Like Us On Facebook

RAY C AWAANIKA MATEJA WENZAKE

SIKU chache baada ya kutangaza kuyakacha madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ amewaanika vijana wenzake waliokuwa wakitumia dawa hizo na kuacha.Ray C aliwaanika vijana hao kwa picha waliopiga pamoja akaiweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo zaidi alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuleta dawa aina ya Methadone ambayo inatolewa bure katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mwananyamala iliyowasaidia.
“Mungu ni mkubwa sana, wote tuliokaa hapa tuliathirika na madawa ya kulevya na tumepona kwa kunywa dawa moja tu inayoitwa Methadone inayopatika Muhimbili na Mwananyamala pekee, ni bure kabisa tunamshukuru sana Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutuletea dawa hii,” aliandika Ray C ambapo wengi walimpongeza kwa hatua hiyo
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari