Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Wastara alisema, amekuwa mpweke kwa muda mrefu na sasa ni wakati muafaka wa kumpata mtu wa kuziba pengo la marehemu mume wake.
“Inatosha sasa, nadhani muda wa kuwa na mwenzangu umefika. Napenda huyo mwanaume awe mwenye huruma, upendo na kutambua thamani ya mke lakini ni vizuri akiwa mwenye kujituma na awe na fedha nyingi.
“Natamani kuolewa na bilionea. Najua nikiwa na mwanaume wa aina hiyo sitateseka, nitapata kila ninachokitaka. Unajua mimi kama mwanamke nina mambo mengi. Siyo siri natamani itokee siku moja niendeshe Hummer au Prado (aina za magari) kulingana na hadhi yangu.
“Kiukweli nitafurahi sana nikimpata mwanaume wa aina hiyo, maana nitakuwa na uhakika wa kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kunisaidia katika shughuli zangu za sanaa,” alisema Wastara.