Rebecca Shaw aliyevurugiwa nyumba na mpenzi wake aliyemkataa.
Gari la Rebecca ambalo nalo lilimwagiwa 'tomato sauce'.
Gari hilo likiwa limemwagiwa 'tomato sauce' kwa nyuma.
Rebecca aliporudi nyumbani kwake alikuta vioo katika kitanda chake, mashuka yakiwa yamechanwa na nyumba yake ikiwa haitamaniki kwa uhalibifu uliofanywa na Martin aliyekuwa na hasira za kuachwa.
Martin alivunja vyombo na kuvitupa nje kupitia madirisha aliyoyavunja na kuharibu kila kitu alichokiona mbele yake pamoja na gari la Rebecca lililokuwa nje ya nyumba. Pia alivunja midoli ya mtoto wa Rebecca mwenye miaka minne na kurusha vyakula hovyo pamoja na 'tomato sauce' ukutani na sakafuni.
Baada ya kukiri kuhusika na tukio hilo, Martin aliihukumiwa kwenda jela miezi 18.