Ilidhaniwa kuwa labda alipata pesa za muda tu lakini wiki zimepita na mpaka leo makazi ya Odoh yapo sehemu inaitwa Independence Layout hapa Enugu na hiyo sehemu yake sasa inaonekana kama mbingu ya starehe za wine na vyakula. Marafiki wapya na wazamani wanafurika kwake kupata wine na vyakula.
Ukiachia mbali kwa yeye kuhama chumba chake alichokuwa anaishi chuoni kwao ambako walikuwa wanaishi wane wane Odoh anazunguka tu mjini akisukuma mkoko Sports wenye gharama balaa, na kampani yake ni wasichana wazuri wa aina yoyote atakayo yeye na wengi wao ni wanafunzi wa IMT au ESUT. Wakati watu wengi wakijiuliza ni nini amefanya Odoh kilichomfanya awe tajiri ghafla watu wengine wa karibu wanajua kuwa pesa hizo hazitokani na wizi wa kwenye mitandao bali aliuza figo yake mwenyewe alipoenda nchini Malaysia.
“Kama utapenda nitakuunganisha kwa wahusika. Ukweli ni kwamba hakuna kosa kwa kile nlichokifanya. Kama watu wanaweza kujitolea figo zao bure na kuokoa maisha ya wengine, kwanini mtu mwingine asitumie figo yake kuokoa maisha ya wengine na vilevile kujipatia pesa ambayo itamkwamua kutoka kwenye umasikini. Hiko ndio nilichofanya na sijilaumi” aliliambia Sunday Express.
Odoh akaendelea kurusha kombora: “Sasa hivi navyoongea na wewe, kuna Wanigeria wengi sana wako kwenye foleni nchini Malaysia ambao tayari wameshafanya utaratibu wa kuuza figo zao. Wengine wanashauku ya kupata hela ili kuanzisha vitu ambavyo vitaendesha maisha yao. Siwezi kusema wote wanaziuza lakini ukweli ni kwamba hata wale ambao wachagua kuzichangia bure bado wanapewa pesa za kufutia jasho. Kwahiyo tofauti iko wapi?” alisema Odoh. Story Ya Odoh inaendelea kwa<<BOFYA HAPA INAENDELEA KWA KIINGEREZA>>