Like Us On Facebook

"JAMANI JB NI MWANANGU,NDIYE ATAKAYENIZIKA....KUNA WATU WANATUGOMBANISHA ILI KUTUHARIBIA"....MZEE MAJUTO



          Lejendari wa vichekesho Bongo, Amri Athuman a.k.a Mzee au King Majuto amefunguka kuwa kuna watu wanamgombanisha na mwigizaji Jacob Steven ‘JB’ ili kumharibia mambo yake ikiwa ni siku chache tangu alipotangaza kuwa atagombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015 jijini Tanga.
Akizungumza wikiendi iliyopita baada ya kudaiwa kuwa kwenye bifu baya na JB, Mzee Majuto alisema: “Jamani JB ni mwanangu, ndiye atakayenizika. Tunaheshimiana sana sema tu kuna watu wanatugombanisha ili kutuharibia.”
Kwa upande wa JB alifunguka kuwa:  “Nimefanya kazi nzuri na mzee wangu hadi tukapata tuzo. Tunajiandaa kurekodi filamu ya kuchukua tena tuzo sasa watu wanaleta maneno ili kutuvuruga.”
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari