Mtu
mmoja aliejulikana kwa jina la Burhan Islam(fundi wa gari) amenusurika
kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria aina ya Fuso kugonga lori
lingine nae kubanwa na bodi na kuokolewa baada ya
jitihada zilizofanywa na baadhi ya Abiria waliokuwa wakisafiri katika barabara kuu ya Dar es salamu kwenda Mtwara na Lindi.
Gari
hilo lenye namba za usajiri T 56ANQ lililokuwa likiendeshwa na Kunja
Mshamu limepata ajali hiyo leo katika kijiji cha Mkwajuni wilayani Lindi
baada ya kutaka kulipita gari lenye namba za usajili T 402 AJG Scania
lililokuwa likiendeshwa na Amos Chadenyile na kushuhudiwa jitihada
zilizokuwa zinafanywa kuokoa maisha ya kijana huo.Majeruhi
huyo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo alikimbizwa katika kituo cha
afya kitomanga kwa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa katika hospital
ya Mkoa wa Lindi kwa Uchunguzi zaidi
Katika ajali hiyo iliyousisha malori hayo hakuna majeruhi mwingine
aliepata jeraha huku gari hiyo ya Fuso likiwa limeharibika sana