Aina
fulani ya unyanyasaji iliyojificha ambayo inajulikana kama ‘breast
ironing,’ ambapo wasichana wadogo kama miaka 10 wanayachoma maziwa yao
na vitu vya moto ili kujifanya wamekua inaweza kuwa inafanyika UK.Unyanyasaji
huu wakimila za kikameruni uliwekwa ili kuondoa matamanio ya kimapenzi
ya wanaume,mimba zisizohitajika na ubakaji kwa kuzuia dalili za kuwa
mtoto wa kike anapevuka/anakuwa mtu mzima,gazeti la independent
liliripoti.Kwa wajuzi wanasema kuwa maelf ya wakameruni wanaoishi UK wanafuata mila hii. Kuchoma
matiti (Breast ironing)inatambulika na UN kama moja ya makosa ya jinai
dhidi ya wanawake na kwa makadirio wasichana wadogo milioni 3.8
wameathiriwa na mila hii.ukiachia
mbali kuwa inamaumivu makali,pia mila hii inahatarisha afya ya wasichan
hao na kusababisha magonjwa na titi moja au matiti yote kupotea.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.