Binti Komando, Anaconda, Lady Jay Dee bado hajakamilisha mpango wa kuuweka wazi wosia wake, lakini hivi karibuni watanzania na wadau wa muziki wanaweza kuushuhudia wosia huo kabla hatujauanza mwaka 2014.
Hii inatokana na tweet ya Jide ya December 18,2013.
Katika hatua nyingine, Yahaya hit maker ameweka wazi moja kati ya ndoto ambazo anatamani sana kuzitimiza ikiwa ni pamoja na kukutana na daktari wa midundo duniani ‘Dr. Dre’, na mkali wa R&B Usher Raymond.
Jide ameandika kwenye blog yake:
“Kati ya NDOTO zangu mbili kubwa zilizobakia hapa duniani ni kukutana na watu hawa wawili Dr. Dre na Usher Raymond 2013 hiyoooo inayoyoma ndoto imekuwa ndoto, hebu tusaidiane kusali tujaribu tena 2014.”