DODOMA, Tanzania — MBUNGE wa kuteuliwa na Rais, Dk. Asha-Rose Migiro, leo saa 3 asubuhi, ameapishwa kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania.
Akizungumza nje ya viwanja vya Bunge, baada ya kuaspishwa, na Spika wa Bunge Anna Makinda, Dk. Asha-Rose ameahidi utumishi wenye uadilifu, uaminifu na wa kujituma.
Alisema ubunge ni uwakilishi uwe wa kuteuliwa, kupitia viti maalum au majimbo na kwamba nafasi hiyo aliyopewa sio ya

"Unapopewa fursa kama hiyo sio yako binafsi bali ni heshima ya wanawake wote kwa sababu nimeongeza idadi ya waliopo bungeni’’
“Hivyo ni nafasi nyingine kuwa wanawake tunawajibu na tunapopata fursa basi tuna kila sababu ya kutumikia umma na Nchi yetu kwa moyo wote na kwa nguvu zote,"alisema Dk. Migiro.
Kwa mara nyingine Dk. Migiro alimshukuru Rais Dk. Jakaya Kikwete kwa uteuzi wake kwake kwa kuwa umempa heshima na fursa nyingine ya kutumikia Taifa.
"katika maisha mtu anaweza akafanya kazi yoyote na kazi yoyote ina thamani lakini nafikiria kazi ya kutumikia umma ni heshima ya pekee kwa sababu kama utaweza kufanya shughuli kwa ufanisi basi matokeo yake yanasambaa kwa watu wengi zaidi,"aliongeza Dk. Migiro.