kwa njia ya simu ya mkononi ili azungumzie madai hao lakini hakupatikana. Hata hivyo, habari zinasema kuwa mtu aliyemtukana Rose kwenye mtandao alitumwa na Wema au Wema mwenyewe.

Tangu Diamond kurudiana na Wema na kusambaza picha zao katika mitandao ya kijamii, hivi karibuni Wema kufiwa na baba yake mzazi (Isaac Sepetu) na baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi kususia msiba huo, kumeibuka makundi ya watu kazi yao kubwa ni kutukana watu ambao wako tofauti na Wema.

"NIMEPOTEZA MTU MUHIMU SANA MAISHANI".....WEMA SEPETU

MWIGIZAJI wa kike wa filamu mwenye jina kubwa Bongo Wema Sepetu ‘Madam’ hivi karibuni alimpoteza baba yake mzazi aliyefariki katika Hospitali ya TMJ kufuatia msiba huo Wema alifunguka kwa kudai kuwa baba yake kilikuwa ni kiungo muhimu sana katika harakati zake za urembo na sanaa kwa ujumla kwani baba yake alimuunga mkono katika kufanikisha ndoto zake.

Nimepoteza mtu muhimu sana katika maisha yangu baba alikuwa akinisupport katika sanaa kwani hata awali nilipotaka kuingia katika mambo ya ulimbwende baba yangu aliniunga mkono, kulingana na nafasi yake kwa mzazi mwingine isingekuwa rahisi kunikubalia kuingia katika mashindano ya umiss,”anasema Wema.

Wema anasema hadi dakika za mwisho kabla ya baba yake kufariki alikuwa akimwita Miss world, hata alipoingia katika sanaa ya uigizaji wa filamu bado mzazi wake huyo alimuunga mkono jambo ambalo kwake lilikuwa ni faraja na kujivua kuwa na mzazi anayetambua umuhimu wa kipaji cha mwanaye.

WATAZAMAJI WA KIPINDI CHA WEMA SEPETU "In My Shoes" WAMESEMA HAWAKIELEWI KABISA SABABU, ANAONGEA SANA KINGEREZA..

Ilani: Ukitaka kuangalia kipindi cha reality TV cha Wema Sepetu, ‘In My Shoes’ na shule hukwenda, nakushauri ukae na kamusi ya Kiingereza – Kiswahili ili uweze kwenda naye sawa. Hii ni kwasababu, asilimia 50 ya lugha anayoitumia mrembo huyu ni Kiingereza ambayo kwa Watanzania wengi imewapita kushoto. 

 Nimesikia watu wengi mno wakilalamika kuwa matumizi ya Kiingereza kingi kwenye show yake yamewafanya wasikipende kipindi hicho na kunifanya nihoji, nani walengwa hasa wa kipindi chake? Kwa niaba yao ningependa kulifikisha ombi lao kwa Wema kuwa atumie zaidi Kiswahili katika kuongea ili wengi wamwelewe. 

Pamoja na kwamba Wema ndivyo alivyo na hata wakati akihojiwa kwenye TV/RADIO ndivyo huongea, ajizuie katika kipindi chake ili kila mtu amfuatilie.

 

Katika elimu yangu ya uandishi wa habari na utangazaji wa radio/TV nilifundishwa kuwa, wakati wa kuandaa kipindi chochote kile, ni lazima ubainishe, walengwa wa kipindi chako (target audience).
 Kwa kuangalia umaarufu wa Wema Sepetu, hakuna shaka kuwa walengwa wake wakubwa, ni watu wa kawaida kabisa ambao ndio wanunuaji wakubwa wa magazeti ya udaku yaliyolikuza jina lake nchini na wamekuwa wakimpenda sana. 

Kwa namna anavyokiendesha kipindi chake kwa kusimulia matukio yanayooneshwa kwenye kipindi, walengwa ni wale wanaokielewa Kiingereza. Swali ni je, wasomi, raia wa kigeni au watoto wa Masaki, Osterbay na maeneo mengine ya watu wa hali ya juu wanaosoma ama waliosoma kwenye shule za kishua wanakiangalia kipindi hicho? 
Sio kweli na kama wapo basi ni wachache. 

Watu kama hao kwanza hawatumii ving’amuzi vinavyotumika na watu wa hali ya kawaida ambako TV za kibongo zipo. Watu wa maeneo hayo, huangalia DSTV zaidi ambako huko hupenda kuangalia vipindi vya kinyamwezi kama, Keeping Up With the Kardashians, Ice Loves Coco, The Hustle Family ya T.I na Tiny ama The Real Husbands of Hollywood na zingine kibao. 

TV za kibongo huangaliwa kwa nadra na tena labda wakati wa taarifa ya habari saa 2 usiku, na baada hapo huendelea kuangalia TV za nje.
Kipindi cha Wema Sepetu ambacho huoneshwa na runinga ya EATV, kinaangaliwa zaidi na watu wa kawaida ambao kwa bahati mbaya amekuwa akiwatenga kwa kupenda mno kuongea Kiingereza.

 Tanzania bado hatujafika huko na hilo Wema anapaswa aliweke kichwani mwake. Asiletee maisha ya Hollywood kwenye kipindi kinachoangaliwa na Mtanzania wa kawaida.
Kama angekuwa hajui kabisa Kiswahili, basi hilo lingeeleweka. Abadilike..


TAZAMA PICHA CHAFU ZA NUSU UCHI ALIZOPIGA WEMA SEPUTU ZILIZOZAGAA MTANDAONI.




Wema ambaye ni msanii maarufu wa bongo movie ambaye alipiga picha hizi na kuweka kwenye mtandao wa instagram ,kiukweli siyo vizuri kwa msanii mkubwa kama huyu kufanya hivyo

WEMA AIPASUA BONGO MUVI BAADA YA KUSUSIWA MSIBA WA BABA YAKE.


KLABU ya mastaa wa filamu jijini Dar es Salaam, Bongo Movie ‘Bongo Muvi’ imepasuka katikati kisa kikidaiwa kuwa ni lile tamko linalodaiwa kutolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Vincent Honorati Lasasi Kigosi ‘Ray’ kuwa mwanachama yeyote wa kundi hilio asitie miguu kwenye msiba wa baba mzazi wa mwenzao, Wema Sepetu, marehemu Balozi Isaac Sepetu.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria mazishi ya baba'ke Wema Visiwani Zanziabar.
  Tukio hilo la katazo lilitokea wakati wa maombolezo ya kifo cha mzee Sepetu kilichotokea Oktoba 27, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ kwa ugonjwa wa kisukari ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
LAWAMA ZOTE KWA RAY
Kufuatia madai hayo, baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi (majina tunayo) wamekuwa wakitoa lawama zao kwa Ray huku wengine wakidai wamejitoa kwenye kundi hilo kwa sababu halina umoja na limejaa unafiki.
Maneno hayo yalianza kusambaa baada ya Wema kumaliza kumzika baba yake Oktoba 31, mwaka huu mjini Zanzibar.


 
RAY AAGIZWA AITISHE KIKAO CHA DHARURA KUMJADILI
Habari za uhakika zinasema kwamba, wasanii waliotangaza kujiengua klabuni humo wameshamuomba Ray aitishe kikao cha dharura kwa ajili ya kuzungumzia hatua yake ya kuwapiga marufuku wasanii hao kutoshiriki msiba wa mzee Sepetu huku akijua wema wa binadamu unapatikana kwenye kushiriki mazishi ya wenzake.

“Kikubwa zaidi ni kwamba, Ray wakati akisambaza zile meseji alisahau kuwa kuna siku Wema aliwahi kuwaalika wasanii wa Bongo Muvi nyumbani kwake Makumbusho (Dar) wakala na kunywa, mbona hawakugoma kwenda?” alihoji staa mmoja aliyepinga katazo la Ray.
Vincent Kigosi ‘Ray’
NJAMA ZA KUINGAMIZA KABISA BONGO MUVI ZAUNDWA CHINI KWA CHINI
Habari zaidi kutoka kwenye kundi linalodaiwa kujimega kwenye mpasuko huo zinasema kuwa kuna njama za makusudi za kuiangamiza klabu hiyo kwa kuwa mbali na mwenyekiti huyo kuwazuia wajumbe wasiende msibani kwa mzee Sepetu lakini imekuwa ikiendeshwa kitemi na kibaguzi.

Ilisemakana kuwa kuna wasanii wameifanya klabu hiyo kama yao huku wengine wakiwa hawatakiwi hata kukohoa jambo walilosema si sawasawa.
“Kwa mpasuko huu, wasanii waliochukizwa na Ray wamesema nao wao wanakazia hapahapa, Bongo Muvi lazima iangamie moja kwa moja, isiwepo tena,” alisema msanii mmoja ambaye jina lake linapanda kwa kasi.

KISINGIZIO CHA WASANII WANAFIKI CHAPINGWA
Maumivu makali zaidi yaliibuka kufuatia baadhi ya wasanii waliotaka kujifanya hawajapata meseji ya Ray ambapo walisema walishindwa kushiriki msiba huo kwa sababu walikuwa ‘shooting’.
“Kuna wasanii walishindwa kuweka wazi kwamba walipokea meseji ya katazo ya Ray, walipopigiwa simu na wenzao kuulizwa kwa nini hawaonekani msibani kwa Wema walisingizia eti wako location wanarekodi!
“Kwa akili za kawaida, mwenzenu kafiwa mnaweza kushikwa na ubize wa kurekodi filamu? Hawa ni wanafiki, walisingizia vile ili ionekane wana hudhuru,” alisema staa mwingine.

MAMA WEMA ASHTUSHWA
Akizungumza na waandishi wetu kwa mara ya kwanza baada ya kusikia mwanaye alisusiwa msiba wa baba yake, mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu alionesha kusikitishwa sana na kitendo hicho.
Alisema kitendo hicho kilitokea wakati ambao Wema au familia nzima ilikuwa inasaka faraja na si mfarakano kwa vile kufiwa kupo na hakuna dalili wala kujiandaa.
“Nilisikitika sana, lakini siwezi kusema mengi kwa sababu vijana wanataka mwongozo ili kwenda mbele, naamini watakaa na kuondoa tofauti zao,” alisema mama huyo mwenye mapenzi makubwa na mastaa wa filamu Bongo.

KATAZO LA RAY
LILISIMAMIA HIVI
Habari kutoka chanzo chetu makini zilidai kuwa hoja dhaifu iliyotumiwa na Ray ni kwamba Wema huwa haendi kwenye misiba ya wenzake hivyo walitaka na yeye amzike baba yake mwenyewe.

MISIBA ILIYOTOLEWA MFANO
Ulitolewa mfano msiba wa aliyekuwa staa wa filamu za Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia Januari 2, mwaka huu ambapo Wema alishindwa kufika kwa sababu alikuwa studio akirekodi wimbo wake mpya ambao haujatoka hadi leo.

MISIBA ALIYOSHIRIKI
Ilidaiwa kuwa Wema huwa hashiriki misiba ya wenzake, ikatolewa mifano misiba miwili aliyoshriki kuwa ni marehemu Sharo Milionea (Hussein Mkiety) na (Steven) Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake.

ANACHOSIMAMIA WEMA
Akizungumzia tukio la kususiwa msiba wa baba yake, Wema alifunguka:
“Nimesikitishwa na kitendo hicho naamini hakikuwa cha haki, mimi nimekuwa nikihudhuria misibani kwa watu mbalimbali na si kweli kwamba niko kivyangu, nimehukumiwa bure.”

RAY AINGIA ‘PANGONI’
Juzi Jumanne, Amani lilimsaka Ray kwa njia ya simu ili aelezee ukweli wa madai hayo lakini aliingia ‘pangoni’ (hakupokea simu).
Hata hivyo, katika gazeti ndugu la hili, Ijumaa la Ijumaa, Novemba Mosi, 2013 ukurasa wa mbele ambapo kuna habari yenye kichwa; WEMA SEPETU ASUSIWA MSIBA, Ray aliulizwa kuhusu madai hayo ambapo alijibu:
“Mh! Kweli Wema haendagi kwenye misiba ya watu, hata mimi sikumuona kwa Sajuki ingawa sijui kama alionekana baadaye ila kwa sasa niko sehemu mbaya nitakupigia baadaye tuongee kwa kirefu.”
Hakupiga.

MASTAA KIDUCHU MSIBANI
Pamoja na katazo hilo la Ray, wasanii wengine waliamua kwenda msibani Sinza – Mori (Dar) na wachache sana kwenye mazishi, Zanzibar.
Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Kajala Masanja, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Jacob Stephen ‘JB’, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Salum Mchoma ‘Chiki’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ na Jacqueline Wolper.

WASIOFIKA MSIBANI
Wengi walimsusia msiba Wema, lakini majina makubwa zaidi wakiongozwa na Ray mwenyewe ni Single Mtambalike ‘Richie’, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, Irene Paul, Blandina Chagula ‘Johari’, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ na Ruth Suka ‘Mainda’.

MAHAKAMA YAAMURU WEMA SEPETU AKAMATWE HARAKA,NI BAADA YA KUKAIDI AMRI YA MAHAKAMA IYO



Mahakama ya mwanzo Kawe jijini dar es salaam imetoa hati ya kumkamata miss tanzania 2006 Wema Sepetu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni dharau ya wito wa mahakama hiyo. 
 
Chanzo cha ndani kilichoomba kuhifadhiwa ya jina kimempasha mwandishi wetu kuwa hati hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya wema kushindwa kuhudhuria kesi yake iliyopo mahakamani hapo na bila kutolewa udhuru wowote. 

Aidha imeelezwa kwamba mahakama hiyo pia imetilia mashaka udhuru uliotolewa septemba 30 kwamba wema ni mgonjwa baada ya kuvuja kwa picha katika mitandao zikimuonyesha Wema akila bata  Hong Kong China na mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Diamond. 

Wema alitolewa udhuru huo na kijana aliefahamika kwa jina la Martini .
 Kesi inayomkabili wema katika mahakama hiyo ni ya kumtukana matusi ya nguoni pamoja na kumpiga meneja wa hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe beach jijini Dar es salaam bwana Godluck kayumbu. 

Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu alimtafuta mlalamikaji wa kesi hiyo bwana Kayumbu na kumuuliza kuhusu hati iliyotolewa na mahakama ambapo alithibitisha kuwepo kwa jambo hilo. 

Bwana Kayumbu alisema kuwa amepewa hati  maalum ya kumkamata wema octoba 30 mwaka huu ambayo kesi hiyo ilitajwa tena mahakamani hapo.
Alisema kuwa Wema Sepetu anaweza kukamatwa muda wowote kuanzia sasa kwani octoba 30 mwaka huu kesi hiyo ilitajwa tena mahakama ya Kawe chini ya mheshimiwa hakimu Ikanda lakini wema hakutokea na hakuna mtu yeyote aliyekuja kwaajili ya kumtolea udhuru.
Kayumbu alibainisha kuwa mshtakiwa wake wema sepetu hakuja mahakamani mara mbili mfululizo kuanzia septemba 30 2013 na kudaiwa kuwa anaumwa lakini picha zake katika mitandao zilimuonyesha  akitanua hong kong china na mara ya pili kesi hiyo ilitajwa octoba 30 2013 ambapo hakutokea mtu yeyote anayemuhusu wema katika mahakama hiyo. 

"Kesi ilikuwa ya kwanza kutajwa lakini nilikuwa peke yangu sasa nikaamuliwa mimi nipewe hati maalum ya kumkamata wema ambapo nilipewa na nimeshaikabidhi kituo cha polisi cha kawe kwa utekelezaji maana naona muda unazidi kwenda na kesi haiishi," alisema kayumbu.
Mwandishi  wetu alipomtaarifu bwana kayumbu kuwa octoba 30 Wema Sepetu alikuwa kwenye msiba baada ya kufiwa na  baba yake mzazi mzee Isaac Sepetu na kwamba siku hiyo alikuwa safarini kwenda zanzibar kwa ajili ya mazishi ya mzazi wake huyo, bwana kayumbu alisemaa kuwa suala hilo halimuhusu kwani hata yeye amefiwa na wazazi wake. 
"Kama kafiwa hata mimi nimefiwa na baba na mama yangu pia, kinachotakiwa ni kutii sheria za nchi ikiwemo mahakama ,kama alifiwa kwanini asitoe udhuru? sina mazungumzo tena kinachotakiwa ni sheria ichukue mkondo wake, popote atakapopatikana wema ni lazima akamatwe," alisema Godluck. 
Wema hakupatikana kwenye simu ili kuzungumzia jambo hilo.

-Gazeti  la  Kiu  toleo  la  leo.

"SITASAHAU KAMWE JINA ALILOKUWA AKINIITA BABA...." WEMA SEPETU

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’

WEMA Isaac Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa kamwe hatasahau jina la Miss World ambalo marehemu baba yake, mzee Isaac Abraham Sepetu alikuwa akimuita.
Akizungumza na mwanahabari wetu wakati wa kuaga mwili wa baba yake nyumbani kwao, Sinza-Mori jijini Dar, Jumanne iliyopita, Wema alisema baba yake alikuwa akimuita jina hilo kama utani kutokana na masuala ya urembo aliyokuwa akiyafanya hivyo alipofariki dunia jina hilo ndiyo kumbukumbu yake ya muhimu.
Marehemu Isaac Abraham Sepetu.
“Sitalisahau jina la Miss World, baba ndiye alikuwa akiniita hivyo kila nilipokutana naye. Aliponiita hivyo nilikuwa nikifurahi sana,” alisema Madam.
Mwili wa baba Wema ulisafirishwa Jumatano (jana) kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya mazishi.

BONGO MOVIE WAMTENGA WEMA MSIBA WA BABA YAKE.

KATIKA hali isiyotarajiwa katika wasanii wanaounda kundi la Bongo movie wamejikuta wakijitenga kushiriki msiba wa Baba mzazi wa msanii mwenzao Wema Isack Sepetu, baada ya kuundwa zengwe na mmoja wa watu wenye ushawishi katika kundi hilo, Wema akiongea kwa uzuni amesema kuwa hata wale waliofika jana katika msiba huo hawakufika kwa ajili ya kumfariji bali walifika kwa ajili ya kumsanifu. 

FC ilifanya utafiti ili kubaini hilo kwa kuwapigia simu baadhi ya wasanii wanaotoka katika kundi hilo nao bila kusita kwa masharti ya kutotajwa majina walitiririka kwa kusema kuwa ni kweli uongozi wa kundi hilo umetoa agizo watu wasishiriki kutokana na tabia ya msanii huyo kutoshiriki katika misiba ya wasanii wenzake.
“Ni kweli hilo lipo na lina ukweli kwa njia moja au nyingine Wema bwana huwa hashiriki katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti katika kundi la Bongo Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo na Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake,”anasema kijana huyo.
Hili si jambo la kulifurahia kwa wasanii kwani halijengi bali linaleta mgawanyiko wa moja kwa moja, msanii mwingine alikiri kuwa Wema anabagua kushiriki misiba kwani wakati amefariki marehemu John Maganga alipigiwa simu ili ashiriki katika msiba lakini alisema yupo Location, hivyo wasanii wenzake wanamtenga ili aone umuhimu wa kushiriki misiba ya wenzake.

Jana jioni nyumbani hakukuwa na wasanii zaidi ya mtangazaji wa kipindi cha Take One Zamaradi Mketema akiwa na Rais wa shirikisho la wasanii Simon Mwakifwamba na waombolezaji wengine, huku baadhi ya wasanii wakifika pale na kuondoka jambo ambalo Wema alilitafsiri kama walifika pale kutoa lawama ili asiwaone kama hawajafika lakini hawakuwa na dhamira ya kweli mioyoni mwao.

VIDEO: WEMA SEPETU AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA AKIELEZEA JINSI BABA YAKE ALIVYOTESEKA MPAKA MAUTI ILIPOMKUTA

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akielezea kuhusu msiba wa baba yake mzazi Balozi Abraham Isaac Sepetu alipoongea na GLOBAL TV. Balozi Sepetu alifariki asubuhi ya Jumapili Oktoba 27, 2013 katika hospitali ya TMJ jijini Dar na mwili wake unaagwa leo nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar es Salaam tayari kwa mazishi yatakayofanyika kesho Visiwani Zanzibar.

angalia video hapo chini 

 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari