Like Us On Facebook

LUCCI AMVISHA PETE MWANAMKE MWINGINE BAADA YA KUTUHUMIWA KUTOKA KIMAPENZI NA JOKATE



                      Hivi sasa producer wa wimbo wa" kaka dada" ameamua kumvisha pete mpenzi wake ambaye amekuwa mchumba wake rasmi.

Akiongea na millardayo,Lucci  alikuwa  na  haya  ya  kusema:“Baada ya mambo ya project ya Kaka Dada kukamilika nimeona ni muda muafaka kabisa kumvisha pete mpenzi wangu Lisa Semgeliwa au marafiki zake huwa wanamuita Lizzyblazzer. 

"Unajua like seriously tumekuwa kwenye dating kwa muda zaidi ya miaka 2. Muda huo unatosha kabisa naamini ni vizuri kuingia kwenye hatua nyingine ya mahusiano yetu” .
 
Wengi  wanajiuliza, huyu shemeji yetu alikuwa na hali gani kipindi kifupi kilichopita wakati "Kaka Dada"  ikiwa  JIKONI  na  baada  ya  kutoka????...

Lucci  analitolea  ufafanuzi  jambo  hilo:
”Unajua ukishakuwa kwenye mapenzi na mtu anayejitambua na anaefahamu kazi yako. Basi atafahamu kabisa entertainment inahitaji vitu tofauti ili kufanikisha. 

"So mimi na yeye tuliongea kwamba muda huu tunaitoa kazi ya kaka dada na plan nzima alikuwa anaijua. So hakukuwa na tatizo lolote”
 
Baada  ya  maelezo  hayo,Lucci  aliamua  kuelezea   kuhusu mchumba wake:

”Lisa ni director wa kampuni yetu mimi na yeye inaitwa  Tsere. Kazi tunayofanya ni creative and marketing, pia anafanya kazi ya HR kwenye hii kampuni”

Ni  imani  yangu  kuwa  Lucci  ameamua  kufunguka  ili  kuzima  tuhuma  zilizokuwa  zikisambaa  kwa  kasi  kuhusu  kutoka  kimapenzi  na  Jokate. 
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari