Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Zainabu anayefanya biashara hiyo maeneo ya Sinza Afrika Sana, alisema umbo lake limekuwa likiwadatisha wanaume kibao.
“Kaka si unaiona hii shepu yangu, hapa kuna mwanaume anayeweza kunipita na kwenda kwa wale vimbaumbau,” alisema Zainabu huku akimuonesha paparazi wetu wasichana wembamba waliokuwa mbele yao.
Sara aliongeza kuwa, wanaume wengi anaotoka nao wamekuwa wakimsifia kwa umbo lake ‘pana’ na kudai kwa siku huwa hakosi shilingi 50,000 na siku nyingine anapata hadi 80,000.
Karibu wanawake wote mabonge waliozungumza na paparazi wetu maeneo ya Kinondoni, Buguruni, Manzese na Oysterbay ambako biashara hiyo imeshamiri walidai maumbo yao yamekuwa yakipendwa sana na wanaume hususan waume za watu.
Paparazi wetu alipomuuliza Sara, Zainabu na mwenzao aliyejitambulisha kwa jina la Sikitu kwamba hawaoni kama wanaharibu soko la wenzao wembamba, kama vile waliambiana jibu wakasema watajiju!
Huyu naye akiwa lindoni.
Baadhi ya madadapoa wembamba waliozungumza na paparazi wetu, waliwafungukia majimama hao na kudai wamewaharibia soko lao na kusababisha wajiuze kwa promosheni.Source:GPL