Jeshi
la Polisi mkoani Ruvuma linafanya uchunguzi kuhusu tukio la mume na mke
kumshambulia mtalaka wake Faustina Komba (35) mkazi wa jiji la Mbeya
kwa kumpiga ngumi, makofi na kumng'ata mdomo wake wa chini na kuuondoa
wote.
Jeshi
la Polisi mkoani Ruvuma linafanya uchunguzi kuhusu tukio la mume na mke
kumshambulia mtalaka wake Faustina Komba (35) mkazi wa jiji la Mbeya
kwa kumpiga ngumi, makofi na kumng'ata mdomo wake wa chini na kuuondoa
wote.
Habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na kamanda wa
polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdebit Nsimeki zimewataja watuhumiwa hao
kuwa ni Hamidu Mapunda na Regina Mpangala wakazi wa Mshangano, nje
kidogo ya Halmashauri ya manispaa Songea.
Imedaiwa Desemba 7, jioni huko Faustina alishambuliwa kwa kupigwa
ngumi, makofi na kung'atwa mdomo wake wa nchini ambao uliondolewa kabisa
na Regina ambaye alishirikiana na mume wake Mapunda.
Inadaiwa chanzo cha ugomvi wao Faustina na Mapunda ambaye alikuwa mume wake wa zamani ni kugombea mtoto wao Mussa Mapunda (5).
Imeelezwa kuwa wakati wakigombana mke wake wa sasa (Regina) aliingilia kati akiwa na lengo la kumsaidia mume wake Mapunda.
Kamanda Nsimeki alifafanua zaidi kuwa wakati ugomvi unatokea mke wa
sasa wa Mapunda alikuwepo na alishuhudia Mapunda akipigwa kipande cha
tofali kichwani ambacho kilisababisha atokwe na damu nyingi, ndipo
alipoingilia kati na kuanza kumsaidia mume wake lakini Faustina inadaiwa
alimkamata Regina na kumng'ata sehemu ndogo ya mdomo wake wa chini
ndipo naye Regina aliamua kumng'ata sehemu ya mdomo wake wa chini na
kuundoa wote.
Kamanda Nsimeki alisema kuwa Faustina na Regina wamelazwa katika
hospitali ya mkoa Songea kwa matibabu na shauri hilo linasubiri wao
wapate nafuu.