Katika hali ya kusikitisha nay a ukali wa hali ya juu dereva bodaboda aliyefahamika kwa jina moja laMbikano
anasakwa na jeshi la polisi Mkoani Mtwara kwa kusababisha mauji ya
mtoto mdogo ambae alimgonga wakati akiendesha bodaboda yake na kumuumiza
mguu kisha akambeba na kukimbia nae na baadae kumtupa kwenye kichaka na
fisi wakaja kumla na kubakisha kafuvu kadogo tu.
XDEEJAYZ INAKUBA ISHU NZIMA:
Habari
za uhakika zilizonaswa na mwandishi wa Xdeejayz aliyeko Masasi na Mtwa
zilisema tukio hilo la kusikitisha limewaliza watu wengi, akiongea na
xdeejayz kwenye mahojiano maalum mjomba wa mtoto huyo aliyejitambulisha
kwa jina la Mjomba wa mrehemu Yusuph Hashim (30) alisema tukio hilo
lilitokea tarehe 29, saa 12:30 jioni.
Mjomba huyo aliendelea kueleza kuwa siku hiyo mtoto huyo aliyeitwa kwa jina la Shabiru
Muhidin (4) ambapo wanaishi katika Kijiji Mkaseka wote na mtoto huyo
muda huo alikuwa ametumwa dukani na mamaake mzazi aliyefahamika kwa jina
la Thawabu Hakhim Nakanje.
Hata
hivyo katika ha ilisiyotajia mjomba huyo alisema kuna kundi la vijana
waliokuwa wanatoka kwenye kutizama mpira kwenye kijiji cha Jirani cha
Mkururu huku wakiwa wamepakizana kwenye bodaboda walivyofika maeneo ya
Mkaseka ndipo walipomgonga mtoto huyo na kumjeruhi mguuni na walipoona
watu wameanza kujaa ndipo walipomchukua mtoto huyo ambae alikuwa akilia
kwa uchungu na kuondoka nae kusikojulikana.
Mjomba
huyo aliendelea kuileza xdeejayz kuwa kijana huyo aliyekuwa anaendesha
bodaboda aliendelea kutokomea kizani na mtoto huyo hadi alipofika mahali
penye msitu mkubwa alimrusha kichakani huku mtoto huyo alimsihi
asimuache msituni hapo kwani angeliwa na wanyama lakini bila huruma
dereva huyo wala hakujali hatimae alimuacha mtoto huyo.
Habari
zaidi ziliendelea kusema huku nyuma alipogongewa mtoto habari zilianza
kusambaa ambapo mjomba huyo alipopata taarifa hizo aliondoka na majirani
zake kuelekea kwenye zahati ya kijiji hicho kwa kudhani huenda watu hao
waliamua kufanya ubidamu kwa kumpelekea hospitali baada ya kumuumiza
ambapo alipofika kwenye zahati hiyo hakumkuta mtoto huyo.
Baada
ya kumkosa kwenye zahati hiyo walienda kwenye kituo kikubwa cha Afya
cha Nagaga lakini hapo napo hawamkuta ndipo walishauriana kwenda
kuripoti kwa mkuu wa polisi jamii na mara baada ya kukutana na kamanda
wa polisi jamii aliyefahamika kwa jina la Hamis na baada ya kuwasikiliza
aliitisha kikao cha dharula na wakaanza kumtafuta mtoto huyo hapo
ilishakuwa siku iliyofuata ambapo baada ya msako kfanyika walienda hadi
kwenye sehemu moja yenye kilima msitu.
Baada
ya kufika kwenye mlima huo waliona mburuzo ulioambatana na damu na
walipoenda mbele zaidi waliona damu nyingi zikiwa na vimetapakaa na
vipande vya utumbo na fuvu kipande kidogo tu hali waliyogundua kuwa
mtoto huyo alishapoteza uhai wake kwa kuliwa na fisi ambao eneo hilo
wako wengi kama mbuzi.
Kufuatia
kushuhudia hayo kamanda wa ulinzi shirikishi alipiga simu kituo cha
polisi Masasi ambapo polisi walifika haraka na kupiga picha eneo la tuki
huku wakiondoka na mabaki ya fuvu hilo kwa ajiliya uchunguzi zaidi.
Hata
hivyo hadi sasa mliki wa bodaboda hiyo anashikiriwa na jeshi la polisi
huku mtuhumiwa namba moja akitafutwa kwa udi na uvumba ili kufikishwa
mbele ya mkono wa dola.
Xdeejayz ilifanya jitifahada za kumtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara ili
kuzungumzia ambapo baada ya kupigiwa simu ilipokelewa na mlinzi wake
huku akisema kuwa Kamanda yuko bize na vikao hivyo atafutwe jioni ya
leo.
-XDEEJAYZ