Rais wa TZ , Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kuwa mgogoro baina ya Tanzania na Rwanda umemalizika.
Katika
hotuba yake ya mwisho wa mwezi kwa raia wa nchi hiyo Rais Kikwete
amesema hatua hiyo inafuatia mazunguzo baina ya viongozi hao wawili
yaliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda .
Japo hajataja ni
kwa namna gani mgogoro huo uliokuwa umefukuta baina ya Tanzania na
Rwanda utakuwa umepatiwa ufumbuzi, Rais Kikwete amesema hatua ya
mazungumzo baina yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame ndio chanzo cha
mafanikio hayo yote.
Tanzania
na Rwanda zilingia katika mgogoro wa kidiplomasia hadi kufikia hatua ya
kutunishiana misuli kisiri baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzishari nchi
za Rwanda na Uganda kuzungumza na waasi wa nchi zao waliopo nchini
Jamuhuiri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Jambo hilo lililopingwa
vikali na Rwanda kwa madai kwamba Rais Kikwete aliingilia mambo ya ndani
ya Rwanda kwa kuwashauri kufanya mazungumzo na watu walioua raia wa
nchi hiyo.
Mgogoro huu ulipamba moto na hata kukolezwa zaidi na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Rais
Kikwete ametoa wito kwa vyombo vya habari, wanasiasa pamoja na mitandao
ya kijamii kusaidia kwa upande mwingine kuziba ufa wa uhusiano
uliojitokeza kati ya nchi hizo mbili.
Aidha katika hotuba rais
Kikwete alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa opereshi ya kuwaondoa
wahamiaji haramu nchini humo iliyofanyika hivi karibuni ambapo amesema
kuwa operesheni hiyo iliendeshwa bila kukiuka haki za binadamu.
Kuhusu
wahamiaji waliokaa nchini Tanzania muda mrefu Rais Kikwete amesema watu
hao sasa watepewa uraia rasmi wa Tanzania ili wafuate uratibu.