Like Us On Facebook
Showing posts with label HIP HOP. Show all posts
Showing posts with label HIP HOP. Show all posts

RAY WA MITEGO AMWAGANA TENA NA DEMU WAKE



UCHUMBA wa staa wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mpenzi wake anayefahamika kwa jina moja la Siwema umedaiwa kuvunjika. 
 
        Nay akiwa na mpenzi wake Siwema.
 
Kwa mujibu wa chanzo makini, chanzo cha kumwagana ni baada ya Siwema kukuta meseji za watoto wa kike tofauti katika simu ya Nay wa Mitego katika nyakati tofauti.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa, wawili hao walimwagana tangu Januari 2, mwaka huu, nyumbani kwa Nay wa Mitego, Manzese jijini Dar es Salaam baada ya Siwema kujiridhisha kuwa mpenzi wake huyo anamsaliti kutokana na ushahidi wa meseji alizozifuma.
Hata hivyo, chanzo kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wapendanao hao wamekuwa wakizinguana mara kwa mara na kilichomuuma zaidi Siwema ni baada ya mkali huyo kuachia video yake mpya ya Nakula Ujana ambayo ameonekana katika pozi za kimahaba na warembo kibao.
“Imemuuma sana video ya Nakula Ujana, warembo wale inasemekana hakuishia katika video, sasa aliendelea kuwasiliana nao na Siwema akagundua ndipo mtiti ulipoibuka, Siwema akarudi kwao Mwanza,” kilisema chanzo.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Siwema ambaye alikiri kugombana na Nay na kusema ameshindwa kuvumilia na ameona ili kujiepusha na presha zisizo za lazima arudi kwao Mwanza.
“Kweli tuna ugomvi na Nay na haswa kuna mambo yananikera sana ila kubwa zaidi kwa sasa ni ile video yake mpya kuna parties mle sijazipenda...mchumba wa mtu ufanye video ujiachie vile, unashikwa shikwa ovyo,” alisema Siwema.
Alipotafutwa Nay, alikiri kutokea kwa ugomvi huo na kudai yupo katika jitihada ya kumaliza tofauti hizo kwa kuzungumza na Siwema.

CHIDI BENZ AMEVURUGWA KWELI..!! TAZAMA ALICHOKIONGEA KATIKA HII POST YAKE.


Hakuna tena kitu kizuri kwa Chidi Benz siku hizi. Kwa muda mrefu rapper huyo ambaye hivi karibuni ametokea kukubalika sana nchini Kenya (thanks kwa mashavu anayopewa na Nonini) ameonekana kutoa yake ya rohoni yanayomuumiza kupitia Twitter.

Yeye na Wakazi kuna tatizo?
Picha lilianza jana, baada ya Wakazi kutweet: Na ningependa kusema pia AY, Dimpoz, Ally Kiba, FidQ, Shaa, Cpwaa, Black Rhino, Remi Ongala, Profesa Jay & Lady Jaydee ni other Local heros!
Baada ya kuona ujumbe huo wa Wakazi, Chidi alimuuliza kishari ‘nini?’
Wakazi alichuna. Chidi akaamua kuandika: Hujui kuongea huwezi muoga..unaweza kuandika hapa twitter. Nyie ndio mkianza kushindwa mnasifia maadui.#umal** tuu.”
Ujumbe huo ulivuta hisia za watu wengi akiwemo Madee aliyeuliza: Rasheeed nani tena kazingua?  Chidi alijibu:Mazafanta wanahisi wanajua kuliko wewe wakati mwenyewe saa zingine unaona hujijui..2
Hata hivyo hatuwezi kuthibitisha kama maneno hayo yalikuwa yakimlenga Wakazi ama mtu mwingine kwakuwa kabla ya hapo tayari alikuwa ameanza kuandika tweets za hasira.
“Game ilipo now na propaganda zake inaua vitu vingi tu.sisi tunaonekana tunalalamika ujinga but hatuna maisha mabaya. Viongozi wa nchi sio lazima mdil na bongo freva..haiongezi wewe kufatwa but unatuongezea uadui usio na lazima. Mi natangazwa kwa ubaya tuuuuu.ila nina marafiki bado na wengi wanaongezeka hata hapa.#nakaza roho,” aliandika Chidi.
Kunani?

NEW TRACK: "SIRI YA MCHEZO"- FID Q ft. JUMA NATURE...NI BONGE LA TRACK, ISIKILIZE HAPA


SIKILIZA HAPO CHINI...

CHIDI BENZI ATOA SABABU ZA NEY WA MITEGO KUMCHUKIA...CHEKI VIDEO YAKE AKISEMA HAYO

               Chidi Benz alieleza sababu tatu kuu alizohisi zilimsukuma Nay wa Mitego amdiss. Akiongea kwenye kipindi cha Mkasi cha wiki iliyopita, Chidi alisema baada ya kusikia diss ya Nay, aliamua kumchimba zaidi na kugundua kuwa alikuwa akisikia nyimbo za Nay hata kabla hajajulikana kwa Watanzania wengi.
“Kwanini kanidiss huyo mtoto,” Chidi alisema.

“Design yake kumbe hii, manondonondo, naye mhuni Manzese, na mimi ni Chidi najulikana kwa story za kihuni, kwahiyo mpaka dakika hii amenidiss, either maskani yao ashajipanga. Mbili kashajua kwamba siku tukikutana kwenye show ‘labda Chidi akitaka kuniletea noma, na mimi nasimama nioneshe watu kuwa mimi huniwezi wewe’. Tatu kanizingua kuna mtu ana mchongo wake katika huu muziki kazinguana na mimi kalichukua ‘hilo toto’ kaliambia ‘fanya hivi na hivi, imba sauti kama… fanya hivi beba manondo, tembea kifua wazi ile kama mimi.. eeh unakuwa..halafu tukana jamaa’. Ni mchongo wake kwahiyo hata kama mimi nikibishana ‘nalo’ vipi kuna mtu mchongo wake yeye anachukua hela.”

ROMA:NATAMANI MASHABIKI WA KIKE



ROMA Mkatoliki, Msanii wa Hip Hop Bongo, amesema kuwa amegundua kuwa, kila wakati anapotoa nafasi ya mashabiki wake wote kuchat naye na kumwuliza maswali yoyote kwa njia ya mtandao, kumekuwa na ushiriki mdogo sana wa watoto wa kike/ wanawake, Kitu ambacho ameona kuwa ni tatizo kwake kama msanii.

ROMA ama pia Baba Ivan kama anavyofahamika, amesema kuwa ugunduzi hu umempatia changamoto kuwa kwa sasa anatakiwa kujitahidi kufanya kitu kwaajili ya kuwavuta zaidi jinsia ya pili (them ladies) kwenye pool ya mashabiki wake.
Kutokana na sentensi hii kutoka kwa rapa huyu kuleta hisia kuwa huenda akabadilisha na kulegeza zaidi aina ya muziki anayofanya, Yeye binafsi amesema kuwa hana mpango wowote wa 'kulainisha' muziki wake, ila yupo katika mchakato wa kuufanya uwavutie zaidi warembo.... sooo stay tuned.
 



NEY WA MITEGO,CHIDY BENZ SASA SAFI WAPIGA SHOW SAFI SERENGETI FIESTA 2013

Yeyote ambae damu yake ipo sana kwenye muziki wa bongofleva ni lazima atakua anafahamu kuhusu ugomvi wa muda mrefu, kutoelewana kwa Chidi Benz na Ney wa Mitego, ishu ambayo ilihusishwa hata kwenye nyimbo zao.
Shuhuda mkuu wa tukio lenyewe ni msanii Madee ambae naanza kwa kumkariri anasema ‘hizi ndio faida za Serengeti Fiesta, kujuana na kukutana na watu wengi, hiki ni kitu ambacho nilikipanga mimi… watu wanafikiria tu sisi tunakwenda kule kufanya muziki, mbali na pesa tunazolipwa vizuri sasa hivi kwenye Fiesta, kuna faida nyingine pia, niliposikia Chidi Benz yupo kwenye Fiesta nilijipanga lazima nifanye hivi manake Chidi na Ney wote nawajua, nimekaa nao’
Kwenye sentensi ya pili, Madee anasema ‘niligundua Chidi ni mwepesi kukasirika, kuna wakati kwenye basi la Wasanii kulitokea kama purukushani kuhusu hawa wawili so nikasubiri tu time nzuri ifike nifanye yangu’
‘Nilipoona Chidi katulia nikamfata, nikamchukua alafu bila kumwambia kitu nikampeleka mpaka alipokuwepo Ney wa Mitego, nikamwambia haya…. simama pale nikupige picha, wakati huo sijasema chochote kuhusu ugomvi na Shilole alikua ndio kasimama na Ney, nikawapiga wakiwa watatu alafu badae nikamwambia Shilole aondoke wakabaki wawili, yani Ney na Chidi’ – Madee

Madee anakwambia baada ya kupiga picha hazikuongelewa stori zozote za ugomvi wa Chidi na Ney, kwanza zilipigwa stori za mtaani tu… za ujana alafu kitu kikaitika manake Ney wa Mitego na Chidi Benz wote walikua na furaha na walikua wanachangia mada kwa pamoja, yani kama washkaji….
Hii ishu ilitokea wakati wa show ya Serengeti Fiesta 2013 Singida 89.7 ambapo badae walikwenda Club ambako huko sasa ndio waliongea kwa kirefu, kikubwa alichokua anaongea Chidi ni kuhusu Ney kumuimba vibaya kwenye nyimbo zake lakini Ney aliweka wazi kwamba nia yake sio mbaya na wala anachokitaka sio ugomvi bali ni aina ya muziki wake, kwa mujibu wamaelezo ya Madee.
Kingine anachosema Madee ni ‘Ney ndio aina ya muziki wake, hawezi kung’aa mpaka amtaje mtu kwenye nyimbo zake na hiyo ni bishara yake, lakini anavyofanya hivyo sio kwamba anataka ugomvi, ni mtu muelewa na wala sio mtu wa aina hiyo ya ugomviugomvi, baada ya kuwapatanisha wakashikana mikono, tukawaambia wabadilishane namba za simu alafu bata likaendelea… so sasa hivi kila kitu ni fresh’
Kama ulikua hujui, Ney wa Mitego alishawahi kuwa na ugomvi na Madee zaidi ya miaka 10 iliyopita ambapo mama mzazi wa Madee aliwahi kupigwa chupa ya uso mpaka leo anayo alama usoni wakati akiamulia ugomvi wa Madee na Ney wa Mitego ambae alimfata Madee nyumbani kwao akiwa na wenzake wakitaka kumpiga.
Source:millardayo

CHID BENZ: NAACHA KUVUTA UNGA!

Rapa maarufu Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ ameibuka na kueleza kwamba alikuwa akitumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu lakini sasa ameamua kuacha baada ya kubaini kuna madhara makubwa.
Akizungumza kupitia Kipindi cha XXL cha Clouds Radio juzikati, Chid Benz alisema kuwa, amefikia uamuzi huo baada ya kushtukia kuwa alikoingia siko ndipo alikwenda kwenye matatibu nchini Kenya na hatimaye kufanikiwa kujitoa kwenye orodha ya mastaa wanaobwia kilevi hicho.


“Nilimwambia mama yangu kuwa lazima nitibiwe, nimefanya hivyo bila kwenda ‘rehab’ wala kunywa dawa, sasa niko fresh, niko healthy (nina afya), nakula vizuri, nafikiria vizuri na sasa nimetulia,” alisema Chid Benz na kuongeza:
 “Nilianza kutumia unga miaka mingi iliyopita lakini ilikuwa ni vigumu watu kujua kwa kuwa nilikuwa nakula vizuri, nafanya mazoezi, naoga kwa hiyo nilipokuwa nikitumia yalikuwa hayanitibui ila yananijaza tu chuki na ule unomanoma.”

CHID BENZ ASIMULIA JINSI ALIVYOTHIRIWA NA BANGI NA MADAWA YA KULEVYA....ANASEMA HAWEZI KUMALIZA DK 2O BILA KUVUTA


Rapper Chidi Benz leo kwa mdomo wake mwenyewe amekiri kuwa alikuwa akitumia madawa ya kulevya kwa miaka mingi. Chidi amefunguka leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.Alisema japo hakwenda Nairobi kwaajili ya rehab, mazingira yalimlazimu kutafuta tiba ili aondokane na madhara ya madawa hayo. Alieleza kuwa alipofika jijini Nairobi alikuwa akitakiwa kufanya show nyingi na mwandaaji alimuuliza kama kuna kitu atahitaji ili awezE kufanya show vizuri.


“Nikamwambia Yeah kuna vitu ntavihitaji,” alisema Chidi. “Nikamwambia ‘mimi bana kuna vitu ninavyovitumia nikikaa 20 minutes bila hivyo vitu ni noma nachanganyikiwa na akili tena sina, kwahiyo sijui tutafanyaje’. 
 Akaniambia ‘mimi ntapataje hivyo vitu Chidi na Nairobi ni gharama sana. Nikamwambia ‘mimi pia nina wazo jingine kuna mtu alinitonya kwamba kuna kitu kinaweza kikafanyika na pesa Fulani, pesa nyingi kama milioni 15, 16 hivi za kibongo. 


Akaniambia kikifanyika hicho maanake vinavyofolewa kabisa hivyo vitu vilivyokuwa vinanifanya niwe hivyo. Akaniambia ‘hiyo naijua lakini ni process, ndio maana dunia nzima haifanyi’. Nikamwambia ‘mimi nafanya kwasababu nilishakutwa na vitu vingi mimi ntafanya.”
 
Chidi anasema hela hiyo ilipatakana na wakapanga kwenda kufanya mchakato huo wa kuonana na daktari ili kutibiwa.
 
“Kwahiyo mimi sijaenda rehab na wala sijanywa zile methodone sijui watu wanasema watu wanywe methodone.”Amesema dawa aliyotumia inanunuliwa na mtu huchomwa kama mgonjwa wa kawaida.
 
“Yenyewe inakusafisha wewe pale ambapo ulikuwa ukivuta inakukaa then baada ya dakika kadhaa pakikauka panakuwa pakavu ni kama ile sehemu inakuwa mbichi wewe ukivuta. Huna hela lakini huvuti panakuwa pakavu, pakikauka ndio unachanganyikiwa unaanza sasa kuona alosto lakini kama ukiendelea kuvuta panakuwa pabichi unaendelea. 

So yenyewe inaenda kama mapovu, ni kama sabuni inaenda inakusafisha pale kote panabaki empty. Kwahiyo ni wewe sasa uamue tena kuvuta tena au uache kabisa. Lakini mimi nilienda kusafishwa pote, inakuweka unakuwa na power, inakupa akili, uso rangi, mwili unaanza kubadilika.”
 
Anasema kabla ya kupata tiba hiyo alitakuwa kusaini karatasi kadhaa kuthibitisha kuwa amekubali kupewa dozi.“Mama yangu pia alikuwa anajua, nilimwambia kwamba mimi bana inabidi nitibiwe.”
 
“Niko fresh, niko healthy, nakula vizuri, naishi vizuri, nafikiria vizuri na nimecalm down,” alisema Chidi kuelezea hali yake ya sasa.

Chidi amekiri kuwa alianza kutumia madawa ya kulevya muda miaka mingi iliyopita lakini ilikuwa ngumu wengi kujua kwasababu alikuwa akiutunza vizuri mwili wake.
 
“Naoga vizuri, nakula vizuri, nafanya mazoezi daily, gym daily, kwahiyo hata nikivuta hayanitibui kitu lakini yalikuwa yananijaza tu anger ndani, chuki na ule unoma unoma.”

DOGO JANJA AMPIGIA MAGOTI MADEE ILI AMRUDISHE TENA TIP TOP CONNECTION


Kuna kila ishara kuwa meli ya Watanashati Entertainment iliyomchukua Dogo Janja kwa mbwembwe nyingi, inaelekea kuzama na abiria wawili waliosalia, Dogo Janjaro na PNC wameanza kutafuta maboya haraka kujihami.


Kwa mujibu wa meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale, Dogo Janja amekuwa akimpigia simu Madee ili wakae chini waongee kumaliza tofauti zao na ili arejee Tip Top.


“Unavyomwona Dogo Janja leo hii anampigia simu Madee kumwomba wakae chini,” alisema Tale kwenye kipindi cha Mkasi.
 
“Ni kwamba wale marafiki hawapo tena. Leo hii kwakuwa Dogo Janja anamhitaji Madee atausema ukweli. Dogo Janja hela yake alikuwa anampa mshkaji mmoja anaitwa Doka. Mimi niliyajua hayo baada ya matatizo.”

Dogo Janja alijiondoa Tip Top June mwaka jana kwa madai kibao ikiwa pamoja na kudai kwamba hakuwahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.
 
Alidai kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja. Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show.
 
“Nilikuwa navumilia tu, kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” alikaririwa kwenye kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM.

 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari