KOCHA Jose Mourinho amesema hajutii kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Romelu Lukaku kwenda Everton.
Kocha huyo Chelsea alimshuhudia Lukaku
akifunga mabao mawili dhidi ya Newcastle Jumatatu, akiongezea kwenye bao
lake la kwanza alilofunga dhidi ya West Ham.
Pamoja na kufunga mabao hayo matatu, lakini Mourinho amesema timu yake ni tofauti sana na ya Roberto Martinez.
Macho makini: Jose Mourinho alimshuhudia mshambuliaji aliemtoa kwa mkopo Romelu Lukaku akicheza vizuri Everton
Kwa penalti: Lukaku aliifungia mabao mawili Toffees dhidi ya Newcastle Jumatatu
Chelsea itakwenda kucheza na Norwich
kesho, na Mourinho anatarajiwa kushusha kikosi kikali kilichoifunga
Steaua mabao 4-0 mjini Bucharest Jumanne.
Alipoulizwa kama anajuta kumtoa mchezaji
huyo kwa mkopo, Mourinho alisema: "Hapana. NI kitu kimoja kuchezea
Everton, na kingine kuchezea Chelsea,".