Like Us On Facebook
Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

TENDO LA NDOA NI DAWA YA MATATIZO MENGI YA KIAFYA,SOMA HAPA KUJUA MATATIZO YANAYOWEZA KUTIBIKA KWA KUFANYA TENDO LA NDOA

Kiafya

Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75. Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu
Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji.

Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)
Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

Kupunguza maumivu
Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.

Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)
Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara. Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

Kupunguza mfadhaiko wa moyo
Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen).
Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana
Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

Hupunguza baridi na mafua
Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa. Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.

Wakati mwingine nitawaletea hasara za kufanya tendo hilo mara kwa mara. Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa. Ndiyo maana nikasema ni maalum kwa wanandoa tu.

-JAMII FORUM

SOMA HAPA KUYAJUA MADHARA YATOKANAYO NA NGUO ZA KUBANA (SKIN TIGHT)

Nguo za kubana
                        Nguo za kubana

KADIRI siku zinavyokwenda kumekuwapo na ugunduzi wa vitu mbalimbali vinavyochangia kuleta mabadiliko katika jamii. Mabadiliko hayo yanaweza kuwa hasi au chanya kutegemea na aina ya  bidhaa iliyogunduliwa na matumizi yake. Zipo bidhaa zinazoonekana kuwa na matokeo ya haraka na mazuri baada ya kutumika, lakini wakati huo huo kuwa na madhara kiafya kwa mtumiaji.
Nchi nyingi zinazoendelea hasa zilizopo barani Afrika ikiwamo Tanzania zimekuwa ndizo waathirika wakubwa wa bidhaa zinaotajwa kuwa na madhara huku vijana wakiwa ndiyo kundi kubwa linaloathirika. Sababu za kundi hilo kuathirika zaidi ni kutaka kwenda na wakati kwa kujaribu kutumia kila bidhaa zinazotoka nje ya nchi bila kujua madhara yake.
Miongoni mwa bidhaa hizo ni nguo za ndani zilizoundwa maalumu kwa ajili ya kupunguza unene, pia kutengeneza umbile la mvaaji katika mwonekano wenye mvuto aupendao. Nguo hizo zimetengenezwa kwa mtindo wa mbano, (Skin tight)ambapo ikivaliwa hubana eneo la tumboni hadi kwenye mapaja na hufanya kazi ya kupunguza unene, zikiufanya mwili kuwa mwembamba kulingana na nguo husika ilivyo.
Licha ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kusaidia kwa kiasi kikubwa watu wengi kupunguza miili yao, utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa nguo hizo za ndani huchangia kwa kiwango kikubwa uwezekano wa mvaaji kupata matatizo ya kiafya.
Utafiti uliofanywa na wataalamu mbalimbali wa nchini Uingereza, unaonyesha kuwa uvaaji wa nguo hizo unaweza kumfanya mvaaji kupata maradhi ya mgongo, saratani na kiwango kikubwa cha asidi mwilini.
Mmoja wa wataalamu wa afya katika Hospitali ya The London Clinic, Dk Johnson Wilson, anasema kubana kwa nguo hizo katika eneo la tumbo huzuia mzunguko wa asidi inayozalishwa ndani ya mwili na kuisababisha kupanda juu, badala ya kushuka chini.
Anasema kuwa hali hiyo inatokana na msukomo unaotokea kwenye tumbo, hivyo kusababisha mlundikano wa asidi ndani ya mwili ambayo hupaswa kutoka baada ya kuzalishwa.
“Nguo hii inapovaliwa inatenganisha  eneo la kifuani na tumbo, hivyo asidi inayozalishwa inashindwa kushuka chini na matokeo yake inashia kwenya usawa wa  matiti na kurudi kwenye mrija unaopitisha chakula,”anasema DkWilson.
Kuhusu hatari ya saratani, Dk Wilson anasema kuwa kulundikana kwa asidi katika mrija wa chakula, kunamweka mhusika katika hatari ya kupata saratani ya koo na kinywa.
Anasema kwamba licha ya kuwa siyo watu wengi walioathirika na uvaaji wa nguo hizo, lakini matokea yake huonekana baada ya muda mrefu kutokana muda ambao mhusika atavaa nguo hizo.
“Hatari ipo zaidi kwa wanaovaa nguo hizi mara kwa mara, madhara yake hayawezi kuonekana kwa haraka zaidi, lakini kiafya kuna hatari ya kutengeneza saratani ya koo kutokana na kuzuia asidi na kusababishia irudi na kulundikana kwenye mrija unaosafirisha chakula,”anaonya.
Pamoja na hatari hiyo uvaaji wa nguo hizoi pia unachangia kusababisha ugonjwa wa ngozi unaotokana na mwili kubanwa kupita kiasi, hivyo hewa kushindwa kupita.
Dk Wilson anafafanua kuwa ikifikia hatua hiyo, kuna uwezekano wa kutengeneza mazingira ya bakteria na fangasi kujificha kwenye mwili hivyo kusababisha mvaaji kupata maradhi ya ngozi yaliyo magumu kutibika.
Mtaalamu wa ngozi Dk Sam Bunting anasema, kubanwa kwa ngozi pamoja na joto linalosababishwa na msuguano, vinachangia kuleta madhara makubwa katika mwili wa binadamu.
“Hali hii inasababisha ugonjwa unaofahamika kwa jina la kitaalamu kama Intertirgo, ambao huwatokea watu wanaovaa nguo maalumu za kubana kwa ajili ya kutengeneza maumbile,”anasema.
Nguo hizo pia huchangia kuifanya misuli ya tumbo kuwa dhaifu, kutokana na kubanwa muda mwingi, hata inapoachwa huru inashindwa kuwa na nguvu yake ya kawaida.
“Kwa asili misuli ya tumbo haina nguvu na unapoibana kwa muda mrefu unaisababishia kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi, hivyo hulegea na kuwa  dhaifu zaidi hata inapofunguliwa au kutolewa nguo inayobana,”anasema.
Kwa upande mwingine, mtaalamu wa misuli Dk Robert Shanks anasema kuwa nguo hizo zinachangia pia kusababisha maumivu ya mgongo kwa mvaaji. Anasema nguo hiyo inapovaliwa, kunakuwapo na ugumu kwa viungo vya mgongo kujongea kwa urahisi, hivyo kusababisha maumivu ya mgongo mara kwa mara.
“Viungo na mifupa iliyopo kwenye mgongo inapaswa kujongea, lakini kuibana kupita kiasi kutasababisha kushindikana kwa hali hiyo hivyo mvaaji lazima atakumbana na maumivu ya mgongo mara kwa mara”
Pamoja na madhara hayo, nguo hizi pia huweza kusababisha kizuizi katika mzunguko wa damu kwani mishipa inayotakiwa kufanyakazi hiyo inashindwa, kutokana na maeneo ya tumbo hadi kwenye nyonga yanakuwa yamebanwa.
“Ni vigumu mzunguko wa damu kufanyika vizuri katika maeneo yaliyobanwa kupita kiasi; ni wazi kuwa nguo hizi siyo rafiki, huifanya damu isizunguke inavyopaswa,”anasema Dk Shanks na kuongeza:
“Ikifikia hatua hiyo, kuna dalili mvaaji kuweza kupata maimivu ya miguu kwa kuwa mishipa ya damu iliyopo katika maeneo hayo inashindwa kufanya kazi yake vizuri.”
Kwa upande wake mtaalamu wa masuala ya ngozi nchini Tanzania, Dk Isack Maro, anasema kuwa madhara yanayotokana na uvaaji huo siyo makubwa ikilinganishwa na ripoti ya utafiti unavyoeleza.
“Inawezekana kukawapo uwezekeno wa kupata maradhi ya ngozi kutokana na mwili kubanwa kwa muda mrefu, hivyo jasho kushindwa kutoka na kutengeneza mazingira ya fangasi,”anasema Dk Maro na kuongeza:
“Madhara yapo, lakini siyo kwa ukubwa huo. Inawezekana kuwakumba watu wachache mno kati ya wengi, lakini sidhani kama yanaweza kuwa kwa ukubwa huo.”

JE WAJUA?HIVI NDIVYO WANAWAKE WANAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa za kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na zenye mahitaji makubwa katika jamii.

Waganga wa kienyeji wamekuwa wakitumia dawa hizo kama tiba ya msingi ya kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa wanaume wengi katika jamii yetu.

Hata hivyo, utafiti unaonesha kwamba wengi kati ya wanaume waliowahi kutumia dawa za asili na zile za hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hawakufanikiwa kupata tiba ya kudumu, matokeo yake wamegeuzwa kuwa watumwa wa kila wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie ‘kolezo’ la kuwasaidia kuamsha hisia zao.

Kwa wanaume, ukosefu wa nguvu ni jambo linalouma na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati yao wako tayari kutumia pesa na uwezo wao wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la ndoa ikuwa katika miliki yao daima.

Lakini, watafiti wa masuala ya mapenzi nikiwemo mimi, tumegundua kuwa wengi kati ya hao wanaolalamika kupungukiwa nguvu za kiume, hawafahamu chanzo cha matatizo na namna wanavyoweza kuepukana na kasoro hizo.

Ushahidi uliopatikana kwa waathirika wa tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume wanapokabili upungufu wa nguvu za kiume huishia kujuta na kujilaumu wenyewe bila kutazama upande wa pili wa washirika wao, namaanisha wanawake.

Zipo kesi za wanaume kujiua au kujinyofoa sehemu zao za siri kwa sababu ya kushindwa katika tendo la ndoa. Hali hii inatoa picha kwamba wanaume wengi hujitwika mzigo wa lawama wenyewe.

Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara anasema, wanawake huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo nami nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu ufuatao:


1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu.

Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”

2 : UJUZI

Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.

Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo huo.

Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.

USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.

GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao hao.

USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.

PANYA MWENYE UWEZO WA KUZALISHA DAWA YA UKIMWI AGUNDULIKA NCHINI MAREKANI

  TIMU ya Watafiti katika Chuo Kikuu cha North Carolina nchini Marekani, wamegundua aina ya sumu ambayo ina uwezo wa kuua seli ambazo zimekwishaathiriwa na Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Sumu hiyo iliyopewa jina, 3B3-PE38, inaweza kutumika kutengeneza dawa ambayo ikitumiwa na mtu aliyeathirika kwa VVU, itasaidia kuua virusi.

Watafiti wamebaini pia kuwa dawa hiyo itaweza kusaidia waathirika kutolazimika kutumia dawa za Kupunguza Makali ya Ukimwi (ARVs) maisha yao yote.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanasayansi kuweza kugundua sumu maalumu ya kuua VVU. Tafiti nyingi zinazoendelea sehemu nyingi duniani ni za kupata chanjo.

Kwa kawaida dawa ni sumu inayoua au kuathiri kiumbe kilichokusudiwa wakati chanjo ni njia ya kuufanya mwili kutengeneza wenyewe kinga dhidi ya vimelea, kulingana na aina ya ugonjwa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa wiki hii na Taasisi ya Tafiti za Kukabili Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (NIAID) ya Marekani, inasema ni ugunduzi wa kipekee.

Upekee huo unaoelezwa unatokana na ukweli kuwa kwa sasa dawa zilizopo za ARV zina uwezo wa kuzuia seli nyeupe iliyoshambuliwa isimamishe mvumo wa kuzalisha virusi.

Walivyoendesha utafiti
Utafiti huo uliofadhiliwa na Taasisi ya Afya ya Taifa (NIH) ya Marekani, unaelezwa kuwa panya 40 walitumika katika kutafiti 3B3-PE38.

Walichofanya watafiti hao ni kuwagawa panya kwenye makundi kadhaa na kupewa dozi ya sumu ya 3B3-PE38 kwa viwango na muda tofauti kuanzia wiki mbili hadi nne.

Baadhi walipewa ARV pekee na wengine walipewa pamoja na sumu hiyo ya 3B3-PE38.

Katika utafiti huo, walibaini kwamba wale ambao walitumia ARV pamoja na sumu hiyo, waliweza kupunguza kwa kiwango kikubwa VVU pamoja na seli ambazo tayari zimeathirika.Taarifa za awali zinaelezwa kuwa sumu hiyo inaweza kusaidia kutibu watu walioathirika na mojawapo ya aina ya VVU

MAMA KIKWETE ASISITIZA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO


img_0858_04a5f.jpg
Na Magreth Kinabo – Maelezo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka Watanzania kuongeza juhudi za kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi(VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili katika Tanzania iweze kuwa na kizazi kisichokuwa na VVU na ugonjwa wa Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa wadau wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha mama Kikwete aliwataka Watanzania kuchangia sh. 100 katika kupambana na tatizo kwa mchango utawapa nguvu wadau wengine kuwaunga mkono.
Aliwataka wadau wamaendeleo kuendele kuunga mkno katika juhudi za kuondokana na tatizo hilo.
" Lazima juhudi za makusudi zifanyike bila kuchoka kwa maeneo yote Serikali, NGO's, taasisi za dini mashirika ya kiraia na watu binafsi . Hii itasaidia kunusuru kizazi chetu na kuwa na nguvu kazi iliyobora, kizazi kisichokuwa na maambukizi na VVU na Ukimwi," alisema Mama Kikwete huku akisisitiza Tanzania bila Ukimwi inawezekana.
Aliongeza kuwa mikakati imara na endelevu ni lazima iwepo kama vile kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa kushirikisha jamii na kutoa tiba kikamilifu zinaweza kupunguza maambukizi hayo.(P.T)
Alisema asilimia 98 ya wakina mama wajawazito wanahudhuria kiliniki angalau mara moja na asilimia 43 mara nne wakati wa ujauzito kati ya hao, asilimia 81 wanapimwa VVU.
Aliwataka wakina mama wajazito kuhudhuria kiliniki wakati wa ujauzito kuanzia siku ya kwanza hadi watakapoajifungua ili idadi ya wanahudhuria kiliniki iweze kufikia asilimia 100.
Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alisema hivi sasa Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi hayo kwa asilimia 15 mwaka 2012 kutoka asilimia 19 mwaka 2011 na lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2015.
Alisema asilimia 90 ya wakina mama wajawazito wamepimwa VVU kati yao asilimia 64 wamegundulika wanaishi na VVU , pia asilimia 55 ya watoto wanapatiwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.(ARV's).
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara hiyo , Dk .Neema Rusibamayilla alisema alisema awamu ya pili ya kupambana na tatizo hilo itaanza Januari mwaka huu katika mikoa mingine 16.
Mratibu wa huduma hiyo kutoka Malawi, Dk. Michael Eliya alisema ni muhimu kuweza katika utoaji wa huduma, kuboresha miundombinu ,ikiwemo rasilimali fedha na watu katika kufanikisha malengo hayo.
Mwisho.

JE WAJUA? HIPS AU MAKALIO MAKUBWA..NI ISHARA YA AFYA KITAALAM....?? SOMA HAPA NIKUJUZE..

 
Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani, katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya. 

Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe. Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makaliao 
makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo hayasaidii chochote.

Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa mengineyo kama kisukari. 

Watafiti hao wameeleza kwamba, kuwa na mafuta kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo makubwa ya umetaboli.
Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba, ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno.

Ingawa suala hilo linaonekama kana kama ni kinyume, lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko kuna faida kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi hutoa mada inayoitwa cytokines ambayo huleta uvimbe katika mwili.Mada za cytokines zinahusiana moja kwa moja na magonjwa ya moyo na kisukari.

Kuyeyuka taratibu kwa mafuta katika mapaja pia husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na jinsi mafuta yanavyochomeka.

Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko unene wa tumbo.

ILA IKUMBUKWE MAKALIO NA HIPSI ZINAZOONGELEWA HAPO JUU NI ORIGINAL TU..KWA WALE WALIO YAPATA DUKANI HAPA HAMHUSIKI.

FAIDA 12 ZA MACHUNGWA KWA AFYA YAKO,SOMA ZAIDI

Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.


1. UKOSEFU WA CHOO
Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.


2.UGONJWA WA MOYO
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!
3. SHINIKIZO LA DAMU
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.


4. UGONJWA WA MAPAFU
Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.
5. MIFUPA NA MENO
Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.


6. AFYA YA NGOZI
‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’. 

7. KOLESTRO
Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.

8. UKUAJI WA UBONGO
Chungwa moja lina kiasi cha asilimia 10 ya ‘folic acid’ inayohitajika mwilini kila siku. Madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri.
9. KINGA YA MWILI
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.

10. UGONJWA WA FIGO
Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.
11. UGONJWA WA MAFUA
Kutokana na wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula machungwa mengi kadii uwezavyo ili ujiepushe na mafua.
 
12. KINGA YA MAGONJWA MENGI
Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu, nimonia na kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili kupata faida hizo.

MADHARA YA KUJICHUBUA/ KUJIPODOA AKA KUJI CREAM.

Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango,
hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.
Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.
Madhara ya kujichubua ni yapi?
Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.

HIZI NDIO FAIDA YA JUISI YA MIWA KWA AFYA YAKO

Inafurahisha kuona kuwa wapo wafanyabiashara wengi maeneo tofauti tofauti Nchini mwetu na mitaa tofauti tofauti wanaouza juisi ya miwa.
Kimsingi juisi hii ni sukari halisia ambayo haijachakatwa.
Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho na madini kwa wingi.
Miwa ina faida nyingi kiafya. Juisi ya miwa inafahamika na wataalamu wa afya kwa kuwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo.
Kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina kalori 11. Madini halisi na vitamin zinazopatikana katika sukari ni kama phosphorus, calcium, madini ya chuma na potassium.
Si hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda lenye alkali hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa.
Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.

Virutubisho vilivyopo katika miwa vina manufaa makubwa katika kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu kama figo, moyo, ubongo na viungo vya uzazi.
Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie sukari iliyopo kwenye miwa kwani haina madhara yoyote kwao. Uzuri wa juisi ya miwa ni kuwa sukari yake ni halisia.
 
-manyandahealthy

WAATHIRIKA WA UKIMWI WAGOMA KUTUMIA DAWA ZA ARV'S..



WAGONJWA 272,939 wameacha kutumia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV’s). Kutokana na hali hiyo, virusi vya ugonjwa huo vimeanza kuwa sugu kwa kuwa havipati dawa za kupambana navyo. 
Taarifa hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam.

Tafiti zinazoendelea kufanyika zimeonyesha kuwa, mtu anayetumia ARV’s inavyostahili uwezekano wa kumwambukiza mwenzake unapungua hivyo nawashauri watu waendelee kuzitumia, naomba wasiache kwa sababu sasa tunaambiwa theruthi moja ya walioandikishwa hawatumii ARVs, ”alisema Dk. Bilal.

Pia alizitaka mamlaka husika kuchukua hatua kali kwa watu wanaosambaza dawa bandia za ARV’s.

Kulingana na takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii hadi kufikia Juni mwaka huu watu milioni 1.2 walikuwa wamesajiliwa kwa ajili ya tiba na matunzo na kati yao waliokuwa wameanzishiwa ARV’s ni 736,664 lakini wanaotumia ni 463,725.

Kwa upande wa watoto waliosajiliwa kwa ajili ya ARV’s ni 91,283 na wanaoutumia ni 60,572.

Dk. Bilal alisema tayari serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya mikoa yenye maambukizi makubwa ya Virusi vya Ukimwi kwa kuangalia vichocheo vinavyosababisha maeneo hayo kuwa na maambukizi hayo makubwa.

Pia, alisema wamekamilisha taratibu za uanzishwaji wa mfuko maalum wa ukimwi ambao unalenga kuongeza fedha na kupunguza utegemezi kutoka kwa wahisani.

Katika maadhimisho hayo, Dk. Bilal pia alizindua mkakati wa awamu ya tatu wa kudhibiti ukimwi nchini ambao umejikita katika kutokomeza maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na ukimwi.

Naye Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, alisema mwaka jana wajawazito 73,955 waligundulika kuwa na virusi vya ukimwi na kati yao 44,799 walipewa ARV’s ili kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Hata hivyo, alisema karibu asilimia 50 ya wajawazito wanajifungulia majumbani na kwamba imekuwa ni sababu kubwa ya kutoanzishiwa dawa.

Pia alisema kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wachangiaji damu kwa hiyari kimeshuka kutoka asilimia saba hadi kufikia chini ya asilimia moja.

Kwa mujibu wa Dk. Rashid, kati ya mwaka 2007 hadi Juni mwaka huu, zaidi ya watu milioni 19.1 walipima virusi vya Ukimwi kwa hiyari.

Wakati huo huo, Naibu Waziri huyo alisema jumla ya wanaume 676,225 wametahiriwa katika mikoa 12 ambayo ilionekana kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya ukimwi na kiwango kidogo cha tohara ya wanaume.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Nchini (NACOPHA), Vitalis Makayula, alisema unyanyapaa bado upo na hivyo akawataka watunga sera, watoa maamuzi na vyombo vya habari kuepuka kutoa lugha ya unyanyapaa kwani inarudisha nyuma juhudi za kupambana na VVU.

Pia aliitaka Serikali kuwahakikishia uwepo wa dawa za kutosha na zenye ubora unaozingatia viwango vilivyowekwa ili kila anayehitaji aweze kuzipata kwa wakati.


MAJANGA:BIKIRA kwa wasichana yageuka kitu 'adimu' huko Zanzibar..!!

Photo DAKTARI mwenye dhamana ya kituo cha Mkono kwa Mkono ambacho kinachunguza wanawake waliodhalilishwa ikiwemo kubakwa, Dk Marijani Msafiri amesema asilimia 80 ya watoto wa kike wanaoletwa kituoni hapo na wazazi wao , wanafikishwa kuchunguzwa masuala ya ubikira.
Dk Msafiri alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kupata maelezo zaidi kuhusu matumizi ya kituo hicho ambacho kimewekwa kwa ajili ya kutoa huduma za haraka kwa wanawake wanaopata matatizo ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kulawitiwa.
Alisema kituo hicho kinatumika vibaya kinyume na malengo yake ambapo wazazi wanawalazimisha watoto wa kike kuchunguzwa bikira yao baada ya kuwatilia shaka kwamba wanayo mahusiano ya kimapenzi na wanaume.
Kituo hiki Mkono kwa Mkono malengo yake ni kutoa huduma za dharura kwa wanawake wanaokabiliwa na matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa.....sasa wazazi wanawaleta watoto wao hapa baada ya kuwatilia shaka kwamba wanamahusiano ya kimapenzi na wanaume kwa ajili ya kuchunguzwa kujua ubikira wao,” alisema.
Alisema huo ni aina mpya ya udhalilishaji wa kijinsia kwa sababu wanawake wengi wanapinga kuchunguzwa ubikra huo ambapo kazi hiyo inafanyika kwa nguvu kwa maelekezo ya wazazi tu. Aidha alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa madaktari wa kufanya vipimo na kuchunguza matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa au kuchunguza ubikra ambapo kazi hizo hufanywa na madaktari wanaume.
Kituo cha Mkono kwa Mkono kilifunguliwa miaka miwili iliyopita ambapo lengo lake kubwa ni kurahisisha kupatikana kwa huduma zote katika kituo kimoja za matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo matukio ya ubakaji.
Kituo hicho kinachotoa huduma zake katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini hapa kinatoa huduma zake kwa ushirikiano mkubwa wa mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia afya na maendeleo ya mtoto na mwanamke ikiwemo UNFPA na UNICEF.

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UGONJWA WA FIGO UNAOTOKANA NA KISUKARI (DIABETIC NEPHROPATHY)


YAPO madhara ya ugonjwa wa kisukari katika mwili wa binadamu  na moja wapo ni ugonjwa wa figo (diabetic nephropathy) pamoja na ukosefu wa nguvu za kiume.
Matatizo haya huwapata watu wenye kisukari na hutokea muda mrefu baada ya mtu kugunduliwa kuwa na maradhi ya kisukari.
Tutaeleza baadaye kwa nini wenye ugonjwa wa kisukari wanakuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume lakini leo tuangazie tatizo la figo ambayo ina mamia kwa maelfu ya vijiumbo vidogo viitwavyo Nefroni (Nephrons). Kazi ya hizi Nefroni ni kuchuja damu na kutoa uchafu mwilini mwako kwa njia ya mkojo.

Kwa watu wenye kisukari, Nefroni huwa na tabia ya kunyauka, kuzeeka na kuwa na makovu kadiri miaka inavyopita. Baada ya muda fulani, hushindwa kabisa kazi yake ya kuchuja uchafu, matokeo yake protini ambazo kwa kawaida huwa haziwezi kuchujwa, hufyonzwa na kutoka katika mkojo.
Chanzo hasa chakunyauka na kuzeeka huko au kuwa makovu kwa Nefroni hakijulikani lakini udhibiti mbaya wa sukari husababisha uharibifu wa figo, na madhara huongezeka maradufu kwa watu wenye shinikizo la damu lisilodhibitiwa.
Ifahamike kuwa si kila mwenye kisukari anaweza kupata ugonjwa wa figo lakini watu wengi wenye maradhi haya kwa upande wa wanaume huwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Wagonjwa wa kisukari ambao pia ni wavutaji wa sigara, na wale wenye aina ya kwanza ya kisukari (type 1 Diabetes Mellitus) kilichoanza kabla hawajafika miaka 20, wana hatari kubwa ya kupata matatizo ya figo.
Dalili
Kwa kawaida, mtu mwenye tatizo hili anaweza asioneshe dalili zozote katika miaka ya mwanzo ya ugonjwa. Mara nyingi dalili huanza kujitokeza miaka 5 mpaka 10 baada ya figo kuathirika nazo ni kukosa hamu ya kula, kujihisi uchovu na kwa ujumla kutojihisi vizuri.
Dalili nyingine ni pamoja na kuumwa kichwa, kichefuchefu na kutapika na kuvimba miguu.

Vipimo
Kwa watu wenye kisukari, wanashauriwa kufanya uchunguzi wa figo zao mara moja kwa mwaka ambapo utachunguzwa kama una dalili zozote zinazoashiria matatizo ya figo. Utapimwa mkojo kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha protini iitwayo Albumin au Microalbuminuria.

Kuwepo kwa kiasi kingi cha protini katika mkojo ni mojawapo ya dalili za kuwepo kwa tatizo katika figo.Vipimo vingine ni pamoja na kiasi cha Urea Nitrogen katika damu (BUN), kiwango cha Creatine katika damu (serum creatinine), kiasi cha protini katika mkojo wa saa 24 (24-hour urine protein), kiasi cha madini ya Phosphorus, calcium, bicarbonate, PTH, na Potassium katika damu, kiasi cha wingi wa damu (Hemoglobin), na wakati fulani kufanya Biopsy ya figo kwa ajili ya uthibitisho wa tatizo.
itaendelea wiki ijayo.

AFYA:MAUMIVU YA KORODANI (TESTICULAR PAINS)

KWA kawaida mwanaume ana korodani mbili ambazo zimehifadhiwa katika mfuko maalum wenye tabaka tatu na ndani kuna kiasi kidogo cha maji kinachozunguka korodaniili kuilinda. Mwanaume endapo atakuwa na korodani moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo kubwa. Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume, mwanaume anaweza kuwa na korodani zote mbili lakini akashindwa kuzalisha mbegu za uzazi kutokana na matatizo mbalimbali tuliyoelezea katika toleo lililopita.

Mwanaume mwenye korodani moja anaweza kuzalisha mbegu au asizalishe kabisa, kitu cha msingi akapimwe hospitali kuona
uwezo wa hiyo moja. Mwanaume ambaye hana korodani kabisa hawezi kuzalisha mbegu za uzazi hivyo hana uwezo
wa kumpa mimba mwanamke. Tatizo la kuwa na korodani moja au kukosa kabisa tutakuja kuliona katika makala zijazo.

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Maumivu ya korodani hutokea katika korodani au haswa moja au zote mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi. Maambukizi haya yanaweza kuwa makali na ya muda mfupi,yanakuwa makali kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe au kwa dawa baadaye yanarudi tena yakiwa makali sana kama mwanzo au pia huwa sugu yaani unakuwa na maumivu ambayo siyo makali ila ni ya muda mrefu na yanayokunyima raha. Maumivu ya korodani yanaweza kuwa makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani inavimba kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo hili kitaalam huitwa ‘Fournier’s gangrene’ au inatamkwa ‘Fonias gangrini’.

Vilevile inaweza kutokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha ukapata maumivu makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni, tatizo hili linaitwa ‘Testicular Torsion’. Matatizo haya kwa ujumla wake tutakuja kuyaona katika makala zijazo.

CHANZO CHA TATIZO
Maumivu ya korodani yana vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale yanayochukua takriban zaidi ya miezi mitatu. Maumivu makali na ya ghafla
huwa hayavumiliki na huwa na tiba ya dharura. Maumivu haya sugu huwa kwa kipindi fulani hasa kwa wanaume ambao wametoka kufunga uzazi ‘Vesectomy’ lakini baadaye hupoa. Vilevile husababishwa na maambukizi katika korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits, Prostatis na Orchitis ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi vya mwanaume na husababisha ugumba.

Tutakuja kuona katika matoleo yajayo. Vilevile korodani inaweza kuwa na vivimbe kwa ndani,pembeni au juu ya kokwa au kuizunguka. Uvimbe au vivimbe hivi vinaweza kuwa na mishipa ya damu iliyojikunja humo, kujaa maji isivyo kawaida, mbegu za kiume kujikusanya na kushindwa kutoka na mengine ya kitaalam ambayo pia tutakuja kuyaona.

Yote haya humsababishia mwanaume ugumba. Maumivu pia husababishwa na kuumia korodani au baada ya kufanyiwa upasuaji kama tulivyokwishaona hapo awali. Maumivu yatokanayo na korodani au kende kujinyonga huwa makali sana na korodani zikiguswa
huuma sana na kawaida huendelea hivyo kwa masaa yasiyozidi sita.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0713354389, 0752133700 kwa maelezo zaidi.


PICHA:NESI ANASWA AKINGONOKA NA DOKTA NDANI YA HOSPITALI,HII NI LAANA


http://theclicktz.blogspot.com/2013/11/je-tanzania-bila-ukimwi-itawezekana.html


http://theclicktz.blogspot.com/2013/11/je-tanzania-bila-ukimwi-itawezekana.html
http://theclicktz.blogspot.com/2013/11/je-tanzania-bila-ukimwi-itawezekana.html

YAFAHAMU MADHARA YA KUJICHORA TATTOO.

 
Producer Pharrell Williams alishawahi kukiri kuwa alipata maumivu makali sana wakati anafuta tatto alizochora wakati wa ujana wake na akajutia kitendo hicho. Alikuwa muoga wa magonjwa atakayopata baada ya tattoo kufutwa na mionzi mikali kwenye mwili wake inayoweza kusababisha saratani na magonjwa mengine.

Picha Zingine Ziko Hapa
Angelina Jolie alibidi afute tattoo ya mpenzi wake wa awali Billy Bob aliyoichora wakati wako pamoja.



Huyu ni mwigizaji Matt" Damon alijichora tattoo kabla hajawa B list Super Star wa filamu marekani na kuamua kuifuta ili kujenga heshima zaidi.

Jamaa aliweka midomo ya rapper Trina kwenye shingo yake wakati wako pamoja na baada ya kuachana nae alibidi afute tattoo, Maumivu yake sasa.

Baada ya kuachana na mke wake Jennifer Lopez, Mac Anthony alibidi afunike tattoo ya jina la Jennifer na kitu kingine. Aliogopa maumivu ya kufuta.


50 Cent kashazoea kufutwa na kuchora tattoo zingine kwenye maisha yake. Akiwa na jambo jipya huongeza tatto anavyo jiskia.

 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari