Like Us On Facebook
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

BAADA YA KUTANGAZA KURUDI SHULE,CHEKA AANZA UTORO SHULENI!

Bondia Francis ‘SMG’ Cheka, amedaiwa kuingia darasani siku moja tu tangu aliposajiliwa kama mwanafunzi mpya wa Chuo cha St Joseph cha mjini Morogoro Septemba mwaka jana.
Akizungumza na MWANANCHI, mwalimu wa Cheka aitwaye Mkisi amesema Cheka ameomba kuendelea na masomo baada ya kutoonekana darasani kwa miezi kadhaa bila taarifa yoyote, na kubainisha kuwa hawawezi kumruhusu kuingia muhula wa pili.
Cheka alipewa ufadhili wa masomo chuoni hapo mwaka jana mara baada ya kutwaa ubingwa wa dunia wa WBF Agosti 30, baada ya kumpiga Phil Williams wa Marekani katika pambano lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkisi amesema kuwa bondia huyo amekosa vipindi kwa muda mrefu hivyo hawezi kuingia muhula mwingine, kwakuwa atakosa vitu vingi hivyo anapaswa kujisajili kama mwanafunzi wa muhula mpya utakaoanza Machi 24.
“Cheka aliingia darasani siku moja na ‘kupotea’ hata hivyo hivi karibuni alikuja na kutuambia anataka kuendelea na shule ingawa hatuwezi kumuendelezea programu yake ya awali,” alisema Mkisi.
-Mwananchi

HII NDO MIZUKA YA SOKA IKIPANDA MTU ANASHINDWA KUJIZUIA KABISA!!

kweli mchezo wa mpira dah ni hatari mashabiki upagawa na kujikuta wakifanya vitendo ambavyo badae wakija kuanaglia hawaamini kama walifanya wao... tazama hii ya huyu jamaa aliyeamua kuingia uchi uwanjani baada ya kufurahishwa na mechi https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxQ2xhq1h68c96Tp4mr_bRtjP66ntXchyphenhyphen6QpI5QbfXVVMyULTjLV3undC2fEJgxoeLFimWMKKpGd5JZNnHIwOQOSwjg3K7Fnc63PlCZXvWKLGWSCXTrZv9wtGqOuYvABqGDvSwZ1vjWXZt/s640/vituko+%25281%2529.jpg

BAADA YA LIVERPOOL KUIPA KIPIGO KITAKATIFU ARSENAL,SHABIKI WA ARSENAL NCHINI KENYA AMUUA SHABIKI WA LIVEPOOL KWA KUMCHOMA KISU

MWANAUME mmoja alichomwa  kisu hadi kufa wakati akitazama mechi ya kandanda mjini Meru baada ya kutofautiana na mwenzake kuhusu mechi iliyokuwa ikiendelea.
Marehemu alikuwa akitazama mchuano kati ya timu ya Arsenal na Liverpool wakati walipoanza vita katika baa ya Marete eneo la Makutano.
Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa Polisi eneo hilo Tom Odero alisema mshukiwa David Mwangi, ambaye ni shabiki wa timu ya Arsenal alimdunga kisu Anthony Muteithia, shabiki wa Liverpool. Bw Odero alisema mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 25 alikufa alipokuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Meru.
“Mshukiwa alilazimika kutoroka lakini wakazi walifanikiwa kupata pikipiki aliyokuwa nayo na kuiwasilisha kwa maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Meru. Msako wa kumkamata umeanzishwa,”alisema Bw Odero.
ars
Mkuu huyo wa polisi alisema uchunguzi umeanzishwa kutambua chanzo cha mzozo wa wawili hao.
Katika mchezo huo Arsenal walichapwa 5-1 na Liverpool.
Credit Swahili hub

AIBU:PICHA ZA WENGER AKIWA AMECHANGANYIKIWA BAADA YA KIPIGO CHA LIVERPOOL CHA GOLI 5 KWA 1 ARSENAL

Strolling through: Wenger arrives at Liverpool Lime Street Station after the defeat

Slipped up: Wenger looks in pain as he takes a tumble coming into the station

Helping hand: A police officer comes over to help Wenger back onto his feet

Back on track: Another police officer helps Wenger with his bag as he is brought back up
On top of their game: Liverpool celebrate their humiliation of title rivals Arsenal on Saturday afternoon

Hit the road, Jack: Arsenal midfielder Wilshere can't believe his side's capitulation against their rivals

MJUE MCHEZAJI WA BRAZIL AMBAYE PIA NI MCHEZAJI WA SHAKHTAR DONETSK ALIYEFARIKI DUNIA JANA KWA AJALI YA GARI


Maicon Pereira de Oliveira
Mchezaji huyo Amefariki akiwa na  Miaka 25 alikua na kipaji na Alikua anachezea katika Club ya Shakhtar Donetsk.. Mshabuliaji huyo anaejulikana kwa jina la Maicon Pereira de Oliviera amefariki kwenye Ajali ya Gari. 
Club ya Shakhtar Donetsk imethibitisha Kifo hicho na kusema amefariki ya Asubuhi 8/2/2014

Maicon ni raia wa Brazil na alijiunga na Shakhtar Donetsk 2008 na ameonekana mara 6 na ameifungia timu hio Goli 1 tu. Hivi karibuni alipelekwa kwa mkopo timu nyingine

Maicon Pereira de Oliviera asifananishwe na Maicon Douglas Sisenando mwenye miaka 32 ambae pia ni raia wa Brazil ambae alikua akikipiga katika club ya Inter Milan amabe sasa anachezea katika club ya Roma.

SOURCE: BLOG YA VIJANA

YANGA YAJIOKOTEA KIBONDE YAKIPIGA GOLI SABA KAMA WAMESIMAMA,WAKOMORO HOI TAIFA

http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/02/Screen-Shot-2014-02-08-at-6.15.41-PM.png
Ubao wa Matokeo.
 Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Hamis Kiiza akiipachikia timu yake bao la nne kati ya saba yaliyotiwa kimiani mpaka sasa wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga inaongoza kwa Bao 7-0.
 Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akiondoka na mpira huku mabeki wa timu ya Komorozine ya nchini Comoro wakimsindikiza wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika unaoendelea kuchezwa hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga imeshinda kwa Bao 7-0.

 Mrisho Ngassa bado yuko na mpiraaaaa.....
 Mrisho Ngassa anapachika bao paleeeee...... Gooooooooo ni goli la sita hili linaungwa hivi sasa na Mrisho Ngassa na kuwa mchezaji pekee aliefunga bao tatu peke yake.
Wachezaji wa timu ya Komorozine wakilaumiana.
 Mshambuliaji wa Pembeni wa Timu ya Yanga,Simon Msuva (27) akiwatoka mabeki wa timu ya Komorozine ya nchini Comoro wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Mshambuliaji wa Pembeni wa Timu ya Yanga,Simon Msuva (27) akichuana vikali na Beki wa Timu ya Komorozine ya nchini Comoro,Ahmad Houmadi (5) wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Wachezajiwa timu ya Yanga wakishangilia bao lao la pili lililotiwa kimiani na Mchezaji Nadir Haroub.
 Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Haroun Niyonzima akiafanya makeke yake wakati alipotaka kumtoka Beki wa Timu ya Komorozine ya nchini Comoro, Ali Mohamed wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mashabikiwa Timu ya Yanga.
 

PICHA:VIJANA WANASWA WAKIJISAIDIA KWENYE MASINKI YA KUNAWIA KATIKA UWANJA WETU MPYA WA TAIFA JIJI DAR


Pichani juu ni baadhi ya wadau wa Soka waliokutwa hivi karibuni wakijisaidia kwenye masinki ya kunawia mikono kama waonekanavyo pichani.
Hapa baada ya kumaliza shughuli yao haoo wakaondoka,je wahusika wanalichukuliaje jambo hili lisilo la kiungwana kabisa ndani ya uwanja wa wetu wa mpira,ambao umejengwa kwa gharama kubwa,lakini kuna baadhi ya watu kama hawa wamekuwa wakiharibu maeneo na vifaa mbalimbali ya uwanja huo ikiwemo na kugeuza matumizi yake.

HUYU NDO MZEE MWENYE HATI MILIKI YA YANGA...ASEMA YEYE NDO MMILIKI HALALI WA YANGA

Mmiliki halali wa Yanga aibuka na kuidai klabu yake kutoka kwa viongozi wa sasa! Asema yeye na Tabu Mangala ndio walioisajili klabu serikalini mwaka 1967. Aongeza tokea Tabu Mangala ajitenge
na kuanzisha Pan Afrika 1975, yeye akabaki na hati zote za klabu na amekuwa akizilipia. Nini maoni yako?
Source: East Africa Television

Girlfriend wa mmiliki wa Chelsea ashambuliwa kwa kuonesha ubaguzi wa rangi, akalia kiti chenye umbo la mwanamke mweusi akiwa nusu uchi


 
Mpenzi wa Billionaire ambaye ni mmiliki wa timu ya mpira wa miguu, Roman Abramovich, alichafua anga baada ya kupost picha inayomuonesha akiwa amekaa juu ya kiti chenye umbo la mwanamke mweusi tena akiwa nusu uchi.
 
Mbaya zaidi mrembo huyo anayejukana kwa jina la Dasha Zhukova, alipost picha hiyo siku ya kumbukumbu ya Martin Luther King, January 20, 2014.
 
Katika picha hiyo iliyowekwa kwenye jarida maalum la mitindo la online ‘Buro 24/7’, Dasha ambaye pia ni mmoja kati ya wahariri wa Jarida la Garage, anaonekana akiwa amechill kwa raha zake wakati msichana huyo (mdoli/kinyago) akiwa amekaa miguu juu akiwa ameuweka mgogo wake chini.
 
Watu wengi walioiona picha hiyo walimshambulia vikali mrembo huyo kupitia twitter ukizingatia ni siku ya kumkumbuka mwanaharakati wa Marekani aliyepinga vikali ubaguzi wa rangi, Martin Luther King.
 
Picha hiyo iliwekwa pia kwenye Instagram na kutolewa baada ya muda mchache.

RONALDO NDIYE MFALME WA SOKA DUNIANI KWASASA ,AWABWAGA MESSI NA RIBERY

MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka wa FIFA kwa mara ya pili katika historia yake, akimuangusha mshindani wake mkuu, Lionel Messi.
Nyota huyo babu kubwa wa Real Madrid alikuwa anakabiliwa na ushindani wa mbali kidogo kwa nyota wa Barcelona, Messi na wa Bayern Munich, Franck Ribery katika kinyang'anyiro cha Ballon d’Or. 
Akiwa mwenye hisia kali, Ronaldo aliyekwenda jukwaani kuchukua tuzo yake akiwa ameambatana na mtoto wake wa kiume, Cristiano alishindwa kujizuia na kumwaga machozi wakati anapokea taji hilo.
Namba 1: Cristiano Ronaldo ameshinda Ballon d'Or na kutajwa ndiye mwanasoka babu kubwa duniani
Family time: A tearful Ronaldo was on stage with his son Cristiano to collect the award
All smiles: Ronaldo couldn't help but grin broadly when he posed with the trophy
Hisia: Ronaldo alishindwa kujizuia na akamwaga machozi jukwaani wakati anapokea tuzo ya Ballon d'Or
Winner: Pele holds up Ronaldo's son Cristiano as the Portuguese star picks up his award
Mshindi: Pele akiwa amemshika mtoto wa Ronaldo, Cristiano wakati Mreno huyo anapokea tuzo yake

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amepewa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 66 katika mechi 56 za klabu na nchi yake, Ureno mwaka 2013 hatimaye kuirejesha tuzo yake aliyoitwaa awali mwaka 2008.
Pamoja na kwamba Ronaldo hakutwaa taji kubwa mwaka 2013, alifunga mabao yote manne Ureno ikiitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya kombe la Dunia baadaye mwaka huu.
"Hakuna maneno ya kusema wakati huu," Ronaldo alisema, huku akifuta machozi. "Nataka kuwashukuru wenzangu wote na washirika pale Real Madrid, katika timu ya Ureno na familia yangu, ambako wako nami,".
"Wale ambao wananifahamu mimi, wanafahamu kwamba  watu wengi wananisaidia: kocha wangu, rais wetu, na sitaki  kusahau kumtaja Eusebio. Mpenzi wangu na mwanangu pia. Nasonga zaidi,". 
Glamorous: Ronaldo with his girlfriend Irina Shark during the awards ceremony
Ronaldo na mpenzi wake Irina Shark katika sherehe za tuzo
Nominees: The trio of Ronaldo, Lionel Messi and Franck Ribery before the ceremony
Washindani: Ronaldo, Lionel Messi na Franck Ribery kabla ya sherehe
Incomparable: Legendary striker Pele won an honourary prize at the Gala in Zurich
Gwiji Pele alipea tuzo katia usiku huo mjini Zurich
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Emotional: The Brazilian couldn't keep back the tears
Mfalme wa soka: Gwiji wa Brazil, Pele alishindwa kujizuia kutoa machozi alipokuwa jukwaani
Out at the top: Retied Jupp Heynckes was named Coach of the Year after winning the Champions League
Retied Jupp Heynckes ameshinda tuzo kocha bora wa mwaka wa dunia baada ya kuiwezesha Bayern Muich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Stunner: Zlatan Ibrahimovic won the Puskas prize for the best goal of the year for his goal against England
Mkali: Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Bao Bora la mwaka, maarufu kama Puskas 
Unreal: His overhead kick was during Sweden's 4-2 friendly win over England in November 2012
Bao lake tik tak Sweden ikiifunga 4-2 England Novemba mwaka 2012 ndilo bao bora la mwaka
Recognised: German keeper Nadine Angerer won the women's Player of the Year award
Kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kike wa mwaka wa Dunia
Duo: Ronaldo and Angerer pose side-by-side after being named the best players in the world
Wawili: Ronaldo na Angerer baada ya kutajwa wanasoka bora wa dunia 
Shot stopper: Angerer in goal for the German national team during a friendly against Japan
Prize: She was part of the Germany team that won the women's European Championships last year
Taji: Angerer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichoshinda Kombe la ubingwa wa Ulaya kwa wanawake

MAN UNITED NI MAJANGA JUU YA MAJANGA, VAN PERSIE SI WA LEO WALA KESHO KUREJEA UWANJANI, ROONEY NAYE APELEKWA MISRI KUTIBIWA

KLABU ya Manchester United inahofia Robin van Persie anaweza kuendelea kuwa nje kwa wiki sita zaidi baada ya kuumia paja sehemu ile ile aliyowahi kuumia alipokuwa Arsenal.
David Moyes anayemuhitaji sana mshambuliaji huyo wake hatari arejee uwanjani kutokana mwenendo mbaya wa timu hivi sasa, jana Ijumaa amethibitisha kwamba Wayne Rooney pia anaweza kukosa mechi ya leo dhidi ya Swansea.
Lakini mtu anayemuumiza kichwa aswa Moyes ni Van Persie, kocha huyo amesema kwamba hawezi kutaja tarehe ya kurejea uwanjani kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, hata baada ya kumpeleka Uholanzi akafanyiwe kazi na kocha wa viungo wa PSV Eindhoven.
Hasara juu ya hasara: Van Persie anaweza kuwa nje kwa wiki sita zaidi baada ya kuumia paja

Kuna wasiwasi Van Persie akawa nje kwa muda mrefu zaidi, kwa sababu ameumia sehemu ile ile ambayo aliwahi kuumia akiwa Arsenal Desemba mwaka 2007 na akakaa nje kati ya Desemba 16 na Machi 9, akicheza mechi 15 tu. 
Mholanzi huyo hajakitumikia kikosi cha Moyes tangu Desemba 10 na jana kocha wa United amesema pia kwamba Rooney amepelekwa Misri kwa matibabu sababu ya hali ya hewa pamoja na maofisa wa dawati la tiba la timu hiyo, ili aweze kuwahi mechi na Chelsea Januari 19.

YANGA WAKWEA PIPA KUELEKEA UTURUKI,CHEKI MAPICHA HAPA

Wachezaji wa Yanga SC, Mrisho Ngassa kulia na Haruna Niyonzima kushoto wakiwa ndani ya ndege ya Turkish Airline kwa safari ya Uturuki Alfajiri ya leo ambako wanakwenda kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara.
Jerry Tegete katika mgahawa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na chini ni Juma Abdul.

MCHEZAJI WA BAYERN MUNICH NA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI AJITANGAZA KUWA SHOGA,MTAZAME HAPA!


thomas 1Nyota wa zamani wa Ujerumani Thomas Hitzlsperger aliyeanzia soka lake kwenye klabu ya Bayern Munich  amejitangaza kuwa shoga.
Aliwahi kucheza kwenye ligi ya England kwa muda wa miaka mitano akicheza kwenye klabu ya Aston Villa kabla ya kujiunga na VFL Stutgart ya nyumbani kwao Ujerumani ambayo aliisaidia kutwaa ubingwa wa ligi ya Ujerumani Bundesliga.
Thomas pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwenye mashindano ya kombe la dunia na kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008 ambako alicheza mechi zote za hatua ya mtoano kuanzia robo fainali, nusu fainali na fainali.
thomas 2Kiungo huyu mshambuliaji pamoja na kuwa raia wa Ujerumani alichea sehemu kubwa ya soka lake nchini England kwenye timu za Aston Villa, West Ham United na Everton ambapo pamoja na Stuttgart, Bayern Munich ndiko alikoanzia soka lake na Werder Bremen.
Moja ya vitu ambavyo Hitzlsperger atakumbukwa navyo ni mashuti makali aliyokuwa anapiga kwa mguu wake wa kushoto na alifunga mabao mengi sana kwa style hiyo kabla ya kustaafu soka mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 31 baada ya kuandamwa na majeraha tofauti ya goti kwa muda mrefu.
thomas 3Thomas Hitzlsperger anakuwa mchezaji wa pili maarufu kujitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia moja baada ya mchezaji wa zamani wa Leeds United Robbie Rogers ambaye kwa sasa anacheza kwenye klabu ya Los Angeles Galaxy naye kujitangaza kuwa shoga.

BASI JIPYA LA AZAM LAWASILI...KAMA LA KLABU KUBWA ZA ULAYA

Hakuna Afrika nzima; Basi jipya la wachezaji wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, lililowasili nchini juzi likiwa tayari kusafirishwa visiwani Zanzibar ambako timu hiyo imekwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi. Hili ni aina ya mabasi ambayo yanatumiwa na klabu za Ulaya kama Manchester United, Bayen Munich na Barcelona ambalo kwa Afrika Azam inaweza kuwa klabu ya kwanza kulimiliki.
Kitu cha maana
Kila siti ina TV
Kuna friji
Kuna choo 
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari