Queen Latifah akiwa na msichana wa ‘I Quit’ Marina kwenye kipindi chake
Msichana huyo aitwaye Marina Shifrin ‘I quit girl’ aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni ya Kikorea iitwayo Next Media Animation amegeuka kuwa staa kwenye internet kwa mzaha huo alioamua kuufanya wiki iliyopita, wa kujirekodi akicheza wimbo wa Kanye West ‘Gone’, huku maneno ya sababu za kuacha kwake kazi yakipita. Video hiyo mpaka sasa imetazamwa mara 13,999,571.
Baada ya Queen Latifah ambaye ana reality show yake ya TV inayoitwa jina lake kuitazama video hiyo alimkaribisha katika kipindi chake baada ya kuitazama video hiyo, na kuamua kumpa ajira Marina katika kipindi chake kwa cheo cha “Digital Content Producer”. Latifa alimwambia msichana huyo kuwa anapenda kufanya kazi na watu watulivu, wabunifu na wanaofurahisha sifa ambazo yeye anazo. Tazama Video ya Queen Latifah akiwa na Marina katika kipindi chake
Tazama video ya Marina iliyompa kazi kwa Latifa