
MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa amekoma kumtangaza mpenzi wake kwani ameshaumizwa sana kwa kuibiwa mwandani wake.
Akichezesha taya na paparazi wetu hivi karibuni, Amanda alisema wasichana wengi wana tabia ya kuchukua mabwana wa wenzao wakati awali kabla hajaanzisha uhusiano naye, hakuna anayemuhitaji lakini wakisikia amemtangaza tu ndiyo nao wakaanza kumfuatilia. “Daah! Nimekoma, sitatangaza tena.
Wasichana wa Kibongo wamezidi, unakuta mwanaume kabla hujawa naye kimapenzi hakuna mtu anayeshughulika naye lakini wakisikia uko naye ndiyo wanamsaka, kwa sasa nikija kumtangaza mchumba basi ujue ndoa soon,” alisema Amanda.
Hivi karibuni Amanda alikuwa akitoka na Mbongo Fleva, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’ kabla ya kumwagana ingawa hakubainisha kama naye ameibiwa na wasichana wenzake au la!