Kwa mujibu wa chanzo chetu, wasanii hao wamebeba mimba hizo kwa nyakati tofauti na wamekuwa wakijificha kukwepa aibu ya kubeba ujauzito kabla ya kufunga ndoa.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka ukweli wa habari hiyo ambapo jitihada zilizaa matunda kwa kupatikana kwa picha za mastaa hao zikionesha tayari vitumbo ndii.
Baadhi yao, picha zilionesha mimba zikiwa ni kubwa huku wengine zikionekana ndiyo bado changa. Aunty Lulu, Belina walionekana dhahiri kuwa ni waleo au kesho, matumbo yao yalionekana ‘live’ ni makubwa, Odama yeye ilionekana bado halijajitokeza vizuri.
“Recho ni mjamzito lakini amekuwa akijificha kukwepa kamera za mapaparazi si unajua tena uchumba wake na Sagunda kila mmoja alikuwa akiufatilia magazetini!”
Baadhi ya mashabiki walioongea , hawakusita kuonesha hisia zao kwa mastaa hao, kila mtu alikuwa na mtazamo wake juu ya mastaa hao. “Unajua kama Belina naona amebeba mimba ila yuko kwenye process ya kufunga ndoa ingawa sijui ni lini kwani niliwahi kumsikia akisema kuwa anaweza kufunga ndoa soon” alisema shabiki mmoja, mwingine akasema hivi:
“Sisi tujuavyo kioo cha jamii maana yake ni mtu kufanya yale yanayofaa kuigwa lakini kwa hawa mastaa wetu wamefanya tofauti, wote wamebeba mimba bila ndoa, sasa jamii itajifunza nini kutoka kwao?”