SIRI ya muonekano mzuri wa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael
‘Lulu’ imefichuka baada ya kubainika kuwa, amekuwa akifanya mazoezi kila
siku kwa kwenda gym.
Lulu akifanya mazoezi.
Lulu alianika siri hiyo hivi karibuni kupitia mtandao wa instargram
kwa kutupia picha zikimuonesha akiwa kwenye tizi na baadae alipozi na
kujifotoa picha ambazo zilimuonesha akiwa na umbo la kuvutia zaidi huku
zikisindikizwa na maneno yasemayo; ‘ndiyo siri ya urembo’. Hata
hivyo, baadhi ya watu walioziona picha hizo walimpongeza kwa uamuzi
wake huo huku ushauri pia ukitolewa kwa kila mmoja kujali afya yake kwa
kufanya mazoezi pale muda unapopatikana.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.