Like Us On Facebook
Showing posts with label Diamond. Show all posts
Showing posts with label Diamond. Show all posts

Baada ya kumtema PENNY...Diamond amtangaza rasmi WEMA SEPETU kuwa ni MKE WAKE MTARAJIWA


Tukio hilo lilitokea  jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika kwenye show hiyo....
 
Kwenye hiyo show, Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”? Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa "ukimwona" akasema:
 “Nasikia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani”.
 
Baada  ya  kauli  hiyo, Wema Sepetu alipanda kwenye stage kisha wakakumbatiana  na kucheza wote.
994992_654719497904805_1370630389_n
379719_654725334570888_100223854_n

1499625_654740321236056_1133727884_n
-Millard Ayo

HAPANA CHEZEA DIAMOND WEWE ...MCHEKI HAPA AKIWA NDANI YA PRIVATE JET AKIELEKEA MWANZA HAPO JANA

JINSI TOTO PARTY YA DIAMOND ILIVYOKUWA LEADERS CLUB HAPO JANA,ILITISHA MBAYA


D7 
Leo msanii Diamond Platnumz aliandaa party kwa ajili ya watoto wote ambao walikusanyika Leaders Club kwa ajili ya michezo mbalimbali,kama kukimbia,kucheza mpira na vingine kibao.
D10
Kizuri kwenye toto party hii Diamond aliwachezesha watoto nyimbo yake ya My number one na walio cheza vizuri alitoa dili ya kuwasomesha kuanzia elimu waliyonayo mpaka wanamaliza.
Hizi ni baadhi ya picha kwenye party hii.
D8
D31
D28

D24
D23
D21
D22
D20
D18
D17
D16
D15
D14
D13
D12
D10
D9
D7
D6
D3


DIAMOND AFUNGUKA!: LULU ANABISHA SIJATEMBEA NAYE???..!!! WAULIZE WEMA NA PENNY WANAJUA

Elizabeth Michael ‘Lulu’.  
STAA kiwango katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekanusha uvumi uliozagaa mitaani kuhusu kutoka kimapenzi na mbabe wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

  Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Imekuwepo minong’ono ya muda mrefu kitaani kuwa, Diamond analilia penzi la Lulu lakini Diamond au Sukari ya Warembo alipoulizwa kuhusu hilo, alisema siyo kwamba analilia tu bali waliwahi kutoka (haijulikani kwenda wapi) naye, madai yaliyotupiliwa mbali na Lulu.

MADAI YA AWALI

Habari zilizotua katika meza ya paparazi wetu zinasema kwamba, wawili hao wanafanya kazi za kisanii pamoja (haikuwekwa wazi ni kazi gani kati ya filamu au muziki) lakini tatizo lililopo kati yao ni Diamond kumtaka Lulu.

Chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake, kilifunguka: “Diamond anashindwa kuelewa, tatizo yeye kila mwanamke anataka kutoka naye. Mwenzake anajua yupo kazini, yeye anataka penzi, ndiyo mzozo uliopo kati yao.

 
Wema Sepetu.

KAZI KWA DIAMOND

Paparazi wetu alimvutia waya Diamond ili kutaka kupata ufafanuzi kwa upande wake, ambapo aliposomewa maelezo yote alicheka sana kisha akasema: “Nililie penzi la Lulu? Acheni hizo... ngoja nikuambie kitu, siyo kulilia, mimi nimeshawahi kutoka naye. Nilitembea naye kishkaji tu kisha kila mmoja akaendelea na yake.

Hayo mambo yalishapita na sikutaka kuyaongelea lakini kwa sababu naona kama yanakuzwa, ndiyo maana nimeamua kuweka wazi. Kwa sasa tunaheshimiana kama kaka na dada. Kuna ugumu gani mimi kuwa naye wakati nimeshampitia?

paparazi wetu: Unasema kweli Diamond?

Diamond: Wa asilimia mia moja.

 
Penny.
paparazi wetu: Una ushahidi gani?

Diamond: Watu wanaojua hii ishu ni wawili tu; Wema (Sepetu) na Penny (Penniel Mungilwa). Niliwaeleza kwa uwazi kabisa hawa ili tusielewane vibaya. Kama huamini waulize. Hawa ndiyo niliowapa siri hii.

Paparazi wetu alijaribu kuwatafuta Penny na Wema kupitia simu zao za mkononi lakini hawakupokea.

TURUDI KWA LULU SASA

Akizungumza kwa sauti ya kujiamini, Lulu alimshangaa Diamond na kusema kwamba, si kutoka naye tu bali hana hata kazi anayofanya naye pamoja.

Nawashangaa sana eti mimi nifanye kazi na Diamond, kazi gani sasa wakati mimi na yeye tupo kwenye fani tofauti? Muziki na  filamu wapi na wapi? Kifupi hayo madai hayana ukweli wowote na kila mtu yupo na yake,” alisema Lulu na kuongeza:

 
Lulu.
Kwanza mimi siwezi kutoka na Diamond... levo zetu ni tofauti kabisa, wala hazilingani. Mimi nilianza kutoka kabla yake, nimeanza kujulikana toka kitambo hicho nina miaka mitano sijui hata kujifuta kamasi vizuri.... hakuna ukweli wowote.”

TUJIKUMBUSHE

Diamond amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na mastaa mbalimbali, huku madai hayo yeye mwenyewe akiyakubali, jambo lililosababisha aitwe Sukari ya Warembo.

Mbali na orodha ndefu aliyotoka nayo Diamond, kinachovuta hisia za wengi ni uhusiano wake wa sasa, ambapo haijulikana kama yupo na Penny, Wema au wote kwa wakati mmoja!

-GPL

MGANGA WA DIAMOND ATABIRI DIAMOND KUFULIA KIMUZIKI NA KIFEDHA HIVI KARIBUNI

Mtu mmoja anayedai kuwa mganga aliyemtoa mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameibuka tena na kueleza kuwa Diamond Platinumz tayari ameanza kushuka kimuziki kama alivyosema awali.
Mtu huyo anayejitambulisha kwa jina la Dr. Yahya Michael ameuambia mtandao wa mamuafrica kuwa kile alichokisema mwanzo kuwa Diamond Platinumz atashuka kimuziki na kurudi pale alipokuwa kimeanza kutokea ingawa watu wengi hawaoni.
“Diamond alikuwa anapiga show kwa milioni 10 lakini sasa hivi hapewi hata show ya milioni 7. Nilizungumza kushuka sio kupanda na nashukuru kwa sababu rekodi ninayo. Nimeongea kushuka sio kupanda, wale walioko nyuma yake hivi sasa ndio wanaonekana kuongoza. Hata katika mambo yenu ya kumi bora za Tanzania yeye hayumo katika mbili.” Amesema Dr. Yahaya

“Sijawahi kumuona mtu anaepanda anaambiwa ameiba nyimbo, sijawahi kuona mtu anaepanda anashindwa na yule ambaye alikuwa anamshinda mwaka jana. Na wala sijawahi kumuona mtu anaeambiwa anapanda halafu anapigwa mawe na watu waliokuwa wanataka wamuone kwa kiingilio kikubwa.” Ameeleza.

“ Kwa sababu Diamond wa mwaka 2010,2011,2012 ni Diamond aliyekuwa anapiga show Mlimani City sehemu alipozaliwa Dar es Salaam kwa kiingilio cha shilingi 50,000, siku tatu kabla ya tukio tiketi zimekwisha. Kwa hiyo Diamond wa hivi sasa ni yule ambaye anapiga show Tabora sehemu ambayo hajawahi kuonekana, kwa kiingilio cha shilingi 5,000 na watu hawaingii na bado walioingia wanampiga mayai viza na mawe.” Ametoa mchanganuo wake.
Mtu huyo akafika mbali na kuapa, “ amini, sitakufa kabla haki hii haijatendeka, naapa…kwa heshima ya mwenyezi Mungu aliyeniumba. Anasema pigania chako ali hali hata ukifa ili mradi ulikuwa unapigania chako.”
Hata hivyo, Naseeb Abdul aka Diamond aliwahi kumkana Dr. Yahya na kueleza kuwa hamfahamu na hajawahi kumuona.

PENZI LA DIAMOND NA PENY LADAIWA KUVUNJIKA,WEMA SEPETU ATAJWA KUWA CHANZO



NDIYO habari ya ‘mujini’ kwa sasa, kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, mtangazaji wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wamemwagana.....

KAMA UTANI, WEMA ATAJWA
Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, ‘mtonyaji’ wetu ambaye ni mtu wa karibu wa wawili hao aliliambia gazeti la Risasi  kuwa chanzo cha Diamond na Penny kuingia kwenye listi ya ‘zilipendwa’ kilianza kama utani.
 
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona mwenye thamani mbele ya mwenzake huku Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo.

“Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.
 
“Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
 
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?” alihoji ‘kikulacho’ huyo ambaye ni rafiki wa Diamond.

RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa za awali kutoka kwa rafiki huyo, timu ya Risasi kwa kuwatumia ‘wahangaikaji’ wake maalum, iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi hizo.
 
Watu kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo rais wake ni Diamond walihojiwa ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa sasa Diamond na Penny imebaki stori!

 SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake makini juu ya uvumi huo, hivi karibuni Diamond alionekana ‘singo’ kwenye pati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya ‘dada wa mjini’, Halima Haroun ‘ Halima Kimwana’ ambayo aliiandaa Diamond.
 
Minong’ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa vitendo vya ufuska.
 
“Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.

“Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana kwa sababu kwenye pati zote huwa wanakuwa pamoja tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi,” alisikika mmoja wa waalikwa katika sherehe hiyo.
 
Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na mwandishi  wetu na kujibu kwa kifupi: “Naumwa. Halafu si lazima nije kwani kila mtu ana ratiba zake.”
 
PENNY KIZIMBANI TENA
Baada ya kukamilisha udadisi huo kupitia kwa watu wao wa karibu, Risasi  lilianza na Penny kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini alionekana kuwa ‘mzito’ kwa kutoingia ndani kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
 
“Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo, lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
 
Mwandishi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini.”

DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya kiganjani, hakupokea licha ya kupigiwa mara kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji yenye maelezo yote, hakujibu.

MAMA DIAMOND
Ili kujiridhisha na madai hayo, waandishi wetu walimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye alisema hajui na hana taarifa hizo.

NDUGU WA KARIBU SANA
Baada ya mama Diamond, paparazi wetu alimpigia simu ndugu wa karibu sana na Diamond, sikiliza:
 
Mwandishi: “Kumbe Diamond na Penny wamemwagana we huniambii. Sasa wifi yako mpya ni nani?”
Ndugu: “Aka! Sikwambii. Kwanza mi nipo mbali, sipo Dar.

WADAU WANAJUA
Haikuishia hapo, timu yetu ilizungumza na wadau mbalimbali ambao walionesha kusikitika huku baadhi yao wakisema walitabiri tangu awali.
 
“Duh! Penny ameachia ngazi mwenyewe. Sisi tulijua hawawezi kufika mbali, maana penzi lenyewe lilikuwa na mbwembwe nyingi,” alisema mwanamke mmoja anayejua kila kitu.

TUJIKUMBUSHE
Siku za hivi karibuni Diamond alifanya mahojiano kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii ambapo moja kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na mpango wa kuoa ambapo alisema kuwa hana mpango huo kwa sasa na hatarajii kumuoa yeyote kati ya wanawake wanaotajwa kwa sana midomoni mwa watu (akiwemo Penny).
 
Source: Gazeti la Risasi / Gpl

"Nitatumia watoto yatima na wasiojiweza kuzindua Video ya 'MY NUMBER ONE REMIX' "....DIAMOND

Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Naseeb Abdul a.k.a Diamond ameweka wazi kuwa video yake ya ‘My Number One rmx’feat Davido iliyofanyika nchini Nigeria watu wa kwanza kuitazama watakuwa ni watoto yatima na watu wasiojiweza kabla ya mtu watu wengine.
 
Akiongea ndani ya 255 ya XXL- Clouds fm amesema kuwa video hiyo itatazamwa kwanza na watoto yatima na watu wasiojiweza ili kuwapa fursa sawa na watu wengine na sio kila siku kuwasahau na kuwatenga bali kuwa nao karibu kwa kila kitu. 
Hali hii itakuwa ni muendelezo wa Diamond kuweka rekodi mpya kila siku kwenye muziki wa Bongo Fleva. 
Baabkubwa inamtakia mafanikio mema na kuipeleka Bongo Fleva kwenye level nyingi ne kubwa kimataifa zaidi.

CHELSEA YAPIGWA NAYO, LIVERPOOL YAUA 4-1, SUAREZ APIGA MBILI, MAN CITY DROO

BAO la dakika ya 90 la Oussama Assaidi, limezamisha Chelsea mbele ya Stoke kwa mabao 3-2 huo ukiwa ushindi wao wa kwanza katika Ligi Kuu ya England dhidi ya The Blues ndani ya miaka 38.
Winga huyo wa mkopo kutoka Liverpool, aliingia uwanjani akitokea benchi zikiwa zimesalia dakika sita na kufunga bao hilo muhimu lililmtoa kichwa chini kocha Jose Mourinho Uwanja wa Britannia.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Andre Schurrle dakika za tisa na 53, wakati mabao mengine ya Stoke yalifungwa Peter Crouch dakika ya 42 na Ireland dakika ya 50.
Mbaya wao: Oussama Assaidi akishangilia baada ya kufunga bao lililoizamisha Chelsea mbele ya Stoke
Title blow: Jose Mourinho watches his side slip to a shock defeat at the Britannia Stadium
Kocha Jose Mourinho akiwa hana raha baada ya kipigo
Dejected: Chelsea players can't believe they lost the game in the dying moments
Wachezaji wa Chelsea wakiwa hawaamini macho yao

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, mshambuliaji Luis Suarez ameendelea kung'ara baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 nyumbani dhidi ya West Ham.
Suarez alifunga mabao yake dakika za 81 na 84, wakati mengine yalifungwa na Demel aliyejifunga dakika ya 42 na Sakho dakika ya 47, huku la kufutia machozi la wageni likifungwa na Skrtel aliyejifunga pia dakika ya 66.
Nayo Manchester City imelazimishwa sare ya 1-1 na Southampton ugenini, Sergio Aguero akitangulia kufunga dakika ya 10 kabla ya Dani Osvaldo kuwasawazishia wenyeji dakika ya 42.
Getting the show on the road: Luis Suarez (second right) saw his shot saved then go in off of Guy Demel
Mkali kweli: Luis Suarez (wa pili kulia) akipongezwa na wenzakeOpener: Suarez celebrates after his shot was saved and went in off of Guy Demel
Suarez akishangilia Tough task: West Ham's defence could not keep Suarez in check for the full 90 minutes
Suarez akitafuta mbinu za kumtoka beki wa West HamOpener: Sergio Aguero scored the first of the game when he connected with Aleksandar Kolarov's cross
Sergio Aguero akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la kuongoza Mancester City
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari