Akizungumza na paparazi wetu, Nisha alisema Nay alimfuatilia kwa kipindi kirefu na alimzungusha kama miaka miwili kabla hata hajawa staa. “Nikivuta ile picha ya kumdengulia kiasi kile mpaka kuamua kumkubali, naamini alinipenda tu na hata kama hakunipenda lakini najivunia kwamba alihangaika kunipata,” alisema Nisha.
Wawili hao walidumu katika uhusiano wa kimapenzi kwa miezi kadhaa kabla ya kuachana na kila mmoja akichukua ‘hamsini zake’.