Showing posts with label BUNGENI. Show all posts
Showing posts with label BUNGENI. Show all posts
DIVA WA CLOUDS FM ETI NAE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE,NI BAADA YA KUPIGWA CHINI CLOUDS FM
Mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho kutoka Clouds Fm ‘The people’s Station’ leo kwenye akaunti yake ya Instagram amepost picha ikiwa na maneno haya chini.

Huo ndiyo ujumbe uliosomeka kwa Diva ingawa bado hajaweka wazi jimbo
atakalogombea,Kama atafanikiwa kuingia bungeni Diva atakua kwenye list
ya miongoni mwa watangazaji na vijana walioingia kwenye siasa wakiwa na
umri mdogo
Dk. Emmanuel Nchimbi ampigia magoti mwenyezi Mungu ili ampe moyo wa kusamehe kwa mambo aliyotendewa hivi karibuni

SIKU chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi kuvuliwa wadhifa wake kwa tuhuma za kushindwa kusimamia wizara yake, kiongozi huyo ametaka apewe moyo wa upendo na kusamehe.
Nchimbi ambaye ni mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya CCM, alisema
hayo juzi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook, wakati
akisherehekea kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa.
“Kama Mwenyezi Mungu angeniuliza ni kitu gani anipatie kwa muda huu,
ningemuomba anipatie moyo wa upendo na kusamehe,” aliandika.
Mawaziri wengine waliovuliwa nyadhifa zao pamoja na Nchimbi, ni
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo na Waziri wa Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
“Sasa nina miaka 42, namshukuru Mungu kwa kunibariki na kunisaidia
kwa kipindi cha mwaka mzima, nawashukuru wazazi wangu, kaka, dada na
marafiki zangu, pia ninawashukuru waajiri wangu watu wa Jimbo la Songea
na Watanzania wote.
“Ninaukubali upendo wenu na kuniunga mkono…Kama Mungu ataniuliza leo
kitu gani anipatie jibu langu litakuwa rahisi, nitamwambia Mungu wangu
naomba moyo wa upendo kwa kila mmoja, moyo wa kumsamehe kila mmoja
pasipo kujali nini nitarudishiwa, anipe moyo wa kuwatumikia watu kwa saa
24 kwa siku,” alisema Dk. Nchimbi.
Dk. Nchimbi na wenzake wanne walienguliwa madarakani baada ya Rais
Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wao mara baada ya kupewa taarifa za
wabunge kuwashinikiza mawaziri hao wajiuzulu kwa sababu ya
yaliyojitokeza katika Operesheni Tokomeza Ujangili.
Kuondolewa kwa mawaziri hao kulitokana na Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, kuwasilisha
taarifa ya kamati yake iliyobainisha unyama mkubwa waliotendewa wananchi
katika operesheni hiyo.
Operesheni hiyo ilikuwa ikizihusisha wizara za mawaziri hao
waliong’olewa ambapo inadaiwa watendaji waliokuwa wakiiendesha waliua
watu, kujeruhi na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo mifugo.
Matukio mengine yaliyobainika kwenye operesheni hiyo ni wanawake
kubakwa na wengine wakilazimishwa kufanya mapenzi na mama, wakwe au
watoto wao.
source:Tanzania daima
source:Tanzania daima
MWIGULU NCHEMBA AMPA ONYO SPIKA ANNE MAKINDA
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba, amemwonya
Spika wa Bunge, Anne Makinda kuacha kutumia vibaya fedha za Serikali kwa
kuwapa posho wabunge kwa ajili ya kwenda kwenye michezo nje ya nchi.
Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi alitoa kauli hiyo jana bungeni
wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushuru
wa bidhaa ya mwaka 2013 iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Saada
Mkuya Salumu.
Mkuya katika
maelezo yake alisema kuwa kodi hiyo imefutwa kwa laini za simu kwa mtu
mmoja mmoja na badala yake imeongezwa katika kodi kutoka asilimia 14.5
hadi asilimia 17.
Katika
mchango wake, mbunge huyo alionya kuwa kumekuwa na tabia ya kutumia
vibaya fedha za umma jambo alilosema linaanzia ndani ya bunge.
"Naomba
tukubaliane katika kubana matumizi, na hivyo ninakuomba Mheshimiwa
Spika tuanze na ofisi yako achana na kutoa fedha kwa kuwapa wabunge kwa
ajili ya kwenda Dubai kwa burudani,"alisema Nchemba.
Alisema
umefika wakati ambao Serikali inatakiwa kufanya uamuzi wa kutumia fedha
katika mambo muhimu ambayo yanaigusa jamii kuliko mambo ambayo hayana
maana. Kwa upande mwingine aliwalaumu watendaji kuwa wameiangusha
Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kushindwa kutoa ushauri na usimamizi
mzuri katika makusanyo ya kodi.
Kwa
upande wake Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia aliinyooshea vidole
Serikali kuwa ndiyo iliyovuruga mchakato mzima wa makusanyo ya kodi
ambayo muswada wake ulishapitishwa.
Mbatia alitoa sababu kuwa ndani ya Serikali wamekuwa wakiamua mambo lakini kwenye utekelezaji wake wanagawanyika.
Breaking News: Mawaziri 4 wavuliwa nafasi zao usiku huu bungeni

Rais Jakaya Kikwete leo ametengua uteuzi wa mawaziri wanne kufuatia shutuma nzito dhidi yao katika sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili.
Mawaziri waliopoteza ajira
zao usiku huu ni pamoja na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), David
Mathayo (Mifugo na Uvuvi), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani) na Shamsi
Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).
Akizungumza Bungeni Dodoma
usiku huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kulikuwa na matatizo
makubwa katika usimamizi wa zoezi hilo.
“Tulifanya
operesheni kwa nia nzuri,” alisema Waziri Mkuu Pinda na kuongeza :
“Tatizo ni namna operesheni hiyo ilivyotekelezwa.”
Katika mdahalo uliogusa nyoyo
za wabunge na wachambuzi mbalimbali wa siasa leo, wabunge waliueleza
umma jinsi ambavyo Operesheni hiyo ilitumika kutesa, kunyanyasa na kuua
raia wasio na hatia na kuwadhulumu mali zao.
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AMJIBU ALIYESEMA KUWA YEYE NI MZIGO KWA SERIKALI,NA HILI NDO JIBU LAKE
Ni swali ambalo limeulizwa bungeni dodoma
Mbunge wa viti maalum Rukia Ahmed:
‘Tulipokua tukijadili taarifa ya kamati ya hesabu za Serikali pamoja na serikali za mitaa kuna Mbunge alisema kwamba kama kuna mzigo, basi mzigo nambari moja ni wewe Waziri Mkuu, hili unalizungumziaje?’
Waziri Mkuu Mizengo Pinda: ‘Kila mmoja anamuhuku mtu kutegemea na alichonacho kwenye fikra zake, Waziri mkuu huyu anasimamia Wizara zaidi ya 20 hivyo kama utamuhukumu kwa sababu ya Wizara moja au mbili humtendei haki, unajua uzuri wa nafasi hizi huombi… ni rahisi kwa maongezi yake kichwani na anavyojaliwa na Mwenyenzi Mungu anaamua kusema ngoja nimpe dada Rukia kuwa Waziri mkuu, kama zipo kasoro, Rais ndie mwenye maamuzi’
Mbunge wa kuteuliwa, Dk Asha-Rose Migiro aapishwa Bungeni Dodoma leo
DODOMA, Tanzania — MBUNGE wa kuteuliwa na Rais, Dk. Asha-Rose Migiro, leo saa 3 asubuhi, ameapishwa kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania.
Akizungumza nje ya viwanja vya Bunge, baada ya kuaspishwa, na Spika wa Bunge Anna Makinda, Dk. Asha-Rose ameahidi utumishi wenye uadilifu, uaminifu na wa kujituma.

Alisema ubunge ni uwakilishi uwe wa kuteuliwa, kupitia viti maalum au majimbo na kwamba nafasi hiyo aliyopewa sio ya

"Unapopewa fursa kama hiyo sio yako binafsi bali ni heshima ya wanawake wote kwa sababu nimeongeza idadi ya waliopo bungeni’’
“Hivyo ni nafasi nyingine kuwa wanawake tunawajibu na tunapopata fursa basi tuna kila sababu ya kutumikia umma na Nchi yetu kwa moyo wote na kwa nguvu zote,"alisema Dk. Migiro.

Kwa mara nyingine Dk. Migiro alimshukuru Rais Dk. Jakaya Kikwete kwa uteuzi wake kwake kwa kuwa umempa heshima na fursa nyingine ya kutumikia Taifa.
"katika maisha mtu anaweza akafanya kazi yoyote na kazi yoyote ina thamani lakini nafikiria kazi ya kutumikia umma ni heshima ya pekee kwa sababu kama utaweza kufanya shughuli kwa ufanisi basi matokeo yake yanasambaa kwa watu wengi zaidi,"aliongeza Dk. Migiro.
Muswada wa kura ya maoni wa mwaka 2013 wapita.
BUNGE limepitisha muswada wa kura ya maoni wa mwaka 2013.
Muswada
huo ambao ulikwama kupitishwa juzi kutokana na hitilafu ya umeme na
kusababisha vipaza sauti kugoma, ulipitishwa jana kwa wabunge kutakiwa
kuitikia ndiyo au siyo.

Hata
hivyo, muswada huo ulikuwa na mvutano mkali kati ya serikali na wabunge
wa upinzani, huku baadhi ya wabunge wakichafua hali ya hewa kwa kudai
kuwa wabunge wa Bara wasijadili mambo ya Zanzibar.
Aliyechafua
hali ya hewa alikuwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), ambaye
alisema hakuna sababu ya wabunge wa Bara kuwasemea wananchi wa Zanzibar
na badala yake wasemewe na Baraza la Wawakilishi.
Kamati ya Bunge yadai TAMISEMI ni sehemu ya mtandao wa ufisadi
Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac), imeilipua Wizara ya
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa madai ya kuwa sehemu
ya Mtandao wa Ufisadi serikalini.
Tamisemi
inaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa
Ghasia anayesaidiana na manaibu waziri wawili, Aggrey Mwanry na Majaliwa
Kassim Majaliwa.
Halikadhalika
kamati hiyo ya Bunge imesema, zipo dalili za wazi za kuwapo kwa mtandao
wa kutisha wa kifisadi unawashirikisha baadhi ya watendaji wa
halmashauri nchini, hazina na Tamisemi.

Tuhuma
hizo zilitolewa Bungeni jana na Mwenyekiti wa Laac,Rajab Mbarouk wakati
akiwasilisha taarifa ya hoja za kamati kuhusu hesabu zilizokaguliwa kwa
mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,2012.
Alisema
bado kuna ubadhirifu,ufisadi na utovu wa nidhamu wa hali ya juu wa
matumizi ya fedha za umma kutokana na Tamisemi kutosimamia ama yenyewe
kuhusika moja kwa moja na ufisadi huo.
“Mfano
mwaka 2011/12, Sh1.6 bilioni zilitumika nje ya bajeti iliyoidhinishwa
katika halmashauri 38 na Sh2.6 bilioni zilihamishwa kutoka akaunti moja
kwenda nyingine bila kurudishwa,”alisema.
Kamati
hiyo imebaini kwamba upo mtindo wa Serikali kutuma kwa halmashauri
kiasi kikubwa cha fedha kuliko kiasi cha fedha kilichoidhinishwa na
Bunge katika fungu husika wakati wa upitishaji bajeti.
Kamati
hiyo imetolea mfano wa Sh2 bilioni zilizotumwa Halmashauri ya Jiji la
Tanga na Sh500 milioni zilizotumwa katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe
ikiwa ni zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa na Bunge.
“Kitendo
hiki ambacho kinafanyika kwa ushirikiano wa hali ya juu wa
Hazina,Tamisemi na Halmashauri kinaashiria kuwapo mtandao wa kutisha wa
kifisadi baina ya mamlaka hizo,”alisema.
Kamati
hiyo imeituhumu pia Tamisemi inayoongozwa na Waziri Hawa Ghasia,
kuwahamisha haraka watumishi wanaotuhumiwa kufanya ubadhirifu kutoka
hamashauri moja kwenda nyingine.
“Kamati
imebaini kwamba Tamisemi imekuwa ikitumia mtindo huu kuwalinda
watumishi mafisadi ndani ya halmashauri na kuifanya kamati iamini
Tamisemi ni sehemu ya mtandao huu,”imesema.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo alisema kwa makusudi,Tamisemi imekuwa ikieneza saratani
hiyo ya ufisadi kwenye halmashauri nyingi iwezekanavyo na kuitaka
Serikali kuachana na mtindo huo.
Kamati
ya Bunge ya Bajeti, imeishauri Serikali kupunguza matumizi na kuongeza
ukusanyaji mapato ili miradi ya maendeleo igharamiwe kwa asilimia 35 ya
bajeti ya Serikali.
Akiwasilisha
ripoti ya kamati hiyo Bungeni jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Andrew
Chenge alisema kwa utaratibu wa sasa hakuna uwiano sawia kati ya
matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo.
Chenge
ambaye pia ni Mbunge wa Bariad Magharibi(CCM) alisema, mwenendo wa deni
la taifa si wa kuridhisha kutokana na kuongezeka kwa mikopo ya masharti
ya kibiashara na malimbikizo ya riba.
-Mwananchi
-Mwananchi
BUNGE LA KATAA KUBARIKI DIVISION 5 KATIKA ALAMA MPYA ZA UFAULU ELIMU YA SEKONDARI.

Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, imevikataa viwango vipya vya alama za ufaulu kwa elimu ya sekondari vilivyotarajiwa kuanza kutumika mwaka huu na kutaka utaratibu na alama zilizotumika mwaka jana, zitumike kupanga matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne wa mwaka huu.
Serikali ilitangaza utaratibu mpya wa alama za Mitihani ya Kidato cha Nne na Sita kwa kufuta Daraja la Sifuri na kuleta Daraja la Tano.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stephen Ngonyani alisema jana kuwa kamati hiyo ilichukua uamuzi huo kwa kuwa pamoja na udhaifu ulio kwenye alama hizo, kamati yao haikuhusishwa katika mchakato wa kuandaa alama hizo.
“Mwenyekiti wangu (Margaret Sitta) alisema kile hakiwezekani, kuna viwango ambavyo wameleta havipo kwenye nchi nyingine duniani, tumewaambia wakavifanyie kazi walete tena,” alisema mbunge huyo wa Korogwe Vijijini, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la Profesa Maji Marefu.
Ngonyani alisema waliagiza watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhakikisha wanaishirikisha kamati yao kwani imejaa walimu wanaoweza kushauri vizuri.
“Hatutaki watuletee mambo ambayo yamewashinda baada ya kuyapeleka kwa wananchi,” alisema Ngonyani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akitangaza uamuzi huo mapema mwezi huu, alisema uamuzi wa kubadilisha mfumo huo umechukuliwa kutokana na changamoto zilizojitokeza mwaka 2012.
Alama zilizokuwa zikitumiwa awali na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), katika kupanga matokeo hayo, kwa Kidato cha Nne ni A=80-100, B=65-79, C=50-64, D=35-49, F 0-34 kwa upande wa Kidato cha Sita, A=80-100, B=75-79, C=65-74, D=55-64, E=45-54, S=40-44 na F= 0-39.
Alama mpya zilizotangazwa ni A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na F=0-19. Alama hizo ni kwa kidato cha nne na sita.
Kwa utaratibu huo, A ilitafsiriwa kuwa ni ufaulu uliojipambanua, B+ ni ufaulu bora sana, B ufaulu mzuri sana, C ufaulu mzuri, D ufaulu hafifu, E ufaulu hafifu sana na F ufaulu usioridhisha.
Katika utaratibu huo, mtihani wa mwisho ulitarajiwa kuwa na alama 60 na alama 40 zitokane na alama za Maendeleo ya Mwanafunzi Shuleni (Continuous Assessment-CA).
Mwaka jana baada ya Serikali kufuta matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne, Necta ilitumia CA ya 30 huku mtihani wa mwisho ukiwa na alama 70.
Wadau wa elimu na wabunge walipinga vikali utaratibu mpya wa alama za mitihani hali iliyofanya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuamuru wizara husika kupeleka bungeni taarifa yenye maelezo juu ya uamuzi huo.
Kabla ya Serikali kutoa kauli yake, watendaji na viongozi wa Wizara ya Elimu walikutana na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii Mjini Dodoma mwezi huu ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikataa viwango hivyo vipya na kuitaka wizara kuendelea kuvifanyia kazi viwango hivyo kwa kuishirikisha Bodi ya Necta.
Mjumbe mmoja aliyekuwa ndani ya kikao hicho alisema hoja kuu zilizosababisha kukataliwa kwa alama hizo ni ile iliyosemwa kuwa ni kushusha sana viwango vya ufaulu, pia kutaka shughuli hiyo ifanywe kwa kushirikisha Bodi ya Necta ambayo kisheria ndiyo yenye jukumu la kutunga sera za mitihani.
“Tulichosema ni kuwa viwango vya ufaulu pamoja na utaratibu uliotumika mwaka jana, viendelee kutumika kwa mitihani ya kidato cha nne inayoendelea kwa sababu viwango vipya vimekosa uhalisia,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
Wajumbe hao walisema haiwezekani ufaulu wa A ukaanzia 75 wakati hakuna nchi duniani yenye A ya namna hiyo, pia haiwezekani 20 ikahesabika pia kama ufaulu.
“Pia ukiangalia, Kifungu cha Nne cha Sura ya 10 ya Sheria ya Necta kinasema kuwa taasisi hiyo ndiyo yenye jukumu la kutengeneza sera ya mitihani,” alisema mjumbe huyo.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema bungeni kuwa daraja sifuri litaendelea kuwapo lakini hakuzungumzia chochote kuhusu alama ambazo kamati ilishauri wizara hiyo izifanyie kazi.
Mulugo ambaye ndiye aliyehudhuria kikao hicho hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo. Hata alipopigiwa simu yake ya mkononi, iliita bila kupokewa.
Ofisa Habari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyanzu alisema kwamba hana taarifa za maagizo hayo ya kamati hiyo.
Ufaulu wa chini
Kwa mujibu wa kitabu kinachoonyesha viwango vya ufaulu duniani kila mwaka cha International Qualification, baada ya Tanzania kutangaza alama hizo mpya, sasa inaongoza duniani kwa kuwa na alama za chini za ufaulu.
Nchi zinazofuatia kwa viwango vya chini baada ya Tanzania ni Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ambazo hata hivyo, viwango vyake vipo juu kwa kiwango kikubwa vikilinganishwa na vile vya Tanzania.
MBUNGE ALIYEOLEWA NA KIJANA MDOGO ADAI KUWA KIJANA NDO ALIMNG'ANG'ANIA WAFUNGE NDOA
Mbunge Roseweeter Kasikila
Hatimaye
Mbunge Rosweeter Kasikila (60), aliyefunga ndoa na kijana mwenye umri
wa miaka 26, amefunguka kwa kusema aliyeng'ang'ania kufunga ndoa hiyo ni
kijana mwenyewe licha ya kumtahadharisha tofauti ya umri wao.
Kasikila alitoa kauli hiyo jana, baada ya kutakiwa kujibu shutuma zilizotolewa na mumewe huyo, Michael Christian (26) ya kung'ang’ania vyeti vyake vya elimu kwa lengo la kumtaka arudi nyumbani.
Christian aliyefika katika ofisi za NIPASHE jana alitoa nakala ya barua aliyoituma kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuomba atumie uwezo wake wa kisheria ili mbunge huyo amrudishie vyeti vyake alinavyovishikilia.
Kufuatia maelezo hayo, NIPASHE ilimtafuta Dk. Nchimbi kwa njia ya simu ili athibitishe kupokea nakala ya barua hiyo lakini simu yake ilikuwa imezimwa.
Nakala nyingine za barua hiyo zilitumwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Binadamu kwa jamii-Madhehebu ya dini nchini, Askofu William Mwamalanga, Mchungaji wa Kanisa la Assembilies of God, Mikocheni B, Mchungaji Getrude Rwakatare na vyombo vya habari.
Akijibu shutuma hizo, mbunge huyo alisema hajawahi kung'ang'ania vyeti vya kijana huyo wala kulazimisha ndoa kama anavyodai Christian.
"Nahisi kuna watu wanamtumia ili wanichafue, siwezi kung'ang'ania vyeti, kwanza vya kazi gani kwangu, ukweli ni kwamba Michael, shida yake anataka nichafuliwe, kwangu aliondoka wakati sipo, sasa hivyo vyeti nimeving'ang'ania saa ngapi," alisema na kuongeza:
"Mwaka jana nikiwa Dodoma nilipata taarifa ameondoka nyumbani, kweli nilivyorudi nilikuta amechukua vitu vyake vyote kasoro tu vile nilivyomnunulia, hivyo vyeti anavyosema nimeving'ang'ania mbona hajawahi kutamka mbele yangu zaidi nimeona kwenye magazeti," alihoji.
Alisema baada ya kufika nyumbani alipata taarifa kuwa, mume wake huyo amepanga chumba na anaishi na mwanamke mwingine (askari) ambaye ni mjamzito.
Alisema utaratibu alioutumia kijana huyo wa kumchafua kwenye magazeti siyo sahihi na kumshauri angeenda mahakamani au kanisani kama aliona haitaki ndoa tena.
Aliongeza kuwa yeye na Christian walifahamiana mwaka 2009 baada ya kufiwa na mume wake aliyemtaja kwa jina moja la Mushi.
"Sikumtongoza kama anavyosema, alikuja katika hospitali ya Bagamoyo akitokea chuo cha Red Cross wakati huo nilikuwa Muuguzi Mkuu, aliponiona alinipenda alianza kunitongoza, nilimkatalia na kumwambia mimi ni mtu mzima sana kwake, " alisema na kuongeza:
"Alikuwa ananitumia email (barua pepe) za kunitaka, nilimwambia umri wangu ni mkubwa, lakini yeye alikuwa ananiambia kwenye vitabu vya dini kuna sehemu gani kumeandikwa umri," alisema.
Alisema alijikuta ametumbukia kwenye penzi la kijana huyo na kuanza mahusiano naye.
"Nina nakala zote za vidhibitisho ambavyo alikuwa akinitumia kunitongoza nimevichapisha kama vielelezo vyangu, tena wakati tumeanza uhusiano Taasisi ya Safina ambayo ilikuwa ikimsaidia katika masomo yake, ilinipigia simu," alisema na kuongeza:
"Safina walitaka kujua kama nina mahusiano na huyu kijana niliwajibu ni kweli, waliniambia kama ndiyo hivyo wanafuta kumsaidia kwa sababu wao huwasaidia wale ambao hawana uwezo, yatima, " alisema.
Alisema wakati taasisi hiyo ikimfuta, ilikuwa imemlipia Christian sehemu ya ada ya masomo aliyokuwa akiyachukua."
"Nililazimika kumlipia ada ya mwaka wa pili na watatu wa masomo yake pamoja na mambo mengine na ilifika kipindi aliniambia anataka kunioa, ndipo tulipofanya mchakato ambapo nilitolewa mahari na ndoa ilifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutangazwa mara tatu," alisema.
Alisema Christian alifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutoa mahari ya Sh. 200,000 na baada ya harusi alipelekwa Kondoa kwa ndugu wa kijana huyo.
"Huko tulienda kati ya mwezi Julai au Agosti, mwaka jana, tulifanyiwa sherehe za kimila na ndugu za mume wangu ambao ni baba mdogo, bibi mzaa baba yake na shangazi, pia ndugu zake wa Kimara na Dodoma wananijua, " alisema.
Hata hivyo, mbunge huyo alipoulizwa kama ndoa hiyo ipo sasa hasa kufuatia shutuma hizo, alisema hawezi kujua kwa sababu mume wake aliondoka bila kumuaga na kwa sasa anaishi na mwanamke mwingine toka Novemba mwaka jana.
Alisema wakati wa mahusiano yao wafanyakazi wenzake Christian walikuwa wakimhoji kwa nini ameamua kuwa na mtu mzima kama (mbunge), lakini yeye aliwajibu hakuna umri kwenye biblia.
Alipoulizwa kama ana mpango wa kuchukua hatua dhidi ya kijana huyo, mbunge huyo alisema hana mpango.
Mbunge huyo alijitetea kuwa, hakumlazimisha kufunga ndoa na kwamba wakati kijana huyo akimtongoza, alimweleza kuwa hawezi kuzaa kwa sababu umri wake umeshapita.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Zitto Kabwe na Godbless Lema waingia ndani ya bifu zito....Chanzo cha ugomvi ni Posho za wabunge. Lema anataka waongezewe Posho, Zitto hataki

Wabunge Wawili Maarufu wa Chadema, Zitto Kabwe (Kigoma
Kaskazini) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wameingia katika vita ya
maneno ambayo chanzo chake ni kauli ya Lema aliyotoa katika kikao cha
wabunge (briefing) kilichofanyika mjini Dodoma Jumanne wiki hii.
Lema akizungumza katika kikao hicho, anadaiwa
kutoa maneno ambayo yalitafsiriwa na wabunge wengi kuwa yalikuwa
yakimlenga Zitto kuhusu hatua yake ya kukataa posho na kumtuhumu kwamba
ana ukwasi ambao unapaswa kuhojiwa.
Mwananchi lilimtafuta Lema likirejea taarifa
iliyotolewa na Zitto akilalamika kwamba Lema alimshambulia katika kikao
hicho cha wabunge wote na kwamba alikuwa akimlenga yeye.
Lema, hata hivyo, alikiri kuzungumzia suala hilo akisema:
“Mimi sikumtaja mtu, kwahiyo kama kuna mtu analalamika hilo ni suala jingine, ila mimi nilimaanisha nilichokisema”.
Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa msimamo wa Lema
ulikuwa unapingana na wabunge wengine wa Chadema, ambao waliwahi
kupendekeza kuwa posho zifutwe.
Zitto alisema kuwa yeye mwenyewe, Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika waliwahi
kupendekeza kuwa posho zifutwe.
“Mimi sipokei posho kabisa, ( posho za vikao ) na
ndo mbunge pekee ambaye hapokei posho ya vikao tangu mwaka 2011,”
aliongeza Zitto, ambaye anahudhuria mkutano unaozungumzia uendeshaji wa
Serikali kwa uwazi huko London, Uingereza.
Zitto alisema malipo ya wabunge mpaka sasa ni
makubwa sana ukilinganisha na hali ya wananchi wakati Serikali
ikishindwa kulipa vizuri walimu na wauguzi.
“Hatuwezi sisi kama wabunge kuanza kulilia posho,
wakati wananchi wetu hawana maji, hatuwezi kulilia posho. Mbunge
anayetaka posho zaidi akafanye kazi nyingine na awaachie wanaoweza
kuwakilisha watu waendelee,” alisema Zitto.
Lema, hata hivyo, alisema kwamba katika mkutano
huo aliweka bayana kwamba umasikini siyo uzalendo na kusisitiza kuwa
wabunge wanapaswa kuwa na maslahi bora na wakati huohuo wana wajibu wa
kuwatetea watumishi wengine wa umma.
“Nilisema huwezi kuzuia taasisi moja kupewa
maslahi bora eti tu kwa sababu watumishi wengine hawalipwi vizuri, ni
haki wabunge kulipwa vizuri na wakati huo wapiganie maslahi ya watumishi
wengine,” alisema Lema na kuongeza:
“Kwahiyo nikasisitiza kwamba nawashangaa wale ambao wanakataa
posho ya Sh80,000 na ukienda kuchunguza wanakatwa fedha zote kutokana na
mikopo waliyochukua, lakini bado wakija sehemu kama Arusha wanalala
kwenye hoteli ya gharama kubwa kati ya Dola za Marekani 150 na 600”.
Alisema katika mazingira hayo kunakuwapo maswali
mengi yasiyokuwa na majibu na kwamba mbunge wa aina hiyo alitakiwa
anapokuwa katika mji wowote nchini aishi katika hoteli yenye thamani
kati ya Sh20,000, 30,000 na hata Sh50,000.
“Kwa hiyo ikiwa unakataa posho ya Sh80,000 halafu
unalala chumba cha Dola 600 hustahili kupata credibility (sifa) stahili,
ni unafiki tu na kutafuta sifa za kipuuzi,”alisema Lema.
Alisisitiza kwamba wabunge wa Tanzania hawalipwi
ipasavyo na kwamba kudai malipo ya ziada hakuwaondolei wajibu wao wa
kuwatetea watumishi wengine wa umma ambao pia malipo yao ni kidogo.
“Kuna hatari ya kuona kwamba Sh80,000 au Sh200,000
ni fedha nyingi, ni kwamba kama sisi wabunge tutalipwa Sh50,000 basi
maana yake ni kwamba walimu au polisi tutaridhika wakilipwa hata
Sh10,000,”alisema
-Mwananchi
-Mwananchi
WABUNGE NA MISHAHARA NA POSHO ZA NAMNA HII....JE NI HALALI KWAO KULALAMIKIA MASLAHI MADOGO?
Imethibitika rasmi kuwa wakati wabunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakilalamikia maslahi madogo,
mbunge mmoja hulipwa mshahara wa Sh. milioni 11 kwa mwezi.
Kiasi hiki hakijumuishi posho ya Sh. 330,000 anayolipwa mbunge kwa kuhudhuria kikao kimoja kwa siku. Posho ni Sh. 80,000 za kujikimu akiwa nje ya jimbo lake, posho ya vikao Sh. 200,000 kwa siku na mafuta ya gari Sh. 50,000, jumla kuwa Sh. 330,000 kwa siku.
Aidha, mbunge mmoja hulipwa ‘gratuity’ (kiinua mgongo au bahashishi) ya Sh. milioni 72 baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano cha ubunge.
Aidha, wabunge hupewa fedha za Mfuko wa Jimbo Sh. milioni 30 kila mwaka kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo katika majimbo yao.

SIRI IMEFICHUKA..!! HIKI NDICHO KILICHOMFANYA YULE MBUNGE WA MIAKA 60 KUOLEWA NA KIJANA WA MIAKA 26..!!

Wiki
hii yote kumekuwa na kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya
kijamii kumefunikwa na tukio la kustaajabisha linalomuhusu mbunge wa CCM
Rosweeter Kasikila mwenye umri wa zaidi ya miaka sitini kufunga ndoa na
kijana mdogo Michael Chstiani (26) Mtandao huu umepata taarifa mpya juu
ya tukio hilo ambalo kwa sasa liko kwenye mgogoro mzito.
Habari
toka kwenye chanzo chetu cha habari zilisema kuwa sababu kubwa ya
Mheshimiwa huyo kuangukia kwenye penzi l "Serengeti boy" huyo ni
kutokana na ufundi wa hali ya juu wa kijana huyo hali iliyofanya Mama
huyo kushindwa kujizuia na kuamua kumfanya kijana huyo kuwa mume kabisa.
mama
mmoja wa makamo ambae alisema ni rafiki wa karibu na Mbunge huyo
alisema " Jamani wanangu acheni mapenzi yaitwe mapenzi ambayo hayana
macho haya hata mkificha lakini baadae kila kitu kitakuwa wazi huyo
kijana ana sifa ya kujua sana mambo anasifika mtaa mzima hivo Mh
alizidiwa na uzalendo akaamua kufunga ndoa nae ili kufaidi ndoa vizuri"
Alisema mama huyo.
Aidha
ishu hii licha kutizamwa kwa jicho la tatu na baadhi ya watu huku ikiwa
na mlengwa wa kisiasa pia watu mbalimbali walitoa komenti zao na
kueleza kuwa Mh huyo hakuwa na kosa kufanya maamuzi ya kuolewa na kijana
huyo ambae kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu huyo kijana ni mtu mzima
kwa maana ya kuvuka miaka 18
WABUNGE WASTAAFU WAPO HOI KIUCHUMI, WAJAZANA KATIKA OFISI YAKE KUOMBA MSAADA...
SPIKA
wa Bunge, Anne Makinda amesema kuwa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi
inayowakabili wabunge wanapomaliza vipindi vyao, ofisi yake imelazimika
kutoa mafunzo ya ujasir
iamali ili waweze kumudu maisha.
Makinda alitoa kauli hiyo jana wakati akibadilishana mawazo na Spika wa Bunge la Uswisi, Maya Graf ambaye yupo nchini kwa mapumziko mafupi na familia yake.
Alisema kuwa kwa kipindi alichokaa katika kiti cha uspika, amebaini matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wabunge waliostaafu.
Makinda alisema kuwa wabunge wengi wamekuwa wakiathirika kiuchumi pindi wanapotoka katika nafasi hiyo, hivyo mafunzo yatawawezesha kuwa na shughuli za kufanya, na kwamba yatatolewa kwa wabunge wote.
Alisema kuwa ni muhimu wabunge wakaichukulia siasa kuwa sio kazi ya kudumu ili wanaposhindwa kuchaguliwa, wafanye shughuli nyingine za kuwaingizia kipato.
“Hata ukiangalia magomvi yanayotokea wakati wa uchaguzi, wengi wasiokubali matokeo ni wale ambao hawana shughuli za kufanya,” alisema.
Spika Makinda alisema kuwa kwa wabunge ambao wana shughuli za kufanya, kwao ubunge unakuwa sio tatizo kwa kuwa wana uwezo wa kuendesha maisha yao.
Alisema tangu ashike nafasi hiyo, wabunge wengi walioshindwa uchaguzi wamekuwa wakifika ofisini kwake na kuomba msaada wa kifedha wakati ofisi hiyo haina fungu la wastaafu hao.
“Kuna siku nilikuwa ofisini walikuja wabunge wastaafu zaidi ya watano wakiomba msaada, ikanilazimu nitoe akiba yangu nikawasaidia baadhi, lakini wale ambao hawakupata chochote walinung’unika sana,” alisema.
Makinda alisema kuwa kabla ya mwaka 1995, Bunge liliweka utaratibu wa pensheni kwa wabunge wastaafu, lakini uliondolewa na anachopata sasa mbunge ni posho ya kumaliza vipindi vyake vya ubunge.
Alisema kuwa na hiyo inatokana na mishahara midogo wanayopata wabunge ukilinganisha na mabunge mengine.
“Hata ukiangalia fedha unayopata, unatakiwa kuigawa na nyingine kupeleka jimboni, nyingine wengine wanatumia wakati wa uchaguzi jambo linalofanya mbunge akikosa kuchaguliwa akose la kufanya,” alisema.
Naye Graf, alisema kuwa wabunge wa nchi yao hawana shida pale wanaposhindwa kuchaguliwa kwa kuwa wana uwezo wa kupata kazi nyingine, na ajira sio tatizo.

-TANZANIA DAIMA.
MBUNGE MBARONI KWA WIZI WA GARI ...
Makalla anamtuhumu Ngonyani a.k.a Profesa Maji Marefu kuwa alichukua
gari lake aina ya BMW X5 kisha akatokomea nalo kisha akawa anampigia
simu hapokei na hata akimtumia SMS hajibu.
Kutokana na malalamiko hayo, hivi sasa Maji Marefu anasakwa na polisi wa Kituo cha Kati (Central), Dar es Salaam, tuhuma zikiwa ni wizi wa kuaminiwa, shauri lipo kwenye kitabu cha ripoti za polisi (Report Book ‘RB’) kwa namba CD/RB/13336/2013.
NYEUPE NA NYEUSI YA TUHUMA ZENYEWE
Nyeupe na nyeusi (black and white) ya tuhuma hizo, inawekwa wazi na ‘sosi’ wetu ambaye aliliibia siri kwamba sakata kati ya Maji Marefu na Makalla lilianza tangu Julai, mwaka huu wakati waheshimiwa hao walipokuwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam.
“Maji Marefu aliomba gari la Makalla ili alitumie kwa mizunguko ya siku moja tu lakini hakurudisha,” kilisema chanzo chetu. “Mgogoro mkubwa ulianza kuibuka kuanzia hapo na mpaka leo waheshimiwa hao hawazungumzi kwa salamu wala kutakiana heri.”
Chanzo chetu kiliendelea kusema: “Siku ya kwanza tu ilipopita, Makalla alimpigia simu Maji Marefu akawa hapokei, akimtumia SMS hajibu. Kwa kifupi Makalla alipoteza mawasiliano na Maji Marefu lakini aliendelea kusubiri kwa sababu anajua ni mtu wake.”
Habari zaidi zinasema kuwa kilipita kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja bila ya Makalla kumpata Maji Marefu kwenye simu lakini walikutana katika Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioketi kati ya Agosti 27 hadi Septemba 13, mwaka huu, Dodoma.
“Walipokutana Makalla alimuuliza Maji Marefu gari lake lipo wapi? Maji Marefu alimjibu alilikabidhi Lamada Hotel, Dar es Salaam,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza: “Unajua makabidhiano ya lile gari yalifanyika Lamada Hotel, kwamba angelirudisha baadaye lakini ikawa kimya.
“Hata hivyo, Makalla aliona siyo kesi kubwa, akafuatilia Lamada Hotel, menejimenti ya hoteli hiyo ilijibu kuwa gari hilo halijapelekwa pale. Vilevile baada ya kuzungumza siku hiyo, Maji Marefu alitoweka na bungeni hakuonekana tena.
“Baada ya kupata majibu hayo kutoka kwa Profesa Maji Marefu na Lamada, Makalla alifungua mashitaka Central, akidai kuibiwa gari lake na Maji Marefu.”
MAKALLA AFUNGUKA
Makalla ambaye ni Mbunge wa Mvomero (CCM) alipozungumza na mwandishi wetu alikubali kila kitu kisha akafunguka: “Niliomba polisi wanisaidie maana kwa hali iliyokuwepo ni kama nilikuwa nimeshatapeliwa. Vilevile niliripoti kwa Kamanda Mohamed Mpinga (mkuu wa kikosi cha usalama barabarani) ili naye awaambie vijana wake wanisaidie kunitafutia gari langu.
“Nilimpa alama zote, rangi na namba za usajili. Oktoba Mosi, mwaka huu, ikiwa ni karibu miezi mitatu imepita tangu nimpe gari, polisi Tanga waliliona gari langu likiwa linaendeshwa na mheshimiwa Ngonyani (Maji Marefu) kwenye msafara wa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
“Nilimtumia SMS kumwambia kuwa gari langu ameonekana nalo katika msafara wa makamu wa rais. Polisi Tanga walitaka kumkamata lakini nikaomba aachwe kwanza, kukamatwa katika msafara wa makamu wa rais angeona amedhalilishwa.
“Nilimuomba baada ya msafara akalikabidhi gari kwa RPC Tanga kwa sababu linatafutwa na polisi. Akaniambia hawezi kulipeleka polisi kwa sababu tulikabidhiana vizuri. Nikamwambia sitaki kwa sababu alikuwa ananizungusha sana kunirudishia gari langu, mara aseme amelipeleka Lamada kumbe bado analo na wakati huohuo hapokei simu wala hajibu SMS zangu.”
USHAHIDI WA SMS
MAKALLA: “Mhe. pamoja na kutopokea simu na kutojibu meseji zangu, nakujulisha leo Oktoba Mosi, umeonekana na gari langu kwenye msafara wa makamu wa rais. Polisi walitaka wakukamate nikashauri wasubiri umalize mkutano. Kwa meseji hii naomba kesho asubuhi ukakabidhi gari langu kwa RPC Tanga, bila kukosa. Utamkuta ndugu Rajabu alipokee gari hilo baada ya ukaguzi mbele ya RPC.”
MAJI MAREFU: “Sawa nimekuelewa, yote ni makosa yangu na hii ni mali yako ila gari hatukupeana polisi, ungeniambia ulipo nikuletee.”
MAKALLA: “Sitaki umenizungusha sana, nilikukabidhi kwa heshima lakini umegeuka adui, hupokei simu huu ni mwezi wa tatu.”
MAJI MAREFU: “Ok nitafanya hivyo.”
MAKALLA ANAENDELEA
“Hakupeleka gari kwa RPC Tanga kama nilivyomtaka. Zilipita kama siku tatu, ndipo mtu mmoja akaenda kulitelekeza gari langu Lamada Hotel usiku. Walinzi walimuuliza yule mtu aliyetekeleza lile gari kwa nini anaacha gari na anakimbia? Hakujibu, akarukia kwenye pikipiki ambayo ilikuwa inalifuata lile gari kwa nyuma kisha akatoweka.
“Uongozi wa Lamada baada ya kuliona gari langu walinipigia simu, wakanijulisha nami nikapiga simu polisi, wakaenda kulichukua. Mpaka sasa gari lipo polisi central, wanasubiri kumkamata Mhe. Ngonyani ili kesi iendelee mbele.”
KAZI YA UWAZI
baada ya kuzungumza na Makalla, lilikwenda kufanya upekuzi wake central na kubaini kwamba kesi hiyi ipo na madai yapo kama yalivyoelezwa.
Baada ya hapo, mwandishi wetu alimpigia simu Maji Marefu ambaye alipokea akiwa Nairobi, Kenya, na aliposomewa tuhuma dhidi yake, alijibu: “Subiri nirudi Dar, nitaeleza kila kitu.” Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;
MWANDISHI: Kuna madai kwamba ulichukua gari la Mheshimiwa Makalla, umekaa nalo miezi mitatu, kipindi chote hicho simu ulikuwa hupokei wala hujibu SMS zake.
MAJI MAREFU: Siyo kweli.
MWANDISHI: Labda ukweli ni upi.
MAJI MAREFU: Labda kwa sababu sipo Dar, nisubiri nirudi tutakaa tuzungumze.
MWANDISHI: Ungeniambia kwa kifupi tu ni kwa nini Makalla akushitaki, maana hii kesi ipo polisi, RB ipo na unatafutwa kwa tuhuma za wizi wa kuaminiwa.
MAJI MAREFU: Polisi wananitafuta mimi?
MWANDISHI: Ndiyo wanakutafuta wewe.
MAJI MAREFU: Kwa vile nipo Nairobi na wewe upo Dar, naomba usubiri tukutane kwanza ndipo nitaweza kueleza ukweli halafu ndipo mtaamua kuendelea mbele.
MWANDISHI: Sawa mheshimiwa, swali lingine wewe una ugomvi na Mheshimiwa Makalla?
MAJI MAREFU: Aah, ndiyo nikasema tukikutana ndiyo italeta picha nzuri. Kama natafutwa au kuna tukio lolote nitaeleza.
MWANDISHI: Sawa mheshimiwa, basi nijibu swali hili, wewe una ugomvi na Makalla?
MAJI MAREFU: Sina ugomvi naye.
MWANDISHI: Sasa kwa nini akushtaki kwa wizi wa gari lake?
MAREFU: Naomba tukutane nikirudi nitaongea tu.
MWANDISHI: Inasemekana hilo gari uliwahi kumwambia Makalla kwamba uliliacha Lamada Hotel lakini baadaye ukaonekana nalo kwenye msafara wa makamu wa rais Tanga. Hili limekaaje?
MAJI MAREFU: Mimi nina magari zaidi ya 15, nitakupeleka uone kama mimi nina shida ya gari. Nyumbani kwangu kuna magari ya kila aina.
MWANDISHI: Ni kweli Makalla alikukabidhi gari?
MAJI MAREFU: Subiri nirudi Dar nitaongelea hilo.
MWANDISHI: Nijibu tu hilo moja tu, alikupa au hakukupa?
MAJI MAREFU: Kwani yeye anasema nilimnyang’anya au alinipa?
MWANDISHI: Anasema alikupa.
MAJI MAREFU: Sasa subiri nirudi nitaeleza ukweli wangu.
MWANDISHI: Kwani mheshimiwa inashindikana nini kunijibu swali hili moja tu? Alikupa au hakukupa?
MAJI MAREFU: Ukweli mtaupata nikisharudi Dar.
POLISI NAKO
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alipoulizwa kuhusu kesi hiyo, kwanza alisema hajapata taarifa yoyote kuhusu sakata hilo mpaka afuatilie.
Siku iliyofuata, Kova alipigiwa tena simu akaulizwa kuhusu sakata hilo, akajibu: “Kuna mtu alinipigia simu jana kuhusu hii kesi, unajua mimi ni kamishna, hii kesi ni ndogo na siyo kila kesi lazima nijibu mimi.
-Gazeti la uwazi Via Gpl

TAZAMA PICHA ZA MJENGO WA KISASA WA MUHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI A.K.A SUGU

SUGU:"NDUNGAI ALIAMURU ASKARI WANIPIGE BUNGENI..."

NI kauli iliyotolewa na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema tukio la kupigwa ngumi na askari ndani ya Ukumbi wa Bunge lilisababishwa na amri ya Naibu Spika, Job Ndugai na wala siyo askari.
Aidha Sugu alisema ilikuwa vigumu kuvumilia konde alilopigwa na askari wakati akitolewa nje kwenye vurugu zilizotokea bungeni hivi karibuni, ndiyo maana aliamua kulipiza kisasi kwa kutaka kumpiga ngumi na si kichwa kama anavyodai askari.
‘Sugu’ alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wakazi wa Chunya Mjini kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dk Willibrod Slaa ambapo viongozi hao wapo ziarani mkoani Mbeya wakifanya mikutano na wananchi kwa lengo la kuwaeleza ukweli wa kilichomtokea Sugu na wabunge wengine bungeni hivi karibuni.
‘ Sugu’ alidai kuwa Ndugai ni adui wa wapinzani bungeni na kwamba kwa vyovyote vile ilikuwa vigumu kuvumilia kwa mtu yeyote baada ya askari kuanza kupiga wabunge kutokana na amri ya Ndugai.
Naye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema kitendo alichofanyiwa Sugu hakikuwa kibaya kwake peke yake, bali hata wananchi waliomchagua.
Hata hivyo, Dk Slaa alisema kwa upande mwingine ili heshima ya Bunge lolote lile duniani iwepo, ni lazima wabunge watandikane makonde ndani ya Bunge na si vinginevyo hivyo hashangai kwa kilichotokea kwa Sugu bungeni.
Dk Slaa, alimjia juu Ndugai akisema alikiuka Kanuni za Bunge kwa kitendo hicho na kubainisha kwamba kanuni za Bunge zipo wazi kabisa kwamba iwapo itatokea vurugu ndani ya Bunge anachotakiwa kukifanya ni kuahirisha Bunge kwa wakati huo.
Pia alisema askari ambao ni wapambe wa Bunge ‘Sargent at arms’ ndio wenye mamlaka ya kuingia ukumbini na endapo itatokea nguvu ya ziada hao ndio wanaotakiwa kisheria na siyo kuwaita askari wa nje ya Bunge kuingia ndani.
Dk Slaa alisema kitendo kilichofanywa na Sugu pamoja na wabunge wengine ni cha kijasiri na aliwataka kutokurudi nyuma na misimamo yao bali waendelee kusonga mbele.
TUNDU LISU AKAZA,AKATAA UAMUZI WA CCM KUTAKA KUIFUTA KESI YAKE

WAKATI viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiwasili mjini Dodoma kuungana na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, katika rufaa ya kupinga ubunge wake inayoanza kusikilizwa leo, mbunge huyo amekataa uamuzi CCM kutaka kuifuta kesi hiyo.
Juzi CCM kupitia kwa wakili wake, Godfrey Wasonga, iliwasilisha barua katika Mahakama ya Rufaa Dodoma na nakala kwa Lissu ikiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo.
Kwa mujibu wa wakili huyo, sababu ya kuomba kufutwa kwa kesi hiyo ni walalamikaji wote kujitoa na kuapa mahakamani kuwa hawakuwa tayari kuendelea na kesi hiyo.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana, zilisema kuwa viongozi kadhaa wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, wajumbe wa Kamati Kuu na wabunge kadhaa wa chama hicho tayari walikuwa wamewasili mjini Dodoma.
Hata hivyo, akizungumzia kesi hiyo, Lissu alisema kuwa hatakubali ‘withdrawal’ isipokuwa anataka ‘dismiss with cost’.
Lissu alisema kuwa Wasonga atalazimishwa kulipa gharama kwa kuwa hati ya kiapo cha Selema ni ya mwezi Juni 25, mwaka huu, na kwamba kutaka kuiondoa siku mbili kabla ni uhuni.
Shabani Selema na Paskali Hallu ni wanachama wa CCM wakazi wa kijiji cha Makiungu, mkoani Singida, ambao walifungua kesi ya msingi ya kupinga ubunge wa Lissu.
Lakini baada ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kumtangaza Lissu kama mbunge halali, walikubaliana na hukumu hiyo ya Aprili 27, mwaka huu.
Mara kadhaa wananchi hao wamenukuriwa wakimlalamikia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwa anawashinikiza kuendelea na rufaa hiyo licha ya kwamba walishajitoa.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Wasonga, ambaye alikuwa akiwatetea wanachama hao katika kesi hiyo, alisema kuwa baada ya kuwasiliana na wateja wake walimwambia hawakuwa tayari kuendelea na kesi hivyo.
“Ni kweli walalamikaji wote wamejitoa na mimi kama wakili sioni haja ya kuendelea; nitakuwa namwakilisha nani?
“Niliongea nao jana hakuna; mwenye nia ya kuendelea na kesi,” alisema.
Rufaa hiyo imepangiwa kusikilizwa katika Mahakama ya Rufani na Jopo la Majaji watatu, Salumu Massati, Engela Kileo na Natalia Kimaro.
Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa hiyo, mahakama ilitarajiwa kusikiliza pingamizi zilizotolewa na upande wa walamikiwa ambao ni Lissu na jamuhuri za kupinga rufaa hiyo na jopo hilo la majaji litatoa maamuzi.
Tayari Lissu alitoa hoja saba za kupinga rufaa hiyo, ambazo ni mkata rufaa Seleman ambaye ndiye mlalamikaji namba moja kupinga kwamba hajakata rufaa kwa hati ya kiapo ya Mei 24 mwaka huu.
Alisema hoja nyingine ni notisi ya kiapo kutopelekwa kwa mjibu rufaa ambaye ni yeye kinyume na masharti ya kanuni ya 84 (1) ya Kanuni za Adhabu za Mahakama ya Rufaa Tanzania za mwaka 2009.
“Vile vile nakala zote rekodi za rufaa hazijathibitishwa usahihi wake na wakata au wakili kinyume na masharti ya Kanuni ya 96 (5) ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa Tanzania za mwaka 2009.
“Rufaa hii pia imepitwa na muda wake kwa sababu hati ya ucheleweshaji iliyotolewa na Msajili wa Mahakama Kuu haijasainiwa, haina tarehe wala muhuri kinyume na Kanuni ya 90 (1) ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa ya Tanzania za mwaka 2009,” alisema.
Lissu aliongeza kuwa walalamikaji walitakiwa kukata rufaa siku sitini baada ya notisi ya rufaa kutolewa na kwamba tarehe ya mwisho ya kukata rufaa ilikuwa Julai 3 mwaka jana lakini rufaa hiyo ilikatwa Mei 7 mwaka huu.
“Hoja nyingine ni kwamba rufaa hiyo si halali kwa kuwa imeacha nyaraka muhimu ikiwemo maombi ya mwenendo wa shauri wa kusamehewa gharama za dhamana,” alisema.
Lissu alisema pia katika rufaa hiyo, amri iliyomshindisha kesi si halali kwa kuwa haionyeshi tarehe ambayo amri hiyo ilitolewa kinyume na kanuni ya 9 ya Kanuni za Masijala za Mahakama Kuu za mwaka 2005.
Alisema pia wakata rufaa wamesindwa kuwasilisha mahakamani hoja za maandishi za kuunga mkono hoja za rufaa yao ndani ya siku 60 au kuomba muda wa kuziwasilisha.
Pia hoja nyingine ni kushindwa kuwasilisha hoja hizo za maandishi kinyume cha Kanuni ya 106 (1), (2) na (9) ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa ya Tanzania za mwaka 2009.
Kesi ya kupinga ubunge wa Lissu ilianza kusikilizwa Machi 12, 2012 na Jaji wa Mahakama Kuu, Moses Mzuna, aliyetoa hukumu April 27, mwaka huu, na kumtangaza Lissu kuwa mbunge halali wa Singida Mashariki kwa kigezo kuwa hoja zote zilizotolewa na wanachama hao wa CCM hazitoshi kutengua au kubatilisha ubunge wake.
-Tanzania Daima

Subscribe to:
Posts (Atom)