Showing posts with label Jackline Wolper. Show all posts
Showing posts with label Jackline Wolper. Show all posts
WOLPER NDANI YA BIFU ZITO NA ZAMARADI.SOMA KISA HAPA
Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amemrushia maneno ya lawama
Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema kuwa ni mnafki na
adui yake mkubwa katika maisha.
Zamaradi Mketema.
Akizungumza , Wolper alisema amegundua kuwa
mtangazaji huyo amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana maisha yake kwa
mtindo wa chanya (negative), akamuomba amuache.
“Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Zamaradi akanifuatilia, juzijuzi nimerudi kundini (kwenye Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya wazazi wangu, akanifuatilia tena.
“Huko
nyuma kupitia kipindi chake alikubali nidhalilishwe na waigizaji
wenzangu kwa faida yake (hakutaka kufafanua), iliniuma sana. Leo (hivi
karibuni) kaniweka hewani (kwenye redio) bila ya ridhaa yangu. Naomba
niseme kuwa naanza kugundua azma yake kwangu ni nini, aniache na maisha
yangu,” alilalama Wolper.
Baada ya Wolper kulalamika sana, lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alisema yeye anawajibika kwa kazi yake hakuna ishu ya kumfuatilia mtu.
“Mimi simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari nikipata habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema Zamaradi.
“Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Zamaradi akanifuatilia, juzijuzi nimerudi kundini (kwenye Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya wazazi wangu, akanifuatilia tena.
Baada ya Wolper kulalamika sana, lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alisema yeye anawajibika kwa kazi yake hakuna ishu ya kumfuatilia mtu.
“Mimi simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari nikipata habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema Zamaradi.
JACQUELINE WOLPER AKANA MADAI YA KUMPIGA KIBUTI DALLAS BAADA YA KUFULIA

Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa suala la yeye
kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’
halikusababishwa na ukata kwani yeye hakufuata fedha kwa mwanaume huyo.
Akijibu swali la paparazi wetu lililomtaka afunguke kama alifuata
mkwanja kwa Dallas, Wolper alisema moyo wake huwa hauna tamaa ya fedha
na aliingia katika penzi la Dallas kwa mapenzi aliyokuwa nayo wakati huo
na kwa kuwa yaliisha, maisha yanaendelea.
“Sikufuata pesa kwa Dallas, pesa ni pesa na mapenzi ni mapenzi. Kama ni
pesa nilikuwa nazo na hata kabla sijawa naye na sasa pia ninazo,
waniache,” alisema Wolper.
HATIMAE JACKLINE WOLPER AFUNGUKA BAADA YA KUBADILI DINI KWA MARA YA PILI
“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabk zangu stak maswal nawapenda wote…”
Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.
Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa?
Baada ya ndoa yake KUBUMA, Jack Wolper autema uislamu na kuurudia Ukristo
STAA anayefanya vyema katika tasnia ya filamu za Kibongo,
Jacqueline
Wolper ameamua kurudi katika imani yake ya awali ya Kikristo ikiwa ni
miezi michache tangu alipotangaza kubadili dini na kuwa Muislamu.

Wolper akiwa katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama wakati wa ibada.
Novemba 3, mwaka huu (Jumapili iliyopita) mwandishi wetu alimnasa
Wolper katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama jijini Dar, akisali
sambamba na waumini wa kanisa hilo.

Waumini wakiendelea na ibada ndani ya kanisa alimokutwa Wolper.
Bila ya kificho, Wolper ambaye alipokuwa Muislamu alikuwa akitumia
jina la Ilham alisimama na kujitambulisha kama muumini mpya wakati
mchungaji wa kanisa hilo alipowataka waumini wapya kufanya hivyo.

Wolper akiwa katika ibada kanisani hapo.
Wakati ibada hiyo ikiendelea, Wolper alionekana kuimba pambio kwa
hisia kali na ibada ilipoisha, alitoka kanisani huku mkononi mwake akiwa
ameshika Biblia.

Wolper (kulia) akiwa na muumini mwenzake nje ya kanisa.
Nje ya kanisa hilo, Wolper alionekana akiongea na wazee wa kanisa
pamoja na baadhi ya waumini ambapo wote walimkaribisha kwa furaha.

Jacqueline Wolper akiwa katika vazi la Kiislamu wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan mwaka jana.
Mwandishi wetu alimfuata Wolper na kumuuliza kilichomfanya arudi
kwenye dini yake ya awali, naye alisema kwamba amefanya hivyo kutokana
na msukumo wa wazazi wake ambao kwa muda mrefu walikuwa wakipinga
kitendo chake cha kuwa Muislamu.
“Nimeamua kuurudia Ukristo kwa kuwa wazazi wangu kwa muda mrefu
walikataa mimi kuwa Muislamu, kwa hiyo kuanzia sasa siyo Ilham tena,
niite Jacqueline kama zamani,” alisema Wolper.
Wolper akiwa ndani ya gari aina ya BMW X6 alilonunuliwa na Abdallah Mtoro ‘Dallas’ baada ya kubadili dini na kuwa muislamu.
Mwaka jana, Wolper alibadili dini na kuwa Muislamu kutokana na kuwa na uhusiano na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Dallas akiwa nje ya nchi akamtaka Wolper kubadili dini ili akirudi
wafunge ndoa ya Kiislamu, Wolper alikubali na kufanya hivyo katika
Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar na kuchagua jina la
Ilham.
Gari aina ya BMW X6 alilonunuliwa Wolper na Dallas baada ya kuwa muislamu.
Dallas alirudi nchini lakini wawili hao hawakufunga ndoa bali penzi
lao likaingia doa na kumwagana, Wolper akaendelea na msimamo wa imani
yake hiyo mpya na mara kwa mara alikuwa akidai kwamba hataiacha dini
hiyo pamoja na kumwagana na Dallas.
---GPL
GONJWA LILE LA HATARI LAZIDI KUMTESA JACKLINE WOLPER

Mrembo huyo ambaye amejizolea sifa nyingi kutokana na filamu zake alikuwa akisumbuliwa na Malaria, gonjwa hatari ambalo limekuwa likimsumbua mara kwa mara...
Wolper aliripoti taarifa ya kuumwa kwake katika account yake ya facebook na kuweka wazi kuwa gonjwa linalomsumbua ni lile lile hatari la Maralia ambalo limekuwa likimsumbua mara nyingi...

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, mwaka 2010 aliwahi kuugua gonjwa hilo na kulazwa kisha akapona.
MFAHAMU JACKLINE WOLPER FEKI ANAEWATAPELI WATU KWENYE MITANDAO YA JAMII

kumekuwa na wimbi kubwa la matapeli kwenye mitandao ya kijamii hususan FACEBOOK, TWITTER, BBM na mingine mingi. Jana katika pita pita zangu kwenye mtanfao wa Facebook nilipokea ujumbe ukionesha Jackline Wolper anaomba urafiki nami bila kusita nika confirm obi lake. Leo nilipoingia inbox yangu ya facebook nilikuta ujumbe huu.
Conversation started today
1:26amJackline Wolper
Hello, sorry naweza kukusumbua kitu nw?
3:04amPablo Junior Calter I
yeah sure.
3:14amJackline Wolper
Naomba nisaidie, niko nyumban and sijatoka bado kuna kaz naifanya kwenye computer, kazi ya ofisini. Umeme Umeniishia naomba niazime 20,000 ninunue then baadae nikitoka nakurudishia.
3:17amPablo Junior Calter I
ohky haina tatizo sasa hizo pesa nitakupatiaje ama una tigopesa?

3:29amJackline Wolper
0712394346, Jina litokee jackline massawe
3:31amPablo Junior Calter I
sawa wng so utanirudishia lini

3:36amJackline Wolper
Baadae nakutumia, kuna kazi nikiimaliza ndo ntatoka, naomba nitumie bas sasa ivi Pablo

3:52amPablo Junior Calter I
poa nakutumia
na hii ni picha ya chat tuliyofanya
chat yangu na jackline wolper feki
Facebook wapo watu wengi sana wenye hii tabia ambayo sio nzuri kwakweli wasanii wetu kila siku wana lalamika kuwa majina yao yanatumiwa vibaya jambo ambalo sio jema guys kwa wewe mwenye huu mchezo nakushauri uache maana iko siku utagundulika tu "ZA MWIZI NI AROBAINI".
fungua hapa kuangalia hio account fake ya Jackline Wolper
JACKLINE WOLPER HALI MBAYA HOSPITALINI...ASEMA "WATANZANIA NIOMBEENI...."
Msanii wa Filam
Tanzania ajulikanae kwa jina la Wolper yuko hoi Hospitalini huku akiomba
Dua kwa wapenzi wake wamuombee ili apone haraka. Wolper ameripot
taarifa za kuumwa kwake katika akaunti yake ya facebook na kuainisha
ugonjwa unaomsumbua ni Maralia na ujumbe huo umesomeka hivi:
WOLPER ANASWA AKITWANGA MBEGE
MWANADADA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’ ameamua kudumisha mila na desturi baada ya kupiga picha akiwa anakunywa pombe ya kienyeji aina ya mbege.
Wolper alitundika picha hiyo katika mtandao wa Kijamii wa Instagram akiwa ameshikilia kikombe maarufu kinachotumiwa na watu wa Kilimanjaro kwa ajili ya kunywea pombe aina hiyo na kuambatanisha na maneno kuwa anadumisha mila.
“Nyumbani Arusha nikinywa wine nitakosea jamani, leo mbege tu Wachaga mtanielewa tu,”aliandika Wolper.
Baada ya kuweka picha na maneno hayo watu mbalimbali walionekana kumfagilia staa huyo na kumsifu kwamba ameonesha kujali mila tofauti na watu wengine pindi wanapokuwa mastaa huzibeza mila zao.
Mashabiki wengi walikuwa wakimpongeza kwa kumuandikia maneno kwa lugha ya Kichaga kuonesha kwamba wamemkubali.
WOLPER AWAPA USHAURI WA BURE WASANII WANAOVAA NUSU UCHI

Muigizaji wa filamu za kibongo maarufu kwa jina Jackline Wolper amewaasa waigizaji wenzake wa kike kuacha kuvaa nguo za nusu uchi kwani ni kinyume na mila na tamaduni za kitanzania .
Wolper aliyasema hayo kufuatia kupigiwa kura na kushinda kama muigizaji wa kike mwenye muonekano wa kistaa...
Akizungumza katika kipindi cha filamu cha Take One kinachorushwa Clouds Tv , Wolper alisemakuwa yeye hawezi kuvaa mavazi ya nusu uchi ila anavaa mavazi yanayomsitiri mwili wake na bado anapendeza kuliko hao wanaovaa nusu uchi halafu hawapendezi.
"Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kunipigia kura hadi kuibuka mshindi, na ni kweli najiamini kwa kuwa mimi hata siku moja huwezi kuniona nimevaa nguo za nusu uchi kama wengine" Wolper
WOLPER AVUNJA GLASI YA DIAMOND
STAA wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvunja glasi ya Rais wa Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Tukio hilo lilijiri Agosti 28, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Serena, Posta jijini Dar ambapo staa huyo alikuwa kwenye uzinduzi wa video ya Diamond.
Ilikuwa wakati Diamond akisalimiana na mastaa mbalimbali, alipofika kwa Wolper aliigusa kidogo, ikaanguka.
Paparazi wetu alipomuuliza Wolper sababu ya glasi hiyo kuvunjika, alijibu: “Hata mimi sijui nini kimetokea, tulikuwa tunasalimiana ghafla tu glasi yake ikadondoka na kupasuka, sijui ni miujiza au nini loh!”
Diamond naye akatia neno: “Nimeshtukia glasi ipo chini tu, daah! Sina hata cha kueleza juu ya hili.”
-GPL
MPASUO WA WOLPER WACHANGANYA MIDUME
GAUNI alilolivaa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacquline Wolper limeonekana kutibua hali ya hewa kutokana na ukubwa wa mpasuo kiasi cha midume kumtolea macho ya matamanio staa huyo.Tukio hilo lilichukua nafasi nje ya hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar wakati wa utambulisho wa video ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la My number One.
Wolper akiwa ameweka mapozi kwa ajili ya kupiga picha, aliwashtua wanaume waliokuwa wakielekea katika magari yao sehemu ya maegesho na kuanza kumtolea macho.
“Father cheki mpasuo huo kushoto kwako hapo ulipokaa ni mahali pake?” alisikika mwanaume mmoja aliyepita karibu na alipokuwa amesimama Wolper.
Baada ya kusikika kauli hiyo, mwigizaji huyo alibaki akicheka na kusema kuwa hashawishiki na maneno yao.
“ Kwani ni peke yangu niliyevaa gauni lenye mpasuo mkubwa?” alihoji Wolper.
Wolper akiwa ameweka mapozi kwa ajili ya kupiga picha, aliwashtua wanaume waliokuwa wakielekea katika magari yao sehemu ya maegesho na kuanza kumtolea macho.
“Father cheki mpasuo huo kushoto kwako hapo ulipokaa ni mahali pake?” alisikika mwanaume mmoja aliyepita karibu na alipokuwa amesimama Wolper.
Baada ya kusikika kauli hiyo, mwigizaji huyo alibaki akicheka na kusema kuwa hashawishiki na maneno yao.
“ Kwani ni peke yangu niliyevaa gauni lenye mpasuo mkubwa?” alihoji Wolper.
Subscribe to:
Posts (Atom)




