Rais Jakaya Kikwete leo ametengua uteuzi wa mawaziri wanne kufuatia shutuma nzito dhidi yao katika sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili.
Mawaziri waliopoteza ajira
zao usiku huu ni pamoja na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), David
Mathayo (Mifugo na Uvuvi), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani) na Shamsi
Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).
Akizungumza Bungeni Dodoma
usiku huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kulikuwa na matatizo
makubwa katika usimamizi wa zoezi hilo.
“Tulifanya
operesheni kwa nia nzuri,” alisema Waziri Mkuu Pinda na kuongeza :
“Tatizo ni namna operesheni hiyo ilivyotekelezwa.”
Katika mdahalo uliogusa nyoyo
za wabunge na wachambuzi mbalimbali wa siasa leo, wabunge waliueleza
umma jinsi ambavyo Operesheni hiyo ilitumika kutesa, kunyanyasa na kuua
raia wasio na hatia na kuwadhulumu mali zao.