Like Us On Facebook

HAYA NI MANENO YA TUNDU LISSU BAADA YA ZITTO KABWE KUSHINDA KESI ZIDI YA CHADEMA

 Tundulisu aklizungumza na waandishi nje ya mahakama

Jana Januari 7 2014 ni siku ambayo Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam ilitoa uamuzi juu ya Kesi iliyokuwa ikiwahusu Mbunge wa Kigoma Kaskazini  Zitto Kabwe na Chadema ambapo baada ya uamuzi kutangazwa, paparazi wetu aliongea na wakili wa Chadema Tundu Lissu juu ya uamuzi huo wa Mahakama.

Tundu Lissu ameanza kwa kuongea >> 

‘Walau leo Mahakama imethibitisha kwamba ni mbunge wao kwa hiyo bunge la Tanzania lina wabunge watatu sasa hivi ambao ni wabunge wa Mahakama,  Hamad Rashidi Mohamed, David Kafulila na Mheshimiwa Zitto Kabwe’


‘Mahakama kuu ilichosema ni kwamba Zitto Kabwe asijadiliwe uanachama wake mpaka kesi itakapoisha, tunasubiri aje athibitishe mashtaka yake Mahakamani amri ya kuzuizi ni ya kumlindia Ubunge tu na uenyekiti wake wa P.A.C kama alivyosema Jaji’


‘Ni hivi Zitto Kabwe ni mbunge wa Mahakama na ubunge wa Mahakama una mwisho wake, kama mbunge wa Mahakama  atapokea posho, atapokea mishahara ataenda safari za PAC kwa hiyo ana haki zote kama mbunge, Kwenye vikao kama ni  mwanachama kwenye tawi lake atashiriki lakini kwenye vikao vingine vya chama kama sio mjumbe hatoweza kushiriki’


‘Kambi rasmi ya Upinzani ina taratibu zake vile vile na moja ya taratibu ni kwamba kama mjumbe wa kambi haendani na matakwa ya kambi, moja ya adhabu ni kuzuiliwa kuingia kwenye vikao vya  kambi na tutavuka huo mto tukiufikia’


‘Zitto Kabwe anaweza kuzungumzia masuala ya chama mahali popote amri ya Mahakama inasema kuwa kamati kuu au chombo kingine cha chama kisizungumzie wala kuamua uanachama wake tu, haijamziba mdomo kuzungumza masuala ya chama kama ambavyo mimi naweza kuzungumzia mambo ya chama’


‘Suala ambalo tumelisema ni muhimu ni kwa wanachama wetu tu wahakikishe kwamba hawampi nafasi lakini kama atataka kuandaa mikutano kwa jina lake ye mwenyewe kama ambavyo amekua anafanya si umeona kwenye mikutano yake hana bendera ya chama, ile anaweza kuendelea kwa sababu kwa mujibu wa Mahakama Zitto Zuberi Kabwe bado mwanachama wa Chadema’


‘Hati ya kiapo sisi tulishindwa kuwasilisha, tumewasilisha hati ya kiapo iliyosainiwa na wakili Kibatala na kama tulivyosema Mahakamani, Mahakama ya rufaa ilishasema kwamba wakili ana uwezo wa kula kiapo kwa niaba ya mteja wake kulingana na mazingira ya kesi’


‘Tulimwambia Jaji kwamba kesi siku ya kwanza iliisha saa12 na nusu jioni tukaambiwa tuwasilishe hati ya kiapo kesho yake saa 2 na nusu asubuhi sasa kwa mazingira hayo wakili kama ambavyo Mahakama ya rufani ilivyosema wakili anaweza kula kiapo lakini sisi tunavyoamini kiapo kile kilikua sahihi kabisa katika mazingira ya kesi hii, kwa kusema tulikurupuka wakati tuliambiwa tupeleke kiapo saa 2 na nusu kesho yake asubuhi kwa kweli sio sawa sawa’


‘Tulishindwa kuwasilisha hati ya kiapo ya Dokta Slaa kwa sababu hakuwepo kwa sababu usiku tumetoka hapa tumeambiwa tupeleke kiapo saa 2 asubuhi, huo muda wa kumtafuta dokta Slaa ulikuwa wapi’

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari