Like Us On Facebook
Showing posts with label Rose Ndauka. Show all posts
Showing posts with label Rose Ndauka. Show all posts

WEMA,ROSE NDAUKA NDANI YA VITA KALI


MASTAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka na Wema Sepetu wanadaiwa kuingia vitani, mpambe mmoja wa Wema akitumia mtandao wa kijamii wa Instagram alimtuhumu Rose kwamba aliwahi kushiriki kikao kimoja kilichokuwa kikimjadili ‘madam’ huyo sanjari na kumtukana.

Mpambe huyo aliyetumia picha ya Wema (huenda akawa Wema mwenyewe), alisema kuwa siku moja isiyokuwa na jina hivi karibuni, Rose alishiriki kikao hicho kilichofanyika kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam ambapo sehemu kubwa ya mazungumzo ilikuwa ikimchambua Wema.

Akizungumza na Amani kwa njia ya simu juzi kuhusiana na tuhuma hizo, Rose alisema anashangaa matusi anayotukanwa na mtu huyo kwani ana mwaka mmoja hajawahi kukanyaga katikia viwanja hivyo vilivyopo Kinondoni, Dar.

“Kiukweli huyo mtu amenitukana bure, hajakaa na kufanyia uchunguzi hizo taarifa alizopewa, mimi sikumbuki kama kuna siku niliwahi kukaa Leaders na kuanza kumsema vibaya Wema kwani nina mwaka sijawahi kufika Leaders.

“Binafsi sina muda huo wa kumzungumzia mtu au kukaa na mtu ambaye hana faida kwangu. Mimi rafiki yangu ni mchumba wangu (Malick Bandawe), mama yangu na ndugu zangu zaidi ya hapo tunakutana shutingi tukimaliza narudi kwangu, namsihi huyo mpambe wa Wema afanye tena uchunguzi,” alisema Rose.

Juzi, Amani lilimsaka Wema kwa njia ya simu ya mkononi ili azungumzie madai hao lakini hakupatikana. Hata hivyo, habari zinasema kuwa mtu aliyemtukana Rose kwenye mtandao alitumwa na Wema au Wema mwenyewe.

Tangu Diamond kurudiana na Wema na kusambaza picha zao katika mitandao ya kijamii, hivi karibuni Wema kufiwa na baba yake mzazi (Isaac Sepetu) na baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi kususia msiba huo, kumeibuka makundi ya watu kazi yao kubwa ni kutukana watu ambao wako tofauti na Wema.

MIMBA YAHARIBU SURA YA ROSE NDAUKA BAADA YA USO KUVIMBA KILA MAHALI



Mwanamke mjamzito hatambuliki kwa tumbo lake tu, bali hata usoni. Miongoni mwa mabadiliko anayoanza kuyapata mwanamke awapo na ujauzito ni uso wake kuvimba hasa sehemu ya pua.
 
Hali hii ndio iliyoanza kumtokea, staa wa filamu nchini, Rose Ndauka ambaye ni mjamzito wa miezi kadhaa.
Akiweka picha aliyopiga na mchumba wake, Malick Bandawe aka Chiwaman wa kundi la TNG Squad kwenye Instagram, Ndauka ameandika:
 
“Unanafasi nyingi sana kwenye maisha yangu mwenyezi mungu akupe umri mrefu na afya tele @don_chiwaman ...nakupenda sana hubby wangu.”

ROSE NDAUKA ACHOSHWA NA MOVIE ZA KIBONGO AAMUA KUACHA KUIGIZA KWA MUDA

Mwigizaji Rose Ndauka amesema kuwa anapumzika kwenye tasnia ya filamu kwa mwaka mmoja kwakuwa filamu za Tanzania zinafanana sana na anataka aje na kitu kipya na tofauti.

Kwa mujibu wa gazeti la mwanaspoti Rose Ndauka amesema wazo hilo limetokana na tatizo la kufanya kazi zinazojirudia mara kwa mara, hali iliyomfanya aamue kujipa likizo ya muda ili kujipanga.
Hata hivyo kauli hiyo inaweza kuwa na utata muigizaji huyo ni mjamzito kwa sasa na huenda hiyo ndio ikawa ni sababu kubwa ya yeye kusimama kwa muda.

ROSE NDAUKA: "SIJAJIBEBEA TU MIMBA HOVYOHOVYO

STAA wa sinema za Bongo, Rose Ndauka amesema suala la kubeba mimba ya mpenzi wake, Malick Bandawe kabla ya ndoa halikutokea bila mpangilio, walishauriana kabla. 
Akipiga stori na paparazi wetu, Rose alisema hajutii kubeba mimba hiyo ambayo ameitangaza kwa vile alishauriana na mwandani wake huyo na anamuamini.

“Sijajibebea tu mimba hovyohovyo hata Malick alipogundua hali hii alifurahi sana, ndiyo maana sina presha hata kidogo kwa kuwa sisi ni wapenzi wa muda mrefu na tunaaminiana,” alisema Rose.

HUYU NDO MSANII WA BONGO MOVIE ANAYESADIKIWA KUWA NA MATITI MAZURI KULIKO WOTE!!

Msanii wa Bongo Filamu Super Star Rose Ndauka + Le Big Shoow

PICHA ZA CHUMBANI ZA ROSE NDAUKA, MCHUMBA’KE ZAVUJA!

                PICHA za chumbani za mwigizaji Rose Ndauka na mchumba wake, Malick Bandawe zimevuja  baada ya rafiki wa karibu wa wapenzi hao kuzisambaza kitaani.
 
Rafiki huyo wa karibu alizungumza na Weekly Star Exclusive na kusema kuwa wapendanao hao walikuwa wakilala katika hoteli moja iliyopo maeneo ya Mbezi Beach, jijini Dar kwa ajili ya kuilea mimba aliyonayo bibie.
“Huwa wanalala kwenye hoteli tangu mimba ilipoanza kuonekana, kusema kweli Malick anamlea Rose kama yai wasiwasi wangu atamlemaza wakati mjamzito anatakiwa afanye mazoezi,” alisema rafiki huyo kwa sharti la kutochorwa gazetini.
Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, Weekly Star Exclusive ilimuendea hewani Malick na kumuuliza juu ya picha hizo na suala la kuhamisha maskani hotelini hapo kama ni la kudumu au la! Alitiririka:
“Ni kweli nyumbani tunaenda mara mojamoja kwa sababu nahitaji mchumba wangu asiwe na msongo wowote wa mawazo, anahitaji sehemu ambayo imetulia ili ujauzito nao utulizane, muda mwingi tunautumia hotelini zaidi,” alisema Malick.

-GPL

ROSE NDAUKA ATANGAZA RASMI KUZAA NJE YA NDOA

          Staa wa filamu za Bongowood, Rose Ndauka ambaye ni mjamzito anadaiwa kuwa atazaa kabla ndoa mwezi Aprili, mwakani. Akizungumza na mwanahabari wetu, mchumbaa’ke, Malick Bandawe ambaye ni memba wa kundi la muziki la TNG alianika aya za Kurani kuwa katika Dini ya Kiislamu si ruhusa kufunga ndoa na mwanamke ambaye ni mjamzito kwani ni sawa na kufunga ndoa na watu wawili hivyo anamsubiri ajifungue kwanza. “Ni kweli mchumbaa’ngu hivi sasa ni mjamzito na anatarajia kujifungua mapema mwezi wanne, mwakani. “Kuhusu kufunga naye ndoa kwa sasa ni ngumu hadi ajifungue kwani kwa dini yetu (Uislam) si ruhusa kufanya hivyo lakini atakapojifungua tu tutafunga ndoa,” alisema Malick. Malick ambaye hivi sasa anatamba na Wimbo wa ‘Crazy Man’ alisema kuwa ana furaha kubwa kuitwa baba mtarajiwa na anamuomba Mwenyezi Mungu Rose ajifungue salama kwani anampenda kupita maelezo. Baada ya kuzungumza na Malick, gazeti hili lilimtafuta mama wa Rose Ndauka, Batuli kufungukia ishu ya mwanaye kubeba ujauzito kabla ya ndoa ambapo aligoma kuzungumza kwani hakubaliani na suala hilo.

NIMEPIMA NA SINA UKIMWI:ROSE NDAUKA

Baada  ya  kukabiliwa  na  skendo  ya  kugawa  uroda  kwa  msanii  Nasry  ndani  ya  Gesti, Rose  ndauka  ameamua  kukimbilia  hospitalini  ili  kuchukua  vipimo  vya  gonjwa  hatari  la  Ukimwi.....


 
Kupitia  ukurasa  wake  wa  mtandao  mmoja  wa  kijamii, Ndauka  aliposti  picha  ya  majibu  ya  vipimo    vya  UKIMWI   vilivyochukuliwa  katika  hospitali  ya   TMJ iliyopo  jijini  Dar es salaam....

Majibu  ya  vipimo  hivyo  yalionesha  kuwa  Rose  Ndauka  yuko  NEGATIVE.

Baada  ya  picha  hiyo, comment  kibao  zilianza  kumiminika  toka  kwa  mashabiki  wake.Wapo  waliompongeza  na  wapo  waliomponda.....

Waliomponda  walihoji  ni  kwa  nini  kawahi  kupima  na  kuyaanika  majibu  mtandaoni  wakati  MIEZI  MITATU  TANGU  ATUHUMIWE  HAIJAISHA??????.

Kwa  kawaida, hawa  wadudu  huonekana  katika  mzunguko  wa  damu  baada  ya  siku  90  tangu  ufanye  tendo  la  ndoa.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari