Akijificha Waandishi wasimpige picha
Tukio hilo lilijiri mahakamani hapo Agosti 22, mwaka huu ambapo mshitakiwa alikana mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi, Joyce Minde.
Trafiki feki huyo alitumia muda mwingi kujificha sura ili kamera zisimchukue lakini alichemsha kwani kila alipojifunua kidogo alikuta kamera ziko mbele yake. ...Akingizwa ndaniHali hiyo ilimfanya mshitakiwa huyo aamue kujiachia kwa kutoa kofia aina ya kapelo kichwani na picha za kumwaga kupatikana.
Akisoma mashitaka hayo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga alisema mnamo Agosti 14, 2013, huko Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, Dar, mtuhumiwa alikutwa amevaa nguo za askari wa usalama barabarani akijifanya ni mwajiriwa wa jeshi la polisi jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Hapa waandishi walimbamba
Hata hivyo, mshitakiwa alipelekwa rumande Segerea, hadi Septemba 5, 2013 baada ya kukosa wadhamini wawili kwa shilingi milioni kumi na nne.