Like Us On Facebook

BABY MADAHA ANASWA LIVE NA MUME WA MTU.

          STAA wa sinema na Bongo Fleva, Baby Madaha amenaswa live akiingia na kula bata hotelini akiwa na mwanaume aliyetajwa kwa jina la Joe Kariuki.

 

Tukio hilo lililopigwa chabo na shushushu wetu lilijiri wikiendi iliyopita, majira ya usiku mnene katika Hoteli ya De France iliyopo Sinza, Dar ambapo Madaha alionekana akiwa amejiachia vya kutosha kwa mwanaume huyo.

 

 

Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilizungumza na Madaha ambaye alikiri kuwa na mwanaume huyo hotelini hapo huku akidai ni meneja wake.

 

“Joe (Kariuki) ni mejeja wangu wa Kampuni ya Candy n’ Candy Records ya Nairobi, Kenya ndiye anayesimamia kazi zangu na tayari nimeachia ngoma moja inayo-hit ya Summer Holiday,” alijitetea Madaha.

 

-GPL

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari