Like Us On Facebook
Showing posts with label WASANII. Show all posts
Showing posts with label WASANII. Show all posts

Baby Madaha atangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na maisha ya presha



IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego  wa kujiuza,  staa wa Bongo, Baby Madaha ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na  maisha ya presha.

Akiongea  na  mwandishi wetu  juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.
 
Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa upande wake.
 
“Nimeamua kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka kutaja), maana naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.

“NILIWAHI KULIPWA MIL 10 KWA KUFANYA SHOW MOJA YA MUZIKI MSIFIKIRI DIAMOND NDIO WA KWANZA”….MB DOG

mbdogKama ulifikiri bongo fleva ilianza kulipa mamilioni miaka ya akina Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na wengine, nikimaanisha kuanzia mwaka ya 2010, kwa leo inabidi ubadili mawazo yako.
“Lakini uzuri wakati mimi naanza kufanya, kazi zilifanyika na misingi za ile kazi zilikuwa zimekaa tofauti na watu wanavyosikia. Kwa hiyo uoga hata wa mapromota ulikuwepo wakati wanatusogelea. Kwa hiyo hatukuwa tunalipwa laki tatu viiile.” Mbwana Mohammed aka MB Dog ameiambia tovuti ya Times Fm.

Huenda inawezekana ulikuwa hujui kwa sababu wakongwe waliokuwa wanahit enzi hizo hawakuwa na tabia ya kuweka wazi kiasi wanacholipwa kama wanavyofanya wakali wa bongo flava wa kizazi hiki cha dijiti.

Mkali huyo wa ‘Latifa’ ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa alikuwa anakutana na milioni kadhaa kwenye show zake, na kwamba kiasi kikubwa zaidi alichowahi kulipwa kilikuwa shilingi milioni kumi nchini Burundi.

“Yaani mimi show ya kwanza nimeanza kuifanya nimelipwa milioni tatu, show ya mwisho mimi kuifanya nimelipwa milioni kumi…ambayo ndiyo ilikuwa show ya maajabu yaani…kwa ubongo wangu  nawaza naweza kufanya show tena ya watu wengi kama wale!! Nadhani ilikuwa mwaka 2006.” Amesema MB Dog na kusisitiza, “milioni kumi za kitanzania”Kumbe Bongo Flava ilianza kulipa zamani japo kwa wachache! Na huenda ni kwa sababu tu watu walikuwa hawaweki wazi wanachoingiza.

Hapa tumpigie picha Mr. Nice wa enzi hizo kwa kutumia mfano wa MB Dog.

Kama kweli mambo yalikuwa hivi, inaweza kuwa moja kati ya sababu zilizozaa wazo kati ya wakongwe Juma Nature na Lady Jay Dee kutaka Leo iwe ‘Kama Jana’.

LINAH ADUNGWA MIMBA NA MDOSI WA KIHINDI

MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga maarufu kama Linah, anadaiwa kupewa ujauzito na kijana mmoja wa Kihindi anayejulikana kwa jina moja la Nagar.
Estelinah Sanga 'Linah'.
Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili kuwa msichana huyo aliyeibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha THT, amekuwa karibu na Mhindi huyo anayedaiwa kuishi Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana kumfurahisha sana msanii huyo.
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na inaonekana hii mimba ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi wake,” kilisema chanzo hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe.
Chanzo hicho kilisema Linah alikutana na mdosi huyo katika harakati zake za kimuziki na kwamba jamaa ameoza mno kwa binti huyo, mkali wa albamu ya Atatamani.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, lakini baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu suala hilo, alipiga simu na kukanusha vikali tuhuma hizo.
“Nani kakwambia kama nina mimba? Hakuna kitu kama hicho, hayo ni maneno ya watu wanasambaza mtaani, mimi hata sijui wananitaka nini,” alisema.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia habari hizo, alisema anazisikia na kusisitiza kuwa siyo za kweli. Lakini alipotakiwa kusema kama anamfahamu Nagar, alimtaka mwandishi kuachana na habari hizo.
“Wewe si umeuliza habari za mimba? Sasa hayo mengine yanatoka wapi, ulichotaka kujua nimekujibu, hayo mambo mengine achana nayo,” alisema bila kufafanua zaidi

KESI YA KIFO CHA KANUMBA... LULU AANIKA UKWELI,MAMA KANUMBA AMWAGA MACHOZI!!

MWANGA umeanza kuonekana juu ya kesi inayomkabili staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kumuua bila kukusudia staa mwenzake wa muvi, Steven Charles Meshack Kusekwa Kanumba ambapo safari hii aliamua kukiri vipengele kibao, Risasi Mchanganyiko lina habari yote.
Elizabeth Michael 'Lulu' aliyeambatana na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ wakiwa eneo la mahakama.
Akikiri mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania juzi (Jumatatu) wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, nyota huyo aliweka wazi mambo ambayo hapo awali hakuwahi kuyakubali kortini jambo lililovuta hisia za wasikilizaji waliokuwa wamefurika ndani ya chombo hicho cha kutoa haki kujua kinachoendelea.
Mwendesha mashitaka wa upande wa serikali, Monica Mbogo alivitaja vipengele kadhaa ambavyo Lulu alitakiwa kuvikana au kuvikubali.
Lulu, mama yake mzazi Lucresia Karugila wakiongea na mwanasheria wao, Peter Kibatala mahakamani.
Katika kesi hiyo iliyoendeshwa kwa ustadi mkubwa wa wanasheria kuoneshana ujuzi wa kusoma na ‘kubugia’ vipengele vigumu vya sheria, Lulu alipata wakati mgumu wa mambo kiasi cha kumwita wakili wake, Peter Kibatala mara kwa mara.
MADAI YA KUMUUA KANUMBA BILA KUKUSUDIA
Lulu alikiri kwamba, mashitaka yake mahakamani hapo yalikuwa ya kumuua bila kukusudia, marehemu Steven Kanumba Aprili 7, mwaka 2012.

Lulu akiongea na mama yake kabla kesi yake kuanza kusikilizwa.
KUWEPO ENEO LA TUKIO NA KUTOKEA KWA UGOMVI
Katika maelezo yake, Lulu aliweka bayana kuwa siku ya tukio alifika nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza ya Vatican jijini Dar saa 6 usiku na kuingia moja kwa moja chumbani.
Alizidi ‘kuchezesha taya’ kuwa, kulitokea ugomvi kati yake na marehemu licha ya kutotaja chanzo cha ugomvi huo.

Aliongeza kwamba, Kanumba alimvuta mkono na kumrudisha ndani wakati alipokuwa akijaribu kukimbia na kuufunga mlango, mwishowe alifanikiwa kutoka na kukimbia kusikojulikana.
KUKAMATWA KWAKE BAMAGA
Lulu aliweka wazi kuwa, siku ya tukio, saa 11alfajiri alikamatwa maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam alipokuwa akijaribu kutorokea kusikojulikana.

KUHUSU UHUSIANO
Bila kupepesa macho wala kuchezesha kope, Lulu alikubali kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Kanumba kwa muda ambao hakuutaja hali ambayo baadhi ya watu walionesha kuwa ‘sapraizidi’.

AMWAGA MACHOZI KORTINI
Awali, Lulu alipofika mahakamani hapo akiwa ameongozana na mama yake mzazi, Lucresia Karugila na staa wa muvi za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ alionekana kuwa na amani.

Msanii huyo alimudu kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda ambalo liliingia mtaani siku hiyo. Lakini baada ya kuanza kwa kesi, ilifika mahali alidondosha machozi hali iliyomlazimu kujifuta uso kwa kitambaa.
Baadhi ya watu walinong’ona kuwa, mrembo huyo alikuwa analizwa na kumbukumbu za tukio la kifo cha Kanumba na kwa sababu ya kuogopa kesi.

MAMA KANUMBA ASUSA
Habari nyingine zilidai kuwa, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa hakutokea mahakamani hapo licha ya umoja na udugu alionao kwa sasa na familia ya  Lulu.

Ilidaiwa kuwa sababu kubwa ya kushindwa kufika kortini ni kukosa uamuzi wa upande gani angekaa kati ya mshtakiwa (Lulu) na mshitaki (Jamhuri) kwa vile kote kuna muhusu kwa sasa.
“Unajua mama Kanumba alipogundua kwamba anayetakiwa kujibu madai ni Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu alimtangaza ni mwanaye na anayelalamika ni serikali, alishindwa kujua akija leo (juzi) angekaa upande gani? Akaamua kutokufika kabisa,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Mchanganyiko lilimsaka kwa simu mama huyo lakini bila mafanikio kufuatia simu yake ya mkononi kuita muda mrefu bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Lulu alikamatwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa galacha wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba mnamo Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza Vatican jijini Dar.

Baada ya kukamatwa na kuswekwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar, Lulu alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo hakutakiwa kujibu ndiyo au hapana.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ya madai hayo.
Aliachiwa kwa dhamana Januari 29, 2013 na kuambiwa kwamba kesi yake itakaporudi, itakuwa chini ya mahakama kuu. Juzi ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza.

-GPL

JUMA NATURE AKANUSHA UVUMI KUWA KAMPONDA DIAMOND KWENYE WIMBO WAKE MPYAA,MSIKILIZE NATURE AKITOLEA UFAFANUZI JAMBO HILO

Hatimaye Juma Nature, amezungumzia utata ulioibuka kwenye wimbo wake mpya Kama Jana, unaohusiana na kama kweli amemdiss Diamond.
Akiongea na kipindi cha Showtime Next Chapter, Juma Nature aka Kiroboto amesema jina la ‘Dada Mondi’ lililofanya wengi waamini kuwa ni version yake ya Diamond, ni jina la msanii mwingine kabisa. “Hamna diss ya kumdiss Diamond, Diamond hajadisiwa,” amesema Nature. “Pale katajwa mtu mwingine kabisa anaitwa Dada Mondi na anakaa mitaa ya kwetu. Bado hajatoka halafu anataka sifa.”
nature
Msikilize hapo chini.

 

AIBU:DIVA WA CLOUDS APEWA MAKAVU LIVE KUHUSU "MATAKO YAKE YA BANDIA

Huddah kushoto na Diva kulia..
Diva Loveness Love apewa maneno mazito na matusi kutoka kwa mashabiki wanaomfatilia katika kazi zake za hapa na pale. katika kauli hiyo shabiki huyo alifunguka na kumjadili Diva vya kutosha
 

Nanukuu "Huyu diva hivi ana akili kweli kudanganya watu kweupe ndio nini ... Embu angalieni hiyo picha ndio mtaelewa Yani Kabisa milima na mabonde kuvaa godoro ndio ili iweje ... Diva acha ujinga unachekwa mjini kwa kutafuta tako kinguvu acha kuvaa maana shape inajulikana ni Ya simba,, cha ajabu ukikutana nae hayupo hivyo kabisaaaaaaa...
 Na camera 360 acha kabisa unajipimp sana wakati We ni mbaya kuvaa malenz mwisho utapata macancer Ya macho Bure... ... Swala ni kuacha kuvaa matako bandia usishindane na hudda mwenzio kaajaliwa"

DIAMOND NA D'BANJ KUJA NA MAMBO MENGINE, YASOME HAPA mambo hayo!


pichani ni Diamond Platnumz na D' BANJ wakiwa studio ready kutengeneza muziki mpya, sasa Diamond kutoa nyimbo nyingine na D'BANJ..Diamond alipost hiyo picha na kuandika maneno haya hapa chini...

Busy day....Studio session with King D'Banj... Cc @iambangalee

MODEL WA TANZANIA HAMISA AZUNGUMZIA KUTOA PENZI KWA MWANAMUZI DIAMOND...HUYU HAPA

MREMBO anayedaiwa kuliingilia penzi la staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliyewahi kushiriki Shindano la Miss Tanzania, Amisa Mabeto amefunguka kuwa  mwanamuziki huyo ni shemeji yake tu, hakuna chochote kati yao.
Amisa Mabeto.
Akipiga stori na safu hii kuhusiana na madai hayo, Amisa alisema alistaajabu kwani hana mazoea na Diamond Kama ni kuonana waliwahi kuonana miaka ya nyuma, tena siyo kimapenzi.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima inajua yupo na Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa, hana chake hapa, siwezi kutembea naye kamwe, namheshimu kama shemeji yangu,” alisema Amisa.
Amisa aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano na Diamond akiwa ni shosti mkubwa wa Wema.

LULU AKUMBUKA MAPENZI YA KANUMBA VALENTINE’S DAY

WAKATI kesi yake juu ya kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, Steven Kanumba ikianza kurindima leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa la moyoni akikumbuka mapenzi ya jamaa huyo aliyetangulia mbele za haki.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Lulu alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) iliyosherehekewa duniani kote Ijumaa iliyopita.
 
Marehemu Steven Kanumba.
“Kuna mtu natamani kumtakia Happy Valentine’s Day kwa kuwa nakumbuka mapenzi yake kwangu lakini kwa bahati mbaya siwezi kwa sababu hayupo na haiwezekani tena,” alisema Lulu.
Hata hivyo, alipobanwa amtaje, staa huyo ambaye ni sura ya mauzo ya filamu za Kibongo alikiri kuwa ni Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012, siku ambayo kamwe hawezi kuisahau maishani mwake.

PICHA YA HUDDAH NA MUSTAPHA YAMUWEKA PREZZO ROHO JUU

Jana, picha ilienea online ya socialite Huddah Monroe na Kanali Mustapha katika nafasi yapose la kula bata.
Hii ilisababisha uvumi kwamba wawili walikuwa design wana date sasa hivi. Siamini katika tetesi hivyo nilikuwa na kupata moyo wa suala hilo na kujua kwa kweli alikuwa kupikia katika kati ya them.And maoni haya kwa Mustapha juu ya Instagram kushika nafasi udadisi wangu "Colonelmustafa Pamoja na bosi wanguLADY @ huddahrepublic I got hottest kifaranga katika mchezo "

lakini chanzo chetu kimemtafuta jamaa na kumhoji lakin mustapha alidai yeye na huddah ni marafiki na hana lengo kumuumiza king mswati prezzo

UJUE UKWELI KUHUSU SKENDO YA IRENE UWOYA KUSAGANA NA MARIAM ISMAIL, SOMA HAPA!



Mariam Ismail
Mastaa wa filamu nchini Mariam Ismail na Irene Uwoya wanadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi(usagaji) na kudaiwa kuishi pamoja kabisa.


wiki kadhaa nyuma muigizaji mmoja chipukizi anayekuja juu kwa kasi aliutonya mtandao huu kwa kusema " Mariam Ismail na Uwoya wanasagana tena wanaishi pamoja kabisa, fuatilieni mtajua". Baada ya habari hizo ilibidi Swahiliworldplanet kuwatafuta mastaa hao, wa kwanza kutafutwa akiwa Irene Uwoya lakini namba yake ya simu kwa takribani wiki 2 ilikuwa haipatikani na hata jana alipotumiwa ujumbe kupitia namba yake nyingine hakujibu.

Baada ya hapo ilibidi kumtafuta Mariam Ismail ambaye wamecheza filamu nyingi na Irene Uwoya kama vile Sobbing Sound, Omega Confusion, The Return Of Omega na Apple, Hata hivyo Mariam anafanya vizuri katika filamu alionekana kuwa busy na kuchelewa kujibu ujumbe wa madai ya kusagana na Uwoya lakini jana star huyo aliyejipatia umaarufu kwa kuuvaa vizuri uhusika katika filamu zake alitoa ushirikiano mzuri kwa kujibu madai hayo akidai sio kweli ila yeye na Uwoya ni marafiki wa karibu sana na wanasaidiana katika shida na raha ndiyo maana baadhi ya watu wameshaanza kusema vibaya...

"Nadhani mimi ndio mtu wa kwanza kupiga vita upumbavu kama huo... mimi ni mwanamke ambae nimeumbwa kikamilifu.. sina kasoro yoyote ya kunifanya niwe na mwanamke mwenzangu....hao wanaofanya upumbavu huo nadhani wana vijikasoro kwenye mili yao.... Irene Uwoya ni rafiki yangu sana tena urafiki wetu sio wa leo wala kesho... ni marafiki wa kushibana kabisa... nikoseapo huwa ananikosoa na yeye akoseapo huwa namkosoa....sometimes huwa tunagombana na kupatana vitu ambavyo ni vya kawaida katika maisha." alisema Mariam ambaye hajawahi kukumbwa na skendo yoyote ile kabla.

Mariam ambaye kipaji chake cha filamu hujionyesha waziwazi alimalizia kwa kusema "Irene ananiheshimu sana na mimi humuheshimu sana Irene, imefikia hatua ya mimi na yeye tukakaa chini na kupanga tuishi wote kitu ambacho sioni tatizo na hilo. Ingekua ni chumba kimoja hapo sawa... lakini ni nyumba kubwa yenye kujitosheleza...kila mtu na room yake...tunaishi kwa amani na kwa kushirikiana penye tatizo hulitatua wenyewe bila kumshirikisha mtu. Ukimya wetu na kupatana kwetu kusiwafanye watu kuanza kuhisi upumbavu juu yetu... natumai ujumbe wangu utawafikia mashabiki wangu wote. Asante. In god I trust."



Irene Uwoya

ROSE NDAUKA CHUPUCHUPU KUVULIWA NGUO NA WATOTO WADOGO,SOMA HAPA KUJUA KISA

MWIGIZAJI mahiri Bongo, Rose Ndauka amefunguka kuwa amenusurika kuvuliwa nguo na watoto ambao walipandwa na midadi baada ya kumuona ‘live’.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika sherehe ya arobaini ya mwanaye iliyofanyika nyumbani kwao, Tandale-Tanesco, jijini Dar ambapo watoto hao walimvizia Rose alipotoka nje, walimvaa na kuanza kumng’ang’ania nguo.

“Hawakutegemea kuniona pale, wengi wamezoea kuniona kwenye TV. Daah nilipata wakati mgumu kidogo maana ilibaki kidogo wanivue nguo, lakini nashukuru Mungu niliwatuliza, wakanielewa nikarudi zangu ndani,” alisema


MWIGIZAJI NA SHOGA MAARUFU WA NOLLYWOOD NIGERIA AFARIKI GHAFLA

 
Mwigizaji maarufu Charles Warren enzi za uhai wake.
Mwigizaji maarufu Charles Warren ambaye ni shoga anayeigiza sinema katika tasnia ya sinema ya Nollywood nchini Nigeria amefariki ghafla alhamisi iliyopita majira ya usiku katika Hospitali moja jijini Lagos nchini Nigeria.
Charles Warren alifariki ghafla wakati akiifanya mapenzi (akimegwa) na mwenzake aliyetajwa kwa jina la Ajah ambapo ghafla alianza kulalamika maumivu ya kiuno na baadaye maumivu hayo yakahamia mgongoni ambapo baadaye alipata haja kubwa mara nne ndani ya muda wa dakika 30.
Baadaye maumivu hayo yalihamia kifuani ambapo ilibidi awahishwe katika hospitali ya Safeway kwa matibabu zaidi. Rafiki yake aitwaye Ajah ambaye ndiye waliyekuwa wakifanya naye mapenzi alijaribu bila mafanikio kumfanyia masaji kifuani ili kumpunguzia maumivu lakini haikusaidia, Warren alifariki dunia usiku huo huo.RIP Charles Warren.

MSANII WA BONGO MOVIES "SABBY ANGEL" AAMUA KUJIUZA MTANDAONI...TAZAMA PICHA ZAKE ALIZOPIGA..

Tanzanian actress Salma Tamim(Sabby Angel) has posed topless for a photoshoot in Kenya. The actress who has already started to make waves in the industry with movies opposite big names including Vicent Kigosi(Ray) and Muhsin Awadhi(Dr.Cheni) looks extremely hot in the shoot. Sabby was in Kenya for almost two weeks and news is that there are some Kenyan film companies which have already shown interest to work with this Tanzanian bombshell actress. No doubt Sabby is one of the most sexiest actresses in Tanzania. She is also a singer and model and you can like her page Here

Check out the exclusive  images below..................
 
          Oooh babyy..................

oohh.......... this is definetly Sabby "Angel"
and we loved the styling....
Does she look hot or not...?
COVER

Part 2 of her photoshoot coming soon right here.........

WEMA AFUNGUKA:"PIGA UA LAZIMA DIAMOND ANIOE"

Licha ya mama yake mzazi kupinga kwa nguvu zote, staa wa filamu nchini na mtangazaji wa Kipindi cha Runinga cha In My Shoes, Wema Sepetu ameapa kwamba hata iweje, lazima msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond’ awe mume wake, Amani lina stori kamili.
Wema akiwa na mpenzi wake Diamond.
NI CHAGUO LAKE
Akizungumza na Amani katika spesho intavyu hivi karibuni, Wema ambaye kwa sasa anapika na kupakua na Diamond alifunguka kuwa, amepita kwa wanaume wengi ila anaamini mwanaume huyo ndiye chaguo lake.
Alisema katika uchunguzi wake aligundua kwamba Diamond anampenda kupita maelezo na kwa mapenzi anayomuonesha hana sababu ya kugoma kumpa nafasi ya kuwa mkewe.
Wema na Diamond katika pozi la kimahaba.
“Yaani watu watasema sana lakini piga, ua, garagaza, lazima Diamond anioe. Amekuwa akilizungumzia hilo na kuonesha kuwa yuko ‘siriasi’ hivyo ipo siku historia itaandikwa bila kujali nani atasema nini.
“Unajua mimi ni mtu ninayejitambua na ninayejali maisha yangu hivyo ninapobaini mwanaume f’lani anaonesha kunijali na kunipa mapenzi ninayoyahitaji, kwa nini nisikubali kuingia naye kwenye maisha ya ndoa…?
“Kwa kifupi nampenda Diamond na yeye ananipenda, that’s it,” alisema Wema.
MKWARA WA MAMA YAKE
Kuhusu mama yake kuchimba ‘biti’ kuwa hamtaki Diamond na kamwe hawezi kukubali mwanaye aolewe na mwanaume huyo, Wema alisema:
“Unajua yule ni mzazi, wakati mwingine si mbaya kuonesha hisia zake lakini nitamseti na naamini kwa kuwa ananipenda atakubaliana na mawazo yangu.”
NDOA LINI?
Alipobanwa kuhusu lini watafunga ndoa kwani wamekaa kwenye uhusiano kwa muda mrefu huku wakiachana na kurudiana, Wema alionekana kutokuwa na jibu la moja kwa moja ila akaishia kusema kuwa, siku ikifika kila kitu kitakuwa wazi.
NUKUU YA MAMA WEMA!
Katika sakata hilo, kwa upande wake mama Wema alikuwa na haya ya kusema: “Ndoa yao watafungia chumbani, si hadharani, tena wakiwa na ndugu wa upande mmoja tu wa Diamond.
“Sisi hatuwezi kushiriki ng’oo, ndugu zangu wakijitokeza tu nitakuwa na panga  mkononi, watakiona cha moto.”
 
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki, Dar, Diamond aliwahi kumvisha pete ya uchumba Wema na ikadaiwa kuwa siku nyingi wangeingia katika maisha ya ndoa lakini haukupita muda mrefu wakaachana.
Baada ya kumwagana, Diamond alikwenda kwa mtangazaji wa DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema alihamishia penzi kwa yule kigogo aliyefahamika kwa jina moja la Clement ‘CK’ kabla ya kumwagana hivi karibuni.

MASOGANGE AWACHARUKIA MIDUME INAYOMTONGOZA

VIDEO Queen matata Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ amewajia juu kundi kubwa la wanaume linalomtaka kimapenzi wakati wanatambua vyema kuwa ana mtu wake.
Agnes Gerald Waya ‘Masogange’.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Masogange alisema tangu atoke Sauz aliponaswa kwa msala wa kusafirisha malighafi haramu, wanaume wakware wamekuwa wakimsaka kama fisi aliyeona mfupa kitu ambacho hakubaliani nacho.
“Sitaki kutongozwa kabisa, waniache. Kinachonikera zaidi wanaonitongoza wengi wanatambua kabisa nina mchumba wangu (Evance), watu wengine sijui wapoje!” alisema Masogange.

DIVA AVUNJA UKIMYA....!!! AAMUA KUWEKA PICHA AKIPIGWA BUSU NA GK AMBAE INASEMEKANA NDIYE MPENZI WAKE KWA SASA.

Diva akipenda, ulimwengu wote utajua. Hajui kuficha siri na haoni shida kuweka wazi hisia zake wote wajue. Na kwakuwa Valentine’s Day ndio hii, mtangazaji huyo wa redio ambaye kwa sasa ana uhusiano na rapper wa East Coast Team, King Crazy GK, amewaonesha followers wake wa Instagram kuwa kwa sasa si Diva the Bawse tu, bali ni ‘Diva the Queen’.

Diva amepost picha inayomuonesha akipigwa busu shavuni na Mfalme wake na kuandika: Me and My GK….. closer .. kisses from US.”
Mambo ya Valentine’s Day.


 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari