Like Us On Facebook
Showing posts with label MSIBA. Show all posts
Showing posts with label MSIBA. Show all posts

INASIKITISHA:MTU MMOJA AJINYONGA UFUKWE WA SPICE HOTEL,MATUKIO KATIKA PICHA


Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Bahati maarufu kwa uuzaji wa mifuko ya plastiki maeneo ya stand kuu ya mabasi Bukoba amekutwa kajinyonga juu ya mti  maeneo ya ufukwe wa Spice Motel majira ya saa nane mchana ..
 
Taarifa za awali  kutoka kwa watu waliokuwa katika tukio hilo zinasema  kuwa , kabla ya kifo cha, marehemu alionekana akiwa na mafurushi ya vitu na alikuwa akifua katika eneo hilo la ufukwe...

Mtu mmoja ambae hakuwa tayari kutaja jina lake  ameueleza  mtandao  huu  kuwa  leo majira ya saa 12.00asubuhi alisalimiana na marehemu maeneo ya stand ya mabasi akiendelea na shughuli yake ya kutembeza mifuko ya plastiki kwenye mabasi yaendayo  mikoani na maeneo mengine akiwa mzima wa afya.

Mwili wa marehemu umepelekwa Hospital ya Mkoa  wa Kagera kuifadhiwa kwa ajili ya utambuzi ( ndugu zake )
 Askari akiwa amepanda mti ili aweze kukata kamba aliyotumia kujinyonga
 Amekutwa katika hali hii
 Haijafahamika ni kwa nini kachukua maamuzi haya
 Mwili wa marehemu ukishushwa
 Kamanda wa polisi wilaya ya Bukoba akishuhudia tukio
 Wananchi waliokusanyika katika tukio
 Mkuu wa kituo cha polisi Bukoba(mwenye koti) akiwa anaangalia baadhi uya vitu vya marehemu alivyokuja navyo kabla ya kujinyonga
 Hivi ni vitu vya marehemu alivyokuja navyo babla ya kujinyonga
 Maeneo ya spice beach
 Mmoja wa watu wa kwanza kutoa taarifa kituo cha polisi Mama Faima
 Mwili wa marehemu ukipakiwa kwenye gari la polisi
Mwili wa marehemu ukipelekwa kuifadhiwa hospital ya mkoa wa kagera

MZEE DUDE WA FUTUHI AFARIKI DUNIA....

 

Mzee Dude enzi za uhai wake.

MSANII wa kundi maarufu la vichekesho na uigizaji la Futuhi, Mzee Dude amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza leo jioni!
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!

MWANAFUNZI IFM AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI, SOMA KILICHOTOKEA HAPA

Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha kupumzikia kilichopo chuoni hapo bila mwili wake kuwa najeraha lolote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea saa 11:30 juzi jioni katika chumba namba 118 jengo namba D kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi akiwamwaka wa pili.
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala nawanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili yamasomo.
“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla hajajiunga na chuohiki, kwa hapa chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea mara kwa mara,” alisema Mushi.
Aliongeza kuwa mara baada ya kupewa funguo alikwenda kupumzika katika chumba hicho na baadaye alikutwa amefariki huku mwili wake ukiwa umelala kitandani.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa katika kituo cha polisi napolisi walifika katika chumba hicho na kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Mushi alisema wamewasiliana na wazazi wake waliopo wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha mwili huo zitafanyika leo.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu, Peter Alphonce, aliliambia NIPASHE kuwa alikuwa na marehemu siku moja kabla ya kifo chake wakicheza mpira na walimaliza kucheza vizuri na kuagana kuelekea hosteli.
“Nilikuwa naye jana (juzi) tukicheza mpira, hadi saa kumi tulipomaliza aliniaga na kuelekea katika MachavaHostel ndiko anakolala,” alisema Alphonce.
@NIPASHE.

Mwigizaji Maarufu wa Filamu ya ISIDINGO afariki Dunia..!

Aliyekuwa muigizaji maarufu katika Tamthilia ya Isidingo The Need ya Afrika Kusini, Lesego Motsepe maarufu zaidi kwa jina la Lettie Matabane, amefariki dunia nchini mwake Afrika Kusini mapema leo.
Lettie, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa katika tamthilia hiyo kuanzia mwaka 1998 hadi 2008 alipoamua kuondoka, alikuwa akiishi na virusi vya Ulimwi kwa zaidi ya miaka 15. Mwaka 2011, aliwashitua
lese
mashabiki wake baada ya kuwatangazia kuwa yeye ni muathirika wa ukimwi. Hata hivyo wengi walimpongeza kwa kuwa na ujasiri wa kujitangaza hadharani, kwani kwa miaka mingi alikuwa akifanya kazi ya ubalozi wa mambo ya ukimwi. Aliianza kazi hiyo ya ubalozi kabla hajaathirika na hata alipoathirika hakushituka sana ingawa hali hiyo ilibadili maisha yake kabisa. Tamthilia ya Isidingo ni miongoni mwa tamthilia kongwe na maarufu nchini Tanzania ambayo imekuwa ikioneshwa na televisheni ya ITV kwa zaidi ya miaka kumi sasa bila kuchosha watazamaji wake.Mungu ailaze roho yake mahala pema – AMEEN!

WENGI WAJITOKEZA KUUGAGA MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA MAREHEMU JAMES KISAKA


 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho.

Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.
 Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho
 Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe
 Mtoto wa mwisho wa marehemu Kisaka, Christopher akitoa heshima za mwisho
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali.
 Wachezaji soka wa zamani wakijadiliana jambo nje ya Kanisa la Muhimbili walipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka. Kutoka kushoto ni Madaraka Selemani, Peter Tino, Khamis Kinye, Bakari Malima na Thomas Kipese.
 Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
 Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu James Kisaka akisoma wasifu wa marehemu kakake
 Msanii wa filamu Jacob Steven JB akitoa heshima za mwisho
 Mchezaji wa zamani wa Simba Malota Soma akitoa heshima za mwisho kwa mchezaji mwenzie marehemu Kisaka.
 Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula akitoa heshima za mwisho
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu, akitoa taarisha ya usafiri wa kwenda kwenye msiba baada ya kutoa heshima za mwisho.

CLEMENT MABINA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM AZIKWA LEO JIJINI MWANZA

Jeneza lenye mwili wa Clement Mabina likiwa mbele ya waombolezaji.
Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Mabina kwenye uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.…
Jeneza lenye mwili wa Clement Mabina likiwa mbele ya waombolezaji.
Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Mabina kwenye uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.
Padre akiongoza ibada ya mazishi katika uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.
Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja akifuatilia ibada ya kuuombea mwili wa Mabina.
Ndugu na jamaa wakishiriki ibada ya kumuombea Mabina.
Jeneza lenye mwili wa Mabina likiwa eneo la kaburi.
...Likiingizwa kaburini.
Ndugu na jamaa wakiweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Clement Mabina.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mazishi hayo eneo la Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, akiongea na wanahabari mara baada ya maziko 
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa (CCM), Clement Mabina (56), amezikwa mchana huu shambani kwake Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza. Mazishi hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, viongozi wa serikali, madhehebu ya dini, vyama vya siasa, wananchi na wakazi wa Kisesa ambao wameungana na ndugu, jamaa na marafiki kumsindikiza marehemu Mabina. Mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyofanyika uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.
-GPL
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari