Wiki
hii yote kumekuwa na kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya
kijamii kumefunikwa na tukio la kustaajabisha linalomuhusu mbunge wa CCM
Rosweeter Kasikila mwenye umri wa zaidi ya miaka sitini kufunga ndoa na
kijana mdogo Michael Chstiani (26) Mtandao huu umepata taarifa mpya juu
ya tukio hilo ambalo kwa sasa liko kwenye mgogoro mzito.
Habari
toka kwenye chanzo chetu cha habari zilisema kuwa sababu kubwa ya
Mheshimiwa huyo kuangukia kwenye penzi l "Serengeti boy" huyo ni
kutokana na ufundi wa hali ya juu wa kijana huyo hali iliyofanya Mama
huyo kushindwa kujizuia na kuamua kumfanya kijana huyo kuwa mume kabisa.
mama
mmoja wa makamo ambae alisema ni rafiki wa karibu na Mbunge huyo
alisema " Jamani wanangu acheni mapenzi yaitwe mapenzi ambayo hayana
macho haya hata mkificha lakini baadae kila kitu kitakuwa wazi huyo
kijana ana sifa ya kujua sana mambo anasifika mtaa mzima hivo Mh
alizidiwa na uzalendo akaamua kufunga ndoa nae ili kufaidi ndoa vizuri"
Alisema mama huyo.
Aidha
ishu hii licha kutizamwa kwa jicho la tatu na baadhi ya watu huku ikiwa
na mlengwa wa kisiasa pia watu mbalimbali walitoa komenti zao na
kueleza kuwa Mh huyo hakuwa na kosa kufanya maamuzi ya kuolewa na kijana
huyo ambae kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu huyo kijana ni mtu mzima
kwa maana ya kuvuka miaka 18