Like Us On Facebook

Muswada wa kura ya maoni wa mwaka 2013 wapita.

BUNGE limepitisha muswada wa kura ya maoni wa mwaka 2013. 
 
Muswada huo ambao ulikwama kupitishwa juzi kutokana na hitilafu ya umeme na kusababisha vipaza sauti kugoma, ulipitishwa jana kwa wabunge kutakiwa kuitikia ndiyo au siyo.
  
Hata hivyo, muswada huo ulikuwa na mvutano mkali kati ya serikali na wabunge wa upinzani, huku baadhi ya wabunge wakichafua hali ya hewa kwa kudai kuwa wabunge wa Bara wasijadili mambo ya Zanzibar.
 

Aliyechafua hali ya hewa alikuwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), ambaye alisema hakuna sababu ya wabunge wa Bara kuwasemea wananchi wa Zanzibar na badala yake wasemewe na Baraza la Wawakilishi.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari