Showing posts with label Ney Wa Mitego. Show all posts
Showing posts with label Ney Wa Mitego. Show all posts
"NILISHAWAHI KUMPA KICHAPO CHA MBWA MWIZI BABA YANGU ALIPOMPIGA MAMA YANGU".....NEY WA MITEGO
Nay
wa Mitego ni moja kati ya wasanii wenye tungo zenye utata sana tangu
anaanza kufanya muziki ambapo alikuwa akisikika kwenye baadhi ya ngoma
akimchana hata baba yake mzazi kwa kushindwa kuwa responsible kwake.
Hit maker wa ‘Muziki Gani’ ambae anakiri kuwa zamani alikuwa mkorofi sana na kwamba sasa hivi amebaki kuongea tu kwenye muziki, amewahi kufunguka kuwa alimpa kichapo baba yake wa kambo/baba yake wa kufikia ambae alikuwa akimtunza kwa muda huo.
Kisa cha kumpa kichapo mzee wa watu.. ni kwa sababu alikuwa anampiga sana mama yake Nay wa Mitego kitu ambacho kilikua kinamuumiza sana yeye, na mwisho wa siku akachukua uamuzi wa kumpiga akimtetea mama yake.
Tukio hilo lilimsukuma Nay wa Mitego kuandika mashairi ya wimbo unaohusu wanawake akiwaambia wanaume wenye tabia kama za baba yake wa kufikia kwamba ‘Mwanamke hapigwi, anatulizwa na mapenzi.’
“Ule wimbo ulikuwa ni dedication kwa mama yangu mzazi, mama yangu mzazi alikuwa anaishi na baba yangu wa kufikia, yule baba yangu alikuwa mkorofi sana, alikuwa anampiga sana mama bila sababu, kiasi kwamba alisababisha mimi na mama tusielewane kwa sababu mimi nilikua sipendi vile alivyokuwa anamfanyia mama, mi nakumbuka kwa bahati mbaya nilishawahi kumpiga yule mzee and then mama yangu akachukua hatua ambayo mimi sikuitegemea kwa sababu mimi nilikuwa namtetea mama.
“Mi nikajifunza kwamba mwanamke hatakiwi kupigwa hata siku moja, na ndo maana nikaimba, so ilikuwa dedication kwa mama yangu na wanawake wote Afrika.” Alisema Nay wa Mitego.

"BASATA KUNA KITU WANATAFUTA KUTOKA KWANGU....." NEY WA MITEGO

kizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu Nay amesema amekuwa akivaa mlegezo kwa kipindi cha miaka ishirini hali ambayo itamwia vigumu kubadilika kutokana ni mtindo ambao ata mashabiki wake wengi wameuzoea.
“Nahisi kuna kitu kingine wanakitaka toka kwangu kuhusu muziki wangu ndiyo maana wananitishia kunifungia wakati mimi nafanya muziki kama ndiyo maisha yangu, kwahiyo kubadilika kwa haraka kuvaa mlegezo siwezi labda baada ya miaka 3 ila inategemea” Alisema Nay.
Aidha katika mahojiano mengine na kipindi cha Showtime kupitia kituo cha RFA ya Mwanza Nay amesema kuwa Baraza hilo lina majukumu mengi ya kufanya kwaajili ya kuboresha maslahi ya wasanii badala ya kuhangaika na kumzuia kuvaa mlege ili hali wanaovaa hivyo ni wengi.
“Sasa hata baraza la sanaa Tanzania wana shughuli nyingi sana za kufanya nyingi sana ili sanaa yetu isonge mbele mambo yetu yaani wasanii tuishi maisha mazuri lakini si swala la kufuatilia mlege wa Nay, hapana kuna kitu behind ambacho kinaendelea sijui ni nini maybe wameamua waanzie hapo ili wastopishe kile ambacho nakifanya.”
RUNGU LA BASATA KUMWANGUKIA NEY WA MITEGO BAADA YA KUKAIDI AGIZO LAO NA KUENDELEA KUVAA MLEGEZO JUKWAANI.
Msanii wa Hip pop Ney wa mitego 'TRUE
BOY' Amewaonyesha uso wa mbuzi Basata ambao awali walimwonya kutokana na
tabia yake ya kuvaa mlegezo "KATA K" akiwa jukwaani kwa madai ya kuidhalilisha sanaa hiyo..
Katika hali ya kushangaza kabisa Msanii huyo ameonekana kupuuzia agizo hilo la basata na kendelea kuvaa mlegezo wakati akilishambulia Jukwaa huku akishangiliwa na mashabiki lukuki wa Bongo Fleva .
Tukio hilo lilitokea jana wakati wa Show ya FIESTA DAY 2 iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaderz Club alipokuwa akiwapagawisha wapenzi wake na kibao chake cha "MUZIKI GANI" Akiwa sambamba na Msanii mwenzake Diamond Platinumz.
Sasa wapenzi wa Bongo fleva wanasubiri Rungu la Basata liweze kufanya kazi yake huku wengi wakionekana kumtetea kwa kudai kuwa kila mtu ana aina ya maisha yake 'Life Style'

MOHOMBI,DAVIDO,NAY WA MITEGO NA DIAMOND KUPIGA SHOW YA BURE LEO KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB KUANZIA SAA TISA ALASIRI

Ni katika uwanja ule ule, jukwaa lile lile la Serengeti Fiesta Dar es Salaam ambapo Diamond,Davido,Mohombi pamoja na Nay wa Mitego watapanda kuanzia saa 9 jioni mpaka saa 12.Show hiyo ya bure itapambwa pia na bendi ya Twanga Pepeta.
BASATA WAMTAKA NEY WA MITEGO KUTOVAA MILEGEZO ( KATA K ) KATIKA SHOO ZAKE

Kwenye interview yake na millardayo Ney amesema alipigiwa simu sana na namba moja lakini alikua amelala, alipoamka akakuta missedcalls nyingi so ikabidi apige ndio akaambiwa BASATA kuna barua yake ambapo baada ya kushindwa kwenda alipelekewa Manzese.
Ney anasema: "Sielewe kama BASATA ndio wameamua kudili na milegezo, sijaelewa wao wanaangalia nini zaidi, nimejaribu kuuliza wakasema nikiendelea watanifungia kazi zangu....
"Ni kweli navaa mlegezo lakini kuna vitu vingi sana vya kufanyia kazi wao kama BASATA manake tunaibiwa kazi zetu kila siku mbona hawashughulikii hizo?’
"Mi tangu niko shule mlegezo ni tatizo langu kubwa ila nitajitahidi kupunguza japo nashangaa nimeandikiwa barua mimi mwenyewe wakati kuna wasanii wanavaa mlegezo hata kuliko mimi"
NEY WA MITEGO AWEKWA SERO BAADA YA KUTUMIA SARE ZA POLISI BILA KIBALI KUFANYA VIDEO YAKE YA "SALAM ZAO".
Rapper Ney
Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea Jana
wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao'.
Ney Wa
Mitego Amesema ' Nikweli nilitupwa sero jana baada ya raia wasio
julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu kwasababu kulikuwa na waigizaji
waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha
kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video
yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi.
Mitego
ameendela kusema kuwa baada ya kuka sero kwa dakika kama 15 mkuu wa
kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya
kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuonekana uraiani.
Ney aliwekwa
sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo
video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania.
NEY WA MITEGO ATISHIWA KUUAWA...

Ingawa anaandamwa na watu hao msanii huyo hakuwa tayari kuwataja wala kuwaweka wazi watu hao anaodai kumtishia maisha.
Msanii huyo anatamba na single yake inayojulikana kwa jina la 'Salaam Zao' ameandika taarifa hiyo ya kuandamwa na watu hao ambao hadi sasa hawajajulikana ni akina nani katika ukurasa wake wa Istagram.
Ney aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya watu wanamchukia yeye kutokana na kazi zake za muziki huku akibainisha kuwa watu hao wanatamani yeye apoteze maisha.
"Huu muziki sasa utanitoa roho sina ugomvi na mtu lakini kumbe kuna watu wananichukia kweli na wanatamani hata nife leo au wanitoe roho, mimi nafanya muziki vita yenu juu yangu namuachia mungu" aliandika katika mtandao wake wa Istagram.
Aliweka wazi kuwa yeye anaamini anafanya kazi nzuri hivyo hakuna mtu yoyote wa kumshusha wa kumrudisha nyuma, huku akisisitiza kuwa hata wakitumia imani za kishirikina hawatafanikiwa kwani yeye si wa kawaida.
SAKATA LA MADAWA YA LAMGEUKIA NEY WA MITEGO....MAAFISA WA USALAMA WAANZA KUCHUNGUZA NYENDO ZAKE
Rapper Nay Wa Mitego amesema amekuwa akisumbuliwa mno na maafisa
usalama pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wanaomdhania kuwa
anajihusisha na biashara ya madaya ya kulevya kitu ambacho amekuwa
akikanusha kwamba sio kweli.
Akiongea na Bongo leo kwa njia simu Nay amesema anasikitishwa kupokea taarifa zinazodai kuwa anajihusisha na biashara hiyo haramu, kitu ambacho hakifanyi kwakuwa anategemea shughuli zake za muziki zinazomlipa vizuri.
“Watu wamekuwa wakishangaa sifanyi show hata mwaka mzima lakini maisha yanaenda namiliki gari ndio maana wanaongea mengi huku media na maafisa usalama wananichunguza kila siku,” alisema Nay.
Msanii huyo wa Salam Zao amesema yupo kwenye maongezi na kampuni ya simu ili imfanye kama balozi wake.
“Nasubiria mambo yangu yaende poa, nimeingia mkataba wa kuwa balozi wa mtandao wa simu hapa nchini bado muda wake kuuweka wazi kwasababu tupo kwenye makubaliano zaidi na pia ikifika muda nataka kuanika vyanzo vyangu vyote vya mapato, ” alisema.

MADAM RITA AZIDI KUJIPENDEKEZA KWA NEY WA MITEGO SASA AMPA UJAJI BSS
ANAYEJIITA MDOGO WAKE DIAMOND AMPA SALAMU ZAKA NEY WA MITEGO AMCHANA MBAYA MSIKILIZE MWENYEWE HAPA
Hii ni kali hata kuliko ule wa Diamond kabla hajatoka.Dogo anamuita Nay wa Mitego Dada Neema wa Manzese Darajani na aache kujishaua ashatolewa barua.Mchumba wake ni CHIDI Benzi na mshenga ni Dully Sykes.Anajichora maua kwa kuwa ni Bibi Harusi mtarajiwa.
Anashangaa anajiita Nay wakati wazazi wake walimpa jina la Neema.Kiukweli dogo kaua ajabu.Nay akimkamata sijui itakuaje.Ni bonge moja la ngoma na sina mbavu kwa kweli.Isikilize hapa Chini na kuidownload.
ZITTO KABWE AJIBU SALAAM ZAO YA NAY WA MITEGO

Kwake mbunge huyo, Nay ni msanii wa pili wa Hip Hop anayemkubali zaidi Tanzania baada ya Roma na kwamba anakiheshimu kile alichokisema kwenye wimbo huo kwakuwa ni kazi ya sanaa.
Tazama tweets hizi.
CarolNdosi @CarolNdosi
I wonder if @zittokabwe ever listens to hip hop..local or international..
“@CarolNdosi: I wonder if @zittokabwe ever listens to hip hop..local or international..” I do. Roma is my favourite followed by Ney
@zittokabwe @CarolNdosi surprising, after everything Nay Wamitego said in his new truck Salam zao ft Neiba Hon: Zitto still ranks him his n2
@SadiqAbdallah @CarolNdosi Ney amefanya sanaa. Nachukua maneno yake kama changamoto. Ni kazi ya Sanaa ninayoithamini sana
VIDEO:TAZAMA SHOW YA NEY WA MITEGO ILIVYONOGA BAADA YA KUIMBA NA SHABIKI HUU NI MUZIKI GANI..NOMA

Ni shabiki ambae hakuwa ameandaliwa lakini anamkubali Diamond na bahati nzuri siku hiyo alikua amevaa t shirt yenye jina la Diamond… leo sijui show ya Ney wa Mitego itakuaje hapa 88.1 Mwanza CCM Kirumba. VIDEO:
NAY WA MITEGO AKAMATWA NA POLISI KWA MATUMIZI MABAYA YA BARABARA MKOANI MOROGORO
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limemkamata msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo wa kasi wakati alipokuwa akiwahi shoo ya Fiesta iliyofanyika mjini hapa Jumapili iliyopita.
Kwa mujibu wa askari mmoja wa kikosi cha usalama wa barabarani aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo, walimkamata msanii huyo eneo la Msamvu baada ya kugoma kutii amri ya kusimama kama alivyotakiwa na askari wa barabarani ‘trafiki’ eneo la Nanenane nje kidogo ya mji.
“ Msanii huyo akiwa na gari lake aina ya Alteza alitumia vibaya barabara na kuendesha gari kwa mwendo kasi kiasi cha kupiga ovateki eneo lisiloruhusiwa na askari alipomsimamisha akagoma kutii amri hiyo.
“Askari huyo aliwajulisha wenzake kwa njia ya simu ya upepo na Nay alipofika Msamvu alikamatwa na kupigwa faini papohapo,” alisema askari huyo.
Baada ya kulimwa faini ya shilingi 30,000 msanii huyo aliachiwa na kuwahi shoo ya Fiesta iliyokuwa ikifanyika ndani ya Uwanja wa Jamhuri ambapo wasanii mbalimbali walitoa burudani ya kiwango cha juu.

NEY WA MITEGO NA MADAM RITHA HAKUNA BEEF KAMA WATU WADHANIAVYO

Katika Uzinduzi wa Video mpya ya Diamond ya wimbo unaoitwa Number 1 , Madamme Ritha wa BSS alikutana Live live na Ney wa Mitego ambaye alimchana sana kwenye wimbo wake mpya akiuliza milion 50 za BSS zinaenda wapi ? kwani washindi stil bado wamechoka kimaisha...ili kuonyesha kuwa hawana Beef kati ya yao waliamua kupiga picha ya Pamoja....
Hongera Madamme Ritha kwa kuonyesha ukomavu..Ingekuwa mwenzangu na Mie hapo mbona Beef lingekuwa Another Level....
NISHA:NAY HAKUNIPATA KIRAHISI
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema hata kama msanii Nay wa Mitego akiwa na mpenzi mwigine kwa sasa lakini anajivunia kupendwa na kijana huyo kwani alihangaika sana kumpata
Akizungumza na paparazi wetu, Nisha alisema Nay alimfuatilia kwa kipindi kirefu na alimzungusha kama miaka miwili kabla hata hajawa staa. “Nikivuta ile picha ya kumdengulia kiasi kile mpaka kuamua kumkubali, naamini alinipenda tu na hata kama hakunipenda lakini najivunia kwamba alihangaika kunipata,” alisema Nisha.
Wawili hao walidumu katika uhusiano wa kimapenzi kwa miezi kadhaa kabla ya kuachana na kila mmoja akichukua ‘hamsini zake’.

"NIKIFA SIHITAJI KAMATI YOYOTE YA KUENDESHA MSIBA WANGU .....KAMA WALIKULA ZA NGWEA, WATASHINDWA NINI KWANGU?".. NAY WA MITEGO
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Ney wa Mitego, ameweka wazi kuwa ikitokea amefariki dunia hatohitaji kamati kwa ajili ya kuendesha mipango ya msiba wake, kwa kile anachodai kuwa kamati hizo zipo kwa ajili ya kuvuna pesa.
Hayo aliweka wazi baada kupokea ujumbe mfupi kwenye simu yake wenye vitisho uliotokana na mashairi alioimba kwenye single yake mpya ya 'Salaam zao' .
Ujumbe huo wa vitisho ambao umepokelewa na msanii huyo umekuja mara baada ya msanii huyo kuachia single yake hiyo ambapo moja ya mashahiri ni juu ya hela za rambirambi zilizopatikana katika msiba wa msanii Ngwear pamoja na Kanumba kushindwa kuwafikia walengwa.
Akizungumza na jarida la Maisha, mara baada ya kutuma ujumbe alioupokea wa vitisho kwenye ukurasa wake wa 'Instagram', Ney wa Mitego aliweka wazi kuwa amepokea ujumbe wa vitisho mara baada ya kuachia nyimbo hiyo.
Alisema kuwa amepokea ujumbe mbalimbali ambazo zipo zinazowataja wahusika moja kwa moja wale waliohusika kula rambirambi, huku wengine wakimtumia ujumbe wa kumtisha kwa kile alichokiimba katika nyimbo hiyo.
"Mimi hata ikitokea nakufa leo sihitaji mtu yeyote wa kuweka kamati ya mazishi yangu kwani najua kitakachotokea siyo mazishi bali ni kula hela na rambirambi hizo kushindwa kutimiza malengo kama yalivyokusudiwa" alisema Ney wa Mitego.
Aliongezea kuwa hawezi kuacha kuimba ukweli hata kama ataendelea kupokea vitisho.
NAY WA MITEGO ATEMANA NA DEMU WAKE.
JANA Nay wa Mitego alikuwa akiandika ujumbe wenye mafumbo kwenye Instagram na baada ya kuusoma ndani ya mistari ilibainika kuwa huenda mambo si mazuri kati yake na mpenzi wake ambaye hivi karibuni alikuwa akitarajia kumzalia mtoto lakini mimba ikaharibika.
Nay ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Munisi, jana alianza kwa kuandika ujumbe huu: Sasa mapenzi basi# by diamond Platnumz..!! Single boy# Ally Kiba#966’
Baada ya muda kidogo aliandika tena:
"Niko ivi,,, nikikupenda nakupenda kwa asilimia 100# na kila m2 atajua juu ya upendo wangu kwako..!! Bt ukizingua nakuacha na ninakusahau kwa asilimia 200# na kwa muda mchache 2.
"Nikiamua huwa sirudi nyuma..!!# Mwanamke mjinga ataivunja ndoa yake kwa mikono yake ye mwenyewe# by Linex.#966’

NAY WA MITEGO AMPA MAKAVU ZITTO KABWE....AMTAKA AACHANE NA BONGO FLEVA NA BADALA YAKE AFANYE SIASA
Mfalme wa kudiss Tanzania, Nay wa Mitego amerejea tena kuchafua hali ya hewa kwa kutengeneza mijadala kwenye radio na kwenye mtandao kwa ngoma yake mpya, Salam Zao.
Kwenye Salam Zao, Nay ameendeela kufanya kile akifanyacho kwa uzuri (do what he does best) kuponda.
Awamu hii list ya aliowadiss imeongezeka zaidi na kuingia pia kwenye siasa huku akiendelea kuwapa madongo wana hip hop wenzie.
Ameanza kwa kumdiss Madee kwa kusema kuwa yeye ndio rais wa Manzese na kwamba Madee amesanda. “Mi ndo rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda,” anachana Nay.
Nay wa Mitego ameendelea kuwadiss wana hip hip huku akiijita kuwa yeye ndio gangster rapper na anatengeneza hela huku wengine wakinuka vikwapa. Hakusita pia kuwarushia bombshell Weusi. “Yo Mchomvu wape salam ‘Kubumkubum’ waimbie watakufa njaa muziki umebadilika,” anarap Nay.
Nay pia amemdiss Zitto Kabwe kwa kurap:
“Word up Diamond, mwanangu wewe si mtoto wa Kigoma, mpe salama Zitto Kabwe mwambie afanye siasa aachane na Bongo Flava huku hatumtaki kabisa, maneno mengi, propaganda hajui kutekeleza, Kigoma Allstars tayari kawatelekeza.”
Rapper huyo pia amerap kuwa wapo watu waliojipatia utajiri kutokana na misiba ya Mangwea na Kanumba.
“Wanamiliki gari, wameota na vitambi kwa hela za rambirambi, mkizingua nawataja,”anasisitiza. Anasema tangu kifo cha Kanumba Bongo Movies imekufa na haiuzi tena.
Pia hajamuacha mwanzilishi wa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen kwa kudai kuwa licha ya kuwapa zawadi kubwa washindi, wameendelea kupigika mtaani.
“Hizi Salam ziende kwa madam Rita na Bongo Star Search. Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?! Namuona Walter Chilambo kapigika kama zamani, Haji Ramadhani kachoka yupo kitaani. Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani.”

Subscribe to:
Posts (Atom)