Like Us On Facebook
Showing posts with label Unyama. Show all posts
Showing posts with label Unyama. Show all posts

UNYAMA: KIJANA AUA MAMA YAKE KWA JEMBE HUKO KAHAMA,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA

Katika hali ya kusikitisha ,kuhuzunisha na isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakuhenga wilayani Kahama mkoani Shinyanga amemuua mama yake kwa kumkata na jembe kichwani na kusababisha kifo chake.
Habari kutoka Kahama zinasema tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili usiku na chanzo halisi cha tukio hilo bado hakijajulikana.

Habari kamili kuhusu tukio hili tutakuletea kupitia kwenye blog hii

CHANZO: MALUNDE BLOG

MWANDISHI WA HABARI WA MWANANCHI AMEJERUHIWA NA KUNDI LA WANANCHI LINALODAIWA KUWA NI WANACHAMA WA CHAMA FULANI CHA SIASA.!

Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd mkoani Mara, Christopher Maregesi amejeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Bunda, baada ya kundi la watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa moja ya vyama vya siasa wakiwa na viongozi wao kumteka ambapo walimmpiga, kumtesa na kumjeruhi huku wakimpora vitendea kazi vyake ikiwamo kamera.
 

 Habari zinasema Maregesi alikutwa na mkasa huo wilayani Bunda juzi saa 12:30 jioni, wakati akipiga picha tukio la vijana wa chama hicho kumteka na kumpiga kijana anayedaiwa kuwa kada wa Chadema.

 Akisimulia mkasa huo akiwa katika wodi ya wanaume Hospitali ya Bunda, Maregesi anadai kuwa alikabwa na viongozi wa chama hicho wakati akipiga picha za tukio la kada huyo wa Chadema aliyeshushwa kutoka ndani ya gari na kuanza kushambuliwa na vijana waliokuwa pamoja na viongozi hao.

 Anafafanua wakati akiendelea kupiga picha tukio hilo, ghafla Mwenyekiti wa chama hicho wa mkoa alimkaba kwa madai kuwa atawaumbua na kusaidiana na kiongozi mwenzake ambaye alichukua kamera na ghafla kundi la vijana wa chama hicho wakamvamia,kuanza kumpiga na kumpora mkoba aliokuwa nao, kisha wakamfungia ndani ya chumba
cha ofisi yao.

 "Ndani ya chumba nikaingizwa mimi na huyo kijana anayedaiwa kada wa Chadema na kuanza kutupiga, ndipo mtu mmoja akasema mtawaua hawa iteni polisi baadaye askari wa JKT walioletwa maalumu wilayani Bunda kulinda Kata ya Nyansura ndiyo waliotufikisha Kituo cha Polisi Bunda," alibainisha Maregesi.

 Anataja vitu alivyoporwa kuwa ni kamera aina ya Sony digital, risti zake, daftari la kuandikia habari (Note Book), Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, simu ya mkononi aina ya Adio pamoja na vitu vingine mbalimbali.

 Akizungumzia hali ya Maregesi mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Bunda, Dk Nimrod Mzuma alisema mwandishi huyo anakabiliwa na maumivu makali katika uti wa mgongo, kichwani na mkono wa kulia na kwamba alifikiswa hospitali hapo akiwa na watu wengine wawili waliojeruhiwa katika tukio hilo pia.

 Akizungumzia tukio hilo, Emanueli Imanani Katibu wa Chadema wilaya anavitaka vyama vya
siasa kuheshimu taaluma ya uandishi wa habari.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Fernandi Mtui,alikanusha kuumizwa kwa Maregesi na kueleza kuwa ameonana na mwandishi huyo kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi akiwa hana majeraha yoyote.

 Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mara (MRPC) Emanuel Bwimbo,alilaani tukio hilo akisema linavunja haki ya upatikanaji habari na kwamba limefanywa na viongozi waliopaswa kuwa mfano wa kuigwa.

 "Tunaomba wamuombe radhi Maregesi na waandishi wote, pia wamrudishie vifaa vyake haraka ili aendelee na majukumu yake. Wasipotekeleza hayo chama kitachukua hatua ikiwa pamoja na kumsaidia kuendesha kesi mahakamani ili kupata haki yake,"alisema Bwimbo.
source: mwananchi.

UNYAMA:.Polisi 8 watuhumiwa kumtesa mahabusu mwanamke kwa kumvua nguo na kumwingizia chupa ya bia katika sehemu za siri

ASKARI Polisi saba wa kiume na mmoja wa kike, wanakabiliwa na tuhuma za kumtesa mahabusu mwanamke kwa kumvua nguo na kumwingizia chupa ya bia katika sehemu za siri.
 
Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi wa mjini Sumbawanga, Rosalia Mugissa, mshitakiwa katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Clara God (32), alidai kufanyiwa unyama huo na askari wa kiume mbele ya askari mwanamke.
 
Clara, ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa kitongoji cha Chanji na washtakiwa wengine watatu wa kiume akiwemo mganga wa kienyeji, wanakabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na wako rumande kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana.
 
Kabla ya kutoa madai hayo, kesi hiyo ililetwa jana kwa ajili ya kutajwa na Mwendesha Mashitaka, Wakili wa Serikali, Simoni Peresi aliomba shauri hilo liahirishwe kwa kuwa upelelezi wake bado haujakamilika.
 
Hata hivyo, Hakimu Mugissa aliwauliza washtakiwa iwapo wana hoja yoyote ile ya kueleza mahakamani hapo, ndipo Clara alipoieleza mahakama hiyo kuwa ana hoja.
mahabusu
 
Kukamatwa
Huku akibubujikwa na machozi alidai kuwa usiku wa Desemba 11 mwaka jana, askari Polisi walifika nyumbani kwake katika kitongoji cha Chanji na kumtaka aeleze alipomficha mumewe ambaye alikuwa akituhumiwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
 
“Mie niliwajibu kuwa mume wangu yupo mjini Namanyere (wilayani Nkasi) kwa mke mwenzangu, ndipo wakanichukua kwa nguvu na kunibambikia kesi hii ya unyang’anyi wa kutumia silaha,” alidai.
 
Alipofika mahabusu kabla ya kuanza kuhojiwa, Clara alidai alipekuliwa na askari saba wa kiume ambao walimlazimisha kuvua nguo zote pamoja na za ndani.
 
Alidai askari hao walianza kumwingizia vidole katika sehemu zake za siri kwa zamu huku wakimlazimisha ataje mahali alipojificha mumewe, na yeye akubali kuwa alishiriki katika uhalifu huo wa unyang’anyi wa kutumia silaha.
 
Huku baadhi ya watu waliohudhuria mahakamani kusikiliza shauri hilo wakidondokwa na machozi, Clara alidai askari wote saba wanaume na askari mmoja mwanamke anawakumbuka.
 
“Mheshimwa Hakimu askari wote saba wa kiume pamoja na askari mmoja wa kike wote waliokuwa wakinifanyia ukatili huo nawafahamu kwa sura … hata wakijipanga mstari na kuchanganyika na wengine nawafahamu,” alidai.
 
Aliendelea kueleza kuwa akiwa amewekwa katika chumba maalumu akiwa uchi wa mnyama, askari hao wa kiume walimwamuru akalie chupa ya soda huku ikiingia pole pole sehemu zake za siri na askari huyo wa kike akishuhudia, alikuwa akipigwa kwa nguvu mabegani.
 
“Nilipata uchungu mkali wakati mdomo wa chupa hiyo ukiingia, lakini ilishindikana chupa nzima kuingia ndipo wakaamuru nipumzike baadae wakanilazimisha niingize chupa ya bia zile za zamani zenye shingo ndefu huku nikiwa nimeikalia, damu zilitoka nikaumia vibaya na kusikia maumivu makali sana,” alidai.
 
Aliongeza kuwa askari hao kila waliposikia sauti za watu nje, walimwamuru avae nguo zake na baadae walimwamuru avue nguo zake zote baada ya kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kuingia humo, na kuendelea kumdhalilisha huku wakimtukana matusi ya nguoni.
 
Mumewe alipo
Clara aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa mumewe hatimaye alikamatwa mjini Namanyere wilayani Nkasi na kusafirishwa hadi mjini Sumbawanga na kuwekwa mahabusu ambapo alikufa akiwa mikononi mwa askari Polisi.
 
Alidai kuwa mumewe pia alilazimishwa kuingiza chupa sehemu zake za siri ambazo zilichanika na kumsababishia kifo kutokana na kupoteza damu nyingi na haijulikani hadi sasa wapi alipozikwa.
 
Baada ya Clara kutoa hoja yake hiyo mbele ya Mahakama, Hakimu Mugissa aliahirisha shauri hilo ambalo litatajwa tena Februari 18, mwaka huu na kuamuru washitakiwa wote kurejeshwa rumande kwa kuwa shauri hilo kisheria halina dhamana.
 
Mshitakiwa Clara na wenzake watatu, Daniel Mangi (28), mkulima na mganga wa kienyeji mkazi wa Kaswepepe, Hassan Ahmid (24), mkazi wa Jangwani na Magembe Masanja ‘Msukuma’ (39) mkazi wa kijiji cha Majimoto wilayani Mlele katika mkoa wa Katavi, wanadaiwa kutenda kosa hilo Desemba 11 , mwaka jana.
 
Inadaiwa kuwa siku ya tukio washitakiwa hao kwa pamoja walimvamia na kumtishia kwa kisu John Mazimba mkazi wa Jangwani na kumpora simu ya mkononi yenye thamani ya Sh 60,000.
SOURCE:HABARI LEO

VIDEO:UKATILI MKUBWA HUU JAMANI..MWANAMKE ABAKWA NA KUNDI LA WANAUME NA KUZIKWA HAI...!TAZAMA HAPA...!

TAHADHARI..VIDEO HII NI KWA WATU WAZIMA TU NA PIA INATISHA..
CHEKI VIDEO HAPA CHINI.. 
 

ANGALIA PICHA MUME AMMWAGIA TINDIKALI MKE WAKE KATIKA UGOMVI WA KUGOMBEA MALI HUKO KAKOLA KAHAMA

MARIA Nkwabi [33] Mkazi wa Kijiji cha Kakola akiwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya kumwagiwa Tindikali na Mumewe;Ray Chobe katika ugomvi unaodaiwa kugombea mali.
Jeshi la Polisi Wilayani Kahama limethibisha kutokea kwa tukio hilo na bado wanaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo.
MWONEKANO WA BI MARIA NKWABI BAADA YA KUPATA HUDUMA YA KWANZA.

AL SHABAAB WAPIGA MARUFUKU RAIA KUTUMIA INTERNET NCHINI SOMALIA,SOMA ZAIDI

Wanamgambo wa Al Shabaab wenye uhusiano na Al-Qaeda, wamesema kuwa wamepiga marufuku raia wanaoishi katika maeneo wanayodhibiti kutumia internet.
Wapiganaji hao wametoa onyo kwa kampuni zote zinazotoa huduma ya internet siku 15 kufunga biashara zao. kampuni yoyote au mtu yeyote atakayepatikana akipuuza onyo hilo atajulikana kama mtu anayewafanyia kazi maaduzi zetu, na ataadhibiwa kulingana na sheria za kiislamu,” ilisema taarifa ya kundi hilo ambayo ilitumwa kwenye mitandao yake.



Wanamgambo hao hutumia sheria kali za kiisilamu katika maeneo wanayotawala na kuwakamata watu mara kwa mara kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Internet hutumiwa sana nchini Somalia, taifa ambalo limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili, huku kundi hilo likionekana kuwa kikwazo kikubwa kwa amani.
Kundi la Shebab zamani lilikuwa likitawala katika sehemu kubwa za Kusini mwa Somalia na Kati, lakini likaondoa wapiganaji wake baada ya kushindwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanaopambana nao. Majeshi ya Afrika wakiwemo wanajeshi kutoka Uganda, Burundi na Kenya, tangu hapo wamedhibiti sehemu kadhaa kutoka kwa wapiganaji hao.
Lakini mashambulizi ya kuvizia yanayofanywa na kundi hilo dhidi ya maslahi ya majeshi ya serikali na yale ya kigeni, yameondoa matumaini ya kunusuru taifa hilo kutokana na vita vya miaka mingi.

Chanzo: BBC Swahili

DOKTA MAARUFU JIJINI DAR " MAMBO" ANASWA AKITAKA KUMTOA MIMBA BITI...ANGALIA PICHA ZA FUMANIZI

Dokta Mambo baada ya kunaswa na OFM.

MWAKA umeanza, mambo mapya pia yapo! Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers imeingia kazini kwa kasi zaidi. Safari hii imemnasa daktari anayejulikana kwa jina moja la Mambo maarufu sana kwa jina la Dokta Mambo katika jaribio linalodaiwa kuwa ni la utoaji mimba.

Baadhi ya vifaa anavyotumia Dokta Mambo.
Tukio hilo lilitokea katika zahanati yake (jina lipo) iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam ambapo daktari huyo anayejulikana sana na wateja wake, hasa akina mama alipoingiliwa na OFM wakishirikiana na polisi baada ya kumuwekea mtego wa mbinu za kishushushu.
MALALAMIKO YA AWALI
Mwishoni mwa Desemba, mwaka jana, mtu mmoja (jina lipo) alituma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda OFM akimlalamikia dokta huyo kwamba amekuwa na mchezo wa kutoa mimba wanawake wakiwemo mabinti wa shule, kitendo alichodai haoni kama ni sawa.

Mjamzito aliyepangwa na OFM kutolewa mimba na Dokta Mambo.
“Naitwa….(jina lipo), nilikuwa naishi Kawe lakini kwa sasa nimehamia Mbezi (hakusema Mbezi gani). Kama hapo ni OFM (Oparesheni Fichua Maovu) naomba mumshughulikie daktari mmoja anaitwa Dokta Mambo wa Kawe. Huyu daktari jamani amekuwa na tabia ya kutoa mimba wanawake hata wasio na matatizo.
“Ninavyojua mimi hakuna hospitali inayoruhusiwa kutoa mimba Tanzania, labda pale ambapo itathibitika kwamba mjamzito ana kifafa, kwa hiyo hatari inakuwepo ya kumpoteza mama au mtoto tumboni ndiyo mimba hutolewa. Wananchi wa Kawe wamekilalamikia kitendo hicho hadi wamechoka. Polisi Kawe wamemshindwa,” alisema raia mwema huyo.
Polisi akikagua vifaa anavyotumia Dokta Mambo kuchoropoa mimba.
OFM YAANZA KAZI
Baada ya kupokea tuhuma hizo, OFM ilijipanga na kuingia kazini. Ilimwandaa paparazi wa kike na kumtengenezea ujauzito wa bandia na paparazi wa kiume ambaye ni mchumba wake (wa bandia) ili kwenda naye kwa Dokta Mambo kuona kama kweli anajihusisha na kazi hiyo au la!

JUMANNE, DESEMBA 31, 2013
Ilikuwa Jumanne ya Desemba 31, 2013, OFM na paparazi huyo walitia timu kwenye zahanati hiyo na kukutana na dokta huyo ambaye alikubali kumtoa ujauzito paparazi huyo.
‘Mchumba’ wa paparazi huyo alimwambia dokta kwamba wamekubaliana kuitoa mimba hiyo kwa sababu ya hali ya uchumba, daktari akasema haina shida.

Dokta Mambo na msaidizi wake baada ya kunaswa.
AWEKA MASHARTI MAGUMU   
Katika hali ambayo OFM hawakuitarajia, daktari huyo alisema kwa kawaida kabla hajamchoropoa mimba mteja wake lazima aipime kwanza ili kujua ina muda gani.
Zoezi hilo lilikuwa gumu kwa OFM kwa sababu paparazi huyo hakuwa na ujauzito. Ilibidi ‘wateja’ hao waondoke kwa kisingizio kwamba wanakwenda kujipanga kwa fedha aliyoitaka ambayo ni shilingi laki moja na kwamba wangerudi siku iliyofuata (Jumatano).

OFM WAJIPANGA UPYA
‘Wachumba’ hao waliondoka na kuungana na Timu ya OFM ambayo ilikuwa mahali imekaa mkao wa mtego. Baada ya kupata simulizi za ndani ya zahanati hiyo, OFM ilirejea ofisini na kumweleza kamanda mkuu wake ambaye alikaa na timu hiyo na kupanga mpango mpya.

Vitendea kazi vya kutolea mimba anavyotumia Dokta Mambo.
“Bosi, Dokta Mambo ameshakubali, lakini sera zake ni kwamba hawezi kumtoa mimba mjamzito hadi ampime kwanza na kujua ina miezi mingapi. Sasa huyu (paparazi) hana ujauzito, tungekubali ampime tungeumbuka, tukamwambia tunakwenda kusaka fedha kwanza,” OFM  mmoja alimwambia kamanda mkuu.
OFM YATUMWA MTAANI KUSAKA MWENYE MIMBA YA UKWELI
Kamanda Mkuu wa OFM (jina lipo) aliagiza timu yake kuingia mtaani ili kumsaka mwanamke mwenye mimba ya ukweli ambaye ndiye angekuwa na sifa za kutolewa ujauzito na daktari huyo.
Hayo yote yalifanyika baada ya pia uchunguzi wa kina kufanyika maeneo ya Kawe kuhusu tabia ya daktari huyo na kudaiwa kuwa, hawezi kuacha ‘kamchezo hako ka siku nyingi’.

Polisi akiwa chumba cha kutolea mimba.
Mjamzito wa kweli alipatikana (jina lipo), akiwa na mimba ya miezi mitatu.  Akashirikishwa katika zoezi hilo ambapo hata yeye aliumia kusikia kwamba kuna daktari anayetoa mimba wanawake hata wale ambao hawana sababu za kufanya hivyo kama sheria za utabibu zinavyotaka.
WATINGA POLISI KAWE
Baada ya kupatikana kwa mjamzito huyo, OFM ilimchukua hadi Kituo cha Polisi Kawe, Dar es Salaam na kuwaambia wahusika kuhusu tabia ya daktari huyo inayolalamikiwa na watu ili ikibidi watoe askari kwa kuungana na OFM kwenda kumtia nguvuni.

Vifaa vinavyotumiaka katika zoezi hilo.
POLISI KAWE WAONESHA ‘MAAJABU’
Katika hali ya kushangaza, polisi wa kituo hicho, awali waliwataka OFM watoke nje ili wajadili wao. Baadaye waliwaita na kusema kwamba hawawezi kutoa polisi, kama ishu ni daktari huyo kulalamikiwa na watu, watamwita na kumkanya aache mchezo huo!

“Hatuwezi kushirikiana nanyi katika hilo zoezi, kama ni kweli kuna hayo maneno ya watu, sisi tutamwita tumuonye aache mara moja,” alisema mmoja wa askari wa Kituo cha Kawe.
Katika hali iliyoshangaza zaidi, polisi hao waliwataka waandishi wote walio kwenye msafara kuandika maelezo ya malalamiko kuhusu daktari huyo kwenye kitabu cha ripoti kituoni hapo (Report Book ‘RB’).
Maelezo yaliandikwa. Jina……, umri…., makazi…., kazi…., dini….. na aina ya malalamiko. Baada ya hapo wakatakiwa kuondoka zao.

OFM WARUDI KWA DOKTA MAMBO
Januari 3, 2014, OFM wakiwa na mjamzito wa kweli  walikwenda kwa dokta huyo ambapo kama ilivyo utaratibu wake, alimpima kwanza na kutoa majibu kwamba ana mimba ya miezi 3 na wiki mbili, akasema ni kubwa sana, hivyo zinatakiwa shilingi 160,000.

Hata hivyo, mchumba mtu alisema hana kiasi hicho cha pesa. Ikatokea vuta nikuvute hadi kufikia shilingi 100,000. Ikumbukwe kwamba, mpaka hapo Dokta Mambo hakuwa anajua kwamba mchezo wa pili ni uleule wa kwanza.
“Basi dokta tunaomba tuje kesho na hiyo laki moja,” mchumba mtu alimwambia daktari huyo ambaye alikubali huku na yeye akiomba kuwa, hiyo kesho iwe saa kumi na moja jioni.
OFM, POLISI, MJAMZITO NA MCHUMBA’KE
Kesho yake ilifika, OFM ikiwa na mjamzito huyo akiwa na mchumba’ake walikwenda maeneo ya Kawe jirani na zahanati ya Dokta Mambo kujaribu kupanga namna ya kufanikisha oparesheni hiyo.

Bado tatizo lilikuwa uwepo wa polisi baada ya kubaniwa na wale wa Kawe. Mungu si Athumani, wakiwa wanashangaashangaa eneo, ilipita pikipiki ya askari wa doria ‘Tigo’ na mara moja OFM ikawasimamisha.
Bila kupoteza muda, OFM waliwaeleza polisi wale mchezo mzima ulivyokuwa na kwamba walihitaji msaada wao ili kufanikisha zoezi hilo, walikubali bila kinyongo na mara moja wakaongozana hadi eneo la tukio.
OFM mmoja kati yao aliingia ndani ya zahanati hiyo akijifanya amekwenda kupima malaria, wale polisi wawili na OFM wengine walikaa mafichoni kutega mingo, wachumba nao waliingia mpaka kwa dokta wakiwa na kitita cha shilingi laki moja mkononi.
MJAMZITO APELEKWA CHUMBA CHA KAZI
Baada ya kuwapokea na kutoa kiasi hicho cha pesa, mjamzito huyo alipelekwa chumba kinachodaiwa ni cha kutolea mimba huku mchumba mtu akikaa kwenye fomu kusubiri matokeo.

UTAALAM WA OFM
Kilikuwa kipindi kinachotaka mawasiliano ya hali ya juu, OFM ikitambua kuwa kosa moja goli moja, walikuwa makini kwa mawasiliano. Mjamzito chumbani kumwambia mchumba wake kwenye fomu, naye kuwaambia OFM wa nje hatua kwa hatua.

Katika mazingira hayo, hakuna OFM aliyetakiwa kupokea simu wala kutuma meseji kwa mtu asiyehusiana na kazi hiyo.
TUKIO LANASWA
Ilikuwa wakati daktari huyo akiwa na glovsi mikononi, mjamzito wa kweli akiwa kitandani na nesi mmoja wa kumsaidia daktari wakiwa ndani ya chumba, ndipo OFM na polisi walipovamia na kunasa tukio ambalo lilionekana dhahiri kwamba lilikuwa jaribio la kutoa mimba.

Hapo ndipo Dokta Mambo alipogundua kuwa kumbe ‘kazi’ aliyopewa ilikuwa feki na wale walikuwa makamanda wa OFM wakishirikiana na polisi waaminifu, wazalendo na wanaopenda kazi yao sawasawa.
KWA NINI?
Lilikuwa jaribio la kutoa mimba kwa sababu, ndani ya chumba zilikutwa zana za shughuli hiyo huku mjamzito akiwa kitandani tayari kwa kufanyiwa mchakato.

Huku OFM wakimpiga picha (zipo za kumwaga kwenye maktaba yetu – ukitaka kuziona njoo Bamaga), askari nao wakichunguza mazingira zaidi na kukamata vifaa, daktari huyo alinywea huku msaidizi wake akitokwa machozi.
POLISI WAMWINGIZA NDANI YA GARI
Zoezi hilo lilikamilika kwa daktari huyo kuchukuliwa na askari hao ambao walikodi gari, mmoja akawa na dokta garini akiwa na vifaa vyake chini ya ulinzi, mwingine akiwafuata kwa nyuma na pikipiki.

Askari hao, waliwaeleza OFM kuwa wataitwa Kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kuandika maelezo.
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camillius Wambura ili kujua kama suala hilo limefika mezani kwake, lakini simu yake haikupatikana muda wote ilipopigwa.

Hata lilipomtafuta Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova ili limsimulie mchezo mzima ulivyokuwa, naye hakupatikana hadi tulipokwenda mitamboni.
Bado tunaendelea kuwatafuta viongozi wa polisi na ukweli wa kina kuhusu namna ishu hiyo inavyoendelea, tunawajulisha katika matoleo yetu yanayofuata.

‘FISI MTU AMENIHARIBIA MAISHA’

Nhende Ng’wanandilima akipata matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar.
Jelard Lucas na Makongoro Oging'
“MSEMO wa wahenga, hujafa Hujaumbika ulikuwa sahihi kabisa. Wahenga waliona mbali, wanatakiwa kuheshimiwa kwani misemo yao inaishi mpaka leo. Ni kweli binadamu kamili ni yule anayezikwa, kabla ya hapo hujakamilika.
Nhende Ng’wanandilima.
“Unaweza kuishi na viungo vyako vyote miaka hamsini, lakini siku ya mwisho ukapata ajali, ukakatika mikono na kufa, pale ndiyo umeumbika sasa,” ndivyo anavyoanza kusimulia Nhende Ng’wanandilima (35), mkazi wa Kwimba, Mwanza ambaye amelazwa Jengo la Sewa Haji, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar baada ya sehemu ya uso wake kuliwa na fisi aliyedai ni mtu aliyejibadili.
Akisimulia kwa majonzi tena akiwa hawezi kuzungumza sawasawa, kijana huyo alisema tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Kibetelwa, Nh’ungumalwa, Kwimba usiku wa Mei 10, 2012.
MKASA KAMILI
Akisimulia mkanda mzima wa tukio hilo, Nhende anasema: “Siku hiyo nilitoka kilabuni kunywa pombe kidogo. Nikiwa njiani narudi nyumbani sasa, nilipita kwenye pori la kijiji kile, ndipo ghafla nilianguka na kukumbana na sura ya fisi akiwa mkali sana.

“Yule fisi bila kujali mimi ni binadamu, alianza kunitafuna sura bila huruma. Alinitafuta sehemu za kuzunguka kinywa kama unavyoniona. Lilikuwa jambo la ajabu sana kwangu.
“Wakati nikipigania maisha, fisi aliendelea kunila. Nikapiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa wanakijiji ambapo walifika na kunikuta nikiendelea kupambana na yule fisi huku nikiwa nimelowa damu.
“Alikuwa fisi mwenye nguvu za ajabu na hata ule woga tunaosema fisi anao sikuuona. We fikiria, watu wamefika lakini fisi aliendelea kunitafuna bila kuogopa.

“Ilibidi wanakijiji wafanye kazi ya ziada kunitoa katika miguu na fisi ambapo sasa alikaribia kabisa kunila sehemu za siri kwani alishafika huko. Nilikuwa hoi sana. Ndipo wanakijiji wakanichukua na kunikimbiza Hospitali ya Rufaa Bugando (Mwanza) kwa matibabu zaidi,” alisema kijana huyo.
IMANI YA FISI MTU
Hata hivyo, Nhende alisema kuwa anaamini fisi aliyemfanyia kitendo kile ni binadamu aliyejigeuza kuwa mnyama huyo. Anasema kuwa, si rahisi kwa fisi kumla binadamu, tena mtu mzima.
Alisema vitendo vya watu kuliwa na fisi katika maeneo hayo vinasababishwa na mambo ya kishirikina ambayo hayajapatiwa ufumbuzi kutokana na wahusika kutojulikana.

Alioongeza kuwa, wapo binadamu ambao kama ana chuki au kisasi na mtu anajigeuza fisi usiku na kumrarua kama alivyofanyiwa yeye na si ajabu mtu huyo huyo akatokea hospitali kumjulia hali.
KWA MUJIBU WA MADAKTARI
 “Nilipofikishwa Bugando, madaktari mashuhuri wa masuala ya koo na mfumo wote wa ‘ogani’ za fahamu walijitahidi kunitibu lakini bila mafanikio. Nikaletwa hapa Muhimbili ambapo pia imeshindikana, sasa natakiwa kupelekwa India kwa matibabu zaidi.

“Wameniambia nikifika kule nitasukwa upya (plastic surgery) sehemu zote nilizoliwa na fisi. Ninachoweza kusema ni kwamba, yule fisi ameniharibia sana maisha, nina mke na watoto watano sijui nitawalisha nini, nimekuwa kilema mimi. Nimekuwa nikipata maumivu makali, sikuwahi kujua kama fisi anaweza kumla binadamu hivi.
KUHUSU KWENDA INDIA
“Kuhusu safari ya India, nimeahidiwa kusafirishwa, lakini awali ya yote mimi mwenyewe natakiwa niwe na pesa zangu zisizopungua shilingi milioni moja ili kukamilisha mipango ya hati za kusafiria.

KAMA SI POMBE ANGEMSHINDA FISI
Nhende hakusita kuweka wazi kwamba, ushauri wake kwa vijana ni kuepuka matumizi ya pombe kupita kiasi, kwani anaamini kama asingekuwa amekunywa pombe angeweza kumshinda yule fisi.

MSAADA ANAOUOMBA KWA WATANZANIA
Nhende ameomba walioguswa na tukio lake wamsaidie kwa hali na mali ili aweze kukamilisha taratibu za usafiri wa kwenda India. Walio tayari wamchangie kupitia namba za simu +255 763 176454.

-GPL

UNYAMA:Wakulima na wafugaji wachinjana kama kuku wilayani Kiteto.....Tunaomba Radhi kwa hizi Picha za Kutisha..!!

Habari kwa mujibu wa Mohamed Hamad, Kiteto -- WILAYA ya Kiteto imeingia kwenye orodha ya maeneo yanayotisha kwa mauaji ya kinyama baada ya wakulima kuuawa mara kwa mara na wafugaji kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kugombea ardhi Miongoni mwa waliouawa kinyama Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni Juma Mlagwa (49) wa Kitongoji cha Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye alivamiwa nyumbani kwake usiku na kundi la vijana wa kifugaji masai (makorianga)

Imeelezwa kuwa wakati anavamiwa zilisikika Risasi zikipigwa juu Kitongojini hapo na baada ya watu kuendelea kujificha ndani vijana hao walianza kunyunyizia nyumba zao mafuta aina ya petrol  kisha kuwasha moto

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ally Mussa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho alisema siku hiyo haitasahaulika mashani mwake kwa yaliyotokea kutokana na vitendo hivyo akisema ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu anachinjwa hadharani

“Nilichomewa Pikipiki zangu mbili pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo nguo, vyakula, lakini nilichonusuru ni roho yangu ambayo hadi leo nasema najivunia uhai nilio nao”alisema Mwenyekiti huyo
  Alisema chanzo cha mauaji hayo ni jamii ya kifugaji wamasai kuingiza mifugo yao kwenye shamba la mmoja wa wakulima Kitongojini hapo na baada ya kukatazwa walimpiga kisha nae kupigwa ndipo wakakusanyana kupanga uvamizi huo

Hata hivyo baada ya kufikishwa taarifa kwa viongozi wa Serikali walidaiwa kulifika Kitongojini lakini walikataa kwenda kuongea nao km chache kwa madai kuwa ni uongo kwamba hakuna watu waliokusanyana

Akielezea hayo Mwenyekiti huyo alisema tatizo ni uongozi dhaifu kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya ambapo alidai kuwa ukabila umeshamiri kwa viongozi kujiona kuwa wanahaki ya kutfanya utetezi katika upande mmoja

Kwa upande wake Lairumbe Mollel Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya akizungumzia sakata hilo alimzodoa mwenyekiti huyo wa Kitongonji kuwa ni muongo kwani baada ya wao kufika kabla ya tukio alikataa kuwataja wahusika

Hata hivyo kauli hiyo ilionekana kutokuwa na mashiko baada ya mwenyekiti huyo wa Kitongoji kuonyesha udhaifu wa viongozi hao akisema baada tu ya kufika hawakuweza hata kukubali kupelekwa walikoweka kambi vijana hao wa kimasai

“Baada ya kufika walitaka nisema majina ya walioleta fujo na nilipowataka twende eneo la tukio wakakata nakuona kuwa hawakuwa na njia njema kisha wakarejea Kiteto ambapo usiku vijana hao wakatekeleza azima yao ya kuchinja mtu mmoja na kumpiga mwingine risasi kisha kuwajeruhi watu saba”alisema Mwenyekiti huyo wa kitongoji

Waliofariki katika uvamizi huo ni pamoja na Juma Malagwa (49) ambaye alichinjwa shingo, Yohana Ivo (33) ambaye alipigwa sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo pamoja na watu wengine saba kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa kujeruhiwa kwa fimbo na mapanga

Waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel matias (21) Juma Bahati (13) Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16) Mwajuma Martin pamoja na Musa Juma (16) aliyepelekwa Dodoma kwaajili ya matibabu

Hata hivyo mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika kitongoji hicho aliwapa siku 30 viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka utaratibu wa kuwatambua wananchi hao ili kuondoa tofauti zao waweze kufanya kazi bila bughdha

“Ninyi wananchi mwende kujisajili Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani maisha bora kwa wananchi yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili mpatiwe huduma za jamiiambazo kwa sasa hamna hata moja,” alisema Mbwillo.

UNYAMA:AUNGUZWA NA MAFUTA YA MOTO KISA VOCHA



MKASA MZIMA ULIKUWA HIVI.....

Kijana mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mke wa mtu anateseka hospitalini baada ya kuchomwa na mafuta ya kupikia ya moto na ndugu yake baada ya kuhisiwa kuiba vocha ya simu ya mtandao wa Telecel yenye thaman ya senti 50 huko Zimbabwe.

Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Otilia Kosa anayeishi Plot 16, Tsungwizi Ridge maeneo ya Nyazura huko nchini Zimbabwe anateseka katika hospitali ya Rusape General Hospital akiuguza majeraha aliyoyapata baada ya kumwagiwa mafuta ya moto na ndugu yake. 
Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 27 Decemba 2013, Otilia alimuuliza ndugu yake Kudakwashe kama yeye ndiye aliyetumia vocha yake ya mtandao wa Telecel yenye thamani ya senti 50 za kizimbabwe.Kudakwashe alikataa kuwa hakutumia vocha hiyo na hapo ndipo mtafaruku mkubwa ulipotokea kati ya wawili hao.

Cha kushangaza ,siku iliyofuata kikao cha familia kilikaa ili kuwapatanisha wawili hao ambao walishindwa kuelewana na mpaka kufikia hatua mbaya ambayo ingepelekea kuvunja udugu wao.Hata hivyo, wanafamilia hao walishindwa kuwapatanisha ndugu hao na hivyo kuongeza mpasuko kati yao.

Ilidaiwa kuwa baada ya kukosa muafaka huo,Kudakwashe alipatwa na hasira kali iliyompelekea yeye kuingia jikoni na kuchemsha mafuta ya kupikia na kummwagia nduguye huyo (Otilia) katika maeneo ya uso,shingo,kifua,mikono na tumboni.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa wa Polisi wa ZRP Nyazura, Inspekta hikima Sanida alinukuliwa akisema "We have arrested the suspect and recorded a warned and cautioned statement in which she admitted scalding the victim with hot cooking oil. She was charged with first-degree assault and criminal violation of the Domestic Violence Act,"

Pia Inspector Sanida aliongeza kuwa kesi ilishafunguliwa Alhamisi iliyopita,lakini kesi hiyo imeahirishwa mpaka Alhamisi ijayo ambapo madaktari wamethibitisha kuwa muathirika anaweza kuhudhuria mahakamani kutoa ushahidi.

UNYAMA..MUME AMCHARANGA MAPANGA MKEWE NUSU YA KUFA, KISA WIVU WA MAPENZI..

Mariamu akiugulia maumivu.
MAMA mmoja mkazi wa Ronsoti, Kata ya Nyamisangura, wilayani hapa, Eliza Marwa,28, hivi karibuni amenusurika kuuawa na mumewe, baada ya majirani kufika kumuokoa kutokana na kukatwakatwa mapanga.
 Mama huyo aliliambia gazeti hili akiwa katika Hospitali ya Wilaya Bomani, Tarime kuwa mume wake Marwa Ogora alimkatakata mapanga baada ya kumtuhumu kuwa akikwenda kwa hawara yake badala ya kwenda kwenye mazishi ya mjomba wake huko Bunchari.
Akifafanua zaidi, Eliza alikuwa na haya ya kusema: ‘’Mjomba alifariki na mazishi yake yalifanyika Desemba, kumi na sita mwaka huu ambapo nilihudhuria baada ya kumwarifu mume wangu kuwa nitahudhuria lakini alinijibu kuwa hakuwa na fedha za kunipa ili niende kwenye mazishi. 
“Nilichukua jukumu la kwenda kwa kutumia nauli yangu kwa kuwa muda huo mume wangu alikuwa kazini na baada ya mazishi kesho yake asubuhi Desemba kumi na saba mwaka huu nilirudi nyumbani na kumkuta mume wangu ambaye alianza kunipiga kwa mpini wa jembe kisha panga akidai kuwa sikuwa nimeenda kwenye mazishi badala yake nilikuwa nimeenda kwa mpenzi wangu.
 “Alinishambulia sehemu mbalimbali za mwili hususani kichwani, kidogo anitoe ubongo, wasingekuwa majirani kuniokoa baada ya kupiga yowe naamini angeniua kwani hivi sasa siwezi hata kuamka na masikio yameziba, miguu ina ganzi, siwezi kutembea. 
“Mume wangu Ogora amekuwa akinipiga mara kwa mara lakini kutokana na watoto tuliozaa naye nimekuwa nikivumilia mateso, naogopa kuondoka na kuacha watoto walelewa na mama wa kambo,”alidai mama huyo. 
Ogora hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwani anasakwa na dola na afisa mmoja wa polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema  wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa. Naye daktari wa hospitali aliyolazwa mama huyo, Nega Malico alikiri kumpokea mgonjwa huy

VIDEO: ANGALIA Sekunde 40 za Kilichojiri Katika Operesheni Tokomeza....TAZAMA HAPA

Like Sabibo Camp like Operesheni Tokomeza. Na hii ni just a drop of ice berg...
Hivi unaweza kujiuliza kwenye hizo kambi vingapi hatujavijua vilifanyika? Kama hadi sasa, kwa mujibu wa  taarifa ya kamati wanaume walilazimishwa kufanya mapenzi na miti hadi wamalize haja zao na mengine mengi....


Shameful condition...but they should know exactly, no condition is permanent (The State of Africa; A History of Fifty Years of Independence [Martin Meredith].


TAZAMA VIDEO HAPO CHINI

DEREVA WA BODABODA ABAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO NA KUMSABABISHIA KUOZA SEHEMU ZA SIRI.

MWANAFUNZI wa kike,miaka 13, (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la tano katika shule ya Msingi Unyakumi, mkoani Singida, amefanyiwa unyama kwa kubakwa na kijana aliyemtaja kwa jina moja la Mapunda ambaye ni dereva wa bodaboda.
Denti aliyebakwa akiwa hospitali

Akizungumza kwa shida kutokana na maumivu makali aliyonayo akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, denti huyo alisema kwamba mkasa huo ulimpata Novemba 19, mwaka huu wakati akitoka shule akielekea nyumbami kwao.

Akisimulia mkasa huo mwanafunzi huyo alikuwa na haya ya kusema:

“Mimi ni mtoto yatima wa kufiwa na baba, mama naye aliachana na baba nikiwa na umri mdogo, nimekulia katika shida tena kwa kulelewa na watu tofautitofauti, niliona kitakachonikomboa ni elimu lakini ndoto yangu sasa imekufa.
“Imekufa kwa kuwa nateseka kitandani kwa muda mrefu sasa kutokana na maumivu yaliyotokana na kubakwa.Nimekua wa kujisaidia kitandani, nawakumbuka wazazi wangu, leo hii wangekuwepo wangekua watetezi wagu, sina uhakika kama nitapona na kwenda shule tena.
“Kutoka shuleni hadi nyumbani ni mwendo wa saa moja, siku hiyo niliyobakwa ilikua Ijumaa, nilikua natoka shule nikielekea nyumbani, njiani kuna vichaka na mashamba ya mikorosho, nilipofika karibu na banda bovu nilimkuta kijana amekaa juu ya jiwe.
“Nilijisikia vizuri sana nilipomuona, uoga ulinitoka juu ya wanyama wakali, sikua na hofu ya aina yoyote kama angenigeuka, nilipomkaribia alinikamata kwa nguvu, alinivuta akanipeleka katika banda bovu.
“Nilijaribu kujinaswa lakini nilishindwa kwani alikua na nguvu kuliko mimi, niliamua kupiga kelele ili nipate msaada toka kwa mtu yeyote anayepita, hata hivyo, hakuna aliyejitokeza, alinifunika mdomo, alinipiga, niliishiwa nguvu, akaniingilia, alipomaliza haja yake, akakimbilia pasipojulikana.
“Nilitokwa damu nyingi zilizotoka sehemu za siri, niliinuka na kutembea kwa shida kwani hata kiuno kilikua kikiuma sana, nilifika nyumbani, sikumkuta dada kwani alikuwa ana kawaida ya kurudi usiku akitokea kazini kwake.
“Aliporudi alikuta nimeshafua nguo zangu na nimeshalala, niliona aibu kumweleza, ilipofika Jumapili maumivu ya kiuno na sehemu za siri yakaongezeka, nilikua nikitembea kwa shida, ilimbidi dada aniulize nina nini? Awali niliogopa kumweleza lakini baadaye nilimsimulia kila kitu kwani maumivu yalizidi.

“Nilishindwa hata kwenda shule, nilipelekwa hosptali ya wilaya lakini hali yangu ilizidi kuwa mbaya. Nikahamishiwa hospitali ya mkoa, Singida lakini sikuweza kupata nafuu, nikaletwa hapa Muhimbili kwa gari la wagonjwa ‘ambulance’ kwani nilishindwa kukaa kwenye kiti cha basi.
“Bado sijaweza kukaa wala kuinuka, hata kulala kwangu ni kifudifudi, nalishwa, naogeshwa kitandani, kwa kweli sina raha hata kidogo tangu nifanyiwe unyama huo maana sijaenda shule, wenzangu wamefanya mitihani mie sipo, nauguza mamivu.
“Nimeoza sehemu za siri hadi makalio, natokwa na usaha, siamini kama nitapona na kwenda shule tena. Aliyenitenda haya tunaishi naye mtaa mmoja na hajawahi kunitongoza ila aliamua kunibaka.
“Nimefikishwa hapa Muhimbili Novemba 20, mwaka huu, naomba taarifa hizi zimfikie mama popote alipo kwani aliachana na baba akarudi kwao Musoma,”alieleza kwa uchungu denti huyo.
Dada wa mtoto huyo anayeishi naye aliyejitambua kwa jina moja la Rose alipoulizwa juu ya madai hayo alikiri kutokea na ameiomba serikali imkamate mtuhumiwa ili haki itendeke.

PICHA NYINGINE YA KUTISHA KATIKA OPERATION YA TOKOMEZA UJANGILI..ILIYO SABABISHA MAWAZIRI 4 KUONDOLEWA

Uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuwaachisha kazi mawaziri wanne Ijumaa, juma lililopita, umemsaidia kuiokoa serikali yake dhidi ya kupigiwa kura na wabunge ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wake. Kama asingechukua hatua hiyo, Rais angekabiliwa na tatizo la au kuvunja serikali yake au yeye mwenyewe kupigiwa kura hiyo na hivyo kulipeleka taifa katika uchaguzi mkuu wa kuchagua serikali nyingine. Mawaziri ambao Rais alitengua kuendelea kusimamia wizara zao ni aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, bwana David Mathayo, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, bwana Shamsi Vuai Nahodha, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, bwana Emmanuel Nchimbi na aliyekuwa Waziri wa Mali asili na Utalii, Balozi Hamisi Kagasheki. Hata hivyo bwana Kagasheki ambaye ni mwanadiplomasia kwa taaluma, anaelekea ‘alitonywa’ na Rais kuwa ataondolewa hivyo akatumia mahusiano yake hayo ya karibu na Rais kutangaza kujiuzulu kwake bungeni kabla Rais hajatangaza uamuzi wake wa kuwaondoa mawaziri wengine watatu Ijumaa hiyo. Pengine jambo la kusikitisha ni utetezi uliofanywa bungeni na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, bwana Mathayo ambaye alidiriki kudai kuwa anaonewa! Huyu ni Waziri ambaye alipewa maagizo tisa na rais mwaka 2006, lakini mpaka alipoachishwa kazi Ijumaa alikuwa hajatekeleza hata agizo moja! Kwa kujitetea kwake bungeni, Waziri huyo ameonyesha bayana kwanini hakupaswa kupewa kazi ya uwaziri! Katika utetezi wake bungeni, bwana Mathayo, alidai kuwa Wizara yake kuanzia mwaka 2006 imekuwa ikipewa fedha kidogo tofauti na zile ambazo ilikuwa ikiomba. Lakini kwa bahati mbaya hakuonesha ni kwa namna gani amekuwa akitumia fedha hizo kidogo katika kutatua moja ya maagizo hayo tisa aliyopewa na rais! Hata hivyo, uamuzi wa Rais kuwaondoa mawaziri hao wanne hautakuwa na tija kama hatawaondoa pia viongozi wa Vyombo vya Dola ambavyo vimelaumiwa Ijumaa na wabunge kwa kuhusisha uvunjaji wa haki za binadamu; vitendo ambavyo vinafanana na vile ambavyo vilikuwa vikifanywa na makaburu wa serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini! Viongozi wa Taasisi hizo wanaopaswa pia kufutwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Kujenga Taifa, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Mkugurugenzi wa Usalama wa Taifa na Kamanda wa Askari wa Wanyamapori. Viongozi hao toka Taasisi nne nilizotaja, wanapaswa pia kuwajibishwa kutokana na usimamizi wao mbaya wa Vyombo vya Dola vilivyohusika moja kwa moja na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza. Serikali pia inapaswa kuwashughulikia Makatibu Wakuu wote na wakurugenzi wao wa Wizara nne husika, pamoja na ile inayosimamia Utawala Bora, Wizara ambayo pia inasimamia Usalama wa Taifa. Hata hivyo serikali pia inapaswa kuchunguza kwa kina yale ambayo yamekuwa yakiendelea, hususan katika Wizara ya Mali asili na Utalii, hasa katika eneo la vitalu vya uwindaji na kadhalika. Kumekuwa na madai lukuki ya rushwa katika eneo hili! Ikumbukwe pia kuwa ni viongozi waandamizi wa wizara hiyo hiyo waliodaiwa kuhuhusika na utoroshaji wa wanyamapori kwenda Jamhuri ya Kifalme ya Uarabuni, UAE, mwezi Septemba, mwaka 2010 wakati umakini wa viongozi wa nchi ulikuwa umemezwa na shughuli za uchaguzi mkuu! Kadhalika ni viongozi hao hao wambao walidaiwa kuhusika, kwa namna moja au nyingine na kashifa ya kuitenga Loliondo na kakabidhi sehemu nyeti ya eneo hilo kwa waarabu chini ya mkataba tata! Suala la Liliondo linalokaliwa na mtoto wa mfalme wa UAE linapaswa kutafutiwa ufumbuzi sasa kwani wakati utakuja wakati Rais wa Tanzania wakati huo atapaswa kuwajibika! Swali ambalo tunapaswa kujiuliza ni; Kwanini viongozi waandamizi katika wizara hii wana kiburi cha kutisha cha hata kutompa ushirikiano aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Balozi Kagasheki? Wabunge siku ya Ijumaa walihoji Usalama wa Taifa walikuwa wapi wakati yote haya yalikuwa yakitokea. Mimi nauliza, Waandishi wa Habari na Vyombo vya Habari walikuwa wapi? Tutafakari! - See more at: http://www.fikrapevu.com/operesheni-tokomeza-serikali-kuwafukuza-mawaziri-wanne-kazi-haitoshi
source-jamiiforums

ACHEZEA KIPIGO CHA PAKA MWIZI MPAKA KUFA BAADA YA KUSADIKIWA KUWA NI MCHAWI MAENEO YA MBEZI BEACH JIJINI DAR

WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.


Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.
Kabla ya kufariki alisema “mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”.



“Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu”.



Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao. 




Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta. 



“Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto” alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo. 



Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema. 



“Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe” alisema mkazi wa eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali
Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.



Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana. 



Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa.

Wakazi wa Mbezi Luis, wakimshambulia mchawi huyo.

Kipigo kinaendelea hadi kupelekea umauti wake.

Wakimsindikiza kuelekea katika mtaro ambao walimpiga na bonge la kitofa na kumuua.


PICHA YA KWANZA YA SABABU ILIYOFANYA MAWAZIRI 4 KUONDOLEWA JUZI BUNGENI DODOMA.



Hii ndio moja ya unyama uliofanyika kwenye Operation Tokomeza Ujangili iliyosimamiwa na washiriki toka Wizara 4 za mawaziri waliondolewa juzi bungeni.


MGANGA WA KIENYEJI AMPIGA MKEWE MPAKA AMVUNJA TAYA

Mariam Crispin Kilimba(52)mkazi wa Ipuli manispaa ya Tabora anayedaiwa kupigwa na mumewe Bw.Himid Hassan Kitebo(58)ambaye ni mganga wa Kienyeji na kusababisha kumvunja taya.
Bi.Joha Aman(38)mkazi wa kata ya Isevya alipigwa na mumewe na kujeruhiwa vibaya ambapo amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.Matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Tabora bado yanaendelea kushika kasi siku hadi siku.

HIVI NDIVYO MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MWANZA ALIVYOUWAWA NA WANANCHI KWA KUPIGWA MAWE.


Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza ndugu Clement  Mabina  ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kisesa jijini Mwanza...
  
 Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda kumhoji iwaje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani?...
  
 Mabina alianza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hovyo  ambapo  alifanikiwa  kumuua  mwananchi  mmoja. Baada  ya  mauaji  hayo, wananchi  nao  walichachamaa  na  kujikuta  wakimuua  kwa  kumpiga  mawe

UNYAMA:Mwanamke abakwa na kuchomekwa chupa za soda katika sehemu zake za siri na kisha kunyongwa huko Chalinze


 
 Mwanamke mkazi wa Chalinze, Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43) amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya kumbaka na kumnyonga...
 
Tukio hilo la kutisha lilijiri usiku wa Desemba 7, mwaka huu Chalinze Kwamwarabu ambapo mwanamke huyo alikwenda kujumuika na ndugu na majirani katika mkesha wa ngoma ya kuwatoa wari siku ya Jumapili.
                                                    
Mkasa huu unasimuliwa kwa majonzi mazito na mdogo wa marehemu ambaye alikuwa mshehereshaji wa shughuli hiyo ‘MC’, Siwema Rashid.
 
Alisema: “Mpaka sasa tunashindwa kuelewa kilichotokea maana siku ya tukio tulikuwa naye kwenye ngoma usiku. Alikuwa mchangamfu sana, aliifanya shughuli ipendeze.
 
“Ilipofika saa nane usiku baadhi ya watu walianza kulala, sasa sijui yeye ilikuwaje mpaka hali hiyo ikamfika maana hao watu walichomfanyia wametuachia historia kubwa sana.

 
“Walimbaka wakaona haitoshi wakamwingiza chupa ya soda sehemu ya siri ya mbele halafu wakamwingiza chupa ya bia sehemu ya siri ya nyuma.
 
“Ili kuzidi kutimiza unyama wao, waliondoka na kumwacha kama alivyozaliwa, inauma sana halafu matukio ya hivyo yamekithiri sana.”
 
Aliongeza: “Marehemu ametuachia jukumu la malezi kwa watoto wake wawili, Sikudhani Juma (18) na Ally Juma (12).”
 
Naye mtoto mkubwa wa marehemu, Sikudhani akisimulia kifo cha mama yake, alisema: “Nasikitika sikuweza kuuona mwili wa mama hata pale watu walipojazana na kumshangaa.
 
“Hata polisi na mganga mkuu wa mkoa walipofika kumchomoa zile chupa sikutaka kusogea kabisa, naamini Mungu atawaonesha jambo hao watu hapahapa duniani.”
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Yurichi Mtei akizungumzia ukatili huo alisema: “Taarifa za tukio hilo bado hazijafika kwangu kutokana na majukumu mengine ya kikazi, isipokuwa nalifanyia kazi kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa.”
 
Tukio hilo lilifunguliwa jalada kwenye Kituo cha Polisi Chalinze kwa namba CH/RB/3767/2013 MAUAJI.
 
Mpaka kifo chake, mwanamke huyo alikuwa akiishi na mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja lakini si aliyezaa naye watoto hao wawili). Alizikwa Jumapili iliyofuata, Chalinze.
  
 Source: Gpl
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari