
Showing posts with label RAY C. Show all posts
Showing posts with label RAY C. Show all posts
RAY C ANATAFUTWA BWANA WA KUMUOA,KAMA UPO TAYARI KUJIZOLEA TOTOZI BOFYA HAPA KUONA VIGEZO VYAKE

Akizungumza hivi karibuni kwenye kituo kimoja maarufu cha runinga, Ray C alisema anahitaji mwanaume mtu mzima anayemzidi miaka kumi, anayejitambua na asiwe mwanamuziki kwani anaamini akiwa na mtu kama huyo uhusiano wao utakuwa mzuri kuliko ule wa awali uliokuwa wa machungu.
“Ninamtaka mwanaume anayenizidi miaka kumi kwani kwa sasa nina miaka 31 japokuwa kwa sasa nafanya kazi kwanza ili nirudi kwenye levo yangu na nitakuwa juu zaidi ya zamani kwa sababu najitambua japokuwa nina hamu sana ya mtoto lakini yote namwachia Mungu.
“Nashukuru sasa hivi niko vizuri nakumbuka meneja wangu wa kwanza alinikataza nisiwe na uhusiano na mwanamuziki lakini ndiyo hivyo nikajikuta niko na Lord Eyes ambaye alianza kunichanganyia cha Arusha (bangi) bila mimi kujua na kujikuta ninaharibikiwa lakini nimeshamsamehe na ninamuombea heri katika maisha yake,” alisema Ray C.
Aidha, Ray C alisema anamshukuru Mungu kwa sababu hana mume wala mtoto kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mwanzo angejenga picha mbaya sana kwa mwanaye.
“Wakati nilipokuwa na matatizo nilijifunza mengi kwamba hakuna rafiki wa kweli kwa sababu walinipenda nikiwa mzima lakini nilipokuwa naumwa hakuna hata mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali zaidi ya mashabiki zangu tu kwa hiyo nimebadilisha mfumo wa maisha yangu,” alisema Ray C.
Miezi kadhaa iliyopita, mwanamuziki huyo alitangaza kuachana na madawa ya kulevya ambayo alikiri kuwa yalimharibia mwenendo mzima wa maisha yake.
HUU NDIO UJIO MPYA WA RAY C...SOMA ZAIDI HAPA..
Pichani
juu ni mdada Rehema Chalamila ‘Ray C’ na chini ni mashairi ya wimbo
mpya anaouandaa mwanadada huyo ambao ameutupia katika ukurasa wake wa
Instagram. Mwanadada huyo kwa sasa yupo busy akiandaa nyimbo mpya.

“Naandaa albamu itayokuwa na ngoma zote kali nilizofanya kwa takriban miaka 10 sasa itaitwa The Best of Ray C. Itakuwa na greatest hits zangu zote nilizofanya kwa kipindi chote hicho. Tumuombe Mungu.
Akinijali na kama mipango itaenda vizuri, Desemba mwaka huu nitarudi rasmi stejini. Nitafanya shoo maalum kwa mashabiki wangu.
Nitakuwa na nyimbo mpya kali na zile za zamani. Sipati picha kwa watu watakaohudhuria kwani watapata burudani adimu kutoka kwangu.” Alisema Ray C.
RAY C NA RECHO HAWAFANANI SAUTI TU, WANAFANANA SURA PIA

Hata hivyo hiyo haikumsumbua, Ray C ambaye alisema kuwa ni faraja kumsikia Recho akiimba kama yeye na tangu hapo wamekuwa marafiki.
Lakini wawili hawa, hawafanani sauti tu. Picha hii (hapo juu) iliwekwa na Ray C kwenye Instagram na wengi walidai kuwa, warembo hao wanafanana kama mapacha vile.
RAY C WAZICHAPA NA NORA STUDIO..KISA NORA KUVAMIA GEMU YA MUZIKI
KATIKA hali ya kushangaza, siku chache baada ya kuripotiwa kupona na
kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray
C’ anadaiwa kugeuka mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro
‘Nora’, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.
Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita ndani
ya studio moja ya kurekodia muziki iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili
hao walikutana walipokwenda kurekodi ngoma zao.Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo, Nora alikutana na Ray C ambaye pia alizama mahali hapo bila mawasiliano na prodyuza anayemtengenezea ngoma mpya.
Chanzo hicho kilipasha kuwa baada ya Ray C kuingia studio hapo alimkuta prodyuza huyo akiandaa ngoma ya Nora ambapo alihoji kilichompeleka mwigizaji huyo mahali hapo.
Ilidaiwa kuwa prodyuza huyo ambaye jina halikupatikana alimwambia Ray C kuwa Nora alifika kurekodi wimbo wake.
Ilisemekana kuwa Ray C hakuridhishwa na majibu hayo, akaomba asikilizishwe ngoma hiyo ya Nora lakini baada ya kusikiliza ilidaiwa kwamba Ray C aliiponda mbele ya Nora, jambo ambalo mwigizaji huyo hakufurahishwa nalo.
Ilidaiwa kuwa Nora alipandwa hasira na kujikuta akimjibu mbovu Ray C.
Habari ziliendelea kutiririka kuwa siku hiyo walimalizana kwa kusonyana na siku iliyofuta walikutana tena studio hapo ambapo Ray C alidaiwa kutinga akiwa ‘masanga’.
Ilisemekana kuwa alipomuona Nora alianza kumpa vijembe, jambo lililosababisha Nora kushikwa hasira ndipo wakavaana na kuzichapa.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Ray C ndiye aliyeibuka bingwa wa ndondi hizo kwa kumtwanga Nora hadi kumvimbisha jicho kabla ya maprodyuza na watu wengine kufanya kazi ya ziada kuwaamulia.
Ilisemekana kuwa baadaye Ray C alitolewa nje ndipo akahamishia hasira kwenye gari la Nora aina ya Toyota Vitz kisha akalivunja kioo na kutambaa zake.
Baada ya kupenyezewa ‘niuz’ hizo gazeti hili lilimtafuta Nora ambaye alikiri kutokea kwa sekeseke hilo huku akibainisha namna alivyoumizwa jicho lake na kuvunjiwa kioo cha pembeni cha gari lake.
Aliongeza kuwa siku hiyo alipoteza pochi wakati wa ugovi huo.
“Ray C alinikuta studio nikifanya wimbo, kilichonishangaza baada ya kuniona tu alibadilika ghafla.
“Nilijua angenishauri kwa kuwa ndiyo ninaanza gemu kumbe mwenzangu alifikiria vingine,” alisema Nora na kuongeza:
“Mbali na kuniumiza jicho lakini alinifanyia mambo ya ajabu sana, kama kusingekuwa na watu wa kutuamulia basi chochote kingetokea.
“Sikwenda kuripoti polisi. Niliamua kusamehe kwa sababu kuna watu walinisihi niachane naye kwa sababu bado kuna mambo yanamwendesha.
Kwa upande wake Ray C alitafutwa kwa kila njia kupitia simu ya mkononi na kumvizia studio lakini hakupatikana hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.
UZURI WANGU UPO NDANI YA MAPAJA YANGU NA SIHANGAIKI NA DAWA ZA KICHINA KAMA WENZANGU...RAY C

Kila mwanamke ana mvuto wake, wapo wanaojivunia nyuso zao zenye macho yaliyoumbwa yakaumbika, nyuso zisizo na chunusi wala aina yoyote ya kovu...
Wapo pia wanaojivunia makalio yao na sote tumekuwa tukishuhudia jitihada mbali mbali za akinadada za kujitengenezea makalio ya bandia ( ya kichina ) ili kujiongezea mvuto kwa wanaume.
Hali ni tofauti kidogo kwa msanii Ray C.Yeye anaamini kwamba mapaja ndo kila kitu na kwamba ni hicho kigezo muhimu kinachoangaliwa na wanaume wengi wa siku hizi...
"Nani asiyejua kwamba kuna makalio ya kichina? Umewahi sikia wapi mapaja ya kichina?..Haya tunayo wachache ambao tumejaliwa na muumba wetu".Hii ni kauli ya Ray C alipokuwa akipiga stori na mpekuzi wetu.

"Sitachoka kuwashukuru watanzania wenzangu ambao walikuwa pamoja nami pindi nikiwa mgonjwa. Nguvu zangu kwa sasa nimezielekeza katika kuiimarisha afya yangu na ndo maana unaniona niko hivi kwa sasa.
"Haikuwa kazi nyepesi kuirejesha afya yangu ndani ya muda mfupi.Nilidhani mapaja yangu hayatarejea tena katika hali yake.Mungu ni mwaminifu, kila kitu kiko vizuri kama nilivyokuwa nataka"..Ray C
RAY C AHAIDI KUTOA URODA WA BURE KWA MTOTO WA WAZIRI AMBAE ALISAIDIA KUOKOA WATU WENGI WAKATI WA MASHAMBULIZI YA KIGAIDI WESTGATE KENYA

![]() |

Tangu asimulie namna alivyopambana na magaidi hao, Haji ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi hasa wasichana na mmoja wa watu aliowagusa ni Rehema Chalamila ambaye amesema anatamani mwanaume mjasiri kama yeye ambaye watazaa naye watoto.
“In love with ths Soldier!i want a soldier like him to marry me,” ameandika Ray C kwenye picha ya gazeti aliyoipost kwenye Instagram ikimuonesha Abdul Haji.
“I love You Abdul Haji,You are my Heroooooooo,” aliandika Ray C kwenye picha nyingine.
Kwenye picha nyingine Ray C aliongeza, “My soldier,My Prince,My Love….Love You Abdul Haji.”
Kijana huyo ni mtoto wa waziri wa zamani wa ulinzi nchini Kenya ambaye alienda kwenye mall hiyo baada ya kupata ujumbe kutoka kwa rafiki yake kuwa kaka yake alikuwa ndani ya Westgate wakati watu hao wenye silaha walipovamia.
Akiongea na NTV, Haji ambaye sio mwanajeshi, alisema alifundishwa kutumia bunduki na baba yake ili kulinda mifugo yao isiibiwe na wezi.
Ujuzi huo ulimsaidia Jumamosi hiyo kuwasaidia wafanyakazi wa Red Cross wafanye kazi yao kwa usalama kwa saa tatu na kusaidia kuokolewa kwa watu wafikao 1,000 nje ya mall hiyo
NANI KAKWAMBIA KWENYE MAISHA HAKUNA MAGEPU?RAY C ATOKA KWENYE UTEJA HADI KUNUNUA MKOKO WA MAANA

STAA wa Bongo Fleva Rehema Chalamila‘Ray C’ ameamua kuianika gari yake ambayo anatembelea kwa sasa ...
Gari hilo ni aina ya Jaguar ambalo namba zake za usajili hazionekani vizuri ila mwishoni zinasomeka T…CHL,huku akiandika kwenye instragram kuwa… Jaguar don't care...CHL means Chalamila Family.....

Pongezi za kutosha zikufikie Ray C popote ulipo. Huo ni mwanzo mzuri baada ya mateso ya madawa ya kulevya yaliyokufanya uwe teja
RAY C NA ZAMARADI MKETEMA WAINGIA NDANI BIFU KALI KISA MWANAUME
So Rehema Chalamila aka Ray C na mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema haziivi? Katika kile kilichoacha wazi midomo ya watu wengi, warembo hao leo wameingia kwenye vita vya maneno kwenye mtandao wa Instagram. Alianza Zamaradi aliyepost picha yenye maneno ya mafumbo:
Picha hiyo aliiandikia maneno haya:Huwezi amini sikuchukii ila nimezidi kukudharau!!!! Katika watu wa mwisho kabisa ambao siwezi kupanic nao hata siku moja ni WEWE.. Dont waste your energy.. you have so much to accomplish ndugu.. mi hunipi tabu kabsa, kabsaa, kabisaaaaaaaaa yani sanasana unanichekesha tu na vituko visivyoisha.. lol!! Ila sikulaumu sana sio kosa lako maskini…
ungekuwa una akili usingefanya hayo ya kitoto tena hasa KWA KIPINDI HIKI.. na huenda hiyo sio akili yako mwaya.. NIMEKUSAMEHE BURE maana hapo ulipo hujielewi bado..
Dramas Dramas Dramas… sizipendagi ila huwa zinanifata zenyewe.. lol!!! Mbona naandamwaga hivi jamani kwani kosa langu nini mimi mtoto wa watu… hahahahahaaaa majanga haya @wemasepetu anyways sorry to my good people jamani kwa mapost ya aina hii..
Dramas Dramas Dramas… sizipendagi ila huwa zinanifata zenyewe.. lol!!! Mbona naandamwaga hivi jamani kwani kosa langu nini mimi mtoto wa watu… hahahahahaaaa majanga haya @wemasepetu anyways sorry to my good people jamani kwa mapost ya aina hii..
sometimes inabidi coz mwisho wa siku mi ni binaadamu tu wa kawaida.”
Wema naye aliongeza kwa kuchangia: Mbona majanga….. dont waste ur tym to fools maamy…. nawe utaonekana a fool… fanya yako… wanaokufatilia wanatamani wawe kama wewe… na si kingine its called ENVY.”
“Sina hata time nae mammy bado ana vichembechembe kwenye ubongo.. maana ghafla tu anaanza kuniparamia jamani.. lol!!! Kishafulia anatafuta kick kwa kugombana na watu.. mtu wa zamani,” aliongeza Zamaradi.
Japokuwa Zamaradi hakutaja wazi nani mlengwa wa ujumbe huo, ni Ray C mwenyewe ndiye aliyejibu kwenye maelezo ndani ya post yake kwenye mtandao huo akisema:
“Hihihi kazi kwelikweli mi naweza posts zangu watu wanajihisi au wanaumia. Tatizo skuliiiii shauri yako #uki skuli kdg wala matatizo hakuna ila km huja skuliii mweeeh unakua mbulula mama we hujui fanya yako achana na watu weusi,” aliandika Ray C.
Aliongeza tena, “Haswa anajiona kichwa kumbe mbulula haswaa Hana lolote,Watu wameanza shughuli hizo anazofanya wenzie tulishazifanya kitambooooooooo,tushauza sura sanaaaaaaaaaa zaid ya miaka. 12 namuangalia simmalizi maana haeleweki.”
Haukuishia hapo, Zamaradi aliongeza tena kwa kuweka post mpya.

“Nashusha sana hadhi yangu kwakweli dealing with watu wenye hasira na maisha ya watu wengine… this is not ME kabisa. Una mengi ya kutukaniwa lkn mi ni binaadamu ninaejua baya na zuri.. maisha yashakushinda wewe sasa USIPANIC.. jipange. Ushafanywa yote ya dunia ntakuweza wapi mie mtu wa zamani,” aliandika Zamaradi kwenye picha hiyo.
Ray C alijibu kwa kupost video hii:
RAY C ALIANIKA "SHAIRI LA PENZI LAKE"INSTAGRAM ALBUM YAKE MPYA IPO MBIONI KUTOKA

Haya wale wenye kiu na ujio mpya wa Ray C mnaweza kuanza kuandaa makoo yenu sababu chakula kimeshawekwa jikoni na muda si mrefu mnaweza kukaribishwa mezani.
Ray C ameshea picha kadhaa akiwa studio na wadau mbalimbali akiwemo Bab Tale na Said Fella, na kama haitoshi ameweka mashairi ya wimbo wake ambao unaonekana ndio aliokuwa akiurekodi wakati anapiga picha hiyo na kuandika “Mashairi ya my new song…,its a very beautiful song…am sooooooo happy..Thank you Lord”.

Unaweza kuyapitia na kuanza kutengeneza taswira ya kile kinachokuja kutoka kwa Rehema Chalamila amabaye anasubiriwa kama nguo ya Christmas au Idd kwa watoto.
Pia Ray C amesema album yake inakuja hivi karibuni
"NAJUTA KUMJUA LORD EYEZ MAISHANI MWANGU"....RAY C
INAWEZEKANA umekuwa ukisikia vitu vingi kuhusu lejendari wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ lakini hukupata chansi ya kumsikia mwenyewe akifunguka mwanzo mwisho juu ya kisanga kilichompata alipojikuta kwenye janga la matumizi ya dawa za kulevya.
Ijumaa Wikienda limefanya naye mahojiano (exclusive interview) ambapo amekidhi kiu yako ya kujua chochote kinachomhusu. UNGANA NAYE…
KWA MTU ASIYEKUJUA, UMETOKEA WAPI?
“Nimezaliwa Mei 15, 1982 mkoani Iringa. Kabla ya kuingia kwenye muziki nilifanya kazi ya utangazaji. Watu wengi walinijua wakati nikiwa Radio Clouds FM. Albamu yangu ya kwanza ni Mapenzi Yangu niliyoitoa mwaka 2003. Kilichofuata ni kujipatia mashabiki wengi sana ndani na nje ya nchi. Baadaye niliachia Albamu ya pili ya Na Wewe Milele ya mwaka 2004. Nilipata mialiko mingi nje ya nchi zote Afrika Mashariki, China, Uingereza na kwingineko. Kilichofuata ni singo kibao na tuzo hadi nilipopata matatizo mwaka jana. Unazikumbuka Mama Ntilie, Mahaba ya Dhati, Touch Me, Na Wewe Milele, Wanifuatia Nini na Nihurumie? Huyo ndiye Ray C mwenyewe.
“Mara ya mwisho kufanya shoo au kuonekana stejini ni Julai, mwaka jana. (anawaza kidogo) Nakumbuka ilikuwa Nairobi Carnival nchini Kenya. Ilikuwa shoo ya kampuni moja ya simu. Nilifanya vizuri sana aisee. It was wonderful.
UTARUDI LINI STEJINI?
(Akiwa Studio za THT na Prodyuza Tudd Thomas na Imma The Boy anarekodi wimbo) Nipo chini ya management (usimamizi) wangu wa mwanzo kabisa wa Ruge Mutahaba. Ruge ni mtu ambaye anajua kumsimamia mtu. Siwezi kumwangusha amefanya kazi kubwa ya kunisimamia. Ni kama baba kwangu. Nina singo mpya kama 4 au 5. Naandaa albamu itayokuwa na ngoma zote kali nilizofanya kwa takriban miaka 10 sasa itaitwa The Best of Ray C. Itakuwa na greatest hits zangu zote nilizofanya kwa kipindi chote hicho. Tumuombe Mungu. Akinijali na kama mipango itaenda vizuri, Desemba mwaka huu nitarudi rasmi stejini. Nitafanya shoo maalum kwa mashabiki wangu. Nitakuwa na nyimbo mpya kali na zile za zamani. Sipati picha kwa watu watakaohudhuria kwani watapata burudani adimu kutoka kwangu.
UMENENEPA SANA NA ULISIFIKA KWA MAUNO STEJINI HADI UKAPEWA JINA LA KIUNO BILA MFUPA. JE, BADO YAPO?
(huku akijinafasi studio) “Hapa hapatoshi ningetoa shoo ya kufa ya mtu. Mauno yapo ya kutosha. Kiuno lainiii…)
SAUTI VIPI?
“(anapandisha sauti nyororo na kuimba moja ya ngoma zake kali zijazo) Umesikia kitu hicho? Sauti bado ipo vizuri mno.”
WATOTO WADOGO WANAKUJA KWA KASI KWENYE GEMU, INAKUPA PICHA GANI?
“Chalenji ni kubwa lakini lejendi atabaki kuwa lejendi. Tumelitoa hili gemu mbali. Nafurahi kuona wadogo zetu wanafuata nyayo zetu na wanafanikiwa. Nafarijika nikimuona Recho wa THT (Winfrida Josephat) anafanikiwa kupitia aina ya muziki niliyoianzisha mimi. Hainipi shida zaidi ya kufurahia kuwa nimemkomboa mwanamke mwenzangu naye anapata shavu na kuweza kuendesha maisha.”
WEWE NI KATI YA WASANII WALIOPATA USIMAMIZI MZURI TANGU MWANZO, NINI KIMETOKEA?
“Ni kweli mwanzoni nilikuwa chini ya menejimenti ya Smooth Vibes. Ilipofungwa au ilipobadilika, niliamua kujitegemea. Nimekaa kwa zaidi ya miaka 6 au 7 bila kusimamiwa na mtu. Kama ulisikia nipo chini ya usimamizi fulani haikuwa rasmi. Sasa nimerudi kwa Ruge. Naamini nitafanya mapinduzi tena katika muziki huu ili ufike mbali zaidi.”
UMEFANYA KOLABO NA MSANII YEYOTE KWA HAWA WALIOIBUKA MIAKA YA HIVI KARIBUNI?
“Nawakubali sana na tayari nimefanya mazungumzo nao. Nashukuru wakikutana na mimi wananiita lejendi. Wananipenda (anaingia Ben Pol, Ray anatabasamu). Nimepanga kufanya kolabo na Ben Pol (kicheko, wanakumbatiana). Pia nitafanya na Diamond (Nasibu Abdul), anafanya vizuri sana, namkubali. Nitafanya na Recho THT na Ommy Dimpoz (Faraji Nyambo) pia.”
WIMBO WAKO WA MWISHO KABLA YA MATATIZO NI UPI?
“Ni Moto Moto niliofanya na akina Red San na Nonini wa Kenya. Sikuupeleka redioni nchini Tanzani lakini ukiingia mtandaoni kwenye You Tube utaona imesikilizwa na kutazamwa na mashabiki zaidi ya 348,142 hadi sasa
- ijumaa wikienda
RAY C: SIJAPATA UKIMWI, SIJAOKOKA
MWANADASHOSTI anayejipanga kurejea kwenye gemu la Bongo Fleva kwa kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya moyoni akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana Ukimwi.
Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema ukweli ni kwamba mwanzoni alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni alibatizwa na maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yake anayesali kwenye kanisa hilo.

“Namshukuru Mungu nimepona, sina tatizo la kiafya kama Ukimwi. Kuhusu kuokoka, mimi sijaokoka. Nilibatizwa na maji mengi. Napenda mahubiri ya Sloam. Nimeungana na mama yangu anayesali kanisani hapo ndiyo maana watu wanatafsiri kuwa nimeokoka.
“Watu wakisikia mtu anasema ameokoka wanatafuta vitu ili kukujaribu. Kweli mimi sijaokoka lakini mahubiri yananiweka huru na nakuwa na amani zaidi,” alisema Ray C.
“Watu wakisikia mtu anasema ameokoka wanatafuta vitu ili kukujaribu. Kweli mimi sijaokoka lakini mahubiri yananiweka huru na nakuwa na amani zaidi,” alisema Ray C. RAY C SASA AAMUA KUOKOKA ABATIZWA RASMI LEO....!!
Subscribe to:
Posts (Atom)



