Kichanga alichojifungua denti.
Tukio hilo lilitokea Septemba 25, mwaka huu maeneo ya Ubungo National
Housing jijini Dar ambapo asubuhi ya siku hiyo, Salma alilalamikia
maumivu ya tumbo lake kiasi cha mama yake aliyejitambulisha kwa jina la
Rahma Shabani kwenda kuomba msaada wa kitabibu.
Denti baada ya kujifunga kichanga.
Mwanamke huyo alieleza kwamba baada ya kurudi ndani alikomuacha
mwanaye, alimkuta akiwa amejifungua kichanga sebuleni, kitu ambacho
hakukitarajia kwa kuwa alizoea kumnunulia vifaa vya kujisitiri wakati wa
hedhi kila alipomlalamikia maumivu ya tumbo akijua yupo kwenye siku
zake.Akiwa na manesi walioongozana naye, walimsaidia Salma huku kila mtu akiwa amepigwa na butwaa kwa kilichotokea kwani hakuna aliyekuwa anajua kama Salma alikuwa na ujauzito.
Mama mzazi wa denti.
Akiongea na waandishi wetu, Salma alisema alipewa ujauzito na
mwanaume aliyemtaja kwa jina la John Vicent ambaye alikuwa mtoto wa
mwenye nyumba wao wa zamani.Salma alisema kuwa John alikuwa akimshawishi kila mara kufanya mapenzi japo alimkatalia kwa kuwa alijua akifanya kitendo hicho atapata mimba.
Mazishi ya kichanga yakifanyika.
Salma alizidi kutiririka kuwa John alikuwa akimpa dawa alizodai ni za kuzuia ujauzito. Baada ya kupata taarifa hizo mama wa Salma pamoja na ndugu zake walitoa taarifa Kituo cha Polisi Urafiki ambapo walifungua jalada la mashtaka lenye namba RB, URP/RB/7316/2013 KUBAKA na kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu na uthibitisho wa daktari.
Kaburi la kichanga.
Walimu wa shule anayosoma Salma, walipigwa na butwaa baada ya kupata
taarifa hizo na kueleza kwamba hawakuwa na taarifa kwamba denti huyo
alikuwa mjamzito.Kichanga hicho kilizikwa makaburi ya Ufi, Shekilango jijini Dar.
-GPL