OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) si mchezo! Safari
hii imenasa tukio la mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jose
kuuza mwili.
Tofauti na matarajio ya familia yake, mrembo huyo alikwenda kukita kambi maeneo hayo akijihusisha na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya kusaka fedha ya kununulia sare za harusi yake ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Dada huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe katika kikao cha harusi ya dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi elfu 50 lakini alishangaa kumuona maeneo hayo hatarishi.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.
OFM ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma kwenye majukumu yao
walimtia mbaroni dada huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa
wanaume huku mmoja wa vijana wa OFM akijifanya mteja na kupatana naye
bei ya kuingia chumbani kwa ‘shoti taimu’.
Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.
Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.
Hata hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki kwani hakikusikika, yeye
na wenzake walionaswa walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha
polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake